Orodha ya kucheza ni mkusanyiko wa video. Mtu yeyote anaweza kutayarisha na kushiriki orodha za kucheza na marafiki wanaweza kuweka video kwenye orodha yako ya kucheza.
Unaweza kwenda kwenye kichupo cha Wasifu ili uangalie orodha zako za kucheza. Unaweza pia kudhibiti orodha zako za kucheza katika Studio ya YouTube.
Fuatilia Chaneli ya Watazamaji wa YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.
Ili upate orodha zako za video, nenda kwenye mwongozo na ubofye Wasifu.
Create and manage a YouTube playlist on your desktop
Kuunda orodha ya video kutoka kwenye video au Video fupi
Ili uunde orodha ya kucheza kutoka kwenye video:
- Nenda kwenye ukurasa wa kutazama wa video ambayo ungependa kuweka kwenye orodha.
- Bofya Zaidi
Hifadhi
Tayarisha orodha mpya
Weka jina la orodha.
- Tumia kisanduku kuchagua mipangilio ya faragha ya orodha yako. Ikiwa ya faragha, ni wewe tu unayeweza kutazama orodha hiyo ya kucheza.
- Bofya Tayarisha.
Ili uunde orodha ya kucheza kutoka kwenye Video fupi:
- Nenda kwenye ukurasa wa kutazama wa Video fupi ambayo ungependa kuweka kwenye orodha.
- Bofya Zaidi
Hifadhi
Tayarisha orodha mpya
Weka jina la orodha.
- Tumia kisanduku kuchagua mipangilio ya faragha ya orodha yako. Ikiwa ya faragha, ni wewe tu unayeweza kutazama orodha hiyo ya kucheza.
- Bofya Tayarisha.
Kudhibiti orodha
Kuhifadhi maudhui kwenye orodha ya kucheza
- Nenda kwenye ukurasa wa kutazama wa video au Video fupi unayotaka kuweka kwenye orodha ya video.
- Bofya Zaidi
Hifadhi
Chagua orodha kama vile Tazama Baadaye au orodha ambayo tayari umetayarisha.
- Ujumbe utaibuka katika sehemu ya chini ya skrini yako ukithibitisha orodha ambayo video yako imewekwa.
Kubadilisha orodha ya kucheza
- Chagua orodha ya kucheza unayotaka kubadilisha katika Mwongozo.
- Bofya Badilisha
katika sehemu ambayo ungependa kubadilisha.
Kuchuja orodha ya kucheza kulingana na aina ya video
- Chagua orodha ya kucheza unayotaka kubadilisha katika Mwongozo.
- Chagua chipu iliyo na aina ya maudhui unayotaka kutazama katika orodha yako ya kucheza:
- Yote: Huonyesha maudhui yote yaliyohifadhiwa kwenye orodha.
- Video Fupi: Huonyesha Video Fupi zilizohifadhiwa kwenye orodha. Kipengele hiki kinapatikana kwenye kompyuta pekee.
- Video: Huonyesha video ndefu zilizohifadhiwa kwenye orodha.
Kupanga upya orodha ya kucheza
- Ili upange video upya: Fungua orodha ya kucheza
Buruta video juu au chini kwenye orodha ya kucheza.
- Ili upange video upya kwa muda: Katika kidirisha cha ukurasa wa kutazama orodha, buruta video juu au chini kwenye orodha.
Kumbuka: Kipengele hiki hakipatikani kwenye orodha zilizo na Video Fupi za YouTube pekee.
Kufuta orodha
- Nenda kwenye mojawapo ya orodha zako za kucheza.
- Bofya Zaidi
.
- Chagua Futa orodha ya kucheza
.
- Thibitisha kuwa ungependa kufuta orodha yako ya kucheza kwa kuchagua Futa.
Baada ya kufuta orodha, jina na URL ya orodha haitaoneka wala kuweza kutafutika tena katika Takwimu za YouTube. Data inayohusishwa na orodha ya kucheza, kama vile Muda wa kutazama, itabaki kuwa sehemu ya ripoti pana, lakini haitahusishwa na orodha ya kucheza uliyofuta.