Unaweza kupata historia ya mambo uliyotafuta kwenye YouTube katika Ukurasa wa Shughuli Zangu. Kuanzia hapo, unaweza:
- Kuangalia historia yako ya mambo uliyotafuta
- Kutafuta historia ya mambo uliyotafuta ili upate video mahususi
- Kufuta historia yote ya mambo uliyotafuta
- Kuondoa utafutaji binafsi kwenye mapendekezo ya utafutaji
- Kusimamisha historia ya mambo uliyotafuta
Kumbuka: Ili uangalie au ufute ulichotazama hapo awali kwenye YouTube angalia ukurasa wa Shughuli Zangu.
Madokezo kadhaa ya kuzingatia:
- Hoja za utafutaji ulizofuta hazitaathiri tena mapendekezo unayoonyeshwa.
- Baada ya kufuta historia ya mambo uliyotafuta, utafutaji wako wa awali hautaonekana tena kama mapendekezo kwenye kisanduku cha kutafutia.
- Mambo uliyotafuta wakati historia ya mambo uliyotafuta imesimamishwa hayatahifadhiwa kwenye historia ya mambo uliyotafuta.
Ikiwa umeondoa video zozote kwenye historia ya video ulizotazama kifaa chako kikikuwa nje ya mtandao, inaweza kuchukua saa chache kwa mabadiliko hayo kusawazisha.
Kusimamisha historia ya mambo uliyotafuta
- Nenda kwenye picha yako ya wasifu .
- Gusa Mipangilio Dhibiti historia yote.
- Gusa Kuhifadhi historia yako ya YouTube Acha kuchagua "Jumuisha utafutaji wako kwenye YouTube."
Kufuta utafutaji mahususi
- Gusa Tafuta .
- Gusa na ushikilie tokeo la utafutaji unaopendekezwa na aikoni ya Historia karibu na aikoni hiyo.
- Gusa Ondoa kwenye dirisha ibukizi.
Televisheni, kifaa cha michezo ya video au kifaa cha kutiririsha maudhui
Kusimamisha historia ya mambo uliyotafuta
- Katika Menyu iliyo mkono wa kushoto, nenda kwenye Mipangilio .
- Chagua Kusimamisha historia ya mambo uliyotafuta.
- Chagua kitufe chaKusimamisha historia ya mambo uliyotafuta.
Futa historia ya mambo uliyotafuta
- Katika Menyu iliyo mkono wa kushoto, nenda kwenye Mipangilio .
- Chagua Futa historia ya mambo uliyotafuta.
- Chagua kitufe cha Futa historia ya mambo uliyotafuta.
Angalia makala yetu mengine kwa maelezo zaidi kuhusu historia ya video ulizotazama, kuondoa maudhui yaliyopendekezwa na kuboresha mapendekezo yako.
Kutafuta Faraghani
Ukivinjari katika hali fiche, historia ya mambo uliyotafuta haitahifadhiwa. Pata maelezo zaidi kuhusu Kutumia Faraghani.