Unaweza kudhibiti historia ya mambo uliyotafuta kwa kufuta utafutaji mahususi, kufuta au kusitisha historia ya mambo uliyotafuta. Pata maelezo zaidi kuhusu data yako kwenye YouTube na kudhibiti shughuli zako kwenye YouTube.
Vidokezo:
- Hoja za utafutaji ulizofuta hazitaathiri tena mapendekezo unayoonyeshwa.
- Baada ya kufuta historia ya mambo uliyotafuta, utafutaji wako wa awali hautaonekana kama mapendekezo kwenye kisanduku cha kutafutia.
- Mambo uliyotafuta wakati historia ya mambo uliyotafuta imesitishwa hayatahifadhiwa kwenye historia ya mambo uliyotafuta.
- Ukivinjari katika hali ya Faraghani, historia ya mambo uliyotafuta haitahifadhiwa. Pata maelezo zaidi kuhusu kutumia hali ya Faraghani.
Kusitisha historia ya mambo uliyotafuta
- Ingia katika programu ya YouTube.
- Gusa picha yako ya wasifu
.
- Gusa Mipangilio
Dhibiti historia yote.
- Gusa kichupo cha Vidhibiti.
- Acha kuchagua "Jumuisha utafutaji wako kwenye YouTube."
Kufuta historia ya mambo uliyotafuta
- Ingia katika programu ya YouTube.
- Gusa picha yako ya wasifu
.
- Gusa Mipangilio
Dhibiti historia yote.
- Chagua moja kati ya yafuatayo:
- Futa: Gusa
kando ya hoja ya utafutaji ili uifute. Ili ufute zaidi ya hoja moja ya utafutaji kwenye historia yako kwa wakati moja, gusa FUTA.
- Tafuta: Gusa
ili upate hoja mahususi.
- Kalenda: Gusa
ili uvinjari historia yako ya kipindi mahususi.
- Futa: Gusa
Kumbuka: Kutumia FUTA kufuta historia ya mambo uliyotafuta pia kutafuta historia ya video ulizotazama katika kipindi cha muda ulichochagua.