Kuangalia au kufuta Historia ya mambo uliyotafuta kwenye YouTube

Unaweza kupata historia ya mambo uliyotafuta kwenye YouTube katika Ukurasa wa Shughuli Zangu. Kuanzia hapo, unaweza:

  • Kuangalia historia yako ya mambo uliyotafuta
  • Kutafuta historia ya mambo uliyotafuta ili upate video mahususi
  • Kufuta historia yote ya mambo uliyotafuta
  • Kuondoa utafutaji binafsi kwenye mapendekezo ya utafutaji
  • Kusimamisha historia ya mambo uliyotafuta
Kumbuka: Ili uangalie au ufute ulichotazama hapo awali kwenye YouTube angalia ukurasa wa Shughuli Zangu.

Madokezo kadhaa ya kuzingatia:

  • Hoja za utafutaji ulizofuta hazitaathiri tena mapendekezo unayoonyeshwa.
  • Baada ya kufuta historia ya mambo uliyotafuta, utafutaji wako wa awali hautaonekana tena kama mapendekezo kwenye kisanduku cha kutafutia.
  • Mambo uliyotafuta wakati historia ya mambo uliyotafuta imesimamishwa hayatahifadhiwa kwenye historia ya mambo uliyotafuta.

Ikiwa umeondoa video zozote kwenye historia ya video ulizotazama kifaa chako kikikuwa nje ya mtandao, inaweza kuchukua saa chache kwa mabadiliko hayo kusawazisha.

Kufuta utafutaji mahususi

Nenda kwenye Shughuli Zangu kisha Karibu na utafutaji unaotaka kuufuta, bofya Futa .

Kufuta historia ya mambo uliyotafuta

Nenda kwenye Shughuli Zangu kisha Bofya Futa shughuli kulingana na… kisha Chagua muda wa shughuli ambayo ungependa kufuta kisha Bofya Futa katika sehemu ya chini ya upande wa kulia wa dirisha ibukizi.

Kusimamisha historia ya mambo uliyotafuta

Bofya shughuli ya Kuhifadhi  kisha ubofye kitufe cha Washa au Zima ili uzime. Chaguo hili litafanya unachotazama na kutafuta kisihifadhiwe, hadi kipengele cha utafutaji na historia ya video ulizotazama kiwashwe tena.

Kufuta kiotomatiki historia ya mambo uliyotafuta na historia ya video ulizotazama

Unaweza kuchagua kufuta mambo uliyotafuta kwenye YouTube na historia ya video ulizotazama kiotomatiki baada ya muda fulani.

  1. Kwenye kompyuta yako, nenda kwenye Akaunti yako ya Google.
  2. Katika kidirisha cha juu kushoto, bofya Data na faragha.
  3. Katika "Mipangilio ya Historia", bofya Historia ya YouTube.
  4. Bofya muda wa kufuta kiotomatiki unaotaka kisha Inayofuata kisha Nimeelewa katika sehemu ya chini kulia ya dirisha ibukizi ili uhifadhi chaguo lako la shughuli ya kufuta kiotomatiki.

Televisheni, kifaa cha michezo ya video au kifaa cha kutiririsha maudhui

Kusimamisha historia ya mambo uliyotafuta

  1. Katika Menyu iliyo mkono wa kushoto, nenda kwenye Mipangilio .
  2. Chagua Kusimamisha historia ya mambo uliyotafuta.
  3. Chagua kitufe chaKusimamisha historia ya mambo uliyotafuta.

Futa historia ya mambo uliyotafuta

  1. Katika Menyu iliyo mkono wa kushoto, nenda kwenye Mipangilio .
  2. Chagua Futa historia ya mambo uliyotafuta.
  3. Chagua kitufe cha Futa historia ya mambo uliyotafuta.

Angalia makala yetu mengine kwa maelezo zaidi kuhusu historia ya video ulizotazama, kuondoa maudhui yaliyopendekezwa na kuboresha mapendekezo yako.

Kutafuta Faraghani

Ukivinjari katika hali fiche, historia ya mambo uliyotafuta haitahifadhiwa. Pata maelezo zaidi kuhusu Kutumia Faraghani.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11649036200703410363
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false