Unaweza kupakua faili za MP4 za video za YouTube ulizopakia kwenye YouTube katika ubora wa 720p au 360p, kulingana na ukubwa wa video. Unaweza pia kutumia programu ya Google Takeout kupakua video zote ulizopakia.
Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.
Kumbuka: Huwezi kupakua video za YouTube za watumiaji wengine. Unaweza kutazama video nje ya mtandao kwenye programu ya YouTube ukiwa na uanachama wa YouTube Premium. Pata maelezo zaidi kuhusu kuhifadhi video nje ya mtandao ukitumia YouTube Premium.
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye kidirisha cha kushoto, chagua Maudhui.
- Elekeza kiteuzi kwenye video ambayo ungependa kuipakua na uchague Menyu kisha Pakua.
Ikiwa ulitia ukungu au kupunguza video yako, unaweza kupakua na kuipakia tena ili uchapishe mabadiliko yako.
Kutatua hitilafu zinazotokea wakati wa kupakua video zako
Huwezi kupakua video zako ikiwa:
- Video yako imeondolewa kwenye YouTube.
- Video yako ina onyo kwa kukiuka hakimiliki au Mwongozo wa Jumuiya.
- Video yako inatumia wimbo wa sauti ulioidhinishwa mapema.
- Tayari umepakua video yako mara tano katika saa 24 zilizopita. Unaweza tu kupakua video mahususi hadi mara tano kwa siku. Baada ya siku moja kupita, utaona chaguo la kupakua video tena.