Sera kuhusu shughuli bandia

Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.

YouTube hairuhusu maudhui ambayo yanaongeza kwa njia bandia idadi ya waliotazama, waliopenda, waliotoa maoni au vipimo vingine kwa kutumia mifumo ya kiotomatiki au kuonyesha video kwa watazamaji wasiotarajia. Pia, hairuhusu maudhui ambayo lengo lake la kipekee ni kuwashawishi watumiaji wachukue hatua (kutoa maoni, kupenda, kutazama nk).

Maudhui na chaneli ambazo hazifuati sera hii zinaweza kufungwa na kuondelewa kwenye YouTube.

Muhimu:  Iwapo unamwajiri mtu atangaze chaneli yako, maamuzi yake yanaweza kuathiri chaneli yako. Mbinu yoyote inayokiuka sera zetu inaweza kusababisha kuondolewa kwa maudhui au chaneli, iwe ni kitendo kutoka kwako au kwa mtu uliyemwajiri.

Tunazingatia matukio ya kushiriki kama njia halali wakati lengo la msingi la mtumiaji ni kuchukua hatua kwenye maudhui kwa njia ya kweli. Tunachukulia matukio ya kushiriki kuwa si halali, kwa mfano, wakati yanasababisha matendo ya kupotosha au kulazimisha au wakati lengo la kipekee la kushiriki ni manufaa ya kifedha.  

Ikiwa utaona maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wetu wa Jumuiya yanapatikana hapa. Iwapo umeona video au maoni machache ambayo ungependa kuyaripoti, unaweza kuripoti chaneli hiyo.

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Ikiwa unachapisha maudhui

Usichapishe maudhui kwenye YouTube ikiwa yanalingana na maelezo yoyote yaliyo hapa chini.

 • Viungo vinavyoelekeza kwenye au vinavyotangaza huduma za wengine ambazo huongeza kwa njia bandia vipimo kama vile idadi ya wanaotazama, wanaopenda na wanaofuatilia chaneli
 • Maudhui yanayounganisha kwenye au kutangaza idadi ya waliotazama au kujisajili kwenye huduma au tovuti za wengine za michezo ya video
 • Kuamua kufuatilia chaneli ya mtayarishi mwingine iwapo tu anafuatilia chaneli yako (“kufuatiliana”)
  • Kumbuka: Unaruhusiwa kuwahimiza watazamaji wafuatilie chaneli, wabonyeze kitufe cha kupenda, washiriki au watoe maoni
 • Maudhui yanayoangazia mtayarishi akinunua utazamaji kutoka kwa washirika wengine kwa nia ya kutangaza huduma hiyo

Sera hii hutumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko ya moja kwa moja na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii haijataja kila kitu.

Jinsi ya kupima matukio ya kushiriki

Idadi za wanaofuatilia zinazoonyeshwa katika maeneo yafuatayo husasishwa katika muda halisi:

 • Ukurasa wa kwanza wa chaneli yako
 • Kibadilisha akaunti
 • Ukurasa wa kutazama video
 • Programu na tovuti za wengine zinazotumia YouTube Data API

Idadi ya wanaofuatilia chaneli katika Takwimu za YouTube inaweza kutofautiana na idadi ya wanaofuatilia iliyo kwenye chaneli yako ya YouTube. Idadi katika Takwimu za YouTube huwa takribani saa 48 nyuma. Kuchelewa huku huturuhusu tufanye uthibitishaji wa ziada na ukaguzi wa taka, kwa hivyo idadi hiyo si sahihi.

Idadi ya wanaotembelea ukurasa ikipatikana kuwa bandia haitajumuishwa kwenye YouTube na inaweza kusababisha maonyo kwenye akaunti yako. Akaunti zinazosimamishwa na wafuatiliaji ambao wanatambuliwa kuwa taka hawatajumuishwa kwenye idadi ya jumla ya wanaotazama au wanaofuatilia chaneli. Watazamaji hawa hawatumii akaunti, kwa hivyo kuondolewa kwao hakuathiri idadi ya waliotazama au muda wa kutazama.

Iwapo video iliondolewa katika idadi ya waliotazama michezo ya video, angalia ukurasa huu katika Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi.

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui yasiyoruhusiwa kwenye YouTube.

 • Ushahidi wa video ambapo mtayarishi anajionyesha akinunua idadi bandia ya wanaotembelea ukurasa kutoka kwa mshirika mwingine
 • Video ambapo mtayarishi anaunganisha kwenye ukurasa bandia wa mshirika mwingine anayetoa huduma za kutembelea ukurasa katika muktadha wa kuhimiza au kutangaza. Kwa mfano: "Nilipata watu milioni 1 waliofuatilia chaneli kutokana na video hii kwa siku moja na wewe pia unaweza kufanya hivyo!"
 • Video ambayo inajaribu kulazimisha au kuhadaa watazamaji watazame video nyingine kwa njia za kupotosha (kwa mfano: kadi ya maelezo yenye lebo inayopotosha)
 • Chaneli zinazotumia hali bandia ya wanaotembelea chaneli au kutangaza biashara kama lengo lake la kipekee

Kumbuka kuwa hii ni baadhi tu ya mifano na usichapishe maudhui iwapo unaona kuwa yanaweza kukiuka sera hii.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Kipindi cha siku 90 kitaanza baada ya mafunzo kukamilika, wala si wakati onyo limetolewa. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu