Chagua njia ya kupakia

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha YouTube kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki.

Kuna njia nyingi za kupakia maudhui kwenye YouTube. Njia ya kupakia maudhui utakayochagua inapaswa kutegemea aina na ukubwa wa faili unazopakia, pamoja na nyenzo za kiufundi zinazopatikana. Kuchagua kwa usahihi njia ya uingizaji wa data kunaweza kuokoa wakati wako.

Upakiaji wa msingi

Njia rahisi zaidi ya kupakia video na metadata yake ni kupitia ukurasa wa Pakia. Njia hii haijumuishi faili ya metadata; hivyo unahitaji kupakia metadata mwenyewe baada ya kupakia video. Soma makala haya ili upate maelezo zaidi.

Njia hii ya kupakia inawafaa washirika wanaopakia video chache kwa wakati mmoja. Huhitaji utaalamu wowote maalum wa kiufundi, na pia, video huonekana kwenye YouTube unapokamilisha kuzipakia. Kikwazo ni kuwa, huwezi kuchakata maudhui mengi kwa wakati mmoja, na njia hii haijaunganishwa kwenye mfumo wowote wa kudhibiti maudhui. Pia, huwezi kutumia ukurasa wa Pakia kupakia rekodi za sauti, nyimbo au video usizomiliki; unahitaji kutumia mojawapo ya njia za upakiaji wa maudhui mengi kupakia aina hizi za maudhui.

Kupakia maudhui mengi

Ikiwa ungependa kupakia maudhui mengi, utahitaji kuyapakia kwenye YouTube kwa pamoja ukitumia Kipakiaji cha Vifurushi, kinachopatikana sehemu ya Upakiaji Maudhui kwa kubofya kitufe cha "Thibitisha na Upakie". Zana hii hukuwezesha kupakia faili zako za maudhui kwa wakati mmoja (rekodi za sauti na video). Soma makala haya ili upate maelezo zaidi.

Unapopakia maudhui mengi kwa wakati mmoja, unahitaji kuwasilisha metadata ya maudhui yote unazopakia katika faili tofauti. YouTube hutoa violezo vya lahajedwali kwa faili za metadata na faili za maudhui munazopakia kwenye YouTube. Kila safu mlalo katika lahajedwali inawakilisha metadata ya kipengee kimoja. Unaweza kuthibitisha mapema lahajedwali ili kuepuka matatizo wakati wa upakiaji. Unaweza kupakua violezo vya lahajedwali kwenye ukurasa wa Uwasilishaji wa Maudhui katika Kidhibiti Maudhui kwenye kichupo cha Violezo.

Studio za muziki zinazowasilisha Video za Picha zinaweza kutoa metadata ya vipengee vyao kupitia lahajedwali la Video za Picha au ka kutumia muundo wa DDEX unaokubalika.

Upakiaji wa vipengee vingi

Washirika ambao hupakia vipengee vingi mara kwa mara (zaidi ya vipengee 100 kwa mwezi) wanaweza kuhamisha faili zao za maudhui na metadata kwa kutumia Itifaki Salama ya Kutuma Faili (SFTP) au Aspera badala ya Kipakiaji cha vifurushi. Aspera ni ya kasi zaidi kuliko SFTP na ndiyo njia bora ya kupakia faili kubwa za maudhui. Kwa washirika walio na Mtaalamu anayesimamia Teknolojia ya Washirika, YouTube pia inatoa diski inayotumika nje ya mtandao, ambapo unapeleka diski yenye maudhui kwenye kituo cha upakiaji cha Google.

API za YouTube

Ili udhibiti kikamilifu faili unazopakia, unaweza kubainisha njia maalum ya upakiaji kwa kutumia API za YouTube. Kutumia API ya Data ya YouTube na API ya Content ID ya YouTube hukuwezesha kudhibiti masasisho na chaguo mbadala.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5267784599915837037
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false