Iwapo unakumbwa na hitilafu unapocheza video yako ya YouTube, jaribu kufuata hatua hizi za utatuzi ili utatue hitilafu uliyo nayo.
Baadhi ya ujumbe kuhusu hitilafu unaojitokeza mara nyingi ni:
- "Hitilafu imetokea."
- "Hitilafu ya uchezaji. Gusa ili ujaribu tena."
- "Muunganisho wa seva umepotea."
- "Video hii haipatikani."
- "Hitilafu fulani imetokea. Gusa ili ujaribu tena."
- "Unakumbana na matatizo? Fahamu ni kwa nini."
Kutatua hitilafu za video
Ukipata ujumbe kuhusu hitilafu unapotazama video, unaweza kujaribu njia hizi za utatuzi unazoweza kutumia.
Kukagua kasi ya intaneti na matumizi ya data yako
- Zima kisha uwashe muunganisho wako wa intaneti.
- Tekeleza jaribio la kasi ya intaneti ili uhakikishe intaneti yako inaweza kucheza katika ubora wa video uliochagua. Kutumia vifaa vingi katika mtandao mmoja kunaweza kupunguza kasi ambayo kifaa chako kinapata. Unaweza pia kubadilisha ubora wa video yako ili uboreshe hali yako ya utazamaji.
- Kagua ubora wa video ya YouTube na kasi inayopendekezwa, inayohitajika kucheza video. Jedwali lililo hapa chini linaonyesha makadirio ya kasi zinazopendekezwa ili kucheza kila kiwango cha ubora wa video.
|
- Ikiwa ungependa kuona maelezo zaidi kuhusu jinsi video zako zinavyochezwa, angalia Takwimu za Wajuaji.
- Kagua mipangilio ya kifaa chako ili uhakikishe kuwa umewasha matumizi ya data ya YouTube katika kifaa chako.
Hakikisha kuwa umeingia kwenye YouTube.
Ili kulinda jumuiya ya YouTube, tunaweza kuzuia watumiaji walioondoka kwenye akaunti kufikia video za YouTube wanapojaribu kupakua maudhui kwa matumizi ya nje ya mtandao.
Iwapo wewe ni mtafiti unayejaribu kufikia data ya YouTube ili uitumie katika utafiti wako wa kitaaluma, unaweza kutuma ombi la kufikia kwenda kwenye mpango wa watafiti wa YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu mchakato na data inayopatikana.
Kufungua upya programu ya YouTube au kuwasha kifaa chako tena
Jaribu kufunga programu ya YouTube au kuwasha tena kifaa chako. Unaweza pia kuondoa kisha uweke upya programu ya YouTube kwenye kifaa.
Kusasisha kivinjari chako
Jaribu kusasisha kivinjari chako au ufute vidakuzi na akiba ya kivinjari chako.
Kusasisha programu ya YouTube
Kutatua hitilafu nyingine
Unaweza kufuata hatua zilizopendekezwa za utatuzi ili kurekebisha hitilafu nyingine zinazojitokeza mara kwa mara.
“Hitilafu fulani imetokea. “Hitilafu fulani imetokea. Onyesha upya au ujaribu tena baadaye.”- Ingia katika YouTube. Huenda baadhi ya vipengee visifanye kazi vizuri ikiwa hujaingia katika akaunti.
- Hakikisha kuwa unatumia toleo jipya kabisa la kivinjari kinachooana, kama vile Google Chrome, Firefox au Safari.
- Ruhusu matangazo kwenye YouTube kisha uzime vizuia matangazo. Ili utazame bila matangazo, YouTube Premium hukuruhusu ufurahie video bila kukatizwa huku ukiwasaidia watayarishi.
- Futa akiba na vidakuzi vya kivinjari chako.
- Thibitisha kuwa unatumia seva za DNS unazopendelea na kuwa hakuna programu za wengine zilizozirekebisha. Nenda kwenye mapendeleo au mipangilio yako ya mtandao ili uangalie mipangilio yako ya DNS.
- Zima kisha uwashe kifaa chako. Baada ya kifaa kuzima kisha kuwaka, rudi kwenye programu ya YouTube kisha ujaribu kucheza tena video yako.
Matatizo ya sauti
Iwapo husikii sauti kwenye video ya YouTube, jaribu:
- Kuhakikisha kwamba umewasha kitufe cha sauti au kiwango cha sauti katika kivinjari au kifaa chako.
- Kagua mipangilio ya sauti ya kifaa chako.
- Kuzima kisha uwashe kifaa au kufungua upya kivinjari chako.