Kuanzisha mtiririko mubashara kwenye YouTube kupitia programu ya kusimba

Kuna njia tatu za kutiririsha kwenye YouTube: kutumia kamera ya wavuti, kifaa chako cha mkononi, au programu ya kusimba (programu ya kutiririsha au programu ya kusimba ya maunzi). Kutumia programu ya kusimba kunakuruhusu:

  • Ushiriki skrini na kupeperusha uchezaji wako
  • Utumie maunzi ya nje ya sauti na video
  • Udhibiti utayarishaji wa kina (kama vile kamera na maikrofoni kadhaa)

Hatua zilizo hapa chini zitakusaidia uanzishe mtiririko wako wa kwanza mubashara.

1. Kuwezesha utiririshaji mubashara

Kuwezesha mtiririko mubashara kwa mara ya kwanza kunaweza kuchukua hadi saa 24. Ukishawezesha, mtiririko wako unaweza kutiririsha mubashara papo hapo. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuanzisha mtiririko mubashara.

2. Kusakinisha programu ya kusimba

Programu ya kusimba hugeuza video yako iwe katika muundo dijitali ili utiririshe kwenye YouTube. Baadhi ya programu za kusimba ni programu zinazopatikana kwenye kompyuta yako na nyingine ni maunzi huru.

Tazama video hii ili upate maelezo zaidi kuhusu ni kwa nini unapaswa kutumia programu ya kusimba na jinsi inavyofanya kazi.

Kutiririsha Mubashara kwenye Programu ya Kusimba: Mambo ya Msingi kuhusu Jinsi ya Kuweka Mipangilio na Kutumia Programu ya Kusimba

Programu za kusimba zilizothibitishwa kwa ajili ya YouTube Moja kwa Moja

Ifuatayo ni orodha ya programu za kusimba zilizothibitishwa kwa ajili ya YouTube Moja kwa Moja. Hamna bidhaa zozote kati ya hizi zilizobuniwa na YouTube. Hakikisha unatathmini bidhaa na kuamua chaguo linalokufaa wewe au biashara yako.

Programu za kusimba

AWS Elemental MediaLive

AWS Elemental MediaLive ni huduma ya kuchakata video ya moja kwa moja katika kiwango cha kupeperusha, inayoruhusu utiririshaji mubashara wa ubora wa hadi 4Kp60 HEVC.

Cinamaker Director Studio

(Mac na iOS)

Programu inayojumuisha kwa pamoja kurekodi video kwa kamera nyingi, kubadilisha na kutiririsha mubashara. Jumuisha hadi iPhone 8 za ndani, kamera za dijitali na wageni wa mbali kupitia Kuvuta karibu kwa ubora wa HD. Weka matangazo yaliyowekelewa juu, picha, sauti, video, skrini na madoido ya video. Tiririsha kwenye YouTube, Zoom, RTMP. Okoa muda wa kuunda maktaba yako ya video kwa kutumia Kihariri cha Ndani ya Programu.

 

Elgato Game Capture Software
Windows, Mac

Rekodi na utiririshe uchezaji wako kwenye Xbox, PlayStation au Wii U.

 

Gamecaster
Windows (toleo lisilolipishwa linapatikana!)

Njia rahisi zaidi ya kutiririsha na kurekodi matukio yako bora zaidi ya michezo kwa kubofya kitufe tu. Inafaa zaidi kwa kushiriki uchezaji wako.

 

Streamlabs Talk Studio

Programu bora zaidi ya kutiririsha mubashara katika ubora wa kitaalamu kwenye kivinjari chako. Waalike wageni kwa urahisi. Ina vipengele, chaguo nyingi za kuweka mapendeleo, michango na haihitaji kupakuliwa.

Open Broadcaster Software

Programu huria ya kurekodi video na kutiririsha mubashara bila malipo.

PRISM Live Studio

Windows

PRISM Live Studio ni programu ya kutiririsha ya Windows ambayo inatambulika kwa kiolesura chake rahisi na urahisi wa kutumia. Watiririshaji wa moja kwa moja wanapenda programu hii kwa sababu ya ubora wake thabiti wa utiririshaji na vipengele vinavyovutia kama vile madoido ya urembo na vibandiko, mchoro, mandharinyuma pepe, kamera pepe na ujumuishaji na programu za vifaa vya mkononi za PRISM. Vipengele vyote havilipishwi.

 

Restream

Studio maarufu ya kupeperusha mtiririko mubashara kwa watayarishi na biashara. Tiririsha mubashara katika zaidi ya mifumo 30 kwa wakati mmoja kutoka kwenye studio yetu ya wingu. Waalike wageni, ongeza vipengele vya kuwekelea, cheza video na uimarishe mtiririko wako – hailipishwi na ni rahisi kutumia.

 

Stage TEN

Tayarisha na usambaze kwa urahisi mitiririko bora mubashara. Unaweza kuwaalika wageni kutoka kokote, kuburuta na kudondosha maudhui na picha, kuongeza biashara mubashara kwenye mitiririko yako, kuwasiliana na hadhira na kuchuma mapato.

 

Streamlabs
Windows, iOS, Android

Streamlabs ni programu maarufu ya kupeperusha ya wanaotiririsha moja kwa moja. Hailipishwi, ni programu huria na ina vipengele thabiti vya kukusaidia kukua, kufahamu na kuchuma mapato.

 

Wirecast
Windows, Mac

Ni programu rahisi kutumia na iliyotuzwa ya utayarishaji na utiririshaji mubashara. Weka kamera, picha za skrini za moja kwa moja, mada, picha na zaidi kwa kubofya tu kitufe. Tiririsha moja kwa moja kwenye YouTube au sehemu yoyote ya RTMP. Hufanya kazi na API ya YouTube ili uweze kudhibiti, kubuni na kuratibu au kutiririsha kituo chako mubashara bila kuondoka kwenye programu.

 

XSplit Broadcaster
Windows (toleo lisilolipishwa linapatikana!)

Programu ya kubuni mseto wa sauti au video inayokuruhusu ubuni matangazo ya kitaalamu ya moja kwa moja na rekodi za video.

 

StreamYard

StreamYard ndio studio maarufu sana ya podikasti na kutiririsha mubashara ulimwenguni. Hoji wageni, angazia magumzo ya moja kwa moja kwenye skrini, weka upekee katika matangazo yako na zaidi. Vyote kwenye kivinjari chako, huhitaji kupakua. Anza kutumia bila malipo!

 

Nimble Streamer

Nimble Streamer ni programu ya seva ya maudhui ya kuunda mitandao yenye gharama nafuu ya kutiririsha na kuwasilisha maudhui. Uwezo wa mtandao ni pamoja na RTMP, SRT, NDI, Dante, WebRTC, Icecast, HLS, DASH na mengine mengi ikiwemo programu jalizi ya Transcoder ya kubadilisha maudhui. Uchezaji, uwekaji wa matangazo, ulingo wa malipo na vipengele vingine huruhusu uchumaji wa mapato kwenye maudhui kwa urahisi.

Programu za kusimba za maunzi

AirServer
Windows, Mac

Akisi kompyuta au kifaa chako cha mkononi kwenye YouTube.

 

AWS Elemental Live

AWS Elemental Live ni programu ya kusimba video katika eneo ambayo huchakata video ya moja kwa moja kwa ajili ya kupeperushwa na kutiririshwa kwenye kifaa chochote.

 

 

Elgato

Elgato ni chapa inayoongoza duniani inayotoa teknolojia ya sauti na picha kwa watayarishi wa maudhui, kwenye mifumo yote ya kushiriki video na ni chapa iliyounda Stream Deck, kidhibiti cha usb kinachoweza kuratibiwa ambacho kina zaidi ya programu jalizi 200 unazoweza kusakinisha au kupanga mikato ya kibodi kwenye vitufe kwa utayarishaji wa mtiririko wako mubashara.

 

 

Epiphan Pearl 2

Pearl-2 ni programu ya kubadilisha, kurekodi, kutiririsha, kugawanya na kukadiria video, yote kwa pamoja. Programu hii ina vipengele sita vya video na nne vya sauti ya kitaalamu ya XLR, hurekodi na kutiririsha katika ubora wa 4K, hutumia NDI, ina huduma ya funguo za chroma na zaidi. Pearl-2 ina vipengele vya kitaalamu na uwezo wa kuchakata unaohitajika katika mitiririko mubashara inayoshirikisha zaidi.

 

Direkt Link

Intinor hutengeneza bidhaa za kutuma video zenye ubora wa juu kwenye intaneti. Bidhaa zetu ni rahisi kutumia, kubeba, imara na za uhakika. Inatumiwa na mashirika ya utangazaji na ndiyo programu ya kusimba inayoaminika na inayopendelewa zaidi kwa matukio makubwa ya michezo kwenye intaneti. Imesanidiwa nchini Sweden.

 

LiveU Solo

Ni programu bora zaidi ya kusimba video ya kuweka na kucheza, inayotoa utiririshaji mubashara kwa kugusa mara moja, kupitia kamera/swicha kwenye YouTube na sehemu nyingine za mtandaoni. Tiririsha kwa uhakika ukiwa popote kwa kutumia teknolojioa bora ya kuunganisha ya LRT™ inayotumiwa na watangazaji maarufu.

 

Nvidia

GPU za NVIDIA zina programu ya kusimba iliyojumuishwa kwenye maunzi (NVENC) ambayo huwa na programu ya kusimba video iliyo katika maunzi yenye vipengele vingi vya kasi, inayoruhusu utiririshaji mubashara wa ubora wa juu na utendaji bora wa mchezo bila kuhitaji kutumia CPU yako.

 

 

SlingStudio

Mfumo wa kwanza unaoweza kubebwa wa upeperushaji wenye kamera nyingi za kielektroniki. Kufuatilia, kurekodi, kubadilisha, kuhariri na kutiririsha mubashara video yenye ubora wa HD kielektroniki kwenye YouTube.

 

 

Teradek VidiU Go

Tiririsha katika ubora wa kupeperusha popote uliko kwenye kamera yoyote, swicha au chanzo cha video. Vidiu Go ni ndogo na inaweza kubebwa; inaruhusu ubora kamili wa 1080p60 SDI na utaratibu wa HDMI kwa mtumiaji mwenye ari zaidi.

 

 

Blackmagic Web Presenter 4K

Suluhisho bora la utiririshaji wa HD na Ubora wa Juu Zaidi wa HD linalojumuisha mtambo wa kitaalamu wa utiririshaji wa maunzi wa kutiririsha maudhui yenye ubora wa hadi 2160p60 moja kwa moja kwenye YouTube.

 

Programu za kusimba za vifaa vya mkononi


AirServer
Windows, Mac

Akisi kifaa chako cha mkononi kwenye YouTube.

PRISM Live Studio

iOS, Android

PRISM Live Studio ni mojawapo ya programu maarufu zaidi za vifaa vya mkononi iliyoboreshwa kwa ajili ya utiririshaji wa michezo ya video na IRL. Inapendwa na watiririshaji wa moja kwa moja kwa sababu ya ubora wake thabiti wa utiririshaji na vipengele vinavyovutia kama vile madoido ya urembo na mapambo, kuwekelea chanzo na ufunguo wa chroma. Vipengele vyote havilipishwi.

 

Streamlabs
Windows, iOS, Android

Imejengwa kwenye CBS na hujumuisha arifa za Streamlabs, njia za mkato, vidokezo na barakoa na maelfu ya mandhari na vipengele vya kuwekelea juu bila malipo.

 

 

Wirecast Go
iOS

Hailipishwi inapopakuliwa kwenye iOS App Store. Tayarisha kwa urahisi matangazo ya moja kwa moja ya kitaalamu kwenye iPhone yako na uyatiririshe kwenye YouTube. Badilisha picha, ongeza picha na zaidi kwa hadi safu tatu kwa wakati mmoja kwa ajili ya matokeo bora kwenye vifaa vya mkononi. Soma maoni kwenye YouTube na gumzo katika muda halisi na uwasiliane na hadhira yako. Ratibu, buni na udhibiti mitiririko yako mubashara kwenye YouTube moja kwa moja ndani ya programu. Tumia toleo linalolipishwa ili utiririshe kwenye sehemu yoyote ya RTMP.

 

 

Larix Broadcaster

iOS, Android

Larix Broadcaster ni programu ya vifaa vya mkononi kwa iOS na Android inayotumika katika kunasa na kutiririsha moja kwa moja kupitia itifaki kama vile SRT, RTMP, NDI, WebRTC, Zixi na zaidi. Watumiaji wanaweza kutumia uwezo kamili wa kamera zao za vifaa vya mkononi ili kuchangia maudhui yaliyowekelewa maandishi na tovuti, michoro, utumiaji nyumbufu wa kamera, mipangilio ya kina ya sauti na mbinu nyingine za kuboresha ili kufanya mitiririko yako ya wakati halisi ya aina yoyote.

3. Unganisha maunzi yako

Iwapo unatumia maunzi, kama vile kamera ya wavuti, maikrofoni au kifaa cha sauti, yaunganishe na uhakikishe kuwa yamewekewa mipangilio pamoja na programu yako ya kusimba.

Kulingana na mtiririko wako, unaweza kutumia maunzi tofauti. Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya kawaida:

Mitiririko mubashara ya kawaida na ya michezo ya video
Watu wengi wanaotiririsha moja kwa moja hutumia vifaa vya nje vya maikrofoni, kamera ya wavuti na vipokea sauti vya kichwani. Wachezaji wanaweza pia kutumia zana nyingine kama vile skrini ya kijani.

Improper encoder setup can cause technical issues with your hardware while streaming.

Mitiririko mubashara ya kitaalamu
Mipangilio ya kina ya mtiririko inaweza kujumuisha zaidi ya kifaa kimoja cha maikrofoni, kamera, kichanganyaji na maunzi ya programu ya kusimba.

4. Kuunganisha programu yako ya kusimba na kutiririsha mubashara

Ili uanze kutiririsha, weka URL yako ya seva ya YouTube Moja kwa Moja na ufunguo wa mtiririko katika programu yako ya kusimba. Iwapo una maunzi ya sauti na video, weka mipangilio yake pamoja na programu yako ya kusimba, inayofahamika kama programu ya kutiririsha.

Tunakuletea Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja - kwa Kutiririsha Mubashara

Anza kutiririsha mubashara sasa

Kwanza, anzisha mtiririko

  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye upande wa juu kulia, bofya ANZISHA kisha Tiririsha Mubashara ili ufungue Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja.
  3. Bofya kichupo cha Tiririsha.
  4. Iwapo ni mtiririko wako wa kwanza mubashara: Badilisha mtiririko wako kisha uchague Buni mtiririko.
    Iwapo umewahi kutiririsha mubashara: Mipangilio ya mtiririko wako wa awali itapakia, ikiwa ni pamoja na ufunguo wako wa mtiririko, hali inayomaanisha kuwa hutahitaji kusasisha programu yako ya kusimba.
    • For users aged 13–17 on YouTube, your default privacy setting is set to private. If you’re 18 or over, your default privacy setting is set to public. All streamers can change this setting to make their live stream public, private, or unlisted.
  5. Iwapo uko katika Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kuchuma mapato kwenye mtiririko wako mubashara. Pata maelezo zaidi.

Kisha, unganisha mtiririko wako kwenye programu yako ya kusimba halafu utiririshe mubashara

  1. Katika mipangilio ya mtiririko ya programu yako ya kusimba, ukiona chaguo la kutiririsha kwenye YouTube, lichague. Vinginevyo nakili URL ya mtiririko kutoka YouTube na uibandike kwenye seva ya mpangilio ya Mtiririko kwenye programu yako ya kusimba. Inaweza kusema seva ya RTMP.
  2. Nakili ufunguo wa mtiririko kwenye YouTube na uubandike kwenye mipangilio ya Kutiririsha ya programu yako ya kusimba ambapo inasema Ufunguo wa Mtiririko.
  3. Weka mipangilio ya programu ya kusimba, kisha uanze kutiririsha kupitia programu yako ya kusimba. Ukurasa wa kutazama sasa umebuniwa kwa mtiririko wako na sasa unatiririsha mubashara kwenye YouTube. Arifa zitatumwa na mtiririko wako utaonekana katika mipasho ya wanaofuatilia.
  4. Ili ukamilishe mtiririko, acha kutuma maudhui kwenye programu yako ya kusimba. Mitiririko yote iliyo na urefu wa chini ya saa 12 itawekwa kiotomatiki kwenye kumbukumbu. Unaweza kupata mitiririko ya awali, ya sasa na ijayo katika Kichupo cha Mubashara kwenye dashibodi ya Studio ya YouTube. Pata maelezo zaidi.

Kuratibu mtiririko mubashara

Kuratibu mtiririko kunakuruhusu utangaze mtiririko wako. Watazamaji wanaweza kupata vikumbusho kuhusu mitiririko ijayo, unaweza kushiriki URL kwenye mtandao jamii na zaidi.

Ratibu mtiririko

  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye upande wa juu kulia, bofya ANZISHA kisha Tiririsha Mubashara ili ufungue Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja.
  3. Bofya kichupo cha Dhibiti.
  4. Bofya Ratibu mtiririko.
  5. Unaweza kutumia tena mipangilio ya mtiririko wa awali na ubofye Tumia mipangilio tena au unaweza kuanzisha mtiririko kwa kubofya Anzisha mpya.
    • For users aged 13–17 on YouTube, your default privacy setting is set to private. If you’re 18 or over, your default privacy setting is set to public. All streamers can change this setting to make their live stream public, private, or unlisted.
  6. Iwapo uko katika Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kuchuma mapato kwenye mtiririko wako mubashara. Pata maelezo zaidi.

Kidokezo: Furahisha hadhira yako kwa kuionyesha kionjo cha mtiririko mubashara ulioratibu. Pata maelezo zaidi.

Ukifika wakati wa kuanza mtiririko wako...

Unganisha mtiririko wako kwenye programu ya kusimba, kisha utiririshe mubashara.

  1. Katika mipangilio ya mtiririko ya programu yako ya kusimba, ukiona chaguo la kutiririsha kwenye YouTube, lichague. Vinginevyo, nakili URL ya mtiririko kutoka YouTube na uibandike katika seva ya mipangilio ya Mtiririko kwenye programu yako ya kusimba. Inaweza kusema seva ya RTMP.
  2. Nakili ufunguo wa mtiririko kwenye YouTube na uubandike kwenye mipangilio ya Kutiririsha ya programu yako ya kusimba ambapo inasema Ufunguo wa Mtiririko.
  3. Weka mipangilio ya programu ya kusimba, kisha uanze kutiririsha.
  4. Katika Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja, subiri onyesho la kukagua mtiririko uonekane, kisha ubofye Tiririsha mubashara.
  5. Ili ukamilishe kutiririsha, bofya Kamilisha Mtiririko na uache kutuma maudhui kwenye programu ya kusimba. Mitiririko yote iliyo na urefu wa chini ya saa 12 itawekwa kiotomatiki kwenye kumbukumbu. Unaweza kufikia mitiririko ya awali, ya sasa na ijayo katika Kichupo cha Moja kwa Moja kwenye dashibodi ya Studio ya YouTube. Pata maelezo zaidi

Kutumia Paneli Dhibiti ya Mubashara

Unapotiririsha mubashara, unaweza kutumia toleo dogo la Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja (Paneli Dhibiti ya Mubashara) ili upunguze eneo la skrini unalohitaji katika mtiririko wako. Paneli Dhibiti ya Mubashara hukuonyesha taarifa muhimu kutoka kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja, kama vile mapato ya Gumzo na Utazamaji, katika eneo dogo zaidi la skrini

Ili ufungue Paneli Dhibiti ya Mubashara:

  1. Katika Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja, nenda kwenye dashibodi ya mtiririko.
  2. Katika kona ya chini kushoto, bofya dashibodi Ibukizi Pop out .

Ili ufunge Paneli Dhibiti ya Mubashara, ondoka kwenye dirisha.

Kumbuka: Unaweza kutumia kipengele cha Paneli Dhibiti ya Mubashara unapotiririsha mubashara ukitumia programu ya kusimba au kamera ya wavuti pekee.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4942752495429265079
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false