Iwapo maudhui yako yaliondolewa kutokana na ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki na unaamini kuwa hali hii imefanywa kimakosa au video imetambulishwa kimakosa, unaweza kutuma arifa ya kukanusha. Hili ni ombi la kisheria kwa YouTube ili irejeshe maudhui yaliyoondolewa kutokana na ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.
Kumbuka:
- Tuma tu arifa ya kukanusha iwapo maudhui yako yaliondolewa kimakosa au kwa kutambulishwa kimakosa. Hii ni pamoja na hali zisizofuata kanuni za hakimiliki, kama vile hali za matumizi ya haki au matumizi yasiyo ya biashara.
- Iwapo maudhui yako hayatimizi masharti yaliyo hapa juu, unaweza kusubiri kwa siku 90 ili muda wa onyo la hakimiliki uishe. Unaweza pia kujaribu kuwasiliana na mlalamikaji moja kwa moja ili umwombe afute dai.
Kutathmini maudhui
Ili ukague maudhui yaliyoondolewa kutokana na ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki:
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
- Bofya upau wa kichujio Hakimiliki.
- Tafuta video husika.
- Katika safu wima ya Vizuizi, wekelea kiashiria juu ya Hakimiliki.
- Iwapo maandishi yaliyowekelewa kiashiria yanasema Hakimiliki – Ondoa inamaanisha kuwa video imeathiriwa na ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, hatua inayofahamika pia kama "uondoaji".
- Bofya ANGALIA MAELEZO.
- Kagua ukurasa wa Maelezo ya hakimiliki ya video, unaoonyesha maelezo zaidi kuhusu maudhui yaliyotambuliwa katika ombi la uondoaji.
- Ikiwa video zingine ziliondolewa na zinatokana na onyo sawa la hakimiliki, hakikisha unakagua ukurasa wa Maelezo ya hakimiliki ya video wa video zingine pia. Ikiwa unaamini kuwa video nyingi ziliondolewa kimakosa, unaweza kutuma arifa moja ya kukanusha kwa video zote.
- Zingatia yafuatayo kabla ya kutuma arifa ya kukanusha:
- Umiliki: Je, unamiliki maudhui hayo na una haki zake zote?
- Ushahidi: Iwapo umetumia kazi za mtu mwingine ambazo zina hakimiliki, una ushahidi wa leseni au ruhusa ya kutumia maudhui hayo?
- Hali zisizofuata kanuni za hakimiliki: Je, utumiaji wako unalindwa na matumizi ya haki au hali kama hiyo isiyofuata kanuni ya hakimiliki?
- Wazi kutumiwa na umma: Je, maudhui hayo ni wazi kutumiwa na umma?
Iwapo hamna hali hapo juu inayotumika kwenye maudhui yako, unaweza kusubiri kwa siku 90 ili muda wa onyo la hakimiliki uishe. Unaweza pia kujaribu kuwasiliana na mlalamikaji moja kwa moja ili umwombe afute dai.
Kutuma arifa ya kukanusha
Ili utume arifa ya kukanusha katika Studio ya YouTube:
- Fuata hatua zilizo hapa juu ili upate video iliyoondolewa katika Studio ya YouTube.
- Chini ya Maudhui yaliyotambuliwa katika video hii, bofya CHAGUA VITENDO Tuma arifa ya kukanusha.
- Soma masharti ya arifa ya kukanusha na uteue visanduku ili uthibitishe ENDELEA.
- Weka maelezo yako ya mawasiliano ENDELEA.
- Hakikisha kuwa unajumuisha anwani yako kamili ya mahali halisi na jina lako rasmi kamili (kwa kawaida huwa jina la kwanza na la mwisho). Usiweke jina la kampuni au la chaneli.
- Weka sababu yako. Kwa kifupi na kwa njia dhahiri, fafanua ni kwa nini unaamini kuwa uondoaji wa maudhui yako ulifanywa kimakosa au video ilitambulishwa kimakosa.
- Kagua kauli kisha uteue visanduku ili ukubali.
- Weka jina lako rasmi kamili liwe saini yako ENDELEA.
- (Si lazima) Iwapo video zingine ziliondolewa kutokana na ombi sawa la kuondoa video na pia unaamini kuwa ziliondolewa kimakosa, unaweza kuchagua video hizi na kuzijumuisha zote katika arifa ya kukanusha.
- Bofya TUMA.
Kinachotokea baada ya kutuma arifa ya kukanusha
Baada ya kutuma arifa ya kukanusha, arifa hiyo husambazwa kwa mlalamishi iwapo inatimiza masharti yote, ikiwa ni pamoja na ufafanuzi dhahiri kuhusu kwa nini unaamini kuwa maudhui yako yalitambulishwa au kuondolewa kimakosa. Arifa za kukanusha ambazo hazitimizi masharti yote zinaweza kukataliwa.
Mlalamishi hupewa siku 10 za kazi Marekani, kwa mujibu wa sheria ya hakimiliki, ilikujibu arifa ya kukanusha. Lazima ajibu kwa kutoa ushahidi wa hatua ya kisheria iliyochukuliwa ili kuzuia maudhui yako yasirejeshwe kwenye YouTube.
Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQ)
Ili uangalie hali ya arifa ya kukanusha uliyotuma:
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Katika menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
- Bofya upau wa kichujio Hakimiliki.
- Tafuta video husika.
- Katika safu wima ya Vizuizi, wekelea kiashiria juu ya Hakimiliki.
- Bofya ANGALIA MAELEZO.
- Angalia chini ya sehemu ya Maudhui yaliyotambuliwa katika video hii ili uone hali ya arifa ya kukanusha.
Arifa za kukanusha za maudhui yasiyo ya video, kama vile maoni au picha za mabango ya chaneli, lazima zitumwe kupitia barua pepe, faksi au posta.
Kumbuka: Kwa sababu picha za wasifu wa chaneli hupangishwa kwenye Google, arifa za kukanusha zinazohusiana na picha za wasifu wa chaneli lazima zitumwe kupitia fomu ya wavuti ya Google.