Vidokezo na zana za wazazi wa vijana kwenye YouTube

Tunaelewa kuwa wakati mwingine wazazi na walezi huwa na maswali kuhusu tabia na maslahi ya vijana wao mtandaoni. Tumeweka pamoja zana na nyenzo fulani ili kukusaidia kudhibiti hali yao ya utumiaji kwenye YouTube.

Kijana wangu anaweza kutumia YouTube akiwa na umri gani?

Ili kuingia katika akaunti ya YouTube, lazima kijana wako awe na Akaunti ya Google inayotimiza masharti ya umri wa chini zaidi katika nchi au eneo unakoishi. 

Ikiwa mtoto wako hajafikisha umri unaohitajika, pata maelezo zaidi kuhusu hali za utumiaji anazoweza kufikia katika Kituo chetu cha Usaidizi cha YouTube kwa Ajili ya Familia.

Vidokezo na ushauri kuhusu kutayarisha maudhui kwenye mtandao

Ikiwa kijana wako angependa kutayarisha maudhui kwenye YouTube, tunapendekeza:

Zana za faragha na usalama

Kulinda maslahi

  • Vikumbusho vya kupumzika kidogo: Kipengele hiki huwashwa kiotomatiki kwa vijana na huwakumbusha wapumzike kidogo wakati wanatazama video au Video Fupi za YouTube. 
  • Vikumbusho vya wakati wa kulala:  Kipengele hiki huwashwa kiotomatiki kwa vijana na huonekana ufikapo wakati wa kuacha kutazama YouTube na kwenda kulala. 
  • Kipengele cha kucheza kiotomatiki kimezimwa: Kipengele hiki kimezimwa kiotomatiki kwa vijana. Kikiwa kimezimwa, video ambazo kijana wako anatazama hazitachezwa kwa mfululizo na atalazimika kuchagua video inayofuata anayotaka kutazama. 
  • Mapendekezo ya video kwa uwajibikaji: YouTube ina mfumo wa kupendekeza video ambao hutoa mapendekezo ya kuwajibika zaidi kwa vijana. Mfumo huu hupunguza kiotomatiki uonyeshaji wa maudhui ambayo yanaweza kuathiri vibaya tabia za vijana au jinsi wanavyojitambua. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyopendekeza maudhui ili kukidhi mahitaji maalum ya vijana.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13774783170908852011
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false