Maudhui yenye mipaka ya umri

Wakati mwingine maudhui hayakiuki Mwongozo wa Jumuiya yetu, lakini huenda yasioane na Sheria na Masharti ya YouTube au yasifae kwa watazamaji walio na umri wa chini ya miaka 18. Katika hali hizi, tunaweza kuweka mipaka ya umri kwenye video. Sera hii hutumika kwenye video, maelezo ya video, vijipicha maalum, mitiririko mubashara na bidhaa au kipengele chochote cha YouTube.

Pata maelezo zaidi kuhusu mipaka ya umri

Hapa chini kuna maelezo zaidi kuhusu aina za maudhui tunayoyazingatia kwenye mipaka ya umri. Ikiwa maudhui yako yanajumuisha majawapo ya mada hizi, tunaweza kuweka mipaka ya umri. Tumetoa mifano ya maudhui ambayo yanaweza kuwekewa mipaka ya umri hapa chini. Bofya sehemu za sera ili uone mifano inayoonyesha mada hizi. Kumbuka hii si orodha kamili.

Usalama wa watoto

  • Video iliyo na watu wazima wanaoshiriki katika shughuli hatarishi ambazo watoto wanaweza kuiga kwa urahisi, kama vile ushughulikiaji wa vilipuzi au mashindano yanayosababisha majeraha ya mwili
  • Video inayolenga hadhira ya watu wazima lakini inaweza kudhaniwa kwa urahisi kuwa maudhui ya familia
Kumbuka: Mipangilio yako ya "inalenga watoto" haitaathiri mipaka ya umri kwenye video zako.

Shughuli hatari au hatarishi, ikiwa ni pamoja na vitu na dawa zilizodhibitiwa

  • Video kuhusu mizaha bandia hatarishi inayoonekana kuwa ya kweli kiasi kwamba watazamaji hawawezi kutofautisha
  • Video inayotangaza kituo cha kuuza bangi

Maudhui ya uchi na yanayochochea ngono

  • Video inayohimiza vitendo vya ngono, kama vile densi zinazochochea ngono au kupapasana
  • Video ambayo mhusika amekaa katika mkao unaokusudia kuamsha hisia za kingono kwa mtazamaji
  • Video ambayo mhusika amevaa mavazi yasiyokubalika katika miktadha ya umma, kama vile nguo za ndani za kike

Maudhui ya kuogofya au yenye vurugu

  • Video yenye muktadha unaoonyesha majeraha ya walionusurika katika ajali kubwa ya barabarani
  • Video inayoonyesha picha zenye vurugu au zinazotisha kama vile kuangazia tu sehemu zinazoogofya zaidi za filamu au mchezo wa video

Lugha chafu

  • Video iliyotumia lugha chafu sana katika jina, kijipicha au metadata inayohusiana nayo
  • Video inayoangazia matumizi ya lugha chafu kama vile mkusanyiko au klipu zilizorekodiwa nje ya muktadha

Itakuwaje iwapo maudhui yana mipaka ya umri?

Video zilizo na mipaka ya umri haziwezi kutazamwa na watumiaji walio na umri wa chini ya miaka 18 au ambao hawajaingia kwenye akaunti. Pia, video zilizo na mipaka ya umri haziwezi kutazamwa kupitia tovuti nyingi za wahusika wengine. Watazamaji wanaobofya video iliyo na mipaka ya umri kwenye tovuti nyingine, kama vile kichezaji kilichopachikwa, wataelekezwa kwenda YouTube au YouTube Music. Wakiwa huko, wanaweza tu kutazama maudhui wanapoingia katika akaunti na ikiwa wana umri wa zaidi ya miaka 18. Mchakato huu husaidia kuhakikisha kuwa haijalishi ni wapi maudhui yamegunduliwa, iwapo video imepakiwa na YouTube itaweza tu kutazamwa na hadhira inayofaa.

Ikiwa unaamini tumekosea, unaweza kukata rufaa ya mipaka ya umri.

Uchumaji wa mapato na mipaka ya umri

Iwapo chaneli yako inatimiza masharti ya matangazo, hakikisha unakagua mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji. Video zilizo na mipaka ya umri zinaweza kutumia matangazo ili kuchuma mapato. Baadhi ya watangazaji wanapendelea kutangaza katika maudhui yanayofaa familia au maudhui yasiyo na mada zilizobainishwa hapo juu. Katika hali hii, video yako inaweza kuwa na matangazo machache au isiwe na matangazo kabisa ya kuchuma mapato.

Wakati mwingine maudhui hayakiuki Mwongozo wa Jumuiya yetu, lakini huenda yasioane na Sheria na Masharti ya YouTube au yasifae kwa watazamaji walio na umri wa chini ya miaka 18.

Kuangalia iwapo maudhui yako yana mipaka ya umri

Unaweza kuangalia iwapo maudhui yako yana mipaka ya umri kwa kwenda kwenye Studio ya YouTube na kutumia kichujio cha ‘Mipaka ya Umri’ au kwa kutafuta “Mipaka ya Umri” katika safu wima ya Vizuizi katika Ukurasa wako wa video. Mifumo yetu inasasishwa mara kwa mara na iwapo tutapata tofauti yoyote katika ukadiriaji wako, kuna uwezekano kuwa itabadilika.

Watazamaji walio na umri zaidi ya miaka 18 na wameingia katika akaunti wanaweza kujua ikiwa video ina mipaka ya umri kwa kuangalia chini ya maelezo. Pata maelezo zaidi kuhusu kutazama video zilizo na mipaka ya umri.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12998724626989836833
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false