Sera kuhusu uigaji

Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.

Maudhui yanayokusudia kuiga mtu au chaneli hayaruhusiwi kwenye YouTube. YouTube pia hutekeleza haki za mwenye chapa ya biashara. Chaneli au maudhui katika chaneli yanaposababisha mkanganyiko kuhusu chanzo cha bidhaa na huduma zinazotangazwa, huenda yasiruhusiwe.

Ukiona maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti.

  • Ikiwa unashuku kuwa chaneli yako au ya mtayarishi mwingine inaigwa, unaweza kuripoti chaneli.

Jinsi sera hizi zinavyohusiana na matumizi yako

Unapochapisha maudhui kwenye YouTube

Usichapishe maudhui kwenye YouTube ikiwa yanalingana na maelezo yoyote yaliyo hapa chini. 

  • Uigaji wa chaneli: Chaneli inayonakili wasifu, mandharinyuma au mwonekano wa jumla wa chaneli ingine kwa njia inayofanya ionekane kama chaneli ya mtu mwingine. Si lazima chaneli ifanane kabisa na ingine, mradi tu nia ya kuiga ni dhahiri.
  • Kuiga mtu mwingine: Maudhui yanayokusudia kufanya ionekane kana kwamba ni mtu mwingine anayachapisha.

Ikiwa unaendesha chaneli ya mashabiki, hakikisha umeweka hilo wazi kwenye jina au utambulisho wa chaneli yako. Inafaa ieleweke kwa watazamaji wako kwamba chaneli yako haiwakilishi mtayarishi, msanii au huluki halisi ambayo chaneli yako inaenzi.

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui yasiyoruhusiwa kwenye YouTube.

  • Chaneli zilizo na utambulisho (jina au utambuisho wa chaneli) na picha zinazofanana na za chaneli nyingine, ambapo tofauti pekee ni nafasi iliyowekwa katikati ya jina au namba sifuri iliyotumika badala ya herufi O.
  • Kutumia jina halisi la mtu mwingine, jina la mtumiaji, picha, chapa, nembo, au taarifa zingine binafsi kuwahadaa watu kuamini kuwa wewe ni mtu huyo. 
  • Kuanzisha chaneli ukitumia kitambulishi (jina au utambulisho wa chaneli) na picha zinazofanana na za mtu mwingine kisha kudai kwamba mtu huyo anachapisha maudhui kwenye chaneli hiyo.
  • Kuanzisha chaneli ukitumia jina na picha ya mtu fulani, kisha kutuma maoni kwenye chaneli zingine kana kwamba yamechapishwa na mtu huyo.
  • Chaneli zinazodai kuwa 'akaunti ya mashabiki' kwenye maelezo ya chaneli, lakini hayo hayajawekwa wazi kwenye jina au utambulisho wa chaneli, au inayodai kuwa chaneli ya mtu mwingine na kupakia upya maudhui yao.
  • Chaneli zinazoiga chaneli iliyopo ya habari.

Kumbuka kuwa hii ni baadhi tu ya mifano na usichapishe maudhui iwapo unaona kuwa yanaweza kukiuka sera hii.

Kitakachotokea iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, huenda tukasimamisha chaneli au akaunti yako. Pata maelezo zaidi kuhusu kusimamishwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5419822256370239383
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false