Arifa

If you’re reaching out about an error message or a blank screen in your Channel Analytics in YouTube Studio, we are aware and working on a fix. You can follow along here for updates. Our teams are currently experiencing high support volumes. Please expect longer than usual wait times for responses to questions from email, chat, and @TeamYouTube on Twitter. 

Kupinga dai la Content ID

Iwapo video yako imepata Dai la Content ID, unaweza kupinga dai iwapo una sababu halisi, kama vile:

  • Kuwa na haki zote zinazohitajika za maudhui yaliyo katika video yako.
  • Kutumia maudhui kwa njia ambayo inakidhi kuwa hali isiyofuata kanuni za hakimiliki, kama vile matumizi ya haki.
  • Kwa kuamini kuwa video yako imetambuliwa isivyo au hitilafu ilitendeka.
Maonyo ya hakimiliki ni tofauti na madai ya Content ID. Iwapo chaneli yako ilipokea onyo la hakimiliki, nenda kwenye makala ya maonyo ya hakimiliki ili upate maelezo zaidi.

Unapopinga dai la Content ID, mtu aliyedai video yako (mlalamikaji) ataarifiwa. Mlalamikaji anapewa siku 30 za kujibu.

Kabla ya kupinga dai

Kabla ya kupinga dai la Content ID, huenda ukahitaji kujifunza zaidi kuhusu uwazi wa kutumiwa na umma na hali zisizofuata kanuni za hakimiliki kama vile matumizi ya haki au matumizi yasiyo ya biashara. Kumbuka kwamba hizi SI sababu halali za kupinga dai:

Iwapo hutawasilisha pingamizi la dai, kuna njia zingine chache za kusuluhisha dai la Content ID, kama vile kuondoa maudhui yanayodaiwa kwenye video yako.

Hatimaye, YouTube haiwezi kuamua kama unapaswa kupinga dai. Iwapo huna uhakika wa hatua za kuchukua, unaweza ukatafuta ushauri wa kisheria kabla ya kupinga dai.

Kumbuka kwamba unapaswa tu kupinga dai ikiwa una uhakika kwamba una haki zote zinazohitajika kutumia maudhui yanayodaiwa. Matumizi mabaya ya mara kwa mara au hasidi ya mchakato wa kupinga dai yanaweza kusababisha upokee adhabu kwenye video au chaneli yako.

Wasilisha pigamizi la dai

Ili kupinga dai la Content ID:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Upande wa menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
  3. Katika kichupo cha Video, tafuta video yenye dai ambalo ungependa kupinga.
    • Ili upate video kwa urahisi, unaweza kubofya upau wa vichujio kisha Hakimiliki.
  4. Katika safu wima ya Vizuizi, wekelea kiashiria juu ya Hakimiliki.
  5. Bofya ANGALIA MAELEZO.
  6. Chini ya sehemu ya Maudhui yaliyotambuliwa kwenye video hii, tafuta dai husika kisha ubofye CHAGUA HATUA kisha Pinga Dai.
Kumbuka: Huenda ukawa na chaguo la Ripoti ili Ukate Rufaa kwa madai ya Content ID ambayo yanazuia video yako. Chaguo hili linaruka hatua ya awali ya kupinga dai na kuanza mchakato wa kupinga dai kwa kukata rufaa. Pata maelezo zaidi kuhusu chaguo la Ripoti ili Ukate Rufaa.

Baada ya kupinga dai

Baada ya kuwasilisha pingamizi la dai, mtu aliyedai video yako (mlalamikaji) anapewa siku 30 za kujibu.

Hatua ambazo mlalamikaji anaweza kuchukua
  • Kuondoa dai: Iwapo mlalamikaji atakubaliana na pingamizi lako la dai, anaweza kuondoa dai lake. Iwapo awali ulikuwa ukichuma mapato kwenye video husika, mipangilio yako ya kuchuma mapato itarejeshwa kiotomatiki madai yote yatakapoondolewa kwenye video. Pata maelezo zaidi kuhusu uchumaji wa mapato wakati wa kupinga madai ya Content ID.
  • Kurejesha dai: Iwapo mlalamikaji anaamini kwamba dai lake bado ni halali, anaweza kulirejesha. Hii inamaanisha kwamba pingamizi lako la dai lilikataliwa na dai litabaki kwenye video yako. Unaweza ukastahiki kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu.
  • Kuwasilisha ombi la kuondoa video: Iwapo mlalamikaji anaamini kwamba dai lake bado ni halali, anaweza kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Iwapo ombi la kuondoa video ni halali, video yako itaondolewa kwenye YouTube na chaneli yako itapokea onyo la hakimilki. Pata maelezo zaidi kuhusu chaguo za kusuluhisha onyo la hakimiliki.
  • Kuruhusu muda wa dai uishe: Iwapo mlalamikaji hatajibu ndani ya siku 30, muda wa dai lake kwenye video yako utaisha na dai hilo litaondolewa kwenye video yako.

 

Pata maelezo zaidi kuhusu mchakato wa kupinga dai katika sura ya video hii ya "Mchakato wa Kupinga Dai la Content ID":

Madai ya Content ID na Mchakato wa Kupinga Madai: Kudhibiti na Kuchukua Hatua Dhidi ya Madai katika Studio

Maswali yanayoulizwa sana (FAQ)

Nini kitatokea iwapo pingamizi langu la dai limekataliwa?
Iwapo pingamizi lako la dai litakataliwa, dai litabaki kwenye video yako. Iwapo bado una uhakika kuwa dai si sahihi, huenda ukastahiki kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Pata maelezo zaidi kuhusu kulikatia rufaa dai la Content ID.
Kumbuka kwamba mlalamikaji anaweza kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki wakati wowote katika mchakato wa kupinga dai. Hali hii ikitokea na ombi la kuondoa video ni halali, video yako itaondolewa kwenye YouTube na chaneli yako itapokea onyo la hakimiliki.
Kwa nini mlalamikaji anakagua pingamizi la dai la awali pamoja na rufaa?

Pingamizi la awali pamoja na rufaa hukaguliwa na mlalamikaji kwa sababu YouTube haiwezi kufanya maamuzi ya umiliki. YouTube haijui ni maudhui gani yalipewa leseni ipasavyo na haiwezi kubainisha hali zinazokidhi kutofuata kanuni za hakimiliki, kama vile matumizi ya haki au matumizi yasiyo ya biashara.

Hatua ya kukata rufaa inahakikisha ukaguzi wa kina zaidi unafanywa na mlalamikaji kwa sababu, akiamua kurejesha dai lake, anahitajika kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki (mchakato wa kisheria) ili kuzuia video. Baada ya hapo, ukiamua kuwasilisha arifa ya kukanusha, mlalamikaji anahitajika kuwasilisha mashtaka ili kuzuia video yako.

Kuna tofuati gani kati ya chaguo za kupinga dai na Elekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa?

Chaguo la awali la kupinga dai linaweza kuchukua hadi siku 30 kabla ya mlalamikaji kujibu mzozo wako. Akikataa dai lako, unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wake. Mlalamikaji ana siku 7 za kujibu rufaa yako.

Chaguo la Kuelekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa linapatikana tu kwa madai ya Content ID ambayo huzuia video. Chaguo hili huruka hatua ya kwanza ya kupinga dai, ambayo inampa mlalamikaji siku 30 za kujibu na huanzisha mchakato wa kukata rufaa. Mlalamikaji ana siku 7 za kujibu, kwa hivyo mchakato huu unaweza kusuluhishwa haraka zaidi.

Iwapo mlalamikaji atakataa rufaa yako, anaweza kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Iwapo ombi la kuondoa video ni halali, video yako itaondolewa kwenye YouTube na chaneli yako itapokea onyo la hakimilki. Kumbuka kuwa bado unaweza kutuma arifa ya kukanusha kama una uhakika kuwa ombi la kuondoa video si sahihi.

Je, video inaweza kuwa na zaidi ya dai moja la Content ID?
Ndiyo, video inaweza kuwa na madai mengi ya Content ID. Kumbuka kuwa video inaweza pia kuwa na ombi zaidi ya moja la kuondoa video, lakini inaweza tu kupata onyo moja la hakimiliki kwa wakati mmoja.
Ikiwa sitapinga dai la Content ID, ninawezaje kusuluhisha?
Ukichagua kutopinga, kuna namna nyinginezo za kusuluhisha dai la Content ID, kama vile kuondoa maudhui yanayodaiwa kwenye video yako.
Je, ninaweza kuacha kupinga dai baada ya kuwasilishwa?
Hapana, ukishawasilisha pingamizi la dai, haliwezi kutamatishwa.

Maelezo zaidi

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4155440707696677475
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false