Muhtasari wa Mtandao wa Vituo Mbalimbali (MCN) kwa ajili ya Watayarishi wa YouTube

Mtandao wa Vituo Mbalimbali (MCN au mitandao) ni watoa huduma wengine wanaoshirikiana na vituo vingi vya YouTube kutoa huduma ambazo zinaweza kujumuisha kukuza hadhira, utayarishaji wa maudhui, ushirikiano wa watayarishi, usimamizi wa haki dijitali, uchumaji wa mapato na/au mauzo. 

Vituo vyote ambavyo ni sehemu ya Mtandao wa Vituo Mbalimbali lazima pia vikaguliwe na kufuata Sera za uchumaji wa mapato kwenye YouTube.

Mshirika na Vituo Vinavyomilikiwa na Kuendeshwa na Mshirika

Mitandao ya Vituo Mbalimbali inaweza kuwa na aina mbili tofauti za vituo chini ya mtandao wake wa YouTube:

  • Vituo vya Washirika hudhibitiwa kwa kiwango kikubwa na Mtandao wake wa Vituo Mbalimbali na vinapatikana kwenye sehemu ya Mmiliki wa Maudhui ambaye ni Mshirika.
  • Vituo Vinavyomilikiwa na Kuendeshwa (O&O) humilikiwa na kuendeshwa na mshirika. Hii inamaanisha kuwa mshirika ana haki za kipekee za maudhui ya YouTube ya kituo na anadhibiti kikamilifu utendakazi wa kituo (k.m. kupakia video) kila siku. Ikiwa mshirika hana umiliki wa kipekee duniani kote wa maudhui yaliyopakiwa kwenye kituo Kinachomilikiwa na Kuendeshwa, ni wajibu wa mshirika kutumia vipengele vinavyofaa kudhibiti upatikanaji wa maudhui kwenye mfumo.

Kutofautisha kati ya aina hizi mbili za vituo huruhusu YouTube kutumia sera zetu na vipengele vya kituo kwa uwazi na haki.

Mitandao ya Vituo Mbalimbali na watoa huduma wengine hawajaidhinishwa na YouTube au Google, lakini unaweza kuangalia orodha ya Watoa huduma Walioidhinishwa kama Stadi wa Masuala ya YouTube kwenye Orodha ya Kampuni zenye Vyeti.

Je, ungependa kuwa mshirika wa Mtandao wa Vituo Mbalimbali? Jaza Fomu yetu ya Kuingiza Biashara kisha tutawasiliana!

Vipengele muhimu vya kufanya kazi na Mitandao ya Vituo Mbalimbali

Kujiunga na Mtandao wa Vituo Mbalimbali ni chaguo muhimu kwa mtayarishi yeyote wa YouTube. Kabla ya kujinga, hakikisha unafahamu huduma na/au matokeo ambayo Mtandao wa Vituo Mbalimbali utakupatia baada ya malipo yako. Unapaswa pia kuhakikisha kuwa unafahamu siku ambayo malipo yako yatasambazwa na unafahamu aina ya ulinzi ulionao iwapo Mtandao wako wa Vituo Mbalimbali utashindwa kukulipa kwa wakati au ukishindwa kukulipa unachodai. Ingawa baadhi ya watayarishi wanaweza kuchagua kushirikiana na Mtandao wa Vituo Mbalimbali, huhitaji kujiunga na Mtandao wa Vituo Mbalimbali ili ufanikiwe kwenye YouTube.

Nyenzo za YouTube kwa ajili ya watayarishi wote

Hakikisha unafahamu jinsi ya kupata usaidizi kama Mtayarishi wa YouTube na utumie chaguo za usaidizi za YouTube ambazo unaweza kuzipata iwe unatumia Mtandao wa Vituo Mbalimbali au la.

YouTube kwa ajili ya Watayarishi ni mahali pazuri pa kupata maelezo kuhusu programu, zana na matukio yote yajayo ambayo yanaweza kukusaidia utayarishe video nzuri. Unaweza pia kupata usaidizi wa kukuza chaneli yako ukiwa na Mpango wa manufaa ya YouTube kwa ajili ya Watayarishi.

Kusaini mkataba na Mtandao wa Vituo Mbalimbali

Mikataba ya Mtandao wa Vituo Mbalimbali ni ya kisheria, kwa hiyo ni muhimu kufanya uamuzi bora. Unaweza kuwasiliana na mshauri wako wa kisheria.

Kabla ya kujiunga na Mtandao wa Vituo Mbalimbali, soma mkataba wako na uhakikishe kuwa angalau unafahamu mambo yafuatayo:

  • Ada zinazotozwa na mtandao
  • Huduma mahususi na kiwango cha usaidizi kinachotolewa kwenye kituo chako
  • Wajibu wako kwa mtandao
  • Muda wa mkataba wako
  • Jinsi ya kusimamisha makubaliano yako
Mapato na kulipwa

Unapojiunga na Mtandao wa Chaneli Mbalimbali, mapato yako yote yatapita kwenye akaunti ya AdSense katika YouTube ya Mtandao wako wa Chaneli Mbalimbali na Mtandao wako wa Chaneli Mbalimbali utaweza kufikia data yako ya mapato ya Takwimu za YouTube.

Kujiunga na Mtandao wa Vituo Mbalimbali hakuathiri ugavi wako wa mapato na YouTube, ambao umebainishwa katika Sheria na Masharti. Kwa kawaida Mitandao ya Vituo Mbalimbali huchukua asilimia fulani ya mapato kwenye sehemu ya mapato ya mtayarishi kabla ya kuwalipa.

Baadhi ya Mitandao ya Vituo Mbalimbali pia hutoa fursa za ziada za kuchuma mapato, kama vile kudhaminiwa na chapa au timu maalum za mauzo, ambazo zinaweza kuchangia mapato kwa kiasi kikubwa kwenye kituo chako. Iwapo mtandao unakupa huduma hizi, unaweza kuhakikisha ikiwa zimebainishwa katika mkataba wako.

Kuzuia na kudhibiti matangazo

Ingawa kudhibiti matangazo kunapaswa kufanywa kwa uangalifu, watayarishi washirika wanaweza kufanya hivi katika akaunti ya AdSense katika YouTube iliyounganishwa na chaneli yao. Pata maelezo zaidi kuhusu kuruhusu na kuzuia matangazo.

Maonyo na uondoaji video

Ingawa Mtandao wa Vituo Mbalimbali unaweza kukusaidia kuelewa au kutatua madai ya hakimiliki, onyo au tukio la kuondoa video kwenye kituo chako, Mtandao wa Vituo Mbalimbali hauwezi kuzuia vitendo hivyo kutokea. Vituo ambavyo vitabainika kukiuka mwongozo wa jumuiya wa YouTube au sera za hakimiliki, kama vile kupakia maudhui ambayo haviyamiliki, vitapokea maonyo au adhabu nyinginezo, iwe ni washirika wa Mtandao wa Vituo Mbalimbali au la.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuepusha kituo chako dhidi ya maonyo na matukio ya kuondoa video kwenye Kitovu cha Sera na Usalama na Kituo cha Hakimiliki cha YouTube.

Ondoa uwezo wa kufikia Mtandao wa Vituo Mbalimbali kwenye kituo chako

Iwapo wewe ni mtayarishi mshirika na unaamini kuwa mkataba wako na Mtandao wa Vituo Mbalimbali unakuruhusu kufanya hivyo, unaweza kuomba kuondoa uwezo wa kufikia Mtandao wa Vituo Mbalimbali kwenye kituo chako.

Mbinu bora za ushirika wa Mitandao ya Vituo Mbalimbali

Mitandao yote ya Vituo Mbalimbali inawajibika kuwapa manufaa watayarishi wao kwa kufuata mbinu bora za YouTube, ikijumuisha:

  • Kuepuka maudhui potofu, lugha potofu ili kusajili vituo kujiunga kwenye Mtandao wa Vituo Mbalimbali.
  • Kuweka bayana katika mkataba huduma na viwango vya usaidizi vinavyotolewa.
  • Kufanya kazi kwa uaminifu na uwazi kuhusiana na huduma zinazotolewa na wajibu kwa mujibu wa mkataba.
  • Utaratibu wa kufahamu mazingira ya kazi na kuachilia vituo kulingana na mikataba yao.

Iwapo Mtandao wa Vituo Mbalimbali hautii mbinu hizi bora, unaweza kupoteza vipengele vya akaunti na uchumaji wa mapato. Iwapo unaamini kuwa Mtandao wa Vituo Mbalimbali haufuati sera za YouTube, wasiliana na Timu ya Usaidizi kwa Watayarishi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15950356925175075643
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false