Kuweka mipangilio chaguomsingi ya upakiaji

Mipangilio chaguomsingi ya video zinazopakiwa ni mipangilio inayotumika kwenye video zote unazopakia kupitia wavuti kulingana na chaguo zako. Unaweza kuteua chaguomsingi za mipangilio ya faragha, aina, jina, lebo, maoni, lugha ya video zako na zaidi. 

Mipangilio chaguomsingi za kupakia huathiri tu video zilizopakiwa kupitia kivinjari chako kwenye youtube.com/upload. Ukipakia video kupitia vifaa vya mkononi, Hangout On Air au kihariri cha video, hazitafuata mipangilio yako chaguomsingi.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka mipangilio chaguomsingi ya hadhira ya kituo chako ili utueleze iwapo video yako inalenga watoto.

Chagua mipangilio chaguomsingi ya kupakia

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio.
  3. Chagua Mipangilio chaguomsingi ya video zinazopakiwa.
  4. Chagua mipangilio yako chaguomsingi katika vichupo vya Maelezo ya msingi na Mipangilio ya kina.
  5. Chagua Hifadhi.

Bado unaweza kubadilisha mipangilio baada ya kupakia video kwenye ukurasa wa Video. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha video ulizopakia.

Ikiwa unashiriki katika Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza pia kuweka muundo chaguomsingi wa matangazo na chaguomsingi za uchumaji wa mapato.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17481368850831351242
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false