Jinsi ya kutumia gumzo la YouTube Moja kwa Moja

Gumzo la moja kwa moja huwashwa kwa chaguomsingi isipokuwa hadhira ya mitiririko mubashara ya kituo chako iwe imebainishwa kuwa inalenga watoto. Mtiririko wako mubashara utakapoisha, utahifadhiwa kwenye kumbukumbu na watazamaji wanaweza kutazama mtiririko mubashara pamoja na gumzo la moja kwa moja.

Kipengele cha gumzo la moja kwa moja kinapatikana kwenye kurasa za kutazama za YouTube pekee, si kwenye vichezaji vilivyopachikwa.

Maswali na Majibu katika mtiririsho wa Moja kwa Moja

Maswali na Majibu katika mtiririsho wa Moja kwa Moja

Maswali na Majibu katika mtiririsho wa Moja kwa Moja ni njia nyingine ya kupanua ushirikiano kati ya watayarishi na watazamaji katika muda halisi. Kipengele hiki kinaweza kutumiwa wakati wa Mitiririko Mubashara na Maonyesho ya Kwanza. Kama Mtayarishi, unaweza kubadilisha zaidi hali ya Maswali na Majibu katika mtiririsho wa Moja kwa Moja kwa kujifunza jinsi ya Kudhibiti Gumzo lako la Moja kwa Moja.

Kumbuka: Maswali na Majibu katika mtiririsho wa Moja kwa Moja na Kura za Maoni hayapatikani kwenye Vifaa vya mkononi. Iwapo unatiririsha kupitia Programu ya YouTube ya Vifaa vya Mkononi, unaweza kudhibiti mtiririko mubashara kwenye kifaa cha mkononi kupitia Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja ili ufikie Vipengele vya Gumzo la Moja kwa Moja.

Ili uanze Maswali na Majibu katika mtiririsho wa Moja kwa Moja:

  1. Ratibu au uanze mtiririko mubashara au Onyesho la kwanza.
  2. Kwenye sehemu ya chini ya dirisha la gumzo, bofya kisha uchague Anza kipindi cha Maswali na Majibu.
  3. Weka kidokezo kisha ubofye Anzisha kipindi cha Maswali na Majibu.
  4. Orodha ya Maswali itaonekana katika dirisha la gumzo baada ya kipindi cha Maswali na Majibu kuanza. Ili ujibu swali, nenda kwenye Orodha ya Maswali, chagua swali unalotaka kujibu, bofya menyu '' na ubofye Chagua Swali. Swali hilo litapachikwa katika sehemu ya juu ya dirisha la gumzo na litaonekana kwa watazamaji wako. Bofya Funga ili uondoe bango la swali kwenye dirisha la gumzo.

Kumbuka: Bofya kishale cha chini katika sehemu ya juu ya dirisha la gumzo na uchague Gumzo Maarufu au Gumzo Yote ili uangalie ujumbe kwenye Gumzo la Moja kwa Moja.

  1. Ili ukamilishe kipindi chako cha Maswali na Majibu katika mtiririsho wa Moja kwa Moja, kutoka kwenye bango la kidokezo katika sehemu ya juu ya gumzo, bofya Kamilisha kipindi cha Maswali na MajibuMaswali yote ambayo hayajajibiwa katika orodha yatafutwa na vipindi vya Maswali na Majibu katika mtiririsho wa Moja kwa Moja vitapatikana katika kipengele cha Kuonyesha Gumzo Tena.

Kumbuka: Maelezo ya Maswali na Majibu katika mtiririsho wa Moja kwa Moja hayapatikani katika Takwimu za YouTube. Watazamaji wanaweza tu kutuma swali 1 kwa kila dakika.

Kuondoa au Kufuta Swali:

Ili ufute swali ambalo umetuma ambalo halijabandikwa kwenye gumzo, nenda kwenye Shughuli Zangu.

  • Ili ufute maswali ambayo yamebandikwa kwenye dirisha la gumzo, bofya menyu '', kisha ubofye Futa.

Mionekano ya gumzo la moja kwa moja

Watazamaji wanaweza kuchagua mionekano miwili ya Gumzo la moja kwa moja wakati wowote.

  • Gumzo maarufu: Mwonekano huu unachuja ujumbe kama vile taka inayoweza kutokea ili kusaidia kufanya gumzo iwe rahisi zaidi kusoma na muhimu zaidi.
  • Gumzo la moja kwa moja: Mwonekano huu haujachujwa. Unaonyesha ujumbe wote wa gumzo jinsi unavyotumwa.

Kumbuka: Mitiririko mubashara ambayo imebadilishwa katika kihariri cha video haitakuwa na kipengele cha kuonyesha gumzo tena. Masharti haya yanatumika kwa aina zote za vipengele vya kuhariri vinavyotumika.

Jinsi Gumzo Maarufu linavyoorodheshwa

Gumzo maarufu huonyesha kile ambacho watazamaji wanaweza kuthamini na kutumia. Kinachoonekana kwenye Gumzo maarufu kinatokana na ishara mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maandishi ya gumzo, maandishi ya kitambulishi, maandishi ya jina la kituo, ishara na video.

Gumzo maarufu huenda lisionyeshe maudhui ambayo YouTube imetathmini kuwa watazamaji huenda wasiyathamini au kujishirikisha nayo. Hii inaweza kujumuisha maoni ambayo yametambuliwa kuwa yasiyofaa, taka au uigaji ambao hauruhusiwi kwenye Gumzo maarufu. Utambuzi hutegemea aina mbalimbali za ishara, kama vile maandishi ya gumzo, maandishi ya jina la kituo cha mtoa maoni au maandishi ya kitambulishi, ishara na mipangilio ya udhibiti wa kituo.

Beji za gumzo la moja kwa moja

Beji za gumzo la moja kwa moja hutambua Anayetiririsha Moja kwa Moja na Mdhibiti . Iwapo kituo chako kimetimiza masharti ya uanachama, unaweza kubuni beji maalum za uanachama ambazo pia huonekana katika gumzo la moja kwa moja.

Emoji

Emoji ni picha ndogo ambazo zinaweza kuonyesha hisia, wazo na zaidi. Mtu yeyote anaweza kutumia idadi ya juu zaidi ya emoji na watayarishi wanaweza kubuni emoji maalum ambayo inapatikana kama manufaa ya uanachama katika kituo.

Weka emoji kwenye maoni au ujumbe wako

Kwenye kifaa cha mkononi: Ukiandika ujumbe wa gumzo, gusa  ili uweke emoji ya YouTube au aikoni ya emoji kwenye kibodi ya kifaa chako ili uweke emoji kutoka kwenye mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako.

Kwenye kompyuta: Ukiandika ujumbe wa gumzo, gusa Weka Emoji.

Kumbuka: Kwenye kompyuta, unaweza kubonyeza na kushikilia emoji ili ubadilishe mwonekano upendavyo. Mipangilio yako itahifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Ili ubadilishe mipangiio yako chaguomsingi, chagua aina tofauti ya emoji. Unaweza pia kufuta mipangilio kwa kufuta vidakuzi vya kivinjari na data nyingine ya tovuti au kwa kuondoka kwenye akaunti ya YouTube.

Weka Picha Tuli za YouTube kwenye maoni au ujumbe wako

Picha Tuli za YouTube ni seti ya picha tuli ambazo zinapatikana kwenye YouTube pekee na zinaweza kutumika tu kwenye gumzo la moja kwa moja na maoni. Picha hisia hizi zimeundwa na wasanii mbalimbali ili uzitumie kueleza hisia au mawazo yako. Zinaweza kupatikana katika kiteua emoji juu ya seti ya kawaida ya emoji.

Kwenye kifaa cha mkononi: Ukiandika ujumbe wa gumzo, gusa ili uweke picha tuli za YouTube.

Kwenye kompyuta: Ukiandika ujumbe wa gumzo, gusa ili uweke picha tuli za YouTube.

Miitikio

Miitikio kwenye Mtiririko Mubashara huruhusu watazamaji kujibu papo hapo kuhusu kinachoendelea katika mtiririko mubashara. Watazamaji wanaweza kuweka miitikio wakati gumzo la moja kwa moja limefunguliwa. Wewe na watazamaji mnaweza kuona miitikio isiyo na utambulisho; haitawezekana kuona ni watumiaji gani walioweka miitikio fulani.

Aina za miitikio

  • Watazamaji wanaweza kuweka miitikio ya Moyo, Uso wa Kicheshi, Kifyatua Vikaratasi vya Sherehe, Uso Wenye Huzuni na miitikio mingine "100".

Zima au washa miitikio

Kama mtayarishi, unaweza kuwasha au kuzima miitikio ya mtiririko mubashara kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja. Unaweza kubadilisha mipangilio hii wakati wowote unapotiririsha.

  1. Katika kompyuta, nenda kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye upande wa juu kulia, bofya ANZISHA  kisha Tiririsha Mubashara  ili ufungue Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja.
  3. Bofya kichupo cha Tiririsha.
  4. Bofya Badilisha, kisha Uwekaji Mapendeleo.
  5. Chagua Miitikio.

Tuma ujumbe

Ili uchapishe katika gumzo la moja kwa moja:

  1. Bofya mahali panaposema, “Toa Maoni” na uanze kuandika maandishi.
  2. Bofya Tuma .

Kujibu mtu katika mipasho ya gumzo

Unaweza kumjibu mtu katika mipasho ya gumzo kwa kutaja jina lake la mtumiaji.

  1. Andika “@”.
  2. Anza kuandika jina lake la mtumiaji.
  3. Chagua jina la mtumiaji.

Wewe na mwanachama wa gumzo aliyetajwa mtaona jina lake la mtumiaji limeangaziwa katika gumzo la moja kwa moja. Hali hii ya kuangazia hufanya iwe rahisi kwake kuona majibu yako katika mipasho ya gumzo.

Vikomo vya ujumbe

Watazamaji wanaruhusiwa tu kuandika herufi 200 na kutuma mara 11 kwa kila sekunde 30. Wamiliki wa tukio wanaruhusiwa kutuma ujumbe bila upeo. Watazamaji hawaruhusiwi kuchapisha herufi maalum, URL na Lebo za HTML.

Gumzo la wanaofuatilia kituo na wanachama pekee

Kituo kinaweza kufanya gumzo lake la moja kwa moja liwe la wanachama au la wanaofuatilia kituo pekee.

Iwapo gumzo ni la wanaofuatilia kituo pekee, kituo kinaweza kubainisha muda ambao watazamaji wanapaswa kuwa wamefuatilia kituo. Ili uone muda ambao unahitaji kuwa umefuatilia na muda ambao tayari umekuwa ukifuatilia, gusa Maelezo  kwenye kisanduku cha ujumbe wa gumzo la moja kwa moja.

Bandika ujumbe

Unaweza kubandika ujumbe wako mwenyewe au ujumbe wa mtazamaji katika Gumzo la Moja kwa Moja.

Ni wewe tu, wala si wadhibiti au watazamaji wako unayeweza kubandika ujumbe. Ujumbe uliobandikwa huonekana chini ya Super Chat.

  1. Nenda kwenye dirisha la gumzo wakati wa mtiririko mubashara au Onyesho la kwanza.
  2. Tafuta ujumbe katika Gumzo la Moja kwa Moja, hata ujumbe wako, kisha uguse au ubofye Zaidi ''.
  3. Ili ubandike ujumbe, gusa au ubofye Bandika .

Kumbuka: Unaweza tu kubandika ujumbe mmoja kwa wakati mmoja. Ili ubadilishe ujumbe uliobandikwa, bandika tu ujumbe mwingine. Ili ubandue ujumbe, bofya Zaidi kwenye ujumbe uliobandikwa kisha uguse Bandua.

Anzisha kura ya maoni ya moja kwa moja

Wamiliki wa kituo wanaweza kuanzisha na kudhibiti kura za maoni za moja kwa moja kwenye mitiririko na Maonyesho yao ya Kwanza. Baada ya mtu kupiga kura, hawezi kuibadilisha.

  1. Ratibu au uanze mtiririko mubashara au Onyesho la kwanza.
  2. Kwenye sehemu ya chini ya dirisha la gumzo, gusa Anzisha kura ya maoni .
  3. Anzisha kura yako ya maoni, na kisha uchague Uliza jumuiya yako.

Ili ukamilishe kura ya maoni na uone matokeo katika gumzo kwenye bango katika sehemu ya juu ya gumzo, gusa Kamilisha kura ya maoni.

Vikwazo

Kura za maoni ya moja kwa moja zinaweza:

  • kuanzishwa tu kutoka YouTube kwenye kompyuta yako.
  • kuwa na chaguo 2 hadi 4.
  • kutazamwa tu mubashara. Hazionyeshwi katika marudio ya gumzo la moja kwa moja.
  • zinadumu tu kwa hadi saa 24.

Pachika gumzo la moja kwa moja

Wakati wa mtiririko mubashara, unaweza kupachika gumzo la moja kwa moja kwenye tovuti yako kwa kutumia iframe.

Kumbuka: kupachika gumzo la moja kwa moja hakupatikani kwenye wavuti wa vifaa vya mkononi.

  1. Kupata kitambulisho cha video kwa ajili ya mtiririko mubashara. Unaweza kupata kitambulisho cha video kwenye URL ya ukurasa wa kutazama (youtube.com/watch?v=12345). Katika hali hii, kitambulisho cha video ni ‘12345’.
  2. Pata URL ya kikoa ya kituo ambacho ungependa kupachika gumzo kwake. Iwapo unapachika gumzo kwenye www.example.com/youtube_chat, kikoa chako cha kupachika ni "www.example.com".
  3. Jumuisha URL iliyopachikwa kwa njia ifuatayo: https://www.youtube.com/live_chat?v=12345&embed_domain=www.example.com.
    • URL hii ni iframe yako. Kumbuka lazima embed_domain ilingane na URL ya ukurasa ambako unapachika gumzo. Iwapo hazilingani, gumzo lililopachikwa halitafunguka.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15942441447516723103
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false