Ninaweza kuchuma mapato kwenye maudhui yapi?

Ili video au Video zako Fupi zitimize masharti ya kuchuma mapato, maudhui lazima yawe halisi na ambayo hayajarudiwa, kati ya masharti mengine ya Sera zetu za uchumaji mapato kwenye chaneli za YouTube. Hakikisha pia kwamba una haki zote zinazohitajika za kutumia vipengele vyote vya picha na sauti kibiashara katika maudhui yako.

Mwongozo wa maudhui uliyotayarisha:

  • Fuata Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube
  • Buni vipengele vyote vya video mwenyewe. Hii ni pamoja na:
    • Blogu za video za kila siku
    • Video za ukurasa wa kwanza
    • Video za mambo ya kujifanyia mwenyewe
    • Mafunzo
    • Video halisi za muziki
    • Filamu fupi halisi
    • Video fupi zilizo na au zisizo na maudhui mseto
  • Hakikisha una haki zote zinazohitajika ili kutumia kibiashara picha zote ulizobuni.
  • Kumbuka kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa watangazaji kuweka matangazo kwenye maudhui yanayofaa watangazaji.

Mwongozo wa maudhui ambayo hukubuni:

Unaweza kujumuisha nyimbo kutoka kwenye Muziki wa Watayarishi katika video bila kupoteza uwezo wa kuchuma mapato. Baadhi ya nyimbo zinaweza kupewa leseni mapema, hali inayowaruhusu watayarishi kudumisha uwezo kamili wa kuchuma mapato. Nyimbo zingine zinaweza kutimiza masharti ya kugawa mapato na wamiliki wa haki za wimbo.
Matumizi ya Haki - Hakimiliki kwenye YouTube

Je, ninaweza kuchuma mapato kwa video yangu iwapo...?

Bofya hapa chini ili uone iwapo aina ya maudhui yako yanaweza kuchumiwa mapato na iwapo unahitaji kuthibitisha haki za matumizi ya kibiashara ili kuyatumia.

Nilibuni maudhui yote ya sauti na video


Unaweza kuchuma mapato kwenye maudhui uliyobuni mradi bado una haki za video hiyo.

Iwapo umesajiliwa na lebo ya muziki, unaweza kuchuma mapato kwenye video yako kulingana na sheria na masharti au vikwazo vya makubaliano hayo. Huenda ukahitaji kupata ushauri wa wakili.

Ninatumia programu ya kuhariri sauti au picha ili kutayarisha maudhui yangu mwenyewe

Programu ya kuhariri sauti na picha inaweza kutumiwa kutayarisha maudhui yanayoweza kuchuma mapato. Uchumaji wa mapato utategemea upeo, vikwazo na ruhusa za kibiashara za leseni. Iwapo ulitumia sampuli au marudio, hakikisha kuwa leseni inaruhusu kimahususi matumizi yake ya kibiashara. Kwa maudhui mseto kwenye Video Fupi, fuata mwongozo huu.

Ninatumia maudhui yasiyo na mirabaha au ya Creative Commons


Unaweza kuchuma mapato kwenye maudhui yasiyo ya mirabaha au ya Creative Commons wakati makubaliano ya leseni yanakupa haki ya kuyatumia kibiashara. Wakati mwingine wamiliki wa haki wanahitaji kutaja mtayarishi wa maudhui au kutoa ithibati ya ununuzi ili kuitumia katika video yako kwa madhumuni ya kibiashara.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kusoma leseni ili kufahamu haki zako.

Nina ruhusa ya kutumia sauti au picha zilizotayarishwa na mtu mwingine

Unaweza kuchuma mapato kwenye maudhui kama hayo, lakini lazima uwe na ruhusa dhahiri iliyoandikwa inayokupa haki za matumizi ya kibiashara wakati wowote kutoka kwa mmiliki wa haki.
Ninacheza au kutoa mwongozo wa mchezo wa video

Iwapo ungependa kuchuma mapato kwenye maudhui ya michezo ya video, utahitaji kupewa haki za matumizi ya kibiashara na leseni kutoka kwa mchapishaji wa michezo ya video. Baadhi ya wachapishaji wa michezo ya video wanaweza kukuruhusu utumie maudhui yote ya michezo ya video kwa matumizi ya kibiashara. Maelezo haya yanaweza kuthibitishwa katika makubaliano yake ya leseni.

Katika makubaliano mengine ya leseni, huenda wachapishaji wasitoe haki za kibiashara kwa video ambazo zinaonyesha tu uchezaji wa mchezo kwa kipindi kilichorefushwa. Kwa sheria na masharti ya utoaji leseni, lazima matumizi ya michezo ya video yawe machache isipokuwa msimulizi atoe:

  • Thamani ya maagizo au elimu
  • Analenga tu kitendo kinachoonyeshwa
Pata maelezo zaidi kuhusu maudhui ya programu na mchezo wa video na uangalie mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa kwa matangazo kwa michezo na uchumaji mapato.
Ninabuni mafunzo yanayoonyesha matumizi ya programu

Maudhui ya kiolesura cha programu unayobuni yanaweza kuchumiwa mapato, lakini hayo pia yanategemea haki za matumizi ya kibiashara zinazotolewa na leseni ya programu.

Wakati mwingine, huenda ukahitaji mkataba na mchapishaji au uthibitisho kuwa umelipia ada ya kutoa leseni. Lazima matumizi ya kiolesura cha programu yawe machache isipokuwa msimulizi atoe:

  • Thamani ya maagizo au elimu
  • Maudhui yanalenga tu kitendo kinachoonyeshwa

Pata maelezo zaidi kuhusu maudhui ya programu na michezo ya video.

Ninatumia maudhui yaliyo wazi kutumiwa na umma
 

Ili maudhui yawe wazi kutumiwa na umma, muda wa hakimiliki ya kazi umeisha, umeondolewa, au hautumiki tena. Ukithibitisha kuwa maudhui katika video yako ni wazi kutumiwa na umma, unaweza kuchuma mapato.

Kumbuka: Hili linategemea upeo, vikwazo na ruhusa za kibiashara za leseni.

Utaratibu wa kustahiki kuwa wazi kutumiwa na umma unaweza kuwa tofauti kulingana na vigezo vingi.
Pata maelezo zaidi kuhusu maudhui yaliyo wazi kutumiwa na umma.
Ina rekodi yangu halisi ya toleo lingine la wimbo

Baadhi ya matoleo mengine ya wimbo yanaweza kutimiza masharti ya uchumaji wa mapato. Ili yatimize masharti, lazima mchapishaji wa muziki adai wimbo kupitia mfumo wa Content ID na uchague kuyatumia kuchuma mapato.

Iwapo wimbo haujadaiwa, huwezi kuchuma mapato kwenye video yako. Ruhusa dhahiri iliyoandikwa kutoka kwa mmiliki wa haki wa nyimbo inapaswa kutolewa mapema.

Matumizi ya rekodi yoyote ya sauti ya kibiashara, kama vile muziki wa ala, rekodi ya karaoke, au onyesho la tamasha la moja kwa moja na msanii hayatimizi masharti ya uchumaji wa mapato.

Pata maelezo zaidi kuhusu kuchuma mapato kwa matoleo mengine ya video yanayotimiza masharti.

Ninatumia rekodi yangu binafsi ya tamasha za umma, matukio, maonyesho na zaidi

Ingawa huenda ulirekodi maudhui mwenyewe, kwa kawaida mtayarishi au mwandishi halisi wa maudhui husika ana haki zinazohitajika ili kutumia maudhui haya kibiashara.

Iwapo ungependa kuchuma mapato kwenye rekodi yako ya maonyesho katika tamasha, unahitaji ruhusa dhahiri iliyoandikwa kutoka kwa mmiliki halisi wa haki.

Nilibuni rekodi kutoka kwa televisheni, DVD au CD

Ingawa huenda ulirekodi maudhui mwenyewe, mtayarishi au mwandishi wa maudhui uliyorekodi anaweza kuwa na haki zinazohitajika ili kutumia maudhui haya kibiashara.

Ili uchume mapato kwenye rekodi yako ya kipindi cha televisheni, DVD au CD, unahitaji ruhusa iliyoandikwa kutoka kwa mmiliki wa haki wa vipengele vya sauti au video vilivyorekodiwa.

Ninapakia maudhui ambayo nilinunua

Ingawa huenda ulinunua kitu mwenyewe, kwa kawaida, ni mtayarishi au mwandishi halisi aliye na haki nyingi zinazohitajika ili kutumia maudhui haya kibiashara.

Huwezi kuchuma mapato kwenye maudhui ya wengine ambayo umenunua isipokuwa mmiliki wa haki zake akupe haki za matumizi ya kibiashara.

Ninapakia maudhui niliyopata mtandaoni

Ingawa huenda ulipata maudhui mtandaoni bila malipo, kwa kawaida watayarishi halisi wana haki nyingi zinazohitajika ili kutumia maudhui kibiashara.

Iwapo ungependa kuchuma mapato kwenye maudhui hayo, hakikisha kuwa una haki zake zote zinazohitajika za matumizi ya kibiashara.

Ina muziki kutoka kwa Maktaba ya Sauti ya YouTube

Unaweza kuchuma mapato kwenye muziki kutoka kwa Maktaba ya Sauti ya YouTube.

Ninatumia maudhui ya wengine chini ya Matumizi ya Haki

Kuna uwezekano mdogo wa matumizi ya kibiashara kuzingatiwa kama "matumizi ya haki," ingawa unaweza kutumia video kuchuma mapato na ujitetee ukitumia kanuni ya matumizi ya haki. Kwa maelezo zaidi, angalia makala ya Matumizi ya haki kwenye YouTube.

Bado unahitaji usaidizi?

Iwapo bado huna uhakika kuhusu aina ya maudhui unayoweza au usiyoweza kutumia kuchuma mapato, kagua mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazajiPata maelezo zaidi kuhusu jinsi hakimiliki hufanya kazi katika YouTube.

Maudhui kwenye ukurasa huu yametolewa kwa madhumuni ya elimu pekee na si ushauri wa kisheria. Unapaswa tu kutafuta ushauri wa kisheria kutoka kwa wakili au mwakilishi wa kisheria.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11310285817793691339
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false