Katika makala haya, utapata maelezo kuhusu sera ambazo watangazaji wote wanapaswa kufuata na jinsi tunavyokagua matangazo.
Sera zetu
Ili uweke matangazo kwenye YouTube, utapaswa kutii:
- Sera za Matangazo kutoka Google
- Sera za matangazo zinazohusu YouTube tu
- Vipengele na miundo ya matangazo
- Kulenga na kuhudumia
- Ukiweka matangazo kwenye YouTube Kids, angalia sera yetu ya kutangaza kwenye YouTube Kids kwa mwongozo mahususi zaidi.
- Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube
- Mwongozo wa Kiufundi
Mwongozo wa sera
Utapata maelezo ya kina zaidi kuhusu mwongozo wetu wa sera hapo chini:
Maudhui yaliyopigwa marufukuMaudhui ambayo hupaswi kutangaza kwenye Mtandao wa Google |
Desturi zilizopigwa marufukuUsichoweza kufanya unapotangaza nasi |
Maudhui yaliyozuiwaMaudhui unayoweza kutangaza, lakini kwa masharti |
Uhariri na kiufundiViwango vya ubora wa matangazo, tovuti na programu zako |
Sera nyingine muhimuMatangazo huonekana haswa yanapoonyeshwa kwenye YouTube. Viungo vilivyo hapo chini vinajumuisha sera nyingine zinazotumika kwa tangazo lolote linaloonyeshwa kwenye mfumo wetu: |
Mahali sera zinatumika
Sera zetu zinatumika kwenye sehemu zote za maudhui yako, ikiwa ni pamoja na:
- Maandishi kwenye tangazo
- Vipengee vya ubunifu kwenye tangazo
- Maudhui kwenye tovuti yako au maudhui kwenye kituo au video yako
Tangazo lako likishabuniwa, litakaguliwa kiotomatiki. Pata maelezo zaidi kuhusu mchakato wetu wa kukagua matangazo hapo chini.
Jinsi tunavyokagua matangazo
Baada ya wewe kubuni au kubadilisha tangazo au kiendelezi, mchakato wa ukaguzi huanza kiotomatiki.
Maelezo ya ukaguzi wa tangazoTunachokagua
- Kichwa
- Maelezo
- Maneno muhimu
- Unakoenda
- Picha
- Video.
Kile wakaguzi huzingatia
Kwa kuwa video ni muundo wa kipekee, tuna mambo mahususi tunayoyazingatia tunapotathmini tangazo lako, kama vile:
- Sehemu lengwa ya video
- Pembe ya kamera na matukio ya muda mfupi
- Jinsi picha zinazoonyeshwa kwa watumiaji zinavyoonekana safi
Unachoweza kufanya
Muktadha ni muhimu na ukiuongeza, utatusaidia kufanya uamuzi sahihi. Mifumo yetu si sahihi kila wakati. Ikiwa mifumo yetu itaweka alama ya kuonyesha kuwa matangazo yako “Hayajaidhinishwa”, unaweza kuchukua hatua ya kutatua hali hii kwa kufuata maagizo hapa. Wakaguzi wetu binadamu watatathmini maudhui na muktadha wako ili wafanye uamuzi wa mwisho.
Pata maelezo zaidi kuhusu mchakato wetu wa kuidhinisha matangazo.
Kuhusu sera zetu
YouTube imejitolea kutoa huduma ya utangazaji iliyo na sera za haki na thabiti zinazonufaisha watumiaji, watangazaji na washirika wetu. Ili kufikia lengo hili, tunadumisha viwango vya juu kwa matangazo yanayoruhusiwa kwenye tovuti yetu. Viwango hivi pia vinajumuisha vile vinavyobainishwa na mwongozo na sera zetu za kiufundi, jumuiya na utangazaji.
Maelezo ya sera za matangazo