Pata maelezo kuhusu maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki ambalo pia linajulikana kama "ombi la kuondolewa kwa video" au "kuondoa", ni ombi la kisheria la kuondoa maudhui kwenye YouTube kutokana na tuhuma za ukiukaji wa hakimiliki.

Kumbuka kwamba maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki yanatofautiana na madai ya Content ID.

Jinsi mchakato unavyofanya kazi

Mwenye hakimiliki akipata maudhui yake yanayolindwa kwa hakimiliki kwenye YouTube bila idhini yake, anaweza kutuma ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.

Baada ya ombi la kuondoa kuwasilishwa

Baada ya ombi la kuondoa maudhui kuwasilishwa, YouTube hulikagua ili kuhakikisha lina maelezo yanayohititajika na sheria ya hakimiliki inayotumika na halionyeshi dalili zozote za matumizi mabaya. Iwapo ombi la kuondoa maudhui litapita hatua ya ukaguzi, YouTube huondoa maudhui yanayodaiwa kukiuka hakimiliki ili kutii sheria ya hakimiliki inayotumika.

Ikiwa ombi la kuondoa maudhui halina maelezo au ikiwa maelezo zaidi yanahitajika, YouTube itawasiliana na mlalamikaji (mtu aliyewasilisha ombi la kuondoa maudhui) kwa maelezo zaidi. Kwa mfano, walalamikaji wanaweza kuombwa:

  • Kutoa jina mahususi zaidi la maudhui yaliyo na hakimiliki
  • Kuwasilisha ushahidi unaoonyesha kuwa ameidhinishwa kuchukua hatua kwa niaba ya mwenye hakimiliki, ikiwa inatumika
  • Kuthibitisha ikiwa hali zisizofuata kanuni za hakimiliki kama vile matumizi ya haki au matumizi yasiyo ya biashara zimezingatiwa.

Huenda maudhui husika yakasalia kwenye YouTube hadi tutakapopokea maelezo yanayohitajika.

Maudhui yakiondolewa

Ombi la kuondoa maudhui likichakatwa, maudhui hayo yanaondolewa kwenye YouTube na onyo la hakimiliki linawekwa kwenye kituo cha aliyepakia. Aliyepakia maudhui husika ana chaguo 3 ili kutatua onyo la hakimiliki.

Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQ)

Je, YouTube hukagua vipi maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki?

Maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki hukaguliwa kwa kutumia mchanganyiko wa mifumo ya kiotomatiki na wahakiki.

Mifumo yetu ya kiotomatiki hutumia mashine kujifunza ili kuchakata maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Mifumo hiyo inaendelea kufundishwa kwa kutumia data inayotokana na maamuzi ya awali yaliyofanywa na wahakiki na huchakata tu maombi ya kuondoa maudhui ikiwa na uhakika wa kiwango cha juu sana kuwa maombi hayo yana vipengele vyote vinavyohitajika kisheria na hayajatumika vibaya. Maombi yanayotumika vibaya yanatokana na hali ambapo mtu anajaribu kwa makusudi na kwa nia mbaya kuondoa maudhui kwenye YouTube kupitia madai ya uongo ya umiliki wa hakimiliki.

Iwapo mifumo yetu ya kiotomatiki haina uhakika iwapo ombi la kuondoa ni halali (lina vipengele vyote vinavyohitajika kisheria na halitokani na matumizi mabaya), mhakiki aliyefunzwa atatathmini ombi hilo. Iwapo atahitaji maelezo zaidi ili kuthibitisha ombi hilo, basi mhakiki atamtumia mlalamikaji barua pepe na kumwomba maelezo zaidi. Kwa mfano, walalamikaji wanaweza kuombwa:

  • Kutoa jina mahususi zaidi la maudhui yao yaliyo na hakimiliki
  • Kuwasilisha ushahidi unaoonyesha kuwa wameidhinishwa kuchukua hatua kwa niaba ya mmiliki wa hakimiliki wanayemwakilisha
  • Kuthibitisha kuwa wamezingatia ikiwa video hiyo inaweza kuwa imelindwa na hali zisizofuata kanuni za hakimiliki, kama vile matumizi ya haki au matumizi yasiyo ya biashara

Mlalamikaji asipojibu barua pepe au hajatoa maelezo yanayohitajika, maudhui husika yatasalia kwenye YouTube.

Kwa nini mifumo ya kiotomatiki inatumiwa kukagua maudhui?

Mifumo ya kiotomatiki hutumiwa kutoa majibu ya haraka na yanayofaa zaidi kwa maombi mengi ya kuondoa maudhui tunayopokea huku ikidumisha viwango vya juu vya usahihi.

Kwa mfano, mwaka 2022, YouTube ilipokea zaidi ya maombi milioni 16 ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Licha ya idadi hii kubwa, kutumia mifumo ya kiotomatiki kuchakata maombi ya kuondoa maudhui yaliyo na uwezekano mkubwa wa kuwa halali hutuwezesha kujibu haraka zaidi na kwa usahihi. Kimsingi, maombi ya kuondoa maudhui yaliyochakatwa na mifumo yetu ya kiotomatiki hukatiwa rufaa mara chache kuliko uondoaji unaochakatwa na wahakiki.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi mifumo ya YouTube inavyokagua maudhui.  

Ninawasilishaje ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki ya video?
Ili uwasilishe ombi la kuondolewa kwa maudhui ya video, fuata hatua zilizo hapa.
Ninawasilishaje ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kwa maudhui yasiyo ya video?
Ili uwasilishe ombi la kuondolewa kwa maudhui yasiyo ya video, kama vile picha za aikoni ya kituo, fuata hatua zilizo hapa. Fomu yetu ya wavuti haiwezi kuchakata maombi ya kuondoa maudhui yasiyo ya video. 
Je, ninaweza kuomba kuondolewa kwa kituo kizima au orodha ya kucheza?
Hapana, huwezi. Unatakiwa kubainisha video unayodai kuwa imekiuka hakimiliki, kwa kutumia URL yake. 

Zifuatazo ni hatua za kufuata ili upate URL ya video:

  1. Tafuta video husika kwenye YouTube.
  2. Katika upande wa juu kwenye sehemu ya anwani, kutakuwa na URL ya video kama hii: www.youtube.com/watch?v=xxxxxxxxxxx

Ili uwasilishe ombi la kuondoa maudhui, fuata hatua zilizo hapa

Kwa nini niwape maelezo yangu yote kila ninapowasilisha ombi jipya la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki?

Kwa mujibu wa sheria ya hakimiliki inayotumika, tunahitaji ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki litumwe kwa kila tuhuma ya ukiukaji wa hakimiliki.

Njia rahisi zaidi ya kuwasilisha ombi lingine la kuondoa ni kuingia katika akaunti ya YouTube na kutumia fomu yetu ya wavuti.

Kumbuka kwamba tunatoa zana za ziada za kudhibiti hakimiliki kwa wenye hakimiliki wenye mahitaji ya mara kwa mara ya usimamizi wa hakimiliki.
Niliieleza YouTube kuhusu video iliyokiuka hakimiliki yangu na ikaondolewa. Kwa nini nimepokea barua pepe inayosema huenda video hiyo ikarejeshwa kwenye tovuti?
Kuna uwezekano kuwa tulipokea arifa ya kukanusha kutoka kwa aliyepakia akijibu ombi lako la kuondoa maudhui. Video itarejeshwa isipokuwa uthibitishe kwamba umechukua hatua ya kisheria dhidi ya mtayarishi ili kuzuia shughuli ya ukiukaji inayodaiwa. Tusipopokea ilani hiyo kutoka kwako ndani ya siku 10, tunaweza kurejesha maudhui hayo kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu kujibu arifa ya kukanusha.
Ninawezaje kuripoti video zinazotoa manenosiri au programu zinazozalisha funguo zinazowezesha matumizi yasiyoidhinishwa ya kazi zangu zilizo na hakimiliki?
Iwapo video inatoa maelezo kuhusu jinsi ya kukwepa vizuizi vya programu yako kupitia manenosiri, programu zinazozalisha funguo au kukwapua, tumia fomu yetu ya Matatizo Mengineyo ya Kisheria kutujulisha.
Ninaondoaje nakala ya video yangu kwenye mfumo mwingine?

Endapo utakuta video yako ya YouTube kwenye mfumo mwingine bila ruhusa yako, utapaswa kufuata mchakato wa mfumo huo ili kuomba video iondolewe. YouTube haiwezi kuomba video iondolewe kwa niaba yako.

Tovuti nyingi zinazowapatia watayarishi ruhusa ya kupakia video, hutegemea kanuni inayotoa ulinzi dhidi ya Sheria ya Milenia ya Hakimilki Dijitali (DMCA). Zikipokea ombi sahihi na kamili la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, zinapaswa kuondoa maudhui hayo. Kuna baadhi ya hali zisizofuata kanuni, lakini ikiwa una uhakika kwamba nakala ya kazi yako haitimizi vigezo vya hali zisizofuata kanuni za hakimiliki, kama vile matumizi ya haki au matumizi yasiyo ya biashara, unaweza kuomba video iondolewe.

Ili ufahamu vitu unavyohitaji kuweka kwenye ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, kagua mahitaji ya Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali, DMCA, ya ombi la kuondolewa kwa video.

Tovuti nyingi zinahitaji kiungo cha URL mahususi ya video. Usipopata URL, unaweza kujaribu kubofya kulia kwenye video au kubofya muhuri wa wakati wa video ili kupata URL yake.

Tovuti zinazotegemea Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali (DMCA) lazima ziwe na maelezo ya mawasiliano ya mhudumu mahususi wa DMCA aliyeorodheshwa na Ofisi ya Hakimiliki ya Marekani na kwenye tovuti yao. Endapo utakuta video yako katika mojawapo kati ya tovuti hizi bila ruhusa yako, unaweza kutuma ombi lako la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kwenye anwani ya barua pepe inayofaa hapa chini. Ikiwa tovuti unayotafuta haijaorodheshwa hapa chini, unaweza pia kuangalia hifadhidata ya wahudumu wa Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali (DMCA) ya Ofisi ya Hakimiliki ya Marekani.

Dailymotion: notifications@dailymotion.com

Instagram: ip@instagram.com

Facebook: ip@fb.com

TikTok: copyright@tiktok.com

Twitter: copyright@twitter.com

Vimeo: dmca@vimeo.com 

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4555612344661791799
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false