Fahamu jinsi maudhui yako yanavyofikia na kushirikisha hadhira yako

Kichupo cha Maudhui katika Takwimu za YouTube kinakupa muhtasari wa jinsi hadhira yako inapata maudhui yako, maudhui ambayo hadhira yako inatazama na jinsi inavyotumia maudhui yako. Unaweza pia kuona vichupo vifuatavyo ili upate ripoti za ufikiaji na kushirikishwa: Zote, Video, Video Fupi, Mubashara na Machapisho. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuhesabu vipimo vya kushirikishwa.

Kumbuka: kichupo cha Maudhui kinapatikana tu katika kiwango cha chaneli.

Angalia video ifuatayo kutoka kwenye Chaneli ya Watayarishi wa Maudhui ya YouTube ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi maudhui yako yanavyofikia na kushirikisha hadhira.

Kichupo cha Maudhui katika Takwimu (Panga kulingana na Video, Video Fupi, Mubashara au Machapisho)

Pata vidokezo vya kichupo cha maudhui kwa watayarishi.

Angalia ripoti zako kuhusu ufikiaji na kushirikishwa

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika Menyu ya kushoto, chagua Takwimu.
  3. Kwenye menyu ya juu, chagua Maudhui.

Kumbuka: Unaweza kubofya ONA ZAIDI au HALI YA KINA ili uangalie ripoti iliyopanuliwa ya takwimu na upate data mahususi, ulinganishe utendaji na uhamishe data.

Zote

Utazamaji

Ripoti hii inakuonyesha idadi halali ya mara ambazo maudhui yako kwenye video, Video Fupi na mitiririko mubashara yametazamwa.

Maonyesho na jinsi yalivyoathiri muda wa kutazama

Ripoti hii inakuonyesha mara ambazo kijipicha kilionyeshwa kwa watazamaji kwenye YouTube (maonyesho), mara ambazo vijipicha hivyo vilichangia katika utazamaji wa video (asilimia ya mibofyo) na jinsi idadi ya waliotazama ilivyoathiri muda wa kutazama. Fahamu vidokezo zaidi vya kutumia data ya maonyesho na asilimia ya mibofyo.

Maudhui yaliyochapishwa

Ripoti hii inaonyesha idadi ya video, Video Fupi, mitiririko mubashara na machapisho uliyochapisha kwenye YouTube.

Watazamaji kwenye miundo mbalimbali

Ripoti hii inaonyesha mchanganuo na mwingiliano wa watazamaji wa maudhui yako kulingana na muundo (video, Video Fupi na mtiririko mubashara)

Jinsi watazamaji walivyopata maudhui yako

Ripoti hii inakuonyesha jinsi watazamaji wako walipata maudhui yako ndani ya vipengele vya kuvinjari, mipasho ya Video Fupi, video zinazopendekezwa, utafutaji kwenye YouTube, kurasa za chaneli na sehemu nyingine.

Wanaofuatilia

Ripoti hii inaonyesha idadi ya wanaofuatilia uliyopata kutokana na kila aina ya maudhui: video, Video Fupi, mitiririko mubashara, machapisho na mengineyo. "Mengineyo" yanajumuisha usajili kutoka utafutaji kwenye YouTube na ukurasa wa chaneli yako. Maelezo haya yanakusaidia kufahamu ni maudhui yapi yamefanya vizuri katika kuwafanya watazamaji kuwa wafuatiliaji.

Video

Kadi ya vipimo muhimu

Kadi hii inakupa taswira ya muhtasari wa utazamaji, wastani wa kipindi cha kutazama, maonyesho na asilimia ya mibofyo ya maonyesho.

Matukio makuu ya muda wa kutazama

Ripoti hii huonyesha jinsi matukio mbalimbali ya video yako yalivyovutia watazamaji. Unaweza pia kutumia muda wa kawaida wa kutazama kulinganisha video zako 10 za hivi majuzi zenye urefu sawa.

Jinsi watazamaji wanavyopata video zako

Ripoti hii inakuonyesha jinsi watazamaji wako walivyopata video zako katika utafutaji kwenye YouTube, vipengele vya kuvinjari, video zinazopendekezwa, tovuti za nje, kurasa za chaneli na sehemu nyingine.

Video maarufu

Ripoti hii inaangazia video zako maarufu zaidi.

Video Fupi

Kadi ya vipimo muhimu

Ripoti hii inakupa taswira ya muhtasari wa utazamaji, kupendwa na wanaofuatilia chaneli yako.

Jinsi watazamaji wanavyopata Video zako Fupi

Ripoti hii inakuonyesha jinsi watazamaji wako walivyopata Video zako Fupi katika mipasho ya Video Fupi, utafutaji kwenye YouTube, kurasa za chaneli, vipengele vya kuvinjari, tovuti za nje na sehemu nyinginezo.

Inaonyeshwa kwenye mipasho

Mara ambazo Video zako Fupi zilionyeshwa kwenye mipasho ya Video Fupi.

Waliotazama (ikilinganishwa na ambao hawakutazama)

Asilimia ya jumla ya watazamaji waliotazama Video zako Fupi ikilinganishwa na asilimia ya ambao hawakutazama.

Video Fupi Maarufu

Ripoti hii inaangazia Video zako Fupi zilizo maarufu zaidi.

Mseto maarufu

Ripoti hii inaonyesha taswira ya muhtasari wa utazamaji wa miseto, jumla ya miseto na maudhui maarufu ya miseto.

Mubashara

Kadi ya vipimo muhimu

Kadi hii inakupa taswira ya muhtasari wa utazamaji, wastani wa kipindi cha kutazama, maonyesho na asilimia ya mibofyo ya maonyesho.

Jinsi watazamaji wanavyopata mitiririko yako mubashara

Ripoti hii inakuonyesha jinsi watazamaji wako walivyopata mitiririko yako mubashara katika vipengele vya kuvinjari, utafutaji kwenye YouTube, video zinazopendekezwa, tovuti za moja kwa moja au zisizojulikana, kurasa za chaneli na sehemu nyingine.

Mitiririko maarufu ya moja kwa moja

Ripoti hii inaangazia mitiririko yako maarufu mubashara. Unaweza kutumia ripoti ya takwimu iliyopanuliwa ili kuangalia vipimo zaidi, kama vile utazamaji na maonyesho.

Machapisho

Maonyesho

Ripoti hii inakuonyesha mara ambazo chapisho lako lilionyeshwa kwa watazamaji.

Alama za imenipendeza

Ripoti hii inaonyesha mara ambazo watazamaji walipendezwa na machapisho yako ya Jumuiya.

Wanaofuatilia

Ripoti hii inaonyesha idadi ya wafuatiliaji uliowapata kutokana na machapisho ya Jumuiya.

Machapisho maarufu

Ripoti hii inaangazia machapisho yako maarufu zaidi kulingana na mara za kupendwa au kura.

Orodha

Kadi ya orodha maarufu

Ripoti hii inaangazia orodha zako maarufu zaidi na inakusaidia kuzilinganisha. Hapa, unaweza kufikia takwimu za kila orodha. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kufikia takwimu za orodha yako.

Fahamu aina za vyanzo vya watazamaji

Chanzo cha watazamaji kwenye video zako kinaweza kuwa ndani ya YouTube au kutoka vyanzo vya nje. Unaweza kuona vyanzo vyote viwili kwenye ripoti ya Jinsi watazamaji hupata maudhui yako (au video, Video Fupi, Mitiririko Mubashara).

Watazamaji kutoka ndani ya YouTube
Vipengele vya kuvinjari Watazamaji kutokana na ukurasa wa Kwanza, wanaokufuatilia, Tazama Baadaye, Zinazovuma/Gundua na vipengele vingine vya kuvinjari.
Kurasa za chaneli Watazamaji kutokana na chaneli yako ya YouTube au chaneli nyingine za YouTube.
Kadi za kampeni Watazamaji kutokana na kadi za kampeni ya mmiliki wa maudhui.
Skrini za mwisho Watazamaji kutokana na skrini za mwisho za mtayarishi.
Video Fupi Watazamaji kutoka hali ya mtazamo wa wima wa Video Fupi.
Arifa Watazamaji kutokana na arifa na barua pepe zilizotumwa kwa wanaokufuatilia.
  Arifa kwa wafuatiliaji waliowasha kengele Watazamaji kutokana na arifa zinazotumwa kwa wanaokufuatilia waliowasha "Arifa zote" kwenye chaneli yako na arifa za YouTube kwenye vifaa vyao.
  Arifa zingine za programu Watazamaji kutokana na arifa zilizowekewa mapendeleo, arifa za barua pepe, Kikasha na muhtasari.
Vipengele vingine vya YouTube Watazamaji kutoka ndani ya YouTube ambao hawajabainishwa katika aina nyingine yoyote.
Orodha

Watazamaji kutokana na orodha yoyote iliyojumuisha mojawapo ya video zako. Orodha hizi zinaweza kuwa zako au za mtayarishi mwingine. Takwimu hizi pia zinajumuisha orodha za watumiaji za "Video Ulizopenda" na "Video Pendwa".

Video ya mseto Watazamaji kutoka miseto inayoonekana ya maudhui yako.
Kurasa za sauti Watazamaji kutokana na ukurasa ulioshirikiwa wa matokeo ya sauti unaopatikana katika hali ya mtazamo wa wima wa Video Fupi.
Video zilizopendekezwa Watazamaji kutokana na mapendekezo yanayoonekana karibu na au baada ya video zingine na kutokana na viungo vilivyo katika maelezo ya video. Unaweza kuona video mahususi kwenye kadi ya “Chanzo cha watazamaji: Video zilizopendekezwa” katika kichupo cha Ufikiaji.
Kadi za video Watazamaji wanaotokana na kadi katika video nyingine.
Utangazaji kwenye YouTube

Iwapo video yako imetumika kama tangazo kwenye YouTube, utaona “Utangazaji kwenye YouTube” kama chanzo cha watazamaji.

Utazamaji kutokana na matangazo yanayoweza kurukwa yenye urefu wa zaidi ya sekunde 10 huhesabiwa iwapo unaendelea kwa sekunde 30 au hadi mwisho. Matangazo yasiyoweza kurukwa hayatimizi vigezo vya kujumuishwa kwenye Takwimu za YouTube za mara za kutazamwa.

Utafutaji kwenye YouTube Watazamaji kutokana na matokeo ya utafutaji kwenye YouTube. Unaweza kuona hoja mahususi za utafutaji kwenye kadi ya “Chanzo cha watazamaji: Utafutaji kwenye YouTube” wa kichupo cha Ufikiaji.
Kurasa za bidhaa Watazamaji kutokana na kurasa za bidhaa za YouTube.
Watazamaji kutokana na vyanzo vya nje
Vyanzo vya nje Watazamaji kutokana na tovuti na programu ambako video yako ya YouTube imepachikwa au kuunganishwa. Unaweza kuona tovuti na vyanzo mahususi vya nje kwenye kadi ya “Chanzo cha watazamaji: Nje” katika kichupo cha Ufikiaji.
Vyanzo vya moja kwa moja au visivyojulikana Watazamaji kutokana na URL inayowekwa moja kwa moja, alamisho, watazamaji walioondoka kwenye akaunti na programu zisizobainishwa.

Vipimo unavyopaswa kujua

Maonyesho

Mara ambazo vijipicha vyako vilionyeshwa kwa watazamaji kwenye YouTube kupitia maonyesho yaliyohesabiwa.

Asilimia ya mibofyo kwenye maonyesho

Mara ambazo watazamaji walitazama video baada ya kuona kijipicha.

Inaonyeshwa kwenye mipasho Mara ambazo Video yako fupi inaonyeshwa kwenye Mipasho ya Video Fupi.
Waliotazama (ikilinganishwa na ambao hawakutazama) Asilimia ya mara ambazo watazamaji walitazama Video zako Fupi ikilinganishwa na mara ambazo hawakutazama.

Watazamaji wa kipekee

Makadirio ya idadi ya watazamaji waliotazama maudhui yako katika kipindi ulichochagua.

Wastani wa kipindi cha kutazama

Makadirio ya wastani wa dakika zilizotazamwa kwa kila tukio la kutazama katika kipindi na video uliyochagua.

Wastani wa asilimia iliyotazamwa

Asilimia wastani ya video ambayo hadhira yako hutazama kila mara wanapotazama.

Muda wa kutazama (saa)

Muda waliotumia watazamaji kutazama video yako.

Mara ambazo chapisho limependwa Mara ambazo chapisho lako limependwa.
Kiwango cha kupendwa kwa chapisho Asilimia ya watazamaji waliopenda chapisho lako.
Idadi ya utazamaji kutoka kwenye orodha Mara za kutazamwa kwa video kutoka kwa watazamaji wanaotazama orodha hiyo. Hiki ni kipimo sawa kinachopatikana kwenye ukurasa wa nje wa orodha ya hadharani.
Jumla ya mara za kutazamwa Jumla ya mara za kutazamwa kwa video zote katika orodha, bila kujali iwapo zinatoka kwenye orodha au kwingineko. Hii hukokotolewa tu kwa video ulizomiliki katika orodha.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6624117286402647314
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false