Arifa

If you’re reaching out about an error message or a blank screen in your Channel Analytics in YouTube Studio, we are aware and working on a fix. You can follow along here for updates.  Our teams are currently experiencing high support volumes. Please expect longer than usual wait times for responses to questions from email, chat, and @TeamYouTube on Twitter. 

Kukata rufaa dhidi ya dai la Content ID

Iwapo ulipinga dai la Content ID, lakini dai hilo likarejeshwa, bado unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu. Iwapo dai la Content ID lilizuia video yako, unaweza kuruka hatua ya awali ya kupinga dai na uanze mchakato wa kukata rufaa.

Ukikata rufaa dhidi ya dai la Content ID, mtu aliyedai video yako (mlalamikaji) ataarifiwa na ana siku 7 za kujibu.

 

Kabla ya kukata rufaa

Unaweza kuangalia iwapo unatimiza masharti ya kukata rufaa kwenye ukurasa wa vipengele vya chaneli yako. Iwapo hujatimiza masharti, unaweza kukamilisha uthibitishaji wa mara moja kabla ya kukata rufaa.

Kumbuka kuwa unapaswa tu kukata rufaa kama una uhakika kuwa una haki zinazofaa za kutumia maudhui yanayodaiwa. Matumizi mabaya ya mara kwa mara au hasidi ya mchakato wa kukata rufaa yanaweza kusababisha upoteze haki ya kukata rufaa au upokee adhabu nyingine kwenye video au chaneli yako.

Kukata rufaa dhidi ya dai lililorejeshwa

 Iwapo ulipinga dai la Content ID na likakataliwa, dai hilo hurejeshwa kwenye video yako. Unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu. Ili ukate rufaa dhidi ya dai lililorejeshwa:

Programu ya Studio ya YouTube kwenye Android

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Kwenye Menyu ya chini, gusa Maudhui .
  3. Chagua video iliyo na kizuizi, kisha uguse kizuizi hicho.
    • Ili upate video kwa urahisi zaidi, unaweza kubofya upau wa vichujiokisha Hakimiliki.
  4. Gusa Kagua matatizo.
  5. Gusa dai husika.
  6. Weka sababu yako ya kukata rufaa kisha ubofye Tuma.

Kuelekeza kwa wasimamizi wakuu ili ukate rufaa

Iwapo ulipata dai la Content ID ambalo lilizuia video yako, unaweza kuruka hatua ya awali ya kupinga dai na uanze mchakato wa rufaa. Chaguo hili huitwa “Ripoti ili Ukate Rufaa”.

Kwa madai ya uzuiaji ambako una uhakika kuwa si halali, chaguo la Elekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa linaweza kukupa suluhisho la haraka zaidi kwenye mchakato wa kupinga dai kwa jumla, kwa vile walalamikaji hupewa siku 7 za kujibu rufaa. Inamaanisha pia kuwa video yako itaweza kuonekana kwenye YouTube haraka iwezekanavyo.

Kumbuka kuwa iwapo mlalamikaji atakataa rufaa, anaweza kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Iwapo ombi hilo la kuondoa video ni halali, video yako itaondolewa kwenye YouTube na chaneli yako itapokea onyo la hakimiliki. Hata hivyo, kama bado una uhakika kuwa una haki zinazofaa za kutumia maudhui yanayodaiwa, bado unaweza kuwasilisha arifa ya kukanusha.

Kuteua chaguo la Elekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa:

Programu ya Studio ya YouTube kwenye Android

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Kwenye Menyu ya chini, gusa Maudhui .
  3. Chagua video iliyo na kizuizi, kisha uguse kizuizi hicho.
    • Ili upate video kwa urahisi zaidi, unaweza kubofya upau wa vichujiokisha Hakimiliki.
  4. Gusa Kagua matatizo.
  5. Gusa dai husika.
  6. Gusa Pinga dai. Kwenye ukurasa wa Chaguo, teua chaguo la Elekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa.

Baada ya kukata rufaa

Baada ya kukata rufaa, mlalamishi ana siku 7 za kujibu.

Hatua ambazo mlalamikaji anaweza kuchukua

Iwapo video yako imeondolewa kwenye YouTube, lakini bado unaamini kuwa una haki zote zinazofaa za kutumia maudhui yanayodaiwa, unaweza kuwasilisha arifa ya kukanusha.

Jinsi ya kuondoa rufaa

Iwapo utabadilisha nia yako, unaweza kuondoa rufaa yako baada ya kuiwasilisha. Ili uondoe rufaa:

Programu ya Studio ya YouTube kwenye Android

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Kwenye Menyu ya chini, gusa Maudhui .
  3. Chagua video iliyo na kizuizi, kisha uguse kizuizi hicho.
    • Ili upate video kwa urahisi zaidi, unaweza kubofya upau wa vichujiokisha Hakimiliki.
  4. Gusa Kagua matatizo.
  5. Gusa dai husika kisha uguse ondoa rufaa.
Kumbuka: Ukiondoa rufaa, hutaweza tena kukata rufaa dhidi ya dai hilo.
Pata maelezo zaidi kuhusu mchakato wa kukata rufaa katika sura ya video hii ya "Mchakato wa Kukata Rufaa dhidi ya Content ID":

Madai ya Content ID na Mchakato wa Kupinga Madai: Kudhibiti na Kuchukua Hatua Dhidi ya Madai katika Studio

 

Maswali Yanayoulizwa Sana

Kuna tofuati gani kati ya chaguo za kupinga dai na Elekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa?

Chaguo la awali la kupinga dai linaweza kuchukua hadi siku 30 kabla ya mlalamikaji kujibu mzozo wako. Akikataa dai lako, unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wake. Mlalamikaji ana siku 7 za kujibu rufaa yako.

Chaguo la Kuelekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa linapatikana tu kwa madai ya Content ID ambayo huzuia video. Chaguo hili huruka hatua ya kwanza ya kupinga dai, ambayo inampa mlalamikaji siku 30 za kujibu na huanzisha mchakato wa kukata rufaa. Mlalamikaji ana siku 7 za kujibu, kwa hivyo mchakato huu unaweza kusuluhishwa haraka zaidi.

Iwapo mlalamikaji atakataa rufaa yako, anaweza kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Iwapo ombi la kuondoa video ni halali, video yako itaondolewa kwenye YouTube na chaneli yako itapokea onyo la hakimilki. Kumbuka kuwa bado unaweza kutuma arifa ya kukanusha kama una uhakika kuwa ombi la kuondoa video si sahihi.

Ninapaswa kuteua chaguo la elekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa wakati gani?

Iwapo ulipata dai la Content ID ambalo lilizuia video yako, unaweza kuteua chaguo la Elekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa. Uamuzi wa kuelekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa unaweza kuwa bora iwapo una uhakika katika haki yako ya kutumia maudhui hayo na unatafuta suluhu ya haraka katika mchakato wa kupinga dai. 

Kumbuka kuwa iwapo mlalamikaji atakataa rufaa, ana chaguo la kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Iwapo ombi hilo la kuondoa video ni sahihi, video yako itaondolewa kwenye YouTube na chaneli yako itapokea onyo la hakimiliki. Hata hivyo, kama bado una uhakika kuwa una haki zinazofaa za kutumia maudhui yanayodaiwa, bado unaweza kuwasilisha arifa ya kukanusha.

Hakika, ni wewe utaamua wakati wa kuelekeza kwa wasimamizi wakuu ili kukata rufaa. Iwapo huna uhakika kuhusu hatua za kuchukua, unaweza kutafuta ushauri wa kisheria.

Ni kwa nini chaguo la Elekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa linapatikana tu kwa madai ya Content ID ambayo yanazuia video yangu?

Video zinazopokea madai ya uzuiaji haziwezi kuonekana kwenye YouTube, iwe kimataifa au katika nchi au maeneo fulani (kulingana na sera ya mlalamikaji). Kwa madai ya uzuiaji ambayo una uhakika kuwa si sahihi, kuteua chaguo la Elekeza kwa wasimamizi wakuu ili Ukate Rufaa kunaweza kusuluhisha dai hilo haraka. Hii inamaanisha kuwa video yako itaweza kuonekana kwenye YouTube haraka iwezekanavyo.

Kwa madai mengine ya Content ID (kuchuma pesa na kufuatilia) video yako itaendelea kuonyeshwa kwenye YouTube, licha ya dai la Content ID. Kumbuka kuwa kwa madai ya kuchuma mapato, wakati wewe na mlalamikaji mnajaribu kuchuma mapato kwenye video inayodaiwa, mapato ya video hiyo yataendelea kuchumwa huku mchakato wa kupinga dai ukiendelea. Baada ya mzozo kusuluhishwa, mapato hayo yatalipwa kwa mhusika atakayefaa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi uchumaji wa mapato hufanya kazi wakati wa mzozo wa Content ID.
Je, ninaweza kuondoa rufaa baada ya kuiwasilisha?
Ndiyo, unaweza kuondoa rufaa baada ya kuiwasilisha kwa kufuata hatua hizi. Kumbuka kuwa baada ya kuondoa rufaa, hutaweza tena kukata rufaa dhidi ya dai hilo.
Ninaweza kufanya nini iwapo rufaa yangu imekataliwa na video yangu imeondolewa?

Iwapo una uhakika kuwa rufaa yako ilikataliwa kimakosa au maudhui hayakutambuliwa vizuri, ikiwa ni pamoja na hali za matumizi ya haki, unaweza kuwasilisha arifa ya kukanusha. Arifa ya kukanusha ni ombi la kisheria linaloiambia YouTube irejeshe video ambayo imeondolewa kimakosa kwa kukiuka hakimiliki.

Chaguo nyingine zinajumuisha:

Je, iwapo nitakata rufaa za madai mengi kwenye video kwa wakati mmoja, hali hiyo inaweza kusababisha maonyo mengi ya hakimiliki?
Video inaweza kupata zaidi ya dai moja la Content ID au ombi moja la kuiondoa, lakini inaweza kupata onyo moja tu la hakimiliki kwa wakati mmoja.
 

Maelezo zaidi

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
210489813814995686
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false