Omba kurejeshewa pesa kwa ajili ya uanachama wa YouTube Premium
Sera za kurejesha pesa za YouTube Premium na Music Premium
Unaweza kukata uanachama wa YouTube unaolipiwa wakati wowote. Kukata kutazima usasishaji otomatiki wa uanachama wako. Baada ya kukata, hutatozwa tena na manufaa yako yataendelea hadi mwisho wa kipindi cha kutozwa. Hutarejeshewa pesa kwa kipindi hiki kati ya unapokata na wakati uanachama wako unapokwisha.
Baada ya ombi la kurejeshewa pesa kuchakatwa, hutaweza tena kutumia manufaa yako. Pia, hutatozwa tena isipokuwa unapoamua kusasisha uanachama wako.
Ikiwa video na vipengele vinavyohusiana na ununuzi wako wa YouTube havifanyi kazi, huenda ukatimiza masharti ya kurejeshewa pesa. Ikiwa ombi la kurejeshewa pesa limekubalika, tutaondoa ufikiaji wa uanachama wako wa Premium na pesa zako zitarejeshwa ndani ya muda wa kurejesha pesa ulioorodheshwa hapa.
- Kwa kutumia Malipo kupitia Google Play, hutaweza kusitisha uanachama wako. Badala yake, unaweza kukata uanachama wako na ujisajili tena wakati wowote. Ili uelewe jinsi unavyotozwa, nenda kwenye pay.google.com. Ikiwa ungependa kukata uanachama wako wa YouTube unaolipiwa haraka na urejeshewe pesa, wasiliana na timu ya usaidizi ya YouTube.
-
Urejeshaji pesa haupatikani kwa mipango ya kulipia mapema iliyotumika kiasi. Iwapo ulinunua Mpango wa Mwaka au mpango mwingine wa kulipia mapema na ungependa kubadilisha ili utumie mpango wa kulipia kila mwezi unaojirudia, unaweza kufanya hivyo kwa kufuata hatua hizi.
- Ununuzi wa YouTube uliofanywa kupitia duka la Apple unahitaji uidhinishaji kutoka Apple na unategemea sera za kurejesha pesa za Apple. Wasiliana na timu ya usaidizi ya Apple ili utume ombi la kurejeshewa pesa za uanachama wako.