Fahamu jinsi ya kutumia kurasa za chaneli ya YouTube

Angalia kichupo cha Ukurasa wa kwanza wa chaneli ya mtayarishi ili upate video na orodha zake za kucheza alizopakia. Ukiwa kwenye kichupo cha Ukurasa wa kwanza wa chaneli, unaweza pia kujisajili kwenye chaneli, uwe mwanachama katika chaneli na kuvinjari na kununua bidhaa rasmi za mtayarishi.

Kutafuta kituo mahususi

  1. Tafuta kwa kuweka aina, neno muhimu au jina la mtayarishi kwenye upau wa kutafutia .
  2. Unaweza kutumia kichujio kwenye matokeo yako ya utafutaji ili uonyeshe vituo husika.
  3. Bofya kwenye jina la kituo karibu na aikoni ya kituo.

Tafuta kituo kulingana na aina au neno muhimu

  1. Tafuta kwa kuweka aina au neno muhimu kwenye upau wa kutafutia .
  2. Unaweza kutumia kichujio kwenye matokeo yako ya utafutaji ili kuonyesha vituo vinavyohusiana na utafutaji wako.
  3. Bofya kwenye video ambayo ungependa kuiangalia.
  4. Bofya jina la chaneli ili ufungue ukurasa wa chaneli.

Fungua kituo ulichojisajili

  1. Bofya kwenye Usajili .
  2. Bofya kwenye jina la kituo cha mtayarishi ili ufungue kituo chake.

Kufungua kituo kutoka kwenye video

Ukiwa kwenye ukurasa wa video, bofya jina la kituo chini ya maelezo ili ufungue kituo cha mtayarishi.

Kufuatilia na Kujiondoa katika chaneli ya YouTube

Jisajili katika kituo ili uone maudhui zaidi kutoka kwa mtayarishi. Video zozote mpya zinazochapishwa kwenye chaneli unayofuatilia zitaonekana kwenye Mpasho wa chaneli unazofuatilia.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kujisajili na kujiondoa kwenye kituo cha YouTube.

Kutazama aina mbalimbali za video

Ukifungua kichupo cha Ukurasa wa kwanza wa chaneli ya mtayarishi, unaweza kupata video zake mpya, maudhui yanayoangaziwa, sehemu ya “Kwa ajili yako” na aina nyingine za video.

Aina za video

Ili upate aina tofauti za video kwenye chaneli ya mtayarishi, chagua aina ya video katika sehemu ya juu ya ukurasa. Vichupo vinavyoonyeshwa hapa vinatofautiana kulingana na chaneli na aina za video zinazotayarishwa na chaneli. Vichupo hivi vinaweza kujumuisha:

  • Video
  • Video Fupi
  • Mitiririko Mubashara

Sehemu ya 'Kwa ajili yako'

Sehemu ya “Kwa ajili yako” inakupa hali ya utumiaji inayokufaa unapotembelea kichupo cha Ukurasa wa kwanza wa chaneli ya mtayarishi. Sehemu hii huonyesha mseto wa maudhui yaliyowekewa mapendeleo kulingana na historia yako ya video ulizotazama.

Ukizima kipengele cha Historia ya Video Ulizotazama kwenye YouTube, vipengele vya YouTube vinavyotegemea historia yako ya video ulizotazama ili kukupa mapendekezo ya video huondolewa. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti historia yako ya video ulizotazama.

Kuwa mwanachama katika chaneli

Jiunge na uanachama katika chaneli ili upate manufaa ya wanachama pekee kama vile beji, emoji na bidhaa nyingine kwa kulipia kila mwezi.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwa mwanachama wa kituo kwenye YouTube.

Kununua bidhaa rasmi za mtayarishi

Rafu ya bidhaa huwaruhusu watayarishi wanaoshiriki kushiriki bidhaa zao rasmi zenye chapa kwenye YouTube. Unaweza kuona rafu ya bidhaa kwenye kurasa za video za vituo vinavyoshiriki, lakini inaweza isionekane kwenye kurasa zote za video.

Pata maelezo zaidi kuhusu kuvinjari na kununua bidhaa rasmi za mtayarishi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3181706783435897556
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false