AdSense katika YouTube

Tunakuletea toleo jipya la beta linaloleta maelezo ya malipo kwenye kichupo cha 'Chuma mapato' cha programu ya vifaa vya mkononi ya Studio ya YouTube. Toleo hili la beta litawapatia watayarishi wanaostahiki mbinu rahisi ya kuelewa jinsi mapato yao yanavyobadilika kuwa malipo. Kwa kutumia toleo hili la beta, unaweza kuangalia:
  • Hatua ulizopiga kuelekea malipo yako yanayofuata
  • Historia yako ya malipo ya miezi 12 iliyopita ikijumuisha tarehe, kiasi ulicholipa na uainishaji wa malipo
Pata maelezo zaidi kwenye chapisho letu la jukwaa .

Kutokana na vita vinavyoendelea Ukraini, tutasimamisha kwa muda kuwapatia matangazo ya Google na YouTube watumiaji walio nchini Urusi. Pata maelezo zaidi.

AdSense katika YouTube ni mpango wa Google unaotumika kuwalipa watayarishi walio kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube. Ili uanze kupokea malipo kwenye YouTube, weka mipangilio ya akaunti ya AdSense katika YouTube kwenye Studio ya YouTube. Tumia ukurasa huu kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia AdSense katika YouTube ukiwa mtayarishi wa YouTube.

AdSense kwa Watayarishi wa YouTube

 

 

Kuanza kutumia AdSense katika YouTube

Kumbuka, unalipwa mapato yako kwenye YouTube kupitia akaunti yako ya AdSense katika YouTube. Fuata hatua zilizo hapa chini ili uanze kutumia AdSense katika YouTube.

Kuweka mipangilio ya akaunti

Kwanza, weka mipangilio ya akaunti ya AdSense katika YouTube kwenye Studio ya YouTube ikiwa bado hujafanya hivyo. Tumeandaa maagizo ya kina na kushughulikia baadhi ya matatizo ya kawaida kuhusiana na kuweka mipangilio ya akaunti ya AdSense katika YouTube: 

Ni akaunti moja pekee ya AdSense au AdSense katika YouTube yenye jina sawa la anayelipwa ndiyo inaruhusiwa kwa mujibu wa Sheria na Masharti ya AdSense au Sheria na Masharti ya AdSense katika YouTube, kama yanavyotumika. Kwa hivyo, hakikisha kuwa huna akaunti nyingine unapounganisha chaneli yako ya YouTube. Ikiwa ungependa kubadilisha akaunti ya AdSense au ya AdSense katika YouTube iliyounganishwa na chaneli yako, fuata hatua hizi.

Kuthibitisha taarifa zako binafsi

Ukishaweka mipangilio, ni wakati wa kuthibitisha taarifa zako binafsi. Wakati mapato yako yanapita kima cha chini cha kuthibitishwa anwani katika akaunti yako ya malipo kwenye YouTube, tutakutumia Namba Binafsi ya Kuthibitisha (PIN) kwenye anwani yako ya mahali halisi. Unahitaji kuweka PIN hii kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube ili uthibitishe anwani yako kabla uweze kupokea malipo. Pata maelezo zaidi hapa:

Pia, kulingana na mahali ulipo, huenda tukahitaji kuthibitisha utambulisho wako kwa kutumia taarifa kama vile jina, anwani au tarehe yako ya kuzaliwa. Iwapo utahitajika kufanya hivyo, kwa kawaida hutaombwa kuthibitisha anwani yako hadi uthibitishe utambulisho wako. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufanya hivyo hapa:

Kuwasilisha taarifa zako za kodi

Baada ya kutoa taarifa zako binafsi, utahitaji kuwasilisha maelezo yako ya kodi ili uendelee. Google huzuilia kodi za Marekani kwa mapato unayochuma kutoka kwa watazamaji nchini Marekani, kwa hivyo maelezo haya ni muhimu kutolewa ili kubaini kiwango chako sahihi cha kodi ya zuio. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia taarifa zako za kodi na zaidi hapa:

Weka njia ya kulipa

Baada ya taarifa zako kuthibitishwa, utahitaji kupita masharti ya kima cha chini cha kuchagua njia ya malipo kwenye akaunti yako ya malipo ya YouTube. Hiki ndicho kima cha chini zaidi ambacho tunaweza kukulipa, kwa hivyo ukishafikisha kiasi hicho katika akaunti yako ya malipo ya YouTube, utaombwa uchague njia ya kulipa. Pata chaguo na hatua zote hapa:

Kupokea malipo

Mapato yako yaliyojumlishwa kwenye YouTube kila mwezi yatawekwa kwenye salio la akaunti ya malipo ya YouTube kwenye AdSense katika YouTube kati ya tarehe 7 na 12 ya mwezi utakaofuata. Yakishawekwa, unaweza kuona maelezo ya malipo (kama vile makato ya kodi yanayotumika) katika ukurasa wa Miamala:

  1. Ingia katika akaunti ya AdSense katika YouTube.
  2. Katika Menyu ya kushoto, chagua Maelezo ya malipo chini ya Malipo.
  3. Bofya Angalia miamala katika sehemu ya Miamala ya ukurasa.

Unapaswa upokee malipo kufikia tarehe 21 au 26 ya kila mwezi iwapo salio lako linatimiza kima cha malipo na hamna matukio yoyote ya uahirishaji wa malipo kwenye akaunti yako.

Mfano: Ikiwa kima cha malipo ya YouTube ni $100 na ulifikia kima hicho mnamo Juni, basi tutakutumia malipo kufikia tarehe 26 Julai, ama kabla ya tarehe hii.

Akaunti ya malipo ya YouTube na AdSense katika YouTube

YouTube ina akaunti maalum ya AdSense katika YouTube, inayowawezesha watayarishi kufikia kwa haraka mapato yao yaliyokamilika ya YouTube kwenye AdSense katika YouTube.

Malipo ya mapato ya YouTube hutenganishwa katika akaunti yake ya malipo. Hii inamaanisha kuwa akaunti za malipo za YouTube na AdSense zina viwango tofauti vya kima cha malipo. Ni muhimu ufahamu jambo hili iwapo unatumia AdSense kupokea malipo kutoka huduma nyingine kando na YouTube, kwa kuwa hali hii inaweza kuathiri wakati wa malipo.

Maelezo yoyote ya mapato ya YouTube yaliyolipwa kabla ya mwaka 2022 na mapato yoyote mengine ya AdSense yataendelea kuhusishwa na akaunti yako ya malipo ya AdSense. Malipo yoyote ya YouTube ambayo hayajalipwa yatahamishiwa kwenye akaunti ya Malipo ya YouTube.

Maswali yanayoulizwa sana

Itakuwaje iwapo nitatumia AdSense kupokea malipo kutoka kwenye huduma nyingine mbali na YouTube?

Iwapo wewe ni mchapishaji wa AdSense uliye na mapato mengine mbali na ya YouTube, utaweza kudhibiti na kuona mapato yako ya YouTube katika akaunti tofauti ya mapato inayoweza kufikiwa kupitia ukurasa wa Malipo.

Kumbuka kuwa akaunti za malipo za YouTube na AdSense zitahitaji kufikisha kima cha malipo kilichobainishwa ili upokee malipo. Huenda hali hii ikaathiri muda wa kupokea malipo yako.

Ninawezaje kuangalia mapato yangu ya mwisho ya YouTube kwenye AdSense?

Unaweza kupata mapato yako ya YouTube kwenye akaunti yake ya malipo kwa kufuata hatua zifuatazo:

  1. Ingia katika akaunti yako ya AdSense.
  2. Bofya Malipo kisha Maelezo ya malipo.
  3. Bofya menyu kunjuzi ya akaunti za malipo.
  4. Chagua Akaunti ya Malipo ya YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9544213215575357353
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false