Akaunti yako ya AdSense katika YouTube imefungwa.

Huenda akaunti yako ya AdSense katika YouTube imefungwa ikiwa hujakamilisha kuiwekea mipangilio au iwapo haijapokea shughuli au mapato yoyote kutokana na matangazo kwa miezi 6. Ili uitumie tena, utapaswa kufungua upya akaunti yako ya AdSense katika YouTube kwa kuiunganisha na chaneli yako. Iwapo huhitaji tena akaunti yako ya AdSense katika YouTube, unaweza kuisimamisha.
 
Bado unaweza kuingia katika akaunti yako ya AdSense katika YouTube hata ikiwa imefungwa. Ili ufungue upya akaunti yako, utaombwa uthibitishe tena namba yako ya simu. Pia tunapendekeza uhakikishe kuwa anwani yako imesasishwa. Iwapo chaneli yako imetimiza masharti ya kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube au kupokea malipo kutoka YouTube, unaweza kufungua upya akaunti hiyo ya AdSense katika YouTube au ufungue nyingine mpya.
Kutokana na hali ya hivi majuzi ya kusimamishwa kwa mifumo ya utangazaji ya Google nchini Urusi, michakato ya kufungua akaunti za AdSense katika YouTube nchini Urusi na AdSense imesitishwa. Pata maelezo zaidi.

Hatua za kufungua upya akaunti yako ya AdSense katika YouTube

  1. Unganisha akaunti yako ya AdSense katika YouTube kwenye chaneli yako.
  2. Ingia katika akaunti ya AdSense katika YouTube.
  3. Thibitisha namba yako ya simu.

Kwa nini akaunti yako ya AdSense katika YouTube ilifungwa

Kutokamilika kwa hatua za Kufungua Akaunti Mpya

Akaunti za AdSense katika YouTube hufungwa wakati hatua za kufungua akaunti yako na kuiunganisha kwenye chaneli yako ya YouTube hazijakamilika. Iwapo hujakamilisha hatua za kufungua akaunti yako ya AdSense katika YouTube kwa muda fulani, tutaanza kukuarifu.

Baada ya miezi 5 ya kutokamilisha hatua za kufungua akaunti mpya

Utapokea barua pepe kutoka AdSense katika YouTube inayokuarifu kwamba akaunti yako itafungwa usipokamilisha hatua zilizoainishwa katika Makala haya ya Kituo cha Usaidizi.

Baada ya miezi 6 ya kutokamilisha hatua za kufungua akaunti mpya

Akaunti yako ya AdSense katika YouTube itafungwa.

Kutotumika

Akaunti za AdSense katika YouTube hufungwa kwa sababu ya kutotumika. Iwapo akaunti iliyounganishwa na chaneli yako haitumiki kwa muda fulani, tutaanza kukuarifu. Iwapo akaunti yako ya AdSense katika YouTube ina shughuli au mapato kutokana na matangazo, haitafungwa.

Baada ya kuacha kuitumia kwa miezi 5

  • Utapokea barua pepe kutoka AdSense katika YouTube inayokuarifu kwamba akaunti yako itafungwa iwapo haina shughuli au mapato kutokana na matangazo.

Baada ya kuacha kuitumia kwa miezi 6

  • Akaunti yako ya AdSense katika YouTube imefungwa.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Akaunti yangu ya AdSense katika YouTube ilizimwa ilhali bado ilikuwa na pesa ndani yake, ninawezaje kulipwa?

Ikiwa salio la akaunti yako ni zaidi ya kima cha chini cha kufunga akaunti na utatue hali ya kuahirishwa kwa malipo yoyote, huenda ukapokea salio lako la AdSense katika YouTube baada ya kufunga akaunti yako.

Nikifungua tena akaunti yangu, nitalazimika kuthibitisha anwani yangu kupitia PIN tena?

Hapana. Ikiwa umewahi kuthibitisha anwani yako kupitia PIN hapo awali, hutahitaji kuithibitisha tena. Ikiwa hujawahi kuthibitisha anwani yako kupitia PIN hapo awali, utaombwa uthibitishe anwani yako kabla ya kupokea malipo yako.

Akaunti yangu ya AdSense ilifungwa, je, hatua hii inaathiri hali ya chaneli yangu ya YouTube?

Hapana. Hali ya chaneli yako ya YouTube haiathiriwi na kufungwa kwa AdSense. Ukianza kuchuma mapato kutokana na chaneli yako na utimize masharti yote ya kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, utaweza kuunganisha akaunti ya AdSense katika YouTube ili ulipwe.

Chaneli yangu ilianza kuchuma mapato baada ya mimi kupokea barua pepe ya tahadhari, je, akaunti yangu ya AdSense katika YouTube bado itafungwa?

Hapana. akaunti yako ya AdSense katika YouTube haitafungwa tena ukianza kuchuma mapato kwenye chaneli yako ya YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2508459325763109736
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false