Tumia zana zetu za kutayarisha Video Fupi ili uunde maudhui ya kipekee unayopenda. Kuwa mbunifu na utumie chaguo zetu za kuandaa miseto ili uandae mseto wa sauti au uongeze sehemu ya video kutoka video mbalimbali kwenye YouTube.
Video Fupi zilizotayarishwa kwa kutumia maudhui mseto zinahusishwa na kazi halisi na ni fursa nzuri kwa watazamaji wapya kugundua maudhui yako!
Chanzo cha mseto wako wa sauti kinatambulishwa kwenye ukurasa wa Maktaba ya Sauti (mfano hapo juu). Gusa Sauti kwenye Kichezaji cha Video Fupi ili upate kiungo cha video halisi pamoja na Video Fupi nyingine zinazotumia sauti sawa. |
Chanzo cha video yako ya mseto kinatambulishwa katika Kichezaji cha Video Fupi kwa kiungo kinachoelekeza kwenye video husika (mfano hapo juu). |
Kutayarisha Video Fupi zenye mseto wa sauti na madoido
Jinsi ya kuweka sauti kwenye #video fupi za YouTube
Unaweza kutayarisha kwa urahisi Video zako Fupi ukitumia sauti na madoido kutoka kwenye maudhui halisi.
Kwenye kichezaji cha Video Fupi
Ili utayarishe mseto kutoka kwenye Video Fupi nyingine:
- Ingia katika programu ya YouTube kwenye simu.
- Nenda kwenye Video fupi unayotaka kuitumia kama sampuli.
- Kwenye kona ya chini kulia, gusa Sauti ili upate Video Fupi nyingine zilizotumia sauti na madoido sawa.
- Gusa TUMIA SAUTI HII ili utayarishe Video Fupi.
Kwenye ukurasa wa kutazama video
Ili utayarishe mseto wa sauti kutoka kwenye video ndefu:
- Ingia katika programu ya YouTube kwenye simu.
- Nenda kwenye video ambayo ungependa kuitumia kama sampuli.
- Kwenye kicheza video, gusa Andaa mseto Sauti .
Kwenye Chaneli Rasmi ya Msanii
Ili uandae mseto wa sauti kutoka kwenye Chaneli Rasmi ya Msanii:
- Fungua Chaneli Rasmi ya Msanii.
- Nenda kwenye sehemu ya “Sauti maarufu kutoka kwenye Video Fupi”.
- Karibu na nyimbo ambayo ungependa kutumia kama sampuli, gusa TUMIA SAUTI HII ili Utayarishe Video fupi.
Unaweza pia kugusa sauti ili uangalie video nyingine zinazotumia wimbo au uguse ili uhifadhi sauti kwenye maktaba yako.
Kutayarisha Video Fupi ukitumia kiolezo
- Ingia katika programu ya YouTube kwenye simu.
- Nenda katika Video fupi ambayo ungependa kutumia kama kiolezo.
- Gusa Andaa mseto Tumia kiolezo hiki .
- Kidokezo: Au katika Video fupi, gusa Tumia kiolezo.
- Weka klipu zako kwenye kiolezo kisha utayarishe Video yako fupi.
Kutayarisha Video Fupi ukitumia video ya mseto
Jinsi ya KUJIBU Video Fupi kwenye Video Fupi 🗣️
Kwenye kichezaji cha Video Fupi
Ili utayarishe mseto kutoka kwenye Video Fupi nyingine:
- Ingia katika programu ya YouTube kwenye simu.
- Nenda kwenye Video fupi ambayo ungependa kutumia kama sampuli.
- Gusa Andaa Mseto Kata video hii.
- Kidokezo: Ili uchague muundo tofauti, gusa Muundo.
Kwenye ukurasa wa kutazama video
Ili utayarishe mseto kutoka kwenye video ndefu:
- Ingia katika programu ya YouTube kwenye simu.
- Nenda kwenye video ambayo ungependa kuitumia kama sampuli.
- Chini ya kicheza video, gusa Mseto Kata .
- Kidokezo: Ili uchague muundo tofauti, gusa Muundo.
Kutayarisha Video Fupi ukitumia mandharinyuma za video za mseto
Skrini ya Kijani yenye Video Fupi zingine! 🟩🤳
Kwenye kichezaji cha Video Fupi
Ili utayarishe mseto kutoka kwenye Video Fupi nyingine:
- Ingia katika programu ya YouTube kwenye simu.
- Nenda kwenye Video fupi ambayo ungependa kutumia kama sampuli.
- Gusa Mseto Skrini ya kijani.
- Kidokezo: Ili uchague muundo tofauti, gusa Muundo.
Kwenye ukurasa wa kutazama video
Ili utayarishe mseto kutoka kwenye video ndefu:
- Ingia katika programu ya YouTube kwenye simu.
- Nenda kwenye video ambayo ungependa kuitumia kama sampuli.
- Kwenye kicheza video, gusa Andaa mseto Skrini ya kijani.
- Kidokezo: Ili uchague muundo tofauti, gusa Muundo.
Kutayarisha Video Fupi ukitumia Collab
Jinsi ya ✨ KUSHIRIKIANA ✨ na Video nyingine Fupi 🙌
Kwenye kichezaji cha Video Fupi
Ili uandae mseto ukitumia Collab kutoka kwenye Video fupi nyingine:
- Ingia katika programu ya YouTube kwenye simu.
- Nenda kwenye Video fupi ambayo ungependa kutumia kama sampuli.
- Gusa Mseto Collab .
Kwenye ukurasa wa kutazama video
Ili uandae mseto ukitumia Collab kutoka kwenye video ndefu:
- Ingia katika programu ya YouTube kwenye simu.
- Nenda kwenye video ambayo ungependa kuitumia kama sampuli.
- Chini ya kicheza video, gusa Mseto Collab .
Kutayarisha mseto wa video ya muziki katika Video Fupi za YouTube
Watayarishi wa YouTube wanaweza kutumia zana zetu za utayarishaji wa Video Fupi kuandaa miseto ya maudhui ya sauti na video kutokana na video za muziki kwenye YouTube. Unaweza kuandaa miseto ya maudhui ya video za muziki kwa njia kadhaa tofauti, ikiwa ni pamoja na Skrini ya Kijani, kipengele cha Kata na utayarishaji wa miseto ya sauti.
Pata maelezo zaidi hapa chini kuhusu aina za rekodi za sauti na video za muziki zinazoweza kutumika kuandaa miseto kwenye Video Fupi za YouTube.
Jinsi ya kuandaa mseto wa maudhui ya video ya muziki kwenye Video Fupi za YouTube
Unaweza kuandaa mseto kwa njia kadhaa tofauti:
- Skrini ya Kijani: tumia video ya muziki kama mandharinyuma ya Video Fupi yako. Unaweza kutumia video pekee au sauti na video kwa pamoja.
- Kata: tumia kipande cha sekunde 1 hadi 5 cha video ya muziki. Hii inajumuisha sauti na video kutoka kwenye video hiyo ya muziki.
- Mseto wa Sauti: tumia hadi sekunde 60 za sauti kutoka kwenye video ya muziki katika Video Fupi yako.
Kumbuka: Kulingana na makubaliano ya washirika na YouTube, baadhi ya video zinaweza kuruhusu tu sekunde 30 za sauti zitumike katika Video Fupi
Ili upate maelezo zaidi kuhusu vipengele vya 'Kata' na Skrini ya kijani, tazama video hizi kutoka kwenye chaneli ya Watayarishi wa Maudhui ya YouTube:
Pata maelezo zaidi kuhusu kuandaa mseto wa maudhui
Je, ninaweza kutumia maudhui gani kutayarisha Video Fupi?Unaweza kutayarisha Video Fupi kwenye YouTube kwa kutumia:
- Wimbo kutoka kwenye maktaba yetu.
- Sauti halisi katika kwenye Video Fupi na ndefu nyinginezo.
- Sehemu ya video kutoka kwenye video nyinginezo katika YouTube.
- Wimbo uliotayarishwa kwa kutumia Dream Track. Pata maelezo zaidi kuhusu Dream Track.
Huenda baadhi ya video zisipatikane kulingana na mipangilio ya faragha kwenye video hizo au mtu aliyedai umiliki wa hakimiliki. Kwa mfano, hali hii inaweza kujumuisha video za faragha na video zinazodaiwa na wengine wenye hakimiliki ambao hawajaruhusu maudhui yapatikane kwa ajili ya utengenezaji wa Video Fupi. Pia, tunaruhusu watayarishi wadhibiti uandaaji wa mseto unaotokana na video zao ndefu au wafute maudhui yao asili wakati wowote. Wachapishaji na washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube, wanaweza pia kudhibiti utayarishajii wa mseto kutokana na Video zao Fupi. Kulingana na leseni za muziki, baadhi ya miseto ya Video Fupi zinazotumia maudhui ya muziki inaweza kuzuiwa.
Kumbuka kwamba ukitumia maudhui yanayolindwa kwa hakimiliki kwenye Video zako Fupi zilizotayarishwa nje ya zana za utayarishaji za YouTube, video yako inaweza kupata Dai la Content ID au kuondolewa kutokana na ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.
Ndiyo, unaweza kuandaa mseto wa maudhui ambayo tayari yameandaliwa mseto. Unaweza kuchagua kuandaa mseto wa sauti, kujiundia kipengele chako mwenyewe cha Kukata, Kushirikiana na wengine au kutumia kipengele cha Skrini ya Kijani na wengine. Video ya chanzo na miseto yoyote inayofuata iko kwenye Kurasa viini na metadata ya Mchezaji.
Je, ninaweza kuandaa mseto wa Klipu?
Ninawezaje kufahamu mtu anapoandaa mseto kwa kutumia maudhui yangu?
Utapata arifa video yako itakapotumiwa kuandaa mseto. Arifa moja ya muhtasari hutumwa kwa siku; na hadi mara tatu kwa wiki. Hivyo ikiwa watayarishi wengi wametumia video yako kuandaa mseto katika siku moja, utapata arifa isiyozidi moja katika siku hiyo.
Je, ninawezaje kuona watazamaji niliopata kutokana na miseto inayoonekana ya maudhui yangu?
Miseto inayoonekana ya maudhui yako iliyotayarishwa na watayarishi wengine inaweza kusaidia kuleta watazamaji wapya kwenye chaneli yako.
Unaweza kuona ni mara ngapi maudhui yako yametazamwa kutokana na miseto inayoonekana kwa kuangalia ripoti zako za ufikiaji na kupanga kulingana na chanzo cha watazamaji cha “Video ya mseto”.
Video Fupi unazotayarisha zinajumuishwa kiotomatiki kutumika katika uandaaji wa Miseto kwenye YouTube. Washirika walio na uwezo wa kufikia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube ndio tu wanaweza kuondoa Video zao Fupi zisitumike kutayarisha miseto kwa sasa.
Kwa video ndefu zilizo kwenye chaneli yako, unaweza kudhibiti uandaaji wa miseto kwa kufuata hatua hizi:
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, bofya Maudhui.
- Bofya jina la video au kijipicha.
- Nenda kwenye bofya ONYESHA ZAIDI.
- Sogeza ili upate “Kutayarisha miseto ya Video Fupi” chagua ikiwa utaruhusu utayarishajii wa miseto.
- Bofya HIFADHI.
Mapendeleo ya “Kutayarisha miseto ya Video Fupi” yanaweza pia kubadilishwa kwa wingi na unapopakia video kutoka kwenye kompyuta yako.
Maudhui yako, ikiwa ni pamoja Video Fupi na video ndefu, yanapatikana kwa ajili ya kutayarisha mseto kwa chaguomsingi. Hatua ya kuruhusu utayarishaji wa mseto wa maudhui yako inaweza kuhamasisha ubunifu wa maudhui kwenye YouTube na uwezekano wa kupanua ufikiaji wako wa hadhira mpya.
Iwapo utatumia Kidhibiti Maudhui cha Studio, unaweza kudhibiti utayarishaji mseto wa maudhui yako wakati wowote. Ili uzuie utayarishaji wa mseto wa maudhui:
- Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio .
- Kwenye kichupo cha Muhtasari, tafuta "Mseto wa Video Fupi za YouTube" kisha ubatilishe uteuzi kisanduku. Kuzima mipangilio hii kutazima sauti za miseto yote iliyotayarishwa kutokana na maudhui yako.
- Bofya HIFADHI.
Mapendeleo ya “Sampuli za Video Fupi” yanaweza pia kuhaririwa kwa wingi na unapoyapakia kutoka kwenye kompyuta yako.
Miseto ya sauti utakayotayarisha itazimwa sauti, itaainishwa kuwa Haijaorodheshwa na itaratibiwa kufutwa ndani ya siku 30 baada ya mtayarishi halisi kufuta kazi yake au atakapozuia kutumia maudhui yake kuandaa mseto. Utatumiwa barua pepe kuhusu mabadiliko hayo, ili uweze kupakua video yako kwenye Studio ya YouTube bila sauti ya mseto uliyokuwa umetumia kabla haijafutwa. Kisha utaweza kupakia video yako tena ikiwa na sauti tofauti.
Miseto ya video utakayotayarisha itafutwa baada ya mtayarishi halisi kufuta video yake au kuzuia matumizi. Utatumiwa barua pepe hali hii itakapotokea. Huenda usipatiwe leseni ya kupakia tena Video yako fupi kwenye YouTube kwa kutumia video halisi ya mseto, lakini utazamaji uliotokana na Video yako fupi utahesabiwa katika utazamaji wa siku zote.
Kuzuia uandaaji wa miseto kwenye Studio ya YouTube, kufuta video yako, kutia ukungu au kupunguza video kwenye Studio ya YouTube, hutoa arifa kwa watayarishaji wanaoandaa mseto:
- Miseto ya sauti:
- Huzimwa sauti
- Hubainishwa kuwa Haijaorodheshwa
- Huratibiwa kufutwa baada ya siku 30
- Miseto ya video hufutwa.
Hatua ya kuzuia kutayarisha mseto au kufuta video yako pia huzuia utayarishaji wa miseto katika siku za zijazo.
Kwa nini Video yangu fupi imezuiwa?
Kwa nini Video yangu fupi haina sauti?
Miseto unayotayarisha kwa kutumia sauti mseto inaweza kuondolewa sauti wakati wowote mtayarishi anapozuia kutayarisha maudhui kwa kutumia mseto wa kazi yake, anapofuta au anapofanya mabadiliko ya video yake kwenye Studio ya YouTube kwa kutia ukungu au kuipunguza. Iwapo hali yoyote kati ya hizi itatokea, utatumiwa barua pepe kukujulisha kuwa video yako fupi:
- Imezimwa sauti
- Hubainishwa kuwa Haijaorodheshwa
- Imeratibiwa kufutwa baada ya siku 30
Unaweza kupakua video yako isiyo na mseto wa sauti kwenye Studio ya YouTube kabla haijafutwa. Unaweza kuipakia tena video yako, ikiwa na sauti tofauti, kwa kuwa huenda huna tena ruhusa ya kutumia mseto wenye sauti ya awali.
YouTube hujaribu vipengele vipya vya majaribio mara kwa mara. Kwa sasa kipengele hiki kinapatikana tu kwa watayarishi wachache mahususi walioko Marekani. Jaribio la muda mfupi linalenga kuhakikisha kuwa tunafuata hatua zinazofaa ili kujifunza na kufanya uboreshaji wowote baada ya matumizi ya bidhaa tena na tena katika siku zijazo.
Hadhira kote ulimwenguni zinaweza kutumia nyimbo kama zilivyo ili kuziandalia miseto kwenye Video Fupi.
Jaribio letu la kwanza kwenye Video Fupi lilihusisha ushirikiano na wasanii mahususi na sauti zao zilizotayarishwa kwa AI. Sasa tumeongeza chaguo lingine la kutayarisha muziki wa ala tu kwenye Video Fupi kwa usaidizi wa AI.
Baada ya wimbo kuchapishwa, mtu yeyote anaweza kutumia wimbo uliotayarishwa kwa AI kama ulivyo ili kuuandalia mseto kwenye Video zake Fupi. Nyimbo hizi zilizotayarishwa kwa AI zitakuwa na lebo ya maandishi inayoashiria kuwa zilitayarishwa kwa kutumia Dream Track. Tunaanza na watayarishi wachache nchini Marekani na wasanii waliojijumuisha. Kulingana na maoni yatakayotokana na majaribio haya, tunatumai kupanua upatikanaji wa zana hii.
Mwongozo wa Jumuiya wa YouTube unatumika kwenye maudhui yote yaliyo katika YouTube, ikiwa ni pamoja na maudhui yaliyotayarishwa kwa kutumia Dream Track na tumejitolea kuendelea kuondoa maudhui yoyote yanayokiuka sera zetu. Pata maelezo zaidi kuhusu sera za uchumaji mapato kwenye chaneli na sera za uchumaji mapato katika Video Fupi kwenye Dream Track.