Masharti ya kodi ya Mitandao ya Vituo Mbalimbali (MCN) na vituo vya washirika

Muhimu: Tunapoelekea mwisho wa mwaka, watayarishi wanaochuma mapato wanapaswa kuangalia taarifa zao za kodi kwenye AdSense katika YouTube. Hakikisha kuwa umewasilisha fomu ya kodi na ikiwa unastahiki, dai manufaa ya mkataba wa kodi kufikia tarehe 10 Desemba, 2023. Panapofaa, Google itakokotoa upya kodi za mwaka 2023 na kurejesha salio.

Usiposhiriki taarifa za kodi, huenda Google ikahitajika kuzuia kodi kutokana na mapato unayochuma ulimwenguni kote kwa kutumia kiwango cha juu zaidi cha kodi ya zuio. Ukishiriki taarifa zako za kodi, kiwango cha kodi utakacholipa kinaweza kuwa hadi asilimia 30 ya mapato yako nchini Marekani.

Kuangalia taarifa zako za kodi na kudai manufaa ya mkataba wa kodi:

  • Hakikisha kuwa tumepata taarifa zako za kodi. Hakikisha kuwa hali ya fomu yako ya kodi ni kijani kumaanisha kuwa “Imeidhinishwa” kwenye AdSense katika YouTube.
  • Wasiliana na mshauri wako wa kodi ili uthibitishe kuwa unastahiki kudai manufaa ya mkataba wa kodi. Manufaa ya mkataba wa kodi yanaweza kupunguza kiwango cha kodi ya zuio katika aina fulani za mapato:
    • Mirabaha Mingine ya Hakimiliki (kama vile Mpango wa Washirika wa YouTube na Google Play)
    • Huduma (kama vile Google AdSense)

Pata maelezo zaidi kuhusu kuzuia kodi kwenye YouTube au usome Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu kutuma taarifa zako za kodi ya Marekani kwenda Google.

Google inatakiwa kukusanya taarifa za kodi kutoka kwa watayarishi walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP). Iwapo kodi zozote zitakatwa, Google itazuia kodi kwenye mapato ya YouTube yanayotoka kwa watazamaji nchini Marekani. Makala haya yanalenga watayarishi katika mitandao ya vituo mbalimbali (MCN). Pata maelezo zaidi kuhusu kuzuia kodi kwenye YouTube hapa na utembelee makala yetu ya kina yanayohusu Maswali Yanayoulizwa Sana: Kutuma taarifa zako za kodi ya Marekani kwenye Google.

Muhimu: Google haitawahi kukutumia ujumbe ambao hujauomba, unaokuomba nenosiri au taarifa zako nyingine binafsi. Kabla ya kubofya kiungo, hakikisha kila wakati kuwa barua pepe imetumwa kutoka kwenye anwani ya barua pepe ya @youtube.com au @google.com .

Taarifa za washirika

Je, wewe ni mshirika wa mtandao wa chaneli mbalimbali (MCN)? Basi unahitaji kutoa taarifa za kodi ya Marekani katika akaunti ya AdSense katika YouTube iliyounganishwa na chaneli yako. Taarifa hizi zinatumiwa kubaini kodi za zuio, ikiwa zipo. Ili uhakikishe kuwa kodi za zuio zinakokotolewa ipasavyo, ni sharti akaunti yako ya AdSense katika YouTube itumie jina lako rasmi au jina rasmi la biashara yako. Pia, maelezo ya anwani kwenye faili yanapaswa kulingana na makazi yako ya kudumu kwa madhumuni ya kisheria na kodi.

Mapato ya kituo chako yataendelea kulipwa kwa mshirika wako wa MCN. Iwapo kuna kodi zozote za zuio, zitakatwa kwenye malipo yanayofanywa kwa MCN yako kutokana na mapato ya kituo chako.

Kiasi kinachozuiwa hakitaonekana katika Takwimu za YouTube, kwa hivyo utakokotoa mwenyewe kwa kutumia mantiki hapa. Mtandao wako wa Vituo Mbalimbali utapewa ripoti kila mwezi inayoelezea jumla ya kiasi cha kodi inayozuiwa Marekani.

Iwapo uliwasilisha taarifa sahihi za kodi ya Marekani baada ya uzuaji kuanza na unatimiza masharti ya kupunguziwa kodi, kiwango cha kodi ya zuio kitarekebishwa katika kipindi kijacho cha malipo.

Kurejeshwa kwa pesa za kodi kwa washirika

Huenda vituo vya washirika katika Mitandao ya Vituo Mbalimbali (MCN) vikatimiza masharti ya kurejeshewa pesa kuanzia mwaka 2023. Ni lazima washirika watupatie hati halali inayothibitisha kuwa malipo ya awali yalitegemea bei ya chini zaidi. Kodi zilizozuiwa katika mwaka huo huo wa kalenda ndizo tu zitastahiki kurejeshwa. Mabadiliko haya hayatumiki kwa mwaka 2022 au miaka yoyote iliyotangulia. Baada ya kutimiza masharti, pesa zitarejeshwa kwa mmiliki wa maudhui halisi ambaye kodi ilizuiwa kutoka kwake.

Taarifa za Mitandao ya Chaneli Mbalimbali

Mapato ya Mtandao wa Chaneli Mbalimbali (MCN) kwenye YouTube Yanayomilikiwa na Kuendeshwa na wamiliki wa maudhui, yanaweza pia kukatwa kodi za zuio za Marekani. Google itatumia taarifa za kodi ulizotuma kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube kukokotoa kodi za zuio kwa wamiliki wa maudhui unayomiliki na kuendesha. Hii ni pamoja na chaneli nyingine mahususi au wamiliki wa maudhui ambao si washirika waliounganishwa na akaunti.

Iwapo kodi zozote za zuio zitatumika, utaona makato haya katika Ripoti ya Malipo kwenye AdSense katika YouTube. Kwa kodi za zuio za washirika, utapewa ripoti ya ziada. 

Google itatuma fomu za kuripoti kodi (k.m. 1042-S, 1099-MISC) moja kwa moja kwenye chaneli za washirika kulingana na taarifa za kodi zilizowekwa kwenye akaunti ya AdSense katika YouTube iliyounganishwa na chaneli yao.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14626073936062570339
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false