Fahamu chaguo zenu kama familia

Matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube Kids na YouTube: Chaguo za Kutazama kwa ajili ya Familia

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Unaweza kuamua hali ya utumiaji wa YouTube inayofaa zaidi familia yako. Tumia chati iliyo hapa chini ili kujifunza tofauti kati ya akaunti inayodhibitiwa kwenye YouTube na programu ya YouTube Kids.

Kwa maelezo mahususi kuhusu aina ya vipengele vinavyozimwa katika akaunti zinazodhibitiwa, nenda kwenye Nini maana ya matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube?
  Akaunti inayodhibitiwa kwenye YouTube YouTube Kids
Ni kitu gani?

Toleo la kawaida la YouTube linalodhibitiwa na wazazi lenye vipengele vichache na ulinzi wa nidhamu dijitali. Huja na mipangilio ya maudhui kwa vijana wadogo na wakubwa.

Pata maelezo zaidi kuhusu matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube.

Programu tofauti ambayo inatumiwa na watoto kwa usalama na urahisi. Huja na zana kwa ajili ya wazazi na walezi za kuwaongoza watoto wanapotazama maudhui.

Pata maelezo zaidi katika youtube.com/kids.
Je, ni ya nani? Watoto walio chini ya umri wa miaka 13 (au umri unaofaa katika nchi/eneo lao) ambao wazazi wao wameamua kuwa wako tayari kuangalia maudhui kwenye YouTube kwa kutumia mipangilio ya maudhui iliyochaguliwa na wazazi.

Watoto ambao wazazi wao wanataka kuwachagulia maudhui ya kutazama. Watoto ambao wazazi wao wanataka kuwachagulia maudhui ya kutazama kulingana na mipangilio ya maudhui iliyo katika makundi 3 ya umri:

  • Watoto wa Chekechea (Umri usiozidi miaka 4)
  • Watoto Wadogo (Umri wa miaka 5 hadi 8)
  • Watoto Wakubwa (Umri wa miaka 9 hadi 12)
Maudhui kiasi gani yanapatikana kwa ajili ya mtoto wangu?

Inajumuisha video na muziki zaidi kuliko programu yetu tofauti ya YouTube Kids.

Kiasi cha maudhui yanayopatikana hubadilika kulingana na mipangilio ya maudhui unayochagua (kwa mpangilio):

  • Gundua
  • Gundua zaidi
  • Maudhui Zaidi ya YouTube

Inajumuisha chaguo chache za video kuliko akaunti inayodhibitiwa kwenye YouTube.

Kiasi cha maudhui yanayopatikana hubadilika kulingana na mipangilio ya maudhui unayochagua (kwa mpangilio):

  • Watoto wa Chekechea (Umri usiozidi miaka 4)
  • Watoto Wadogo (Umri wa miaka 5 hadi 8)
  • Watoto Wakubwa (Umri wa miaka 9 hadi 12)
Ni nini kilicho tofauti kuhusu kila chaguo la mipangilio ya maudhui?

Akaunti zinazodhibitiwa zinatoa mipangilio ya maudhui ambayo kwa ujumla inalingana na daraja la maudhui kwa watazamaji walio na umri wa miaka 9+, 13+, au maudhui mengi ya YouTube. Hayajumuishi maudhui yenye mipaka ya umri.

Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio ya maudhui ya familia zinazotumia matumizi yanayosimamiwa.

Programu ya YouTube Kids hutoa mipangilio ya maudhui kulingana na rika mbalimbali. Chekechea inalingana na umri usiozidi miaka 4. Watoto wadogo inalingana na miaka 5–8. Watoto wakubwa inalingana na miaka 9–12. Wazazi wanaweza pia kubainisha wasifu kwa ajili ya utazamaji wa watoto wao ili wachague video wanazoweza kutazama.

Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio ya maudhui ya YouTube Kids.
Je, ninaweza kuamua video ambazo mtoto wangu ataona?

Unaweza kuchagua mipangilio ya maudhui ya Akaunti ya Google ya mtoto wako, kisha YouTube ifanye kazi ya kuchuja ipasavyo video zisizohitajika.

Kumbuka: Tunajitahidi kuchuja video zisizofaa, lakini mifumo yetu inaweza kufanya makosa. Huenda baadhi ya video zisiwafae watoto. Iwapo utapata maudhui unayoamini kuwa hayafai kwenye YouTube, unaweza kuyaripoti.
Unaweza kuchagua video ambazo tu ungependa mtoto wako azitazame. Pata maelezo zaidi.
Ninawezaje kuweka mipangilio ya muda wa kutumia kifaa kwa ajili ya mtoto wangu? Tumia programu ya Family Link kutoka Google kudhibiti vikomo vya muda wa kutumia kifaa kwa ajili ya vifaa vya mtoto wako vinavyodhibitiwa. Tumia programu ya YouTube Kids kubainisha mipangilio ya muda wa kutumia kifaa moja kwa moja au utumie programu ya Family Link kutoka Google kudhibiti vikomo vya muda wa kutumia kifaa kwa ajili ya mtoto wako.
Je, Akaunti ya Google kwa ajili ya mtoto wangu inahitajika?

Ndiyo. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kumfungulia mtoto wako aliye na umri wa chini ya miaka 13 Akaunti ya Google (au umri unaofaa katika nchi au eneo uliko). Unaweza kudhibiti Akaunti ya Google ya mtoto wako ukitumia Family Link.

Hapana, Akaunti ya Google haihitajiki.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu kuunda akaunti inayodhibitiwa kwenye YouTube, nenda kwenye Anzisha akaunti zinazodhibitiwa.

Iwapo ungependa maelezo zaidi kuhusu YouTube Kids, angalia Mwongozo wa Wazazi wa kutumia YouTube Kids.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10631602773387250074
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false