Unaweza kutumia kipimo cha watazamaji wapya na wanaorudi tena ili kupanga mkakati wa maudhui kwenye kituo chako. Kwa mfano, unaweza kujenga uaminifu kwa kutayarisha maudhui yanayolingana au unaweza kujaribu mada mpya ili uwavutie watazamaji wapya.
Kwa nini sioni "jumla" yoyote ya data ya watazamaji wanaorudi tena ninapochagua tarehe tofauti?
Je, inamaanisha nini ikiwa watazamaji wapya ndio wanaotazama kituo changu sana?
Hali hii huashiria kwamba watazamaji wanaweza kutazama baadhi ya video zako, lakini kuna uwezekano mdogo wa kurudi kutazama zaidi. Ni kawaida kuona mtindo huu miongoni mwa:
- Vituo vinavyopakia video kuhusu mada tofauti, zinazovutia aina tofauti za watazamaji.
- Vituo vinavyoangazia "jinsi ya kufanya kitu" ambapo watazamaji hutazama video ili kujifunza jinsi ya kufanya jambo fulani, lakini hakuna uwezekano wa kurudi kwenye kituo husika ili kutazama zaidi.
Kumbuka: Mitindo hii itatofautiana kulingana na kituo na hadhira yako.
Je, inamaanisha nini ikiwa Watazamaji wanaorudi tena ndio wanaotazama kituo changu sana?
Hali hii huashiria kwamba kituo kina watazamaji waaminifu ambao wana uwezekano mkubwa wa kurudi kutazama zaidi. Ni kawaida kuona mtindo huu miongoni mwa:
- Vituo vinavyopakia maudhui yanayolingana kuhusu mada zinazofanana au katika muundo unaojulikana.
- Vituo vilivyo na waandalizi wale wale kama vile nyuso na watu wanaojulikana ambao watazamaji huwapenda zaidi.
- Vituo vinavyounda mfululizo maarufu ambao huwafanya watazamaji warudi kutazama zaidi.
Kumbuka: Mitindo hii itatofautiana kulingana na kituo na hadhira yako.
Kwa nini idadi ya watazamaji wanaorudi tena ni ndogo kuliko idadi ya wanaofuatilia kituo changu?
Je, mfumo wa kupendekeza video kwenye YouTube huboresha mapendekezo kwa ajili ya watazamaji wanaorudi tena?
Kuangalia mfano
Tazama video ifuatayo kutoka kwenye chaneli ya Watayarishi wa Maudhui ya YouTube ili upate maelezo zaidi kuhusu data ya watazamaji wapya na wanaorudi tena.
Kuelewa Mitindo ya Watazamaji Wako: Watazamaji Wapya na Wanaorudi Tena katika Takwimu za YouTube