Sera dhidi ya lugha chafu

Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.

Huenda baadhi ya lugha haifai kwa watazamaji walio na umri wa chini ya miaka 18.

Ikiwa utaona maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wetu wa Jumuiya yanapatikana hapa. Iwapo umeona video au maoni machache ambayo ungependa kuyaripoti, unaweza kuripoti chaneli hiyo.

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Ikiwa unachapisha maudhui

Maudhui machafu yanayokiuka sera hii yanaweza kusababisha kuwekwa kwa mipaka ya umri, kuondolewa kwa maudhui au onyo. Tunaweza kuzingatia sababu zifuatazo tunapoamua kuweka mipaka ya umri, kuondoa maudhui au kutoa onyo.

  • Matumizi ya lugha au masimulizi machafu au ya ngono
  • Matumizi ya lugha chafu kupita kiasi kwenye maudhui 
  • Matumizi ya lugha chafu au maneno yanayochochea ngono katika kichwa cha maudhui, kijipicha au metadata husika
  • Matumizi ya sauti zilizokithiri za ngono

Kumbuka: Orodha iliyo hapa juu si kamili.

Maudhui yenye mipaka ya umri

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui yaliyowekewa mipaka ya umri:
  • Video inayoangazia matumizi ya lugha chafu kama vile mkusanyiko, wimbo au klipu zilizorekodiwa nje ya muktadha
  • Video inayotumia lugha chafu nzito kwenye kichwa 
  • Video ambayo hutumia lugha chafu au ya ngono mara kwa mara

Sera hii hutumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko mubashara, sauti na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube. Kumbuka kuwa hii ni baadhi tu ya mifano na usichapishe maudhui iwapo unaona kuwa yanaweza kukiuka sera hii.

Tunaweza kuruhusu lugha chafu wakati lengo kuu ni kutoa elimu, makala yanayoangazia hali halisi, sayansi au kazi ya kisanii na hayana nia ya kuchochea ngono. Kwa mfano, jina la wimbo wenye matusi au wimbo ambao una kiasi kikubwa cha lugha chafu. Kumbuka kuwa hatua ya kuweka muktadha katika maudhui, mada na maelezo itatusaidia pamoja na watazamaji wako kubaini lengo kuu la video.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14844436064480799424
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false