Arifa

Hivi majuzi tulitangaza mabadiliko kwenye kurasa za uchapishaji. Tafadhali soma hapa ili upate maelezo zaidi.

Saidia Google News igundue maudhui yako yanayotambaliwa kwenye wavuti

Tunatumia mifumo ya kiotomatiki kutunga faharasa ya habari zetu. Tunalenga kuonyesha maudhui yako mengi iwezekanavyo. Hata hivyo, hatuwezi kukuhakikishia kuwa tutachapisha kila makala au kuathiri yanavyopewa nafasi. Algoriti zetu za Google News zinatumia ishara mbalimbali kuonyesha maudhui ya habari yanayofaa na muhimu.

Angalia iwapo makala yako yanatimiza masharti ya Google News

Wachapishaji hawahitaji kutuma tovuti zao ili zitimize masharti ya kuonyesha maudhui kwenye maeneo ya Google News. Kwa kutumia algoriti, Google hugundua maudhui mapya kupitia teknolojia za Utafutaji. Hata hivyo, wachapishaji wanahitaji kutii sera zetu za maudhui ili makala yao yaonekane kwenye maeneo ya Google News.

Muhimu: Ili uthibitishe kuwa maudhui kutoka kwa kikoa chako yananakiliwa katika faharasa na Google, tumia huduma ya mtoa huduma wa tovuti “site:yoursite.com.” Bila mtoa huduma huyu, huenda maudhui kutoka kwenye kikoa chako yasionekane iwapo tutakuwa na maudhui mengine kama yako yanayofaa zaidi.

Thibitisha kuwa Google inaweza kutambaa na kunakili tovuti yako katika faharasa

Muhimu: Iwapo makala yako yanaonyesha jina tofauti la chapisho au yameunganishwa kwenye kikoa tofauti cha tovuti, kuna uwezekano kwamba hatuwezi kutambaa kwenye maudhui yako. Tatizo hili linaweza kutokana na maelezo yaliyopitwa na wakati kwenye mfumo wetu. Ili kutatua tatizo hili, sasisha maelezo ya jumla ya tovuti yako na maudhui kwenye Kituo cha Wachapishaji.

Ili uangalie URL mahususi, tumia Zana ya Upekuzi wa URL katika Dashibodi ya Utafutaji. Zana hiyo inaonyesha jinsi programu za kutambaa za Google zinavyoona ukurasa wako na sababu ambazo huenda zinafanya mifumo yetu itatizike kunakili maudhui yako kwenye faharasa.

Ili uangalie tovuti yako yote, tumia Ripoti ya Hali ya Kunakili Maudhui kwenye Faharasa. Kwa maelezo zaidi, tembelea Kituo cha Usaidizi wa Dashibodi ya Utafutaji.

Unaweza kutumia Menyu ya Tovuti ya Google News kusaidia kuboresha jinsi programu yetu ya kutambaa inavyopata maudhui yako na inaweza kutatua matatizo. Menyu za tovuti za Google News ni tofauti na menyu za tovuti za huduma ya Tafuta na Google. Pata maelezo zaidi kuhusu Menyu ya Tovuti ya Google News.

Ili uongeze uwezekano wa makala yako kuonyeshwa kwenye programu na tovuti ya Google News, pata maelezo kuhusu mbinu zetu bora za maudhui Yanayotambaliwa na Wavuti hapa.

Kidokezo: Iwapo unaendesha tovuti katika lugha nyingi, usiwaelekeze kiotomatiki wanaotembelea tovuti kwenda kwenye matoleo tofauti ya lugha. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti tovuti za kikanda na za lugha nyingi.

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13674937058294517860
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
100499
false
false