Makataa ya Sera

Tunasasisha Sera za Mpango wa Wasanidi Programu mara kwa mara ili kuhakikisha hali salama na ya kuaminika kwa watumiaji wetu kwenye Google Play. Kwenye ukurasa huu, naweza kupata maelezo kuhusu mabadiliko tuliyofanya kwenye sera zetu hivi majuzi, ikiwa ni pamoja na mabadiliko yatakapoanza kutumika na nyenzo zitakazokusaidia kujiandaa kwa ajili ya masasisho ya programu. Tarehe zote kwenye ukurasa huu huonekana katika muundo wa mwaka, mwezi, siku. Ili upate makataa ya sera ambayo yamepita miezi 3, angalia Kumbukumbu yetu ya Sera.

Tarehe ya mwisho (YYYY-MM-DD)Mabadiliko ya sera
Nyenzo
2024-08-31  
Kwa hali ya utumiaji inayodumisha faragha ya watumiaji, tunawaletea sera ya Ruhusa za Picha na Video ili kupunguza idadi ya programu zinazoruhusiwa kuomba ruhusa pana za picha/video (READ_MEDIA_IMAGES na READ_MEDIA_VIDEO). Programu zinaweza tu kufikia picha na video kwa madhumuni yanayohusiana moja kwa moja na utendaji wa programu. Programu ambazo zinahitaji kufikia faili hizi mara moja tu au mara chache zinaombwa kutumia kiteuzi cha mfumo, kama vile kiteua picha cha Android.
 
Ilitangazwa tarehe 2023-10-25
2025-01-31  
Tunaanzisha Sera ya Viwango vya Usalama wa Watoto inayohitaji programu za Kijamii na za Kuchumbiana kufuata viwango mahususi na kuthibitisha zenyewe kuwa zinatii sera hii kwenye Dashibodi ya Google Play kabla ya kuchapishwa.
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
2024-08-31  
Tunasasisha sera dhidi ya Maudhui ya Hila ili kujumuisha sauti kama mfano wa ziada wa aina ya maudhui yanayodhibitiwa na sera hii.
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
2024-08-31  
Tunasasisha Sera ya Health Connect ili kurahisisha mchakato wa kutuma maombi wa Health Connect pamoja na kutii sera ya Programu za Afya. Baadye mwaka huu, taarifa mpya ya Dashibodi ya Google Play itatumika badala ya mchakato uliopo wa kutumia fomu.
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
2024-05-31  
Tunafafanua Sera yetu ya Mikopo ya Binafsi ili kuhakikisha kuwa vipindi vya kurejesha mikopo vinatii kanuni za mahali husika.
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
2024-05-31  
Ili kuboresha uonekanaji na udhibiti wa programu zinazohusiana na afya kwenye Google Play, tunaanzisha taarifa ya dashibodi ya Programu za Afya. Ni lazima programu zilizo na vipengele vinavyohusiana na afya au matibabu zithibitishe taarifa hii kwenye Dashibodi ya Google Play. Pata maelezo zaidi
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
2024-05-31  
Tunaongeza sera mpya ya programu za afya chini ya “Huduma na Maudhui ya Afya” ili kutambulisha masharti mapya kwa programu zinazopangwa katika aina za programu za Afya. Tunasasisha pia sera yetu ili kuonyesha mwongozo wa sasa wa afya ya umma.
 
Ilitangazwa tarehe 2023-10-25
2024-05-31  
Ili kuwapa watumiaji hali bora ya utumiaji, tunaanzisha vikomo vipya kwa utumiaji wa ruhusa ya USE_FULL_SCREEN_INTENT. Kwa programu zinazolenga toleo la Android U (kiwango cha API cha 34) na zaidi, tunabadilisha ruhusa hii kuwa ruhusa maalum ya ufikiaji wa programu. Ni programu ambazo utendaji wao wa msingi unahitaji arifa ya skrini nzima tu ndizo zitapewa ruhusa hii kwa chaguomsingi. Programu zingine zote zitahitaji kuomba ruhusa kutoka kwa mtumiaji.
 
Ilitangazwa tarehe 2023-10-25
2024-04-03  
Tunasasisha sera yetu ya Mikopo ya Binafsi ili kuzuia mifano ya hali za ziada za matumizi isifikie ruhusa nyeti.
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
2024-04-03  
Tunasasisha sera ya Vidadisi ili kufafanua mbinu yetu iliyopo ya kuwalinda watumiaji dhidi ya programu, msimbo au shughuli hasidi.
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
2024-04-03  
Tunaunganisha sera zetu za Maudhui ya Ugaidi pamoja na Mashirika Hatari na Makundi (hapo awali ilikuwa chini ya Sera dhidi ya vurugu), kuwa sera moja ya Itikadi Kali yenye Vurugu.
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
2024-04-03  
Tunasasisha Ruhusa zetu za Sera ya Huduma Zinazoendeshwa Programu Inapotumika isipokuwa aina ya huduma ya "dataSync" inayoendeshwa programu inapotumika ili kuruhusu matumizi yake katika utendaji wa Play Asset Delivery.
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
2024-04-03  
Tunasasisha sera yetu ya Maudhui Yasiyofaa kwa kuweka mwongozo kuhusu maudhui ya ngono katika programu za katalogi za vitabu na video.
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
2024-04-03  
Tunasasisha sera yetu dhidi ya Programu za Simu Zisizotakikana ili kufafanua kuwa wasanidi programu hawapaswi kuomba au kuwadanganya watumiaji wazime vipengele vya ulinzi wa usalama wa kifaa kama vile Google Play Protect.
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
2024-04-03  
Tunasasisha Sera yetu ya kudhibiti programu hasidi ili kufafanua kuwa Programu fichamizi ni aina ndogo ya programu hasidi. Programu fichamizi ni programu inayotumia mbinu mbalimbali za ukwepaji ili kumpa mtumiaji utendaji tofauti au bandia wa programu.
 
Ilitangazwa tarehe 2024-04-03
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2973046329549862733
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false