Uwezo wa Kufikia Data

Wasanidi programu hutuambia kuwa data inayoweza kutendewa kazi ni muhimu kwa kuwa huwasaidia kuboresha hali zao za utumiaji na kukuza biashara zao. Tunawapa wasanidi programu idhini ya kufikia kundi pana la data kupitia Dashibodi ya Google Play, katika miundo inayoweza kupakuliwa, pamoja na API na tunaendelea kujitahidi ili kufanya vipimo na maonyesho yawe muhimu zaidi. Tunahakikisha kuwa data tunayokusanya na kushiriki na wasanidi programu kuhusu programu zao hulinda faragha na usalama wa watumiaji wao.

Kukusanya na Kushiriki Data

Wakati mtu anatumia huduma za Google kama vile Google Play, iwe ni mtumiaji au msanidi programu, mtu huyo anaamini kuwa tutalinda taarifa zake vizuri. Tunafahamu kuwa hili ni jukumu kubwa na tunajitahidi kulinda taarifa za watumiaji wetu na kumpa mtumiaji udhibiti. Tafadhali soma sera yetu ya faragha ili ufahamu taarifa ambazo tunakusanya, kwa nini tunazikusanya na jinsi zinavyoweza kusasishwa, kudhibitiwa, kutumwa na kufutwa. Hatushiriki taarifa binafsi za watumiaji wetu na kampuni, mashirika au watu wasio kwenye Google isipokuwa katika hali fulani zilizoelezewa katika sera yetu ya faragha.  Zaidi ya hayo, sera zetu kuhusu ufikiaji wa data huzuia ufikiaji wa data ya programu isiyo ya umma inayoweza kutambulisha msanidi programu mwingine.

Ufikivu wa Data

Data inayoshirikiwa na wasanidi programu huwasaidia kuelewa hatua za programu zao: kuanzia jinsi inavyotambulika kwenye Duka la Google Play hadi jinsi watu wanavyoitumia na kiasi ambacho watumiaji hutozwa. Wasanidi programu pia wana uwezo wa kufikia ukadiriaji na maoni ili kuelewa maoni ya watumiaji na kujibu maswali yao. 

Kwa kawaida, data tunayowapa wasanidi programu hujumlishwa na kufichwa utambulisho ili kulinda faragha ya watumiaji. Kwa mfano, wasanidi programu wana uwezo wa kufikia data ya programu yao inayohusu:

Wasanidi programu pia wana uwezo wa kufikia data iliyojumlishwa ili kulinganisha utendaji wao na wa wengine kwenye mfumo. Kwa mfano, msanidi wa mchezo anaweza kulinganisha kiwango cha data ya watumiaji na aina sawa ya mchezo katika eneo moja. Data hii hujumlishwa ili kulinda taarifa za utendaji wa msanidi programu yeyote ili zisibainishwe.

Tunajitahidi kuhakikisha kuwa wasanidi programu wanapata taarifa wanazohitaji ili wafaulu.  Ili upate maelezo zaidi kuhusu takwimu na maarifa yanayopatikana kwa wasanidi programu, tembelea Kituo cha Usaidizi cha Dashibodi ya Google Play na play.google.com/console/about/.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4740468940469455909
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false