Kukata Rufaa Dhidi ya Hatua ya Utekelezaji
Tutarejesha programu iwapo hitilafu ilifanywa, na tukibaini kuwa programu yako haikiuki Sera za Mpango na Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu wa Google Play. Iwapo ulikagua sera kwa umakini na unahisi kuwa huenda uamuzi wetu ulikuwa na hitilafu, tafadhali fuata maagizo yaliyotolewa kwenye arifa ya barua pepe au bofya hapa ili ukate rufaa dhidi ya uamuzi wetu.
Nyenzo Zaidi
Iwapo unahitaji maelezo zaidi kuhusu hatua ya utekelezaji au ukadiriaji/maoni kutoka kwa mtumiaji, unaweza kurejelea baadhi ya nyenzo zilizo hapa chini au uwasiliane nasi kupitia Kituo cha Usaidizi cha Google Play. Hatuwezi, hata hivyo, kukupa ushauri wa kisheria. Iwapo unahitaji ushauri wa kisheria, tafadhali wasiliana na mshauri wako wa kisheria.
- Ukaguzi wa programu
- Ripoti ukiukaji wa sera
- Kuwasiliana na Google Play kuhusu kusimamishwa kwa akaunti au kuondolewa kwa programu
- Tahadhari za mapema
- Ripoti maoni na programu zisizofaa
- Programu yangu imeondolewa kwenye Google Play
- Kufahamu kuhusu kufungwa kwa Akaunti ya Msanidi Programu wa Google Play