Matatizo ya akaunti, ya usajili na ya malipo

Ukiwa na matatizo wakati wa kujisajili au kutumia akaunti yako ya Dashibodi ya Google Play, unaweza kutatua matatizo mengi ya kawaida wewe mwenyewe na timu yetu ya usaidizi inaweza kukusaidia kutatua yaliyosalia.

Chagua tatizo la akaunti

Hitilafu inayotokea wakati wa kusajili akaunti ya Dashibodi ya Google Play

Wakati wa usajili, ukiona ujumbe kuwa njia yako ya kulipa imekataliwa, unashauriwa kusasisha maelezo ya akaunti yako ya malipo kwa kutumia njia tofauti ya kulipa au anwani ya kutuma bili. Hatua hii isipotatua tatizo, angalia orodha hii ya utatuzi wa matatizo ya kawaida ya malipo.

Ikiwa njia yako ya kulipa haikukataliwa, lakini umekumbana na hitilafu tofauti wakati wa kujisajili, wasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Imeshindwa kuthibitisha barua pepe au nambari ya simu

Ukiwa na matatizo wakati wa kuthibitisha barua pepe au nambari yako ya simu, tembelea ukurasa wetu wa Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQs)

Akaunti imesimamishwa

Kwa kuchapisha programu zako kwenye Google Play, unakubali kufuata Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play na Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu. Google haina wajibu wa kukutumia onyo kabla ya kusimamisha au kufuta akaunti yako.

Maonyo ya kuondolewa kwa programu, kusimamishwa kwa programu na maonyo yote huhesabiwa kuwa maonyo dhidi ya hadhi nzuri ya akaunti yako ya Dashibodi ya Google Play. Ukiukaji wa sera kupita kiasi au mara nyingi huenda ukasababisha kusimamishwa kwa akaunti yako ya Dashibodi ya Google Play.

Ikiwa akaunti yako imesimamishwa

Baada ya akaunti yako ya msanidi programu kusimamishwa, programu zako zote zitaondolewa kwenye Google Play na utapoteza watumiaji, takwimu na ukadiriaji wote unaohusishwa na programu hizo. Pia, hutaweza kuchapisha programu mpya.

Ikiwa akaunti yako ilisimamishwa kwa sababu ya kukiuka Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu, hatutakubali programu zijazo kutoka kwako, hivyo usifungue akaunti mpya ya Dashibodi ya Google Play. Vilevile, akaunti zozote zinazohusiana zitasimamishwa kabisa, akaunti zozote mpya utakazojaribu kufungua zitasimamishwa bila kurejeshewa ada ya usajili wa msanidi programu.

Kataa rufaa ya kusimamishwa kwa akaunti

Timu yetu ya usaidizi inaweza kurejesha akaunti yako ya Dashibodi ya Google Play ikiwa tu iliondolewa kimakosa na ikabainika kuwa akaunti na programu zako hazikiuki Mkataba wetu wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu.

Ikiwa unafikiria akaunti yako haikupaswa kufutwa, unaweza kukata rufaa. Timu yetu ya usaidizi inaweza tu kujibu rufaa zilizotumwa kwa lugha ya Kichina, Kiingereza, Kijapani na Kikorea.

Kushindwa kufikia akaunti yako

Iwapo akaunti yako haikufungwa lakini unatatizika kuingia kwenye Dashibodi ya Google Play, wasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Kufuta akaunti ya Dashibodi ya Google Play

Kufuta akaunti ya Dashibodi ya Google Play iliyo na programu zilizochapishwa

Ikiwa tayari umechapisha programu ambazo watumiaji wamesakinisha, hatuwezi kufuta akaunti yako ya Dashibodi ya Google Play. Kama sehemu ya Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu, watumiaji wanaruhusiwa kusakinisha upya programu bila kikomo, hatua inayolazimu akaunti iwe inatumika.

Hata hivyo, kama msanidi programu aliye na akaunti tofauti ya Dashibodi ya Google Play anataka kununua programu zako, timu yetu ya usaidizi inaweza kuhamishia programu zako kwenye akaunti yake. Baada ya programu zote kuhamishwa kwenye akaunti yako, tunaweza kufuta akaunti yako na kukurejeshea ada ya usajili wa msanidi programu. Hatua ya kufuta Akaunti yako ya Google haitafuta kiotomatiki akaunti yako ya msanidi programu.

Kufuta akaunti ya Dashibodi ya Google Play isiyo na programu zilizochapishwa

Iwapo hujachapisha programu au watumiaji hawajapakua programu zako zozote, wasiliana na timu yetu ya usaidizi. Hatua ya kufuta Akaunti yako ya Google haitafuta kiotomatiki akaunti yako ya msanidi programu.

Kuhamishia programu kwenye akaunti tofauti

Unapohamishia programu kwenye akaunti nyingine ya Dashibodi ya Google Play, takwimu zote za programu huhamishwa pia. Ili uhamishe programu zako kwa haraka, fuatilia maagizo kuhusu jinsi ya Kuhamishia programu kwenye akaunti tofauti ya msanidi programu na uwasiliane na timu yetu ya usaidizi.

Chagua tatizo la malipo

Malipo ya usajili hayajachakatwa

Ikiwa saa 48 hazijaisha tangu usajili akaunti ya Dashibodi ya Google Play, tupe muda zaidi ili tuchakate malipo na tufungue akaunti yako.

Ikiwa saa 48 zimepita tangu ujisajili lakini malipo yako hayajachakatwa, wasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Matatizo kwenye maelezo ya akaunti ya malipo ya wauzaji

Wasanidi Programu katika nchi nyingi wanaweza kujisajili kuwa wauzaji na kuuza programu zinazolipishwa kwenye Google Play. Ikiwa unaweza kufanya biashara kisheria katika nchi inayoruhusiwa na unakubali Sheria na Masharti ya Google Payments ya nchi hiyo, unaweza kujisajili kuwa muuzaji katika nchi hiyo.

Iwapo una maswali mengine kuhusu jinsi ya kuweka mipangilio ya taarifa za malipo, tembelea Kituo cha usaidizi kwa wauzaji cha Google Payments.

Badilisha sarafu katika akaunti ya Dashibodi ya Google Play

Ikiwa ungependa kubadilisha akaunti yako ya Dashibodi ya Google Play ili utumie sarafu tofauti, utahitaji kufungua akaunti mpya ya Dashibodi ya Google Play ukitumia anwani tofauti ya barua pepe. Ikiwa unahitaji kufungua Akaunti mpya ya Google, unaweza kuifungua wakati wowote.

Wakati unafungua akaunti yako, unaweza kuchagua nchi tofauti ili ubadilishe sarafu inayotumika kwenye akaunti yako. Baada ya kufungua akaunti mpya, timu yetu ya usaidizi inaweza kuhamishia programu zako kwenye akaunti yako mpya. Utarejeshewa ada yako ya usajili wa awali baadaye.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16487899112917733818
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false