Weka mipangilio ya bei ya programu yako

Unaweza kuweka programu yako iwe isiyolipishwa au inayolipishwa, kusasisha bei ya programu yako kwa jumla au kulingana na nchi na kutumia violezo vya bei kurahisisha bei ya programu zako kwenye Dashibodi ya Google Play.

Kumbuka : Baada ya kusasisha au kuchapisha programu, ikiwa ni pamoja na kubadilisha bei, kuongeza SKU au kubadilisha mipangilio ya usambazaji wa programu yako, huenda ikachukua saa kadhaa kabla ya mabadiliko uliyofanya kuonekana kwenye Google Play.

Upanuzi wa bei katika sarafu zenye thamani ya chini ya dola kwenye masoko 20

Mnamo Februari 2021, tulipunguza kiwango cha chini cha bei kwa bidhaa kwenye zaidi ya masoko 20 katika Amerika ya Kusini, EMEA na APAC. Sasa unaweza kuweka viwango vya chini vya bei katika masoko haya, hali itakayokuruhusu ufikie wanunuzi watarajiwa kwa kurekebisha bei yako ilingane vyema na mahitaji na uwezo wa ununuzi mahali ulipo.

Soma Blogu ya Wasanidi Programu wa Android ili upate maelezo zaidi.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Bei za programu (Bidhaa > Bei za programu).
  2. Katika sehemu ya "Bei", pembeni ya "Programu yako ni," bofya Iweke programu yako isiwe ya kulipishwa au Iweke programu yako iwe ya kulipishwa.

Kumbuka: Watumiaji katika nchi nyingi wanaweza kupakua programu zinazolipishwa na kufanya ununuzi wa ndani ya programu. Ili uthibitishe upatikanaji wa ununuzi, soma orodha yetu ya viwango vya bei na sarafu zinazoruhusiwa kulingana na nchi.

Mabadiliko katika chaguo la Hailipishwi au Inalipishwa katika programu yako

  • Unaweza kubadilisha programu yako kutoka Inalipishwa iwe Hailipishwi.
  • Programu yako ikibadilishwa na iwe Hailipishwi, haiwezi kurejeshwa tena katika hali ya Inalipishwa. Kama unataka kuuza programu yako tena, utahitaji kuunda programu mpya yenye jina jipya la kifurushi na uweke bei ya programu hiyo.

Kuweka bei

Unapouza programu na bidhaa za ndani ya programu kwenye Google Play, utatozwa ada ya huduma.

Kumbuka: Iwapo husambazi programu inayolipishwa au bidhaa ya ndani ya programu katika nchi unakowekea bei, watumiaji hawataweza kuwa na idhini ya kuifikia.

Programu zinazolipishwa

Kuweka bei ya programu inayolipishwa:

  1. Weka taarifa za malipo. Utatumia Dashibodi ya Google Play ili kubainisha viwango vya kodi.
  2. Kagua orodha yetu ya viwango vya bei na sarafu zinazokubalika kulingana na nchi.
  3. Kwenye ukurasa wa Bei za programu katika Dashibodi ya Google Play, weka bei.
    • Tunatumia bei utakayoweka kuwa msingi wa kukokotoa bei mahususi za soko. Tutabadilisha bei yako iwe katika sarafu ya nchi ulimo, tuweke kodi katika nchi mahususi na tutumie mielekeo ya bei inayotumika katika nchi mahususi pamoja na viwango sahihi vya kubadilisha fedha kulingana na tarehe unayoweka bei ya programu yako. Unaweza kuonyesha upya bei mwenyewe ili uhakikishe kuwa bei ya eneo mahususi inaonyesha bei ya kiwango cha hivi karibuni cha kubadilisha fedha.
    • Bei utakayoweka itatumika katika nchi zote zisizotumia sarafu ya nchi ulimo. Iwapo sarafu ya nchi ulimo haitumiki, tutaweka bei katika sarafu ya USD au EUR. Bei tunazoweka katika sarafu ya USD au EUR zinalingana na bei unayoweka.
    • Tunabaini sarafu inayotumika katika kila nchi na huwezi kuibadilisha.
Bidhaa za ndani ya programu

Ili uweke bei za bidhaa za ndani ya programu, pata maelezo ya jinsi ya kudhibiti bei za bidhaa za ndani ya programu.

Kuangalia au kusasisha bei zinazotumika katika nchi husika

Programu zinazolipishwa

Kumbuka: Bei yako chaguomsingi inatumika kubaini bei za programu yako katika nchi zingine.

Tumia bei chaguomsingi

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Bei za programu (Bidhaa > Bei za programu).
  2. Bofya Weka bei.
  3. Kagua jedwali katika sehemu ya "Bei za nchi mahususi". Katika safu wima ya "Bei", kagua bei za nchi mahususi kwa kila nchi.
    • Bei za nchi husika hutumia kiwango cha kubadilisha fedha cha leo na mielekeo ya bei katika nchi mahususi.
    • Ikiwa nchi haitumii sarafu ya nchi ulimo, bei ya sarafu chaguomsingi uliyoweka itatumika badala yake.

Sasisha bei chaguomsingi za nchi husika

Ili usasishe bei za nchi husika zitumie kiwango cha leo cha kubadilisha fedha na mielekeo ya bei katika nchi mahususi:

  1. Kwenye upande wa juu kulia wa sehemu ya "Bei za nchi mahususi", bofya Sasisha viwango vya kubadilisha fedha
  2. Bofya Tumia bei.

Ili uweke bei yako mwenyewe ya nchi husika:

  1. Katika safu wima ya "Bei" ya nchi ambayo unataka kusasisha, bofya aikoni ya penseli.
  2. Andika bei unayotaka kutumia.
  3. Bofya Tumia bei.

Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye Uza programu katika sarafu mbalimbali.

Vipengee vilivyo ndani ya programu

Ili uweke bei za bidhaa za ndani ya programu, pata maelezo ya jinsi ya kudhibiti bei za bidhaa za ndani ya programu.

Kutumia bei sawa kwa bidhaa nyingi

Unaweza kutumia violezo vya bei kuweka au kudhibiti seti moja ya bei katika programu nyingi zinazolipishwa na bidhaa za ndani ya programu. Ukisasisha kiolezo cha bei, bidhaa zote zilizounganishwa kwenye kiolezo zitatumia bei za hivi karibuni za kiolezo.

Unaweza kutumia hadi violezo 250 tofauti vya bei kwa kila akaunti ya msanidi programu na unaweza kuunganisha hadi bidhaa 1,000 kwa kila kiolezo cha bei.

Masharti ya ruhusa za violezo vya bei
  • Unahitaji ruhusa ya Kudhibiti upatikanaji katika Duka la Google Play kwa kila programu unayotaka kuijumuisha katika kiolezo cha bei.
  • Ili uone programu zote ambazo zimejumuishwa kwenye kiolezo cha bei, unahitaji ruhusa ya Kuona data ya kifedha kwa kila programu.
  • Kama huwezi kubadilisha kiolezo ulichounda, angalia ikiwa mtu yeyote aliweka kwenye kiolezo programu ambayo huna idhini ya kuifikia.
Weka vipengee kwenye kiolezo kipya cha bei
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Violezo vya bei (Mipangilio > Violezo vya bei).
  2. Bofya Weka kiolezo.
  3. Andika jina la kiolezo chako.
  4. Bofya Weka bei na uweke bei ambayo ungependa programu yako inunuliwe. Tutatumia bei ambayo utaweka kama msingi wa kukokotoa bei mahususi za soko. Tutabadilisha bei yako iwe katika sarafu ya nchi ulimo, tuweke kodi (katika nchi mahususi) na tutumie mielekeo ya bei inayotumika katika nchi mahususi na viwango sahihi vya kubadilisha fedha kulingana na tarehe unayoweka bei ya programu yako. Unaweza kubadilisha bei mwenyewe ili kuhakikisha kuwa bei ya nchi ulimo inaonyesha bei ya kiwango kipya cha kubadilisha fedha.
    • Bei utakayoweka itatumika katika nchi zote zisizotumia sarafu ya nchi ulimo.
  5. Chagua ikiwa ungependa kujumuisha kodi katika bei uliyoweka.
    • Bei chaguomsingi inajumuisha kodi: Ikiwa bei yako chaguomsingi ni EUR 9.99 na ungependa bei zote kwenye soko la Umoja wa Ulaya ziwe EUR 9.99 (bila kujali viwango vya kodi vya nchi mahususi), chagua kisanduku hiki cha kuteua ili utumie chaguo hili.
    • Kwa chaguomsingi (hasa, usipochagua Bei chaguomsingi inajumuisha kodi), kodi itaongezwa kwenye bei yako. Hii ina maana kwamba tutachukua bei yako chaguomsingi ya EUR 9.99 na kuongeza kodi inayotumika katika kila nchi.
  6. Kagua bei za nchi mahususi na uchague Weka bei.
  7. Bofya Hifadhi.
  8. Chagua kichupo cha Bidhaa zilizounganishwa.
  9. Kwa kutumia viteuzi vya "Unganisha bidhaa za ndani ya programu" na "Unganisha programu inayolipishwa" upande wa kulia wa kurasa, chagua programu. Iwapo unaunganisha bidhaa za ndani ya programu, chagua kwenye orodha ya bidhaa za ndani ya programu za programu hiyo.
  10. Chagua Unganisha. Ukiunganisha bidhaa kikamilifu, itaonekana chini ya sehemu ya "Bidhaa zilizounganishwa".
Onyesha upya viwango vya kubadilisha fedha katika kiolezo cha bei

Baada ya kuweka kiolezo cha bei, unaweza kusasisha bei zinazotumika katika nchi husika ili zitumie kiwango cha kubadilisha fedha cha leo na mielekeo ya bei ya nchi mahususi.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Violezo vya bei (Mipangilio > Violezo vya bei).
  2. Katika jedwali, chagua kishale cha kulia kilicho kando ya kiolezo cha bei ambayo ungependa kusasisha.
  3. Bofya Badilisha bei.
  4. Kwenye upande wa juu kulia wa sehemu ya "Bei za nchi mahususi", bofya Sasisha viwango vya kubadilisha fedha.
  5. Bofya Tumia bei.
Kuondoa bidhaa kwenye kiolezo cha bei
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Violezo vya bei (Mipangilio > Violezo vya bei).
  2. Chagua kiolezo kisha kichupo cha Bidhaa zilizounganishwa.
  3. Karibu na bidhaa unayotaka kuondoa, chagua Tenganisha.

Kumbuka: Hutaweza kutenganisha bidhaa zozote zilizo kwenye ofa. Utahitaji kusimamisha ofa hiyo au usubiri hadi ofa ikamilike, kabla ya kufanya mabadiliko yoyote kwenye kiolezo.

Kuanzisha ofa au tangazo

Kuna njia kadhaa ambazo unaweza kutumia kwa muda kuchapisha programu zipatikane bila malipo au kwa bei iliyopunguzwa:

  • Uza programu zako zinazolipishwa kwa bei ya punguzo: Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye Weka ofa ya programu zinazolipishwa.
  • Wape watumiaji programu inayolipishwa au bidhaa ya ndani ya programu bila malipo kwa kutumia kuponi ya ofa: Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye Weka ofa.

Maudhui Yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
401108043366324659
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false