Kuhamishia programu kwenye akaunti tofauti ya msanidi programu

Ikiwa una programu ambazo ungependa kuhamishia kwenye akaunti tofauti ya msanidi programu wa Google Play, unaweza kuwasilisha ombi la uhamishaji baada ya kukagua maagizo yaliyo hapa chini.

Kuwa tayari kuhamisha programu yako

Hatua ya 1: Kagua mwongozo wa sera na kiwango cha ada ya huduma

Kwa wasanidi programu wote:

Ni sharti akaunti halisi na programu zote zinazohamishwa zitii mwongozo wote wa sera.

Kwa wasanidi programu waliojiandikisha katikakiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15:

Programu inapohamishwa kati ya akaunti za wasanidi programu kwenye Vikundi tofauti vya Akaunti, mapato yote ya programu yatajumuishwa kwenye jumla ya mapato ya kila Kikundi cha Akaunti katika mwaka huo.

Kwa mfano, ikiwa akaunti ya msanidi programu kwenye Kikundi cha Akaunti cha A kina programu iliyopata mapato ya $100,000 (USD) katika mwaka huu, ambayo kisha yanahamishiwa kwenye akaunti nyingine ya msanidi programu katika Kikundi cha Akaunti cha B, mapato haya ya $100,000 (USD) yatajumuishwa kwenye jumla ya mapato ya Vikundi vyote viwili vya Akaunti ya A na B kwa madhumuni ya kukokotoa milioni $1 (USD) ya kwanza katika mapato ya mwaka huu.

Hatua ya 2: Pakua ripoti ambazo utahitaji baadaye

Unapohamishia programu kwenye akaunti tofauti, watumiaji wa programu zako, takwimu za upakuaji, ukadiriaji na maoni, ukadiriaji wa maudhui na maelezo ya ukurasa wa programu katika Google Play, yote huhamishiwa kwenye akaunti yako mpya.

Ripoti zako za uhamishaji mkubwa, ripoti za malipo na ripoti za mapato hazitahamishwa pamoja na programu, kwa hivyo ni vyema kupakua ripoti zozote utakazohitaji baadaye. Matoleo mapya ya ripoti hizi yatawekwa mara tu programu itakapohamishiwa kwenye akaunti mpya.
Hatua ya 3: Hakikisha kuwa akaunti zako za Msanidi Programu wa Google Play zimesajiliwa na zinatumika

Kabla ya kutuma ombi la kuhamisha programu kutoka akaunti yako ya awali hadi kwenye akaunti tofauti (inayojulikana kama akaunti yako lengwa), akaunti zote mbili za Msanidi Programu wa Google Play zinahitaji kuwa zimesajiliwa kikamilifu na zinatumika.

Ili kuthibitisha kama akaunti inatumika, hakikisha kuwa:

  • Akaunti ya awali: Unaweza kuingia katika akaunti.
  • Akaunti lengwa: Usajili wako umekamilika. Ukiona ujumbe huu "Kwa nini siwezi kuchapisha" kwenye kichwa cha programu, kagua maelezo uliyotoa ili ujaze sehemu yoyote ambayo umeruka.

Kumbuka: Ikiwa unafungua akaunti lengwa mpya, unapaswa kulipa ada ya usajili ya Dola 25 za Marekani. Baada ya uhamisho kukamilika, ikiwa unataka kufunga akaunti yako ya awali, timu yetu ya usaidizi inaweza kukurejeshea ada ya usajili wa akaunti hiyo.

Hatua ya 4: Tafuta kitambulisho cha muamala wa akaunti lengwa

Utahitaji kitambulisho cha muamala wa usajili wa akaunti yako na akaunti lengwa. Ili upate kitambulisho cha muamala, tafuta "ada ya usajili wa msanidi programu" kwenye kikasha cha barua pepe ya mmiliki wa akaunti lengwa.

Ikiwa huwezi kupata stakabadhi ya barua pepe ya kitambulisho cha malipo:

  1. Kwa kutumia anwani ya barua pepe ya akaunti ya mmiliki, ingia katika akaunti ya Google Payments.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Shughuli.
  3. Tafuta na uchague muamala wa usajili wa akaunti yako ya msanidi programu.
    • Kidokezo: Tafuta miamala yako ya “Msanidi Programu wa Google Play.”
  4. Kitambulisho cha muamala wako kimeorodheshwa karibu na sehemu ya chini ya maelezo ya muamala.

Vitambulisho vya malipo ya usajili mara nyingi huwa katika miundo ifuatayo:

  • 01234567890123456789.token.0123456789012345
  • 0.G.123456789012345
  • Registration-1234ab56-7c89-12d3-4567-8e91234567f8
  • PDS.1234-5678-9012-3456

Muhimu: Unapotoa kitambulisho chako cha muamala wakati wa mchakato wa kutuma maombi ya kuhamisha programu, ondoa sehemu ya kwanza ya kitambulisho cha oda (kwa mfano, futa "0.G." au tarakimu kabla ya maneno "token" au "Usajili").

Masharti ya ziada ya programu mahususi

Mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu

Kwa programu zinazotumia mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu, mmiliki halisi na akaunti lengwa zinaweza kuhitaji kuzingatia usalama wa ufunguo wa upakiaji na wa kuambatisha cheti kwenye programu.

  • Ufunguo wa upakiaji: Ikiwa una tatizo la kutumia ufunguo mmoja wa upakiaji kabla na baada ya uhamishaji, akaunti lengwa inaweza kuhitaji ufunguo mpya wa upakiaji kulingana na maagizo yaliyobainishwa kwenye "Je, ufunguo wako wa kupakia umepotea au umeathiriwa?"
  • Ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu: Ikiwa una tatizo la kutumia ufunguo mmoja wa kuambatisha cheti kwenye programu kabla na baada ya uhamishaji, akaunti lengwa inaweza kuhitaji ufunguo mpya wa kuambatisha cheti kwenye programu kupitia huduma ya kusasisha ufunguo kwa ajili ya usanikishaji mpya. Kisha Google Play itatumia ufunguo mpya ili kuambatisha cheti kwenye programu mpya zinazosakinishwa na masasisho ya programu. Kuna baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kutuma ombi la kusasisha ufunguo. Unaweza kupata maagizo kwenye "Sasisha ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu kwa ajili ya usakinishaji mpya."
Programu zinazolipiwa au programu zenye ununuzi wa ndani ya programu

Ikiwa unahamisha programu zinazolipishwa au programu zenye bidhaa za ndani ya programu, akaunti unayolenga inahitaji kuwa na taarifa za malipo zinazotumika.

Ikiwa unatumia sarafu chaguomsingi tofauti kwenye akaunti yako lengwa, mabadiliko ya sarafu chaguomsingi yatafanyika kiotomatiki:

  • Ununuzi wa ndani ya programu pekee: Baada ya programu yako kuhamishiwa kwenye akaunti yako lengwa, uchapishaji wa programu hiyo utabatilishwa hadi utakapoichapisha tena. Mara baada ya kuthibitisha bei mpya kwenye akaunti yako lengwa, chapisha programu tena.
  • Programu zinazolipiwa: Mabadiliko ya sarafu chaguo-msingi yatatumika kiotomatiki katika bei za programu.

Kidokezo: Ikiwa unahamisha programu zisizolipishwa na umekamilisha hatua za awali, nenda kwenye hatua inayofuata.

Programu zinazotumia huduma zilizounganishwa

Ikiwa programu yako inatumia huduma zozote zilizounganishwa kwenye programu zako, ikiwa ni pamoja na Google Analytics, Firebase na huduma za michezo ya Google Play, hakikisha kuwa umesasisha mipangilio ya akaunti na programu zako.

  • Google Analytics: Weka ruhusa za akaunti yako lengwa kwenye akaunti yako ya Google Analytics.
  • Miradi ya Google Developers Console: Weka akaunti unayolenga kuwa Mmiliki wa miradi yako kwenye Google Developers Console. Miradi hii inaweza kujumuisha kuingia kwa kutumia Google+, huduma za michezo ya Google Play na API zingine za Google.
  • Miradi ya Firebase: Tenganisha miradi yoyote ya Firebase kwenye akaunti ya awali ya Dashibodi ya Google Play na uunganishe miradi hiyo kwenye akaunti unayolenga.
  • Viunganisho vya SDK ya matangazo (ikiwa ni pamoja na AdMob): Baada ya kuhamishia programu zako kwenye akaunti lengwa, ili kuhakikisha kuwa trafiki ya matangazo inawekwa katika akaunti sahihi, viunganisho vyote vya SDK ya matangazo vitahitaji kusasishwa katika faili za APK za programu yako.
  • Tafsiri za APK: Ikiwa una miradi yoyote inayoendelea ya tafsiri inayotumia huduma ya tafsiri kwenye Google Play, sharti ikamilishwe kabla ya kuhamisha programu zako.
  • Google Play ya kikazi: Ili uhamishe programu ya faragha, hakikisha kuwa akaunti unayotaka kuhamishia programu yako inahusiana na shirika lako. Kabla ya kukamilisha kuhamisha, utahitaji kubatilisha uchapishaji wa programu yako kwa muda na uondoe vikwazo vya shirika. Timu yetu ya usaidizi itafanya kazi na wewe ili kupunguza muda ambao programu yako itakosa kuonekana. Watumiaji waliopo bado wataweza kutumia na kuweka upya programu kwenye vifaa wakati uhamisho unaendelea.
    • Kumbuka: Programu binafsi zilizosanidiwa kwa kutumia iFrame ya Google Play ya kikazi haziwezi kuhamishiwa kwenye akaunti tofauti ya msani programu

Kidokezo: Iwapo unahitaji usaidizi kuhusu jinsi ya kuhamisha mradi wa huduma za michezo, wasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Kitakachohamishwa pamoja na programu

  • Watumiaji, takwimu, data, maoni, ukadiriaji, usajili, na mengine yote yanayohusiana na programu pia yatahamishwa.
  • Uagizaji uliofanywa kabla ya programu kuhamishwa utasalia kwenye akaunti ya awali. Ikiwa unahitaji kurejesha pesa za uagizaji huo, sharti urudi kwenye akaunti ya awali au utumie API ya Wasanidi wa Programu wa Google Play.
  • Ripoti zako za uhamishaji mkubwa, ripoti za makadirio ya mauzo, na ripoti za mapato hazitahamishwa pamoja na programu.
  • Ofa hazitahamishiwa kwenye akaunti lengwa, lakini Kuponi za Ofa za awali bado zitaendelea kutumika.
  • Vikundi vya majaribio (jaribio la umma, la watumiaji mahususi, la ndani, na kushiriki ndani) haviwezi kuhamishiwa kwenye akaunti nyingine. Utahitaji kuunda upya vikundi vyovyote vya majaribio ya watumiaji mahususi kwenye akaunti yako mpya, na huenda watumiaji wakahitaji kujisajili upya kwenye jaribio.
  • Ruhusa/mipangilio ya huduma zilizounganishwa haitahamishwa. Hakikisha umesasisha programu zako na mipangilio ya akaunti yako.
  • Hati au taarifa yoyote uliyowasilisha awali itahamishiwa kwenye akaunti mpya ya msanidi programu. Huenda hii ikajumuisha, kwa mfano, taarifa kuhusiana na sera au taarifa nyingine uliyowasilisha kupitia ukurasa wa Maudhui ya programu (Sera > Maudhui ya programu).

Tuma ombi la uhamishaji

Baada ya kukamilisha hatua zilizotajwa hapa juu, unaweza kuwasilisha ombi la kuhamisha programu. Ombi hili litapokelewa na msanidi programu lengwa kwa ajili ya ukaguzi na idhini. Hatimaye, timu yetu ya usadizi hukagua na kujibu maombi ya kuhamisha ndani ya siku mbili za kazi.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5070281728679276393
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false