Angalia takwimu za programu

Unaweza kuangalia takwimu za programu mahususi kupitia programu au toleo la wavuti la Dashibodi ya Google Play.

Kupata na kukagua data ya programu yako

Ripoti zinazopatikana

Kuna kurasa kadhaa katika Dashibodi ya Google Play ambapo unaweza kukagua data ya ukadiriaji, mapato, matukio ya programu kuacha kufanya kazi, mara ambazo programu imesakinishwa na kuondolewa.

  • Ukurasa wa Dashibodi: Muhtasari wa vipimo, mitindo, arifa na maarifa muhimu.
  • Ukurasa wa Takwimu: Ripoti za kina unazoweza kubadilisha upendavyo na zinazojumuisha vipimo muhimu na vipimo vinavyoonyeshwa katika vichupo viwili vifuatavyo:
    • Takwimu za programu: Data halisi ya programu yako unayoweza kutumia kufuatilia utendaji.
    • Linganisha na programu nyingine: Data ya wastani ya utendaji ambayo imewekwa kwenye kipimo cha kawaida, ili uweze kulinganisha na vikundi vya programu zingine.

Dashibodi

Ili uone dashibodi ya programu yako, fanya yafuatayo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uchague programu.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Dashibodi. Utaona sehemu mbalimbali zilizo na kadi zinazoonyesha data ya utendaji wa hivi karibuni wa programu yako na maarifa muhimu yanayolingana na wakati uliowekwa.
    • Karibu na eneo la juu kulia kwenye kila sehemu, unaweza kubofya aikoni za kupanua na kukunja ili uone maelezo yanayokufaa zaidi.
    • Sehemu nyingi zina viungo karibu na majina yake, ambavyo vitakuelekeza kwenye ripoti husika za kina.
    • Katika kadi nyingi, unapata maelezo zaidi kwa kubofya kiungo kilicho karibu na sehemu ya chini kulia kwenye kadi.

Kumbuka: Ili upate maelezo kuhusu kipimo mahususi, wekelea kiashiria juu ya aikoni ya alama ya swali .

Weka mapendeleo kwenye KPI katika dashibodi yako

Unaweza kuweka mapendeleo na kubandika vipimo mahususi vinavyokufaa kwenye sehemu ya KPI zenye mapendeleo katika sehemu ya juu ya dashibodi yako. Hatua ya kuweka mapendeleo kwenye KPI haitabadilisha mipangilio yoyote ya watumiaji wengine katika akaunti yako ya msanidi programu.

Ili uweke mapendeleo kwenye KPI katika dashibodi yako, fanya yafuatayo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uchague programu.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Dashibodi.
  3. Nenda chini kwenye sehemu ya "KPI Zako".
  4. Bofya Chagua KPI.
  5. Vinjari sehemu ya "Vipimo vyote vinavyopatikana" ili upate KPI zako. Unaweza kubuni yako au kuchagua kwenye KPI zinazopendekezwa, ambazo ni pamoja na:
    • Kuongezeka na kupungua kwa idadi ya watumiaji: Data ya watumiaji mahususi, ongezeko la hadhira na watumiaji kuondoa programu.
    • Kuongezeka na kupungua kwa idadi ya vifaa: Usakinishaji kwenye vifaa mahususi, kuondoa programu na masasisho; ongezeko la watumiaji wanaosakinisha.
    • Utendaji kwenye ukurasa wa programu katika Google Play: Waliotembelea na walioshawishika kutokana na ukurasa wa programu yako katika Google Play.
    • Kushiriki: Ripoti za watumiaji wanaoendelea kutumia programu ikiwa ni pamoja na Watumiaji Wanaofungua Programu Kila Siku, Watumiaji Wanaofungua Programu Katika Kipindi cha Siku 28 na watumiaji wanaorejea.
    • Ubora: Maarifa ya ubora wa programu yako, ikiwa ni pamoja na hitilafu za kuacha kufanya kazi, ANR na ukadiriaji.
    • Kadi nyingine za dashibodi: Kadi unazopata katika sehemu nyingine za dashibodi ya programu.
  6. Bofya + Ongeza kwenye KPI ili ubandike kipimo kwenye dashibodi yako na uweke mipangilio inayokufaa. Zingatia yafuatayo:
    • Jina la KPI: Weka jina la kadi linalokusaidia kutambua na kuhusisha haraka KPI na muktadha fulani (kwa mfano, “Vifaa vyangu muhimu zaidi”).
    • Kigezo: Chagua vigezo ambavyo ungependa kuona na kuonyesha. Unaweza kuonyesha chaguo maalum au vipimo vya jumla kama vile "5 Bora," hali ambayo huweka kiotomatiki mipangilio ya chaguo tano bora kutoka kwenye kigezo ulichochagua.
  7. Unapomaliza kuweka KPI zako, unaweza kupanga chaguo kwa kuziburuta na kuzidondosha katika sehemu ya “KPI Zilizochaguliwa”. Pia, unaweza kupanga upya KPI zako hapa baadaye.
  8. Hifadhi mabadiliko uliyofanya.

Kidokezo: Mbali na vipimo vilivyobainishwa hapo juu, unaweza pia kuongeza kigae kingine kwenye dashibodi katika KPI zako. Bofya vitone vitatu katika sehemu ya juu upande wa kulia wa kigae husika, kisha ubofye Ongeza kwenye KPI.

Ukurasa wa takwimu

Kumbuka: Kuanzia Julai 2019, tulifanya mabadiliko makuu kwenye vipimo vyetu ili kufanya takwimu zako zionyeshe maelezo ya kina na zikufae zaidi. Ili upate maelezo zaidi kuhusu mabadiliko haya, tembelea tovuti ya Wasanidi Programu wa Android.

Ili uelewe vyema zaidi utendaji wa programu yako, unaweza kutumia ukurasa wa Takwimu kulinganisha vipimo, kuchagua vipindi maalum na kuangalia data kulingana na vigezo. Unaweza pia kulinganisha vipimo vya viwango vya kuimarika na vikundi vya programu zingine kwenye Google Play ili uelewe utendaji wa programu yako.

Kidokezo: Huenda vipimo vilivyosasishwa vimeathiri jinsi unavyoweka na kuelewa ripoti zako. Tunapendekeza uchukue muda uelewe mabadiliko ili uweze kuweka mipangilio ya vipimo kutengeneza ripoti zinazooana na data yako ya awali.

Weka ripoti yako

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Takwimu.
  2. Ili uone utendaji kamili wa programu yako, usiondoke kwenye kichupo cha Takwimu za programu (kichupo chaguomsingi). Ili uone vipimo na ulinganishaji wa kawaida, chagua kichupo cha Linganisha na Programu Zingine.
  3. Kwenye sehemu ya juu kulia mwa skrini yako, chagua kipindi unachotaka kuangalia.
    • ​Ili ulinganishe data katika vipindi viwili, sogeza swichi ya "Linganisha" kuelekea upande wa kulia hadi itakapobadilika rangi na kuwa samawati kisha uchague kipindi cha pili.
  4. Katika sehemu ya "Weka mipangilio ya ripoti", chagua kipimo ambacho ungependa kuona ukitumia kishale cha chini cha samawati.
    • Kumbuka: Baadhi ya vipimo vina chaguo za kina. Kwa mfano, unaweza kuweka mipangilio ya Data ya watumiaji ili kuonyesha watumiaji wapya, watumiaji wanaorejea tena au watumiaji wote.
  5. Fafanua jinsi kipimo huhesabiwa na kuonyeshwa (kipimo unachochagua kitabainisha chaguo utakazopata). Zingatia yafuatayo:
    • Tumia Aina ya tukio kubainisha unayotaka kuhesabu, ambayo ni kama yafuatayo:
      • Matukio yote: Kila hatua ya tukio, kama vile kila wakati programu yako inasakinishwa.
      • Mahususi: Idadi ya watumiaji au vifaa mahususi vinavyotumika kutekeleza tukio, kama vile idadi ya vifaa mahususi ambako programu yako inasakinishwa.
        • Kumbuka: Chaguo la 'Mahususi' linapatikana tu katika vipimo vya mabadiliko na data ya watumiaji wakati unachagua vipindi vya kila wiki au zaidi.
    • Tumia Hesabu ya vipimo kubainisha jinsi ungependa data ifuatayo ihesabiwe:
      • Kwa kila kipindi: Data inayokusanywa kwa kila kipindi, kama vile idadi ya watumiaji wanaosakinisha programu kwa mara ya kwanza kila mwezi.
      • Wastani wa ununuzi wa programu kwa siku 30: Wastani kutokana na data iliyokusanywa katika siku 30 zilizopita.
    • Tumia Vipindi kubainisha muda ambao ungependa kujumlisha data katika vipindi vifuatavyo:
      • Kila saa (inapatikana tu kwa vipindi visivyozidi siku 30)
      • Kila siku
      • Kila Wiki ya Kalenda
      • Kila Mwezi wa Kalenda
      • Kila baada ya Miezi Mitatu
        • Kumbuka: Vipindi virefu vitatumiwa kwenye baadhi ya vipimo kadri data inavyozidi kupatikana.
  6. Iwapo unataka kuweka kipimo cha pili ili kulinganisha na cha kwanza, bofya Ongeza kipimo. Unaweza kuweka kipimo chako cha pili kwa kutumia utaratibu uliofafanuliwa hapa juu.
  7. Teua kishale cha chini kuchagua vigezo ambavyo unataka kutumia, kama vile nchi au matoleo ya Android, ili kuonekana kwenye chati inayoonyeshwa chini ya chaguo zako.
  8. Iwapo ungependa kuweka kikundi kidogo cha kigezo kama vile nchi au toleo mahususi la Android, bofya Ongeza.

Kuchagua vipimo vyako

Baada ya kuweka mipangilio ya ripoti yako, utaona jedwali na chati iliyo na data ya programu yako katika kipindi ulichochagua. Ili kuangalia data kamili kila siku, chagua tarehe kwenye chati.

Hivi ndivyo vigezo vinavyopatikana kwenye ukurasa wa Takwimu:

  • Toleo la Android: Toleo la mfumo wa Uendeshaji wa Android linaloripotiwa kutoka kwenye kifaa cha mtumiaji
  • Kifaa: Jina Linalotumika Kuuza Kifaa cha Mtumiaji na Jina la Kifaa (k.m. Google Nexus 7/Flo)
  • Nchi: Nchi alipo mtumiaji
  • Lugha: Mipangilio ya lugha ya mtumiaji kwenye Mfumo wa Uendeshaji wa Android
  • Mtoa huduma: Kampuni inayompa mtumiaji huduma ya mtandao usiotumia waya (panapowezekana)
  • Mbinu: Jinsi watumiaji wanavyofungua programu yako inayofunguka papo hapo
    • Kumbuka: Unapoangalia data ya kituo, ukibofya Jaribu Sasa utafungua programu yako inayofunguka papo hapo kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play.
  • Umbo: Umbo la kifaa ambako programu yako imesakinishwa.
  • Toleo la programu: Toleo la programu yako iliyosakinishwa kwenye kifaa cha mtumiaji.

Hifadhi na uangalie ripoti za haraka

Ikiwa utaweka mipangilio ya vipimo na vigezo kwenye ripoti ambayo unataka kutumia tena baadaye, unaweza kuhifadhi mipangilio ya ripoti kwa kuchagua Hifadhi kwenye ripoti za haraka chini ya kipindi cha ripoti.

Baada ya kuongeza kichwa na uhifadhi ripoti yako ya haraka, unaweza kuangalia ripoti zako za haraka kwa kuchagua Ripoti za haraka > Ripoti zilizohifadhiwa karibu na sehemu ya juu ya ukurasa.

Hamisha ripoti yako

Baada ya kuweka mipangilio ya ripoti yako, unaweza kuituma kama faili ya CSV kwa kuchagua Tuma ripoti kando ya jina la chati.

Kutathmini data yako

Angalia jinsi kiwango cha kuimarika kwa programu yako kinavyolinganishwa na programu zingine

Unaweza kutumia kichupo cha Linganisha na Programu Nyingine ili uelewe jinsi vipimo ulivyochagua vinatenda ikilinganishwa na vikundi vya programu nyingine, kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Data ya utendaji kwenye kichupo hiki inalingana na vipimo halisi, hali inayokuruhusu kupima utendaji wako katika maeneo muhimu ya mfumo, ili uweze kujua iwapo programu yako inatenda au haitendi vyema, ikilinganishwa na kikundi cha programu zingine.

Vifuatavyo ni viteuzi viwili vinavyopatikana:

  • Kikundi cha programu zingine Tumia kiteuzi cha kikundi cha Programu zingine ili uchague kundi la programu utakazolinganisha na programu yako.
  • Nchi: Chuja ripoti yako katika nchi au eneo mahususi.

Kumbuka: Data ya ulinganishaji itapatikana wakati kuna programu za kutosha kwenye kikundi cha programu zingine kilichobainishwa ambacho kinalingana na kipimo ulichochagua.

Angalia kwa urahisi vigezo ambavyo vimeathiri zaidi data yako

Chati ya "Uchanganuzi wa mabadiliko" hutathmini kiotomatiki kipindi cha kwanza cha muda ulichochagua na kipindi cha mwisho kilicho na data kamili. Huangazia vigezo ambavyo vimebadilika zaidi ili kukuruhusu uelewe sababu zinazochangia zaidi mitindo ya programu yako.

Vidokezo vya ulinganishaji

Zifuatazo ni njia unazoweza kutumia ulinganishaji wa takwimu ili kuchanganua utendaji wa programu:

  • Linganisha jumla ya watumiaji na mara ambazo programu imesakinishwa kwa kipindi fulani.
  • Linganisha matukio ya programu kuacha kufanya kazi na alama ya wastani ya ukaguzi wa kila siku wa maoni kabla na baada ya kuchapishwa kwa toleo linaloshughulikia uthabiti.
  • Linganisha kiwango cha uondoaji wa programu yako kila siku na wastani wa uondoaji wa programu zilizonunuliwa ndani ya siku 30 ili utathmini jinsi tofauti za kila siku zinavyochangia mitindo ya jumla.
Angalia jinsi matukio yanavyoathiri vipimo vya programu yako

Unaweza kuona jinsi mabadiliko yanayofanywa kwenye programu yako yanavyoathiri vipimo mahususi kwa kutumia ratiba ya matukio yako. Kwa kuunganisha data ya programu yako na tarehe za matukio muhimu, unaweza kuona kwa haraka mambo kama yafuatayo:

  • Jinsi punguzo huathiri mapato.
  • Jinsi usambazaji wa toleo jipya unavyoathiri matukio ya programu kuacha kufanya kazi.
  • Jinsi mabadiliko katika bei ya usajili yanavyoathiri idadi ya wanunuzi.

Baada ya kuweka mipangilio ya ripoti kwenye ukurasa wa Takwimuau Usajili, rekodi ya matukio itaonekana chini ya tarehe kwenye chati yako. Weka kiashiria kielee juu ya kila nukta ili uangalie maelezo kuhusu tukio. Nukta kubwa zinaonyesha matukio mengi katika siku moja.

Vipimo

Baadhi ya vipimo vinahesabiwa kulingana na data kutoka kwa watumiaji ambao wamekubali kushiriki data zao na wasanidi programu kwa ujumla. Vipimo ambavyo tunaweka kwenye Dashibodi ya Google Play vinarekebishwa ili vionyeshe kwa undani data kutoka kwa watumiaji wako wote.

Kidokezo: Ili uone ripoti zilizojumlishwa, unaweza kupakua ripoti za kila mwezi.

Takwimu zinazohusiana na usakinishaji

Data ya usakinishaji wa programu inatokana na Saa za Pasifiki (PT).

Kipimo Ufafanuzi

Watumiaji

Mtumiaji mahususi wa Google Play; mtumiaji anaweza kuwa na vifaa vingi.

Watu wanaoendelea kutumia

Idadi ya watumiaji ambao wamesakinisha programu yako kwenye angalau kifaa chao kimoja na wametumia kifaa katika siku 30 zilizopita.

Data ya watumiaji

Idadi ya watumiaji waliosakinisha programu yako na hawakuwa wameisakinisha kwenye vifaa vingine vyovyote wakati huo. Hii inajumuisha watumiaji wanaoanza kutumia kifaa ambapo programu yako imesakinishwa mapema au vifaa ambako programu imeanza kutumika tena baada ya kusitishwa.

Watumiaji walioondoa programu

Idadi ya watumiaji walioondoa programu yako kwenye vifaa vyao vyote au kuacha kutumia vifaa vyovyote ambako programu yako ilisakinishwa kwa zaidi ya siku 30 (kuifanya iache kutumika).

Watumiaji wapya

Watumiaji waliosakinisha programu yako kwa mara ya kwanza.

Watumiaji wanaorejea

Watumiaji waliosakinisha programu yako tena baada ya kuiondoa hapo awali kwenye vifaa vyao vyote. Hii inajumuisha watumiaji walioanza kutumia programu tena baada ya kuacha kuitumia hapo awali.

Watumiaji wote

Watumiaji wapya na wanaorejea kwa mara nyingine

Vifaa

Kifaa cha Android kinachohusishwa na mtumiaji. Iwapo kifaa kitawekewa mipangilio upya au kuhamishiwa kwa mtumiaji tofauti, kitahesabiwa kuwa kifaa kipya.

Vifaa vinavyotumika

Idadi ya vifaa vinavyotumika ambako programu yako imesakinishwa. Kifaa kinachotumika ni kifaa ambacho kimewashwa angalau mara moja katika siku 30 zilizopita.

Vifaa ambako programu ilisakinishwa

Idadi ya vifaa ambapo watumiaji wamesakinisha programu yako. Hii inajumuisha vifaa ambapo programu yako imesakinishwa mapema.

Vifaa ambako programu iliondolewa

Idadi ya vifaa ambako watumiaji waliondoa programu yako. Hii inajumuisha wakati ambapo kifaa hakijatumika kwa zaidi ya siku 30 (kukifanya kiache kutumika).

Vifaa vipya

Vifaa ambako watumiaji walisakinisha programu yako kwa mara ya kwanza.

Vifaa ambako programu imesakinishwa tena

Vifaa ambako programu yako imesakinishwa na ilikuwa imesakinishwa awali. Hii inajumuisha vifaa ambavyo vilianza kutumika tena baada ya kuacha kutumika hapo awali.

Vifaa vyote

Vifaa ambako programu inawekwa mara ya kwanza na ambako inawekwa mara nyingine.

Masasisho kwenye vifaa

Idadi ya vifaa ambako programu yako imesasishwa.

Kuondolewa kwenye vifaa baada ya kusasishwa

Idadi ya vifaa ambako programu yako iliondolewa baada ya kusasishwa hivi majuzi.

Matukio ya kusakinisha

Mara ambazo programu yako ilisakinishwa, ikijumuisha vifaa ambako programu ilikuwa imesakinishwa mapema. Hii haijumuishi programu zilizosakinishwa mapema au vifaa ambako programu ilianza kutumika tena baada ya kusitishwa.

Matukio ya kuondoa

Mara ambazo programu yako iliondolewa. Hii haijumuishi vifaa ambavyo havitumiki.

Idadi ya Watumiaji Wanaofungua Programu Kila Siku (DAU)

Idadi ya watumiaji waliofungua programu yako kwa siku mahususi.

Idadi ya Watumiaji Wanaofungua Programu Kila Mwezi (MAU)

Idadi ya watumiaji waliofungua programu katika kipindi cha siku 28.

Watumiaji wanaorejea kila mwezi

Idadi ya watumiaji waliofungua programu yako kwa siku mahususi na angalau kwa siku nyingine moja katika kipindi cha siku 28.

Usakinishaji wa programu kutoka kwenye Google Play

Idadi ya watumiaji waliotembelea ukurasa wa programu yako katika Google Play na kusakinisha programu yako, ambao hawakuwa wameisakinisha kwenye kifaa chochote.

Waliotembelea ukurasa wa programu katika Google Play

Idadi ya watumiaji waliotembelea ukurasa wa programu yako katika Google Play ambao hawakuwa wameiweka kwenye kifaa chochote.

Kiwango cha hasara Uwiano wa Watumiaji walioondoa programu (watu walioondoa programu yako kwenye vifaa vyao vyote) ikilinganishwa na Walioweka Programu yako kwenye Kifaa (watu walioweka programu yako kwenye angalau kifaa kimoja kilichowashwa katika siku 30 zilizopita).
Kiwango cha watumiaji wanaorejea kila mwezi Uwiano wa watumiaji wako wanaorejea tena Kila Mwezi (watu waliofungua programu yako katika siku mahususi na angalau siku nyingine moja katika siku 27 zilizopita) ikilinganishwa na Watumiaji Wanaotumia Programu yako Kila Mwezi (watu waliofungua programu yako katika kipindi cha siku 28).
Ukadiriaji

Data ya ukadiriaji inalingana na Saa za Pasifiki (PT).

Kidokezo: Ili upate maelezo zaidi kuhusu ukadiriaji wa programu yako, unaweza kulinganisha na kuchanganua data ya ukadiriaji wa programu yako.

Kipimo Ufafanuzi
Alama za wastani Alama za wastani za nyota ambazo programu yako ilipata kati ya ukadiriaji wote uliowasilishwa.

Kiasi cha ukadiriaji

Idadi ya ukadiriaji uliowasilishwa.
Jumla ya alama za wastani Alama za wastani za nyota ambazo programu yako imepata kati ya ukadiriaji wote ambao umewasilishwa ikijumuisha siku iliyopita. Kwa kila mtumiaji anayewasilisha ukadiriaji, tutazingatia tu ukadiriaji wa programu wa hivi karibuni pekee.
Ukadiriaji wa Google Play Ukadiriaji wako wa sasa unaoonyeshwa kwa watumiaji kwenye Google Play. Unahesabiwa kulingana na ukadiriaji wako wa hivi karibuni.
Mapato

Data ya fedha inatolewa kulingana na saa za eneo la UTC. Unaweza kuangalia data ya fedha iwapo una ruhusa ya Kuangalia data ya fedha.

Kidokezo: Ili upate maelezo zaidi kuhusu mapato ya programu yako, unaweza kuangalia uchanganuzi wa kina wa mapato.

Kipimo Ufafanuzi

Mapato

Jumla ya mapato katika muda uliochaguliwa, ikijumuisha mauzo yoyote yaliyofanyika, bidhaa za ndani ya programu na usajili. Data ya mapato inalingana na makadirio ya mauzo (kiasi kinacholipwa na wanunuzi, ikiwa ni pamoja na kodi).

Jumla ya mapato

Jumla ya mapato ambayo programu yako imezalisha tangu izunduliwe. Hii inatokana na makadirio ya mauzo na inajumuisha ushuru wowote au ada nyinginezo.
Wanunuzi Idadi ya watumiaji mahususi ambao walinunua bidhaa katika programu yako.
Wanunuzi wapya

Idadi ya watumiaji mahususi ambao walinunua bidhaa katika programu yako kwa mara ya kwanza.

Jumla ya wanunuzi

Jumla ya watumiaji mahususi waliowahi kununua bidhaa katika programu yako.

Mapato ya wastani kwa kila Mtumiaji Anayefungua Programu Kila Siku

Mapato ya jumla ya kila siku yakigawanywa na Idadi ya Watu Wanaotumia Kila Siku. Sarafu yote ni USD, saa za eneo ni PST8PDT, ili kuwezesha ulinganishaji na programu zingine.

Mapato ya wastani kwa kila Mtumiaji Anayefungua Programu Kila Siku

Jumla ya mapato katika kipindi cha siku 28 ikigawanywa na Idadi ya Watumiaji Wanaofungua Programu Kila Mwezi (ununuzi wa programu kwa siku 28). Sarafu yote ni USD, saa za eneo ni PST8PDT, ili kuwezesha ulinganishaji na programu zingine.

Ununuzi kwa kila Mtumiaji Anayefungua Programu Kila Siku

Idadi ya ununuzi wa kila siku ikigawanywa na Idadi ya Watumiaji Wanaofungua Programu Kila Siku.

Ununuzi kwa kila Mtumiaji Anayefungua Programu Kila Mwezi

Jumla ya ununuzi kwa kipindi cha siku 28 ikigawanywa na Idadi ya Watumiaji Wanaofungua Programu Kila Mwezi (ununuzi wa programu kwa siku 28).

Ununuzi kwa kila mnunuzi wa kila siku

Idadi ya wastani ya ununuzi unaofanywa kila siku na wanunuzi wa kila siku (watumiaji wanaonunua angalau mara moja kwa siku).

Ununuzi kwa kila mnunuzi wa kila mwezi

Idadi ya wastani ya ununuzi uliofanywa katika siku 28 na wanunuzi wa kila mwezi (watu wanaonunua angalau mara moja katika kipindi cha siku 28).

Uwiano wa wanunuzi wa kila siku

Asilimia ya Watu Wanaotumia Programu Kila Siku ambao walinunua angalau mara moja siku hiyo.

Uwiano wa wanunuzi wa kila mwezi

Asilimia ya Idadi ya Watu Wanaotumia Programu yako Kila Mwezi (watu wanaofungua programu yako angalau mara moja katika siku 28) ambao walinunua angalau mara moja katika kipindi cha siku 28.

Thamani ya wastani ya ununuzi wa kila siku

Mapato ya jumla ya kila siku yakigawanywa na idadi iliyonunuliwa siku hiyo.

Thamani ya wastani ya ununuzi wa kila mwezi

Mapato yote ya siku 28 yakigawanywa na idadi ya ununuzi katika kipindi hicho.

Hitilafu za kuacha kufanya kazi na programu isiyorejesha majibu (ANR)

Data ya matukio ya programu kuacha kufanya kazi na ANR inalingana na Saa za Pasifiki (PT).

Kidokezo: Ili upate maelezo zaidi kuhusu ANR na matukio ya programu yako kuacha kufanya kazi, unaweza kuangalia data kuhusu hitilafu mahususi na kufumbua ufuatiliaji wa rafu za matukio ya kuacha kufanya kazi.

Kipimo Ufafanuzi
Programu kuacha kufanya kazi Ripoti za programu kuacha kufanya kazi zilizokusanywa kutoka vifaa vya Android, ambako watumiaji wake wamejijumuisha kushiriki kiotomatiki data ya matumizi na uchunguzi.
ANR Ripoti za Programu isiyofanya kazi (ANR) zilizokusanywa kutoka kwenye vifaa vya Android, ambako watumiaji wake wamejijumuisha kushiriki kiotomatiki data ya matumizi na uchunguzi.
Programu za Android zinazofunguka papo hapo

Ikiwa umechapisha Programu ya Android Inayofunguka Papo Hapo, data ifuatayo inapatikana kwenye ukurasa wa Takwimu. Data ya Programu za Android zinazofunguka papo hapo inatolewa kulingana na Saa za Pasifiki (PT). Ili kusambaza programu ya papo hapo, pata maelezo kuhusu jinsi ya kubuni na kusambaza toleo.

Kumbuka: Kwa sababu za faragha, Google haionyeshi data ya programu inayofunguka papo hapo wakati kuna idadi ndogo ya watumiaji.

Kipimo Ufafanuzi
Jumla ya vifaa ambapo programu ilitumika Idadi ya vifaa mahususi ambapo programu yako inayofunguka papo hapo imefunguliwa angalau mara moja kila siku.
Matukio ya matumizi Mara ambazo programu yako inayofunguka papo hapo imefunguliwa kila siku.
Matukio ya kushawishika kwa wateja Mara ambazo programu yako imesakinishwa kwa siku kwenye kifaa ambapo programu yako inayofunguka papo hapo ilifunguliwa awali.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Kompyuta Android

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3843688675723174629
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false