Viwango vya kodi na kodi ya ongezeko la thamani (VAT)

Katika baadhi ya nchi, bei zinazoonyeshwa kwa wanunuzi kwenye kurasa za maelezo na utafutaji lazima zilingane na kiasi kinacholipwa. Hii ina maana kwamba kodi zote (ikiwa ni pamoja na VAT) lazima zijumuishwe kwenye bei.

Kwa sasa tunatoa uwezo wa kuorodhesha bei zinazojumuisha kodi katika nchi zifuatazo:

Albania, Armenia, Australia, Austria, Azabajani, Bahareni, Bangladeshi, Belarusi, Ubelgiji, Bermuda, Bosnia na Hezegovina, Brazili, Visiwa vya Virgin vya Uingereza, Bulgaria, Kameruni, Chile, Kolombia, Korasia, Kuprosi, Zechia, Denmaki, Misri, Estonia, Ufini, Ufaransa, Jojia, Ujerumani, Ghana, ugiriki, Hungaria, Aisilandi, India, Ayalandi, Israeli, Italia, Japani, Kazakistani, Kenya, Lativia, Lishenteni, Litwania, Lasembagi, Malesia, Malta, Meksiko, Moldova, Montenegro, Moroko, Nepali, Uholanzi, Nyuzilandi, Naijeria, Norwe, Omani, Polandi, Ureno, Pwetoriko, Jamhuri ya Masedonia Kaskazini, Romania, Urusi, Saudia, Senegali, Sabia, Singapoo, Slovakia, Slovenia, Afrika Kusini, Korea Kusini, Uhispania, Sirilanka, Uswidi, Uswisi, Taiwani, Tajikistani, Tanzania, Tailandi, Uturuki, Uganda, Ukraini, Muungano wa Falme za Kiarabu, Uingereza, Urugwai, Uzibekistani na Zimbabwe.

Mwongozo wa maeneo na nchi mahususi

Mwongozo huu unafafanua kuhusu utaratibu wa kodi katika Google Play. Google haiwezi kukupa ushauri wa kodi. Tafadhali wasiliana na mshauri wako wa kodi ili upate mwongozo kuhusu jinsi kodi zinavyoweza kukuathiri na kuathiri mauzo yako kwa wateja kwenye Google Play.

Australia

Wasanidi programu walio Australia

Ikiwa unaishi nchini Australia, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma GST kwa ununuzi wa ndani ya programu na programu zote zinazolipiwa, zilizonunuliwa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Australia.

Iwapo hujasajiliwa kwenye GST, Google inaweza kutoza asilimia 10 ya GST kwenye ada ya huduma unayolipa Google. Tozo ya asilimia 10 ya GST itaonyeshwa tofauti na ada ya huduma pale inapotumika.

Hali yako ya usajili wa kodi hubaini kodi unazotozwa nchini Australia. Unaweza kuipa Google taarifa za kodi za Australia kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo   (Mipangilio Mipangilio > Taarifa za malipo).
  2. Katika sehemu ya "Mipangilio", bofya Dhibiti mipangilio.
  3. Nenda chini hadi kwenye "Taarifa za kodi za Australia" na ubofye aikoni ya penseli Aikoni ya penseli / aikoni ya kubadilisha.
  4. Chagua kisanduku cha kuteua cha taarifa na uweke Namba yako ya Biashara ya Australia (ABN) katika sehemu ya "Namba ya Biashara ya Australia".
  5. Bofya Hifadhi.

Wasanidi programu wasioishi nchini Australia

Kutokana na sheria za kodi za Australia, Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma asilimia 10 ya Kodi ya Bidhaa na Huduma (GST) kwenye mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Australia kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play. Huhitaji kukokotoa na kutuma GST kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Australia.

Kwa ununuzi unaofanywa na watumiaji wanaoishi nchini Australia kwa kutumia mfumo mbadala wa utozaji, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma Kodi yoyote ya Bidhaa na Huduma (GST) inayostahili kulipwa ya miamala iliyofanyika kwa mamlaka husika.

Bahareni

Wasanidi programu wanaoishi Bahareni

Ikiwa unaishi Bahareni, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Bahareni.

Wasanidi programu wasioishi Bahareni

Kutokana na sheria za kodi za Bahareni, Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa mamlaka husika, kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Bahareni.

Huhitaji kukokotoa na kutuma VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Bahareni.

Ikiwa unaishi nchini Bahareni, tozo ya VAT ya eneo husika haitakatwa kwenye ada ya huduma unayolipa Google, lakini huenda ukahitaji kutathmini tozo ya VAT.
Bangladeshi

Miamala inayofanyika kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play

Kwa programu inayolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa na wateja walio nchini Bangladeshi kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play, Google ina wajibu wa kubainisha, kutoza na kuwasilisha kodi ya VAT. Wasanidi programu hawahitaji kukokotoa na kutuma kodi ya VAT kwa utaratibu tofauti.

Miamala inayofanyika kwa kutumia mfumo mbadala wa utozaji

Wasanidi programu wanaoishi nchini Bangladeshi

Kwa ununuzi unaofanywa na wateja wako kwa kutumia mfumo mbadala wa utozaji katika masoko yanayoruhusu mfumo mbadala wa utozaji, Google inaweza kuomba Nambari yako ya VAT. Ikiwa hutaipatia Google tarakimu 13 za Nambari ya VAT ya Bangladeshi inapokuomba, Google itakutoza kodi ya VAT inayokatwa kwenye ada ya huduma unayolipa Google. Tozo ya VAT itaonyeshwa kando na ada ya huduma, pale inapotumika.

Wasanidi programu walio nje ya Bangladeshi

Google haiwajibiki na kodi za nchini Bangladeshi zinazokatwa katika ada ya huduma unayolipa Google.

Belarusi

Wasanidi programu walio nchini Belarusi

Ikiwa unaishi Belarusi, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa ununuzi wa ndani ya programu na programu zote zinazolipiwa zilizonunuliwa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Belarusi.

Ikiwa wewe ni Mjasiriamali Binafsi aliye Belarusi, Google itatumia tozo ya VAT ya eneo husika kwenye ada ya huduma. Kiasi cha VAT kitaonyeshwa tofauti na kiasi cha ada ya huduma.

Ikiwa wewe ni shirika la Biashara lililo Belarusi, Google haitatumia tozo ya VAT ya eneo husika kwenye ada ya huduma, lakini huenda ukahitaji kutathmini tozo ya VAT. 

Hali yako ya kodi hubaini kodi unazotozwa nchini Belarusi. Unaweza kuipa Google taarifa ya kodi ya Belarusi kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo  
  2. Katika sehemu ya "Mipangilio", bofya Dhibiti mipangilio.
  3. Sasisha taarifa yako ya kodi ya Belarusi.
  4. Bofya Hifadhi.

Wasanidi programu wasioishi Belarusi

Kutokana na sheria za kodi za nchini Belarusi, Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma malipo ya VAT kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Belarusi.

Ikiwa huishi nchini Belarusi, huhitaji kukokotoa na kutuma VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Belarusi.

Kambodia

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT ya Kambodia kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja walio Kambodia.

Wasanidi programu wanaoishi nchini Kambodia

Ikiwa unaishi Kambodia na hujawasilisha kwa Google TIN yako ya VAT ya Kambodia, Google itakutoza na kutuma kwa mamlaka husika asilimia 10 ya VAT kwa ada ya huduma inapohitajika. Ada ya VAT ya asilimia 10 itaonekana kando na ada ya huduma.

Taarifa zako za kodi hubainisha kodi unazotozwa nchini Kambodia. Unaweza kuipatia Google taarifa zako za kodi za Kambodia kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Ingia katika Kituo cha malipo ya Google.
  2. Chagua Mipangilio kwenye menyu ya juu.
  3. Kwenye sehemu ya "Maelezo ya TIN ya VAT ya nchini Kambodia", bofya aikoni ya kalamu Badilisha na uweke TIN yako ya VAT ya Kambodia.
  4. Bofya Hifadhi.
Kameruni

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Kameruni. Iwapo unaishi Kameruni, Google hutoza VAT kwenye ada za huduma zinazotozwa kutokana na kupanuliwa kwa mamlaka ya kodi nchini Kameruni, ambayo itaonekana kando na ada za huduma.

Kanada

Wasanidi programu Wanaoishi Kanada wasio na Nambari ya GST/HST au Wanaoishi nje ya Kanada

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma Kodi ya Bidhaa na Mauzo (GST) au Kodi Jumuishi ya Mauzo (HST) kwa ununuzi wa programu zote zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Kanada, ikiwa unaishi Kanada na hujaipatia Google nambari yako ya GST/HST au ukiwa unaishi nje ya Kanada.

Ikiwa unaishi Kanada na hujajisajili chini ya mfumo wa kawaida wa GST au HST, Google itatumia GST au HST kwenye ada ya huduma. Kiasi cha GST au HST kitaonyeshwa tofauti na ada ya huduma.

Wasanidi programu Wanaoishi Kanada walio na Nambari ya GST au HST

Una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma GST au HST kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Kanada, ikiwa unaishi Kanada na umeipatia Google nambari ya GST au HST.

Ikiwa unaishi Kanada na umejisajili chini ya mfumo wa kawaida wa GST au HST, unapaswa kuipatia Google nambari yako ya GST au HST ili usitozwe GST au HST kwenye ada ya huduma.

British Columbia

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma Kodi ya Mauzo ya Wilaya ya British Columbia (BC PST) kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi British Columbia.

Iwapo unaishi British Columbia, Google itatumia BC PST kwenye ada ya huduma. Kiasi cha BC PST kitaonyeshwa kando na ada ya huduma.

Manitoba

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza pamoja na kutuma Kodi ya Mauzo ya Rejareja ya Manitoba (MB RST) kwa programu zote zinazolipishwa za Google Play na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa na wateja wanaoishi Manitoba. Ikiwa hapo awali ulikuwa unakusanya MB RST kupitia Dashibodi ya Google Play, huwezi tena kudhibiti mipangilio hii.

Quebec

Wasanidi programu Wanaoishi Kanada wasio na Nambari ya Ushuru ya Quebec au Wanaoishi Nje ya Kanada

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma Kodi ya Mauzo ya Quebec (QST) kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Quebec, ikiwa unaishi Kanada na hujaipatia Google nambari yako ya ushuru ya Quebec au ukiwa unaishi nje ya Kanada.

Ikiwa unaishi Quebec na hujajisajili chini ya mfumo wa kawaida wa QST, Google itatumia QST kwenye ada ya huduma. Kiasi cha QST kitaonyeshwa kando na ada ya huduma.

Wasanidi programu Wanaoishi nchini Kanada wenye Nambari ya Ushuru ya Quebec

Una jukumu la kubaini, kutoza na kuwasilisha QST kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Quebec ikiwa unaishi Kanada na umeipa Google nambari ya ushuru ya Quebec.

Ikiwa unaishi Quebec na umejisajili chini ya mfumo wa kawaida wa QST, unapaswa kuipatia Google nambari yako ya QST ili usitozwe QST kwenye ada ya huduma.

Saskatchewan

Google ina jukumu la kubaini, kutoza na kuwasilisha Kodi ya Mauzo ya Wilaya ya Saskatchewan (SK.PST) kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Saskatchewan.

Kusasisha Maelezo ya Usajili wa Kodi nchini Kanada

Kwa madhumuni ya ushuru wa Kanada, Google inahitaji taarifa yako ya kodi ya Kanada. Ikiwa hutatoa namba ya ushuru, Google itachukulia kwamba hujasajiliwa na kubadilisha mipangilio ya Dashibodi ya Google Play ipasavyo. Unaweza kuipa Google taarifa za kodi za Kanada kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo (Mipangilio Mipangilio > Taarifa za malipo).
  2. Katika sehemu ya "Mipangilio", bofya Dhibiti mipangilio.
  3. Nenda chini kwenye "Taarifa za kodi za Kanada" kisha ubofye aikoni ya penseli Aikoni ya penseli / aikoni ya kubadilisha.
  4. Weka au usasishe:
    • Nambari ya Usajili ya GST/HST
    • Nambari ya Usajili ya QST
  5. Bofya Hifadhi.
Chile

Wasanidi programu wanaoishi nchini Chile

Iwapo unaishi nchini Chile, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Chile.

Vinginevyo, iwapo hujasajiliwa kulipia VAT, Google itatoza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 19 kwenye ada ya huduma inayotozwa kutokana na kupanuliwa kwa wigo wa sheria ya kodi nchini Chile. Ada ya VAT ya asilimia 19 itaonyeshwa tofauti na ada ya huduma.

Hali yako ya usajili wa kodi hubainisha kodi unazotozwa nchini Chile. Unaweza kufuata utaratibu huu ili kuipa Google hali yako ya usajili wa kodi ili ibaini iwapo itatoza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT):

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo   (Mipangilio Mipangilio > Taarifa za malipo).
  2. Katika sehemu ya "Mipangilio", bofya Dhibiti mipangilio.
  3. Nenda chini hadi kwenye "Taarifa za kodi ya Chile" kisha ubofye aikoni ya penseli Aikoni ya penseli / aikoni ya kubadilisha.
  4. Weka maelezo yafuatayo:
    • Je, umejisajili nchini Chile kuwa unayelipa kodi ya VAT?
      • Chagua Ndiyo iwapo umejisajiliwa.
    • Je, umeruhusiwa kutotozwa kodi ya ziada (Impuesto adicional)?
      • Chagua Ndiyo iwapo umeruhusiwa.
  5. Bofya Hifadhi.

Wasanidi programu wasioishi nchini Chile

Kutokana na sheria za kodi za Chile, Google ina jukumu la kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa mamlaka husika, kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Chile. Huhitaji kukokotoa na kutuma VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Chile.

Kolombia

Wasanidi programu wanaoishi nchini Kolombia

Iwapo unaishi nchini Kolombia, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Kolombia..

Iwapo hujasajiliwa kulipia VAT (hujasajiliwa chini ya mfumo wa jumla wa kodi), Google itatoza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 19 kwenye ada ya huduma inayotozwa kutokana na kupanuliwa kwa wigo wa sheria ya kodi nchini Kolombia. Ada ya VAT ya asilimia 19 itaonyeshwa tofauti na ada ya huduma.

Taarifa zako za mlipa kodi ndizo zitakazobainisha kodi unazotozwa nchini Kolombia. Unaweza kufuata utaratibu huu ili kuipa Google hali yako ya usajili wa kodi ili ibaini iwapo itatoza kodi ya ongezeko la thamani (VAT):

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo   (Mipangilio Mipangilio > Taarifa za malipo).
  2. Katika sehemu ya “Mipangilio” , bofya Dhibiti Mipangilio.
  3. Nenda chini hadi kwenye "Maelezo ya kodi ya Kolombia" na ubofye aikoni ya penseli Aikoni ya penseli / aikoni ya kubadilisha.
  4. Weka maelezo yafuatayo:
    • Je, umesajiliwa chini ya Mfumo wa jumla wa kodi?
      • Chagua Ndiyo iwapo umejisajiliwa.
    • Numero de Identificación Tributaria (NIT)
      • Weka NIT yako ya Kolombia.
    • Tafadhali pakia fomu yako ya RUT (Fomu Mahususi ya Usajili wa Kodi)
      • Bofya Chagua Faili na upakie hati yako ya RUT katika muundo wa PDF.
  5. Bofya Hifadhi.

Wasanidi programu wasioishi nchini Kolombia

Iwapo huishi nchini Kolombia na unauza programu zinazolipishwa au ununuzi wa ndani ya programu kwa wateja nchini Kolombia, utaendelea kuwa na wajibu wa kutoza, kutuma na kuripoti VAT yoyote kwa mamlaka za kodi za Kolombia.

 

Misri

Wasanidi programu wote

Google ina jukumu la kubaini, kutoza na kuwasilisha VAT ya Misri kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja walio Misri.

Wasanidi programu walio Misri

Ikiwa unaishi Misri na hujasajiliwa kulipia VAT, Google itatoza VAT kwenye ada ya huduma. Kiasi cha VAT kitaonyeshwa tofauti na kiasi cha ada ya huduma. 

Ikiwa umesajiliwa kulipia VAT nchini Misri na kuipa Google taarifa zako za kodi, Google haitatoza VAT ya eneo kwenye ada ya huduma, lakini huenda ukahitaji kutathmini VAT mwenyewe.

Hali yako ya kodi hubaini kodi unazotozwa nchini Misri. Unaweza kuipa Google taarifa za kodi za Misri kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo.
  2. Katika sehemu ya "Mipangilio", bofya Dhibiti mipangilio.
  3. Nenda chini hadi kwenye "taarifa za kodi za Misri" na ubofye aikoni ya penseli.
  4. Sasisha taarifa zako za kodi.
  5. Bofya Hifadhi.
Umoja wa Ulaya

Wasanidi programu wote

Kutokana na sheria za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika Umoja wa Ulaya (EU), Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kuwasilisha kodi ya VAT ya ununuzi wa maudhui yote dijitali ya Duka la Google Play unaofanywa na wateja walio katika Umoja wa Ulaya kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play. Google itatuma kwa mamlaka husika kodi za VAT za ununuzi unaofanywa na wateja walio katika Umoja wa Ulaya kwenye mfumo wa utozaji wa Google Play.

Huhitaji kukokotoa na kutuma kodi ya VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja walio katika Umoja wa Ulaya (EU) wanaotumia mfumo wa utozaji wa Google Play. Tutatumia masharti haya ya VAT hata ikiwa huishi katika eneo la Umoja wa Ulaya (EU).

Kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi katika Umoja wa Ulaya wanaotumia mfumo mbadala wa utozaji kama sehemu ya jaribio la chaguo mbadala la utozaji au mpango mbadala wa utozaji bila kujumuisha chaguo kwa mtumiaji, una wajibu wa kubaini, kutoza na kuwasilisha malipo yoyote ya VAT yanayostahili kulipwa ya miamala iliyofanyika kwa mamlaka husika.

Wasanidi programu walio Umoja wa Ulaya

Iwapo unaishi katika nchi iliyopo kwenye Umoja wa Ulaya (EU) isipokuwa Ayalandi, Google haitakutoza VAT ya eneo husika kwa utoaji (kwa madhumuni ya VAT) wa programu yako kwenye Google. Ikiwa unaishi Ayalandi, una wajibu wa kutoza VAT ya Ayalandi kwa utoaji (kwa madhumuni ya VAT) wa programu yako kwenye Google.

Ikiwa unaishi Ayalandi na unauza kwa wateja ukitumia mfumo mbadala wa utozaji kama sehemu ya jaribio la chaguo mbadala la utozaji au mpango mbadala wa utozaji bila kujumuisha chaguo kwa mtumiaji, Google itatoza VAT ya Ayalandi kwenye ada ya huduma ya miamala hiyo ya mfumo mbadala wa utozaji.

Viwango vya VAT vinavyotumika kwa ununuzi unaofanywa katika Umoja wa Ulaya (EU) kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play

Hivi ndivyo unavyoweza kuangalia viwango vya VAT vinavyotumika katika ununuzi wa programu na maudhui kwa wateja walio katika Umoja wa Ulaya (EU).

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo   (Mipangilio Mipangilio > Taarifa za malipo).
  2. Katika sehemu ya "Kodi ya mauzo", bofya Dhibiti kodi ya mauzo.
  3. Chini ya "Ulaya," kagua orodha ya nchi na viwango vya kodi.
Ghana

Wasanidi programu wote

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT ya Ghana kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Ghana.

Wasanidi programu walio Ghana

Ikiwa unaishi Ghana, Google itatumia tozo la VAT ya nchini kwenye ada ya huduma. Kiasi cha VAT kitaonyeshwa tofauti na kiasi cha ada ya huduma.

Aisilandi

Wasanidi programu wote

Google inawajibikia kubaini, kutoza na kuwasilisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa programu zote zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu wa maudhui dijitali na huduma unaofanywa na wateja walio Aisilandi kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play. Google itatuma kodi za VAT za ununuzi unaofanywa na wateja walio Aisilandi kwenye mfumo wa utozaji wa Google Play kwa mamlaka husika. Huhitaji kukokotoa na kutuma kodi za VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi Aisilandi kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play.

Kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi Aisilandi kwa kutumia mfumo mbadala wa utozaji ikiwa ni sehemu ya jaribio la utozaji la chaguo la mtumiaji au mpango wa utozaji mbadala bila kujumuisha chaguo la mtumiaji, una wajibu wa kubaini, kutoza na kuwasilisha malipo yoyote ya VAT yanayostahili kulipwa ya miamala iliyofanyika kwa mamlaka husika.

Wasanidi programu wanaoishi nchini Aisilandi

Ikiwa unaishi nchini Aisilandi, tozo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya eneo husika haitatumika kwenye ada ya huduma unayolipa Google, lakini huenda ukahitaji kutathmini Kodi ya Ongezeko la Thamani.

India

Wasanidi programu wanaoishi nchini India

Ikiwa unaishi nchini India, ni wajibu wako kubaini iwapo unahitaji Nambari ya Utambulisho wa Mlipakodi ya Bidhaa na Huduma (GSTIN) na kubaini kodi zozote husika. Ni wajibu wako kubaini na kulipa kodi inayohusiana na ada za huduma za Google Play zinazotozwa na Google.

Kutokana na sheria za kodi nchini India, Google kama mtoa huduma za masoko ina wajibu wa kutoza na kuweka kodi husika ya zuio na GST TCS (Kodi Inayotozwa wakati wa Ununuzi), ikiwa ipo, kwenye akaunti ya programu na michezo inayolipishwa (ikijumuisha ununuzi wa ndani ya programu) unayouza.

Wasanidi programu wasioishi nchini India

Kutokana na sheria za kodi nchini India, Google ikiwa kama mtoa huduma za masoko, kwa niaba yako ina wajibu wa kubaini, kutoza na kulipa Kodi ya Bidhaa na Huduma pamoja na Tozo ya Moja kwa Moja ya programu zote zinazolipishwa katika Duka la Google Play na ununuzi unaofanywa wa ndani ya programu na wateja wanaoishi nchini India. Kwa ununuzi unaofanywa na wateja kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play, Google itatoza Kodi ya Bidhaa na Huduma (GST) na Tozo ya Moja kwa Moja kwenye mapato yako na kulipa ada na ushuru huo kwa mamlaka husika. Tozo ya Moja Kwa Moja itaonyeshwa kwenye ripoti ya mapato yako kama "Tozo ya Moja kwa Moja ya India."

Kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini India kupitia mfumo mbadala wa utozaji, Google itakutoza kodi na ada husika au zinazotokana na ununuzi wa ndani ya programu uliofanywa na wateja wanaoishi nchini India ambazo huchakatwa kwenye mifumo mbadala ya utozaji. Google italipa ada na ushuru huo kwa mamlaka husika.

Maudhui yanayohusiana

Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye Kodi ya Bidhaa na Huduma Nchini India.

Indonesia

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma asilimia 11 ya VAT kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Indonesia kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play. Wasanidi programu hawahitaji kukokotoa na kutuma VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na watumiaji wanaoishi nchini Indonesia kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play.

Kwa ununuzi unaofanywa na watumiaji wanaoishi nchini Indonesia kwa kutumia mfumo mbadala wa utozaji, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma malipo yoyote ya VAT yanayostahili kulipwa ya miamala iliyofanyika kwa mamlaka husika. Pia, una wajibu wa kutoa ankara za ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Indonesia kwa kutumia mfumo mbadala wa utozaji.

Wasanidi programu wanaoishi nchini Indonesia

Google itatoza na kutuma asilimia 11 ya VAT ya ada ya huduma yenye ankara kwa mamlaka husika, pale inapotumika. Ada ya VAT ya asilimia 11 itaonyeshwa kando na ada ya huduma.

Japani

Kama unatoa programu zinazolipishwa au ununuzi wa ndani ya programu kwa wateja nchini Japani, kuanzia tarehe 1 Oktoba 2015, mabadiliko katika Sheria ya Kodi ya Matumizi ya Japani (JCT) yataathiri majukumu yako ya kodi nchini Japani. Kama una maswali mahususi yanayohusiana na majukumu yako ya kodi nchini Japani, wasiliana na mshauri wako wa kodi.

Wasanidi programu wasioishi Japani

Kama huishi nchini Japani na unauza programu zinazolipishwa au ununuzi wa ndani ya programu kwa wateja nchini Japani, una wajibu wa kutoza, kuwasilisha na kuripoti kodi yoyote ya JCT kwa Shirika la Taifa la Kodi nchini Japani.

Wasanidi programu wanaoishi nchini Japani

Iwapo unaishi nchini Japani na unatoa programu zinazolipishwa au huduma ya ununuzi wa ndani ya programu kwa wateja wanaoishi nchini Japani, una wajibu wa kutoza, kutuma na kuripoti kodi yoyote ya JCT inayostahili kulipwa kwa Shirika la Taifa la Kodi nchini Japani.

Kando ya hayo, ada ya huduma ya Google Play inayotozwa na Google inachukuliwa kuwa muamala wa biashara kwa biashara (B2B).

Una wajibu wa kutathmini na kuripoti JCT ya huduma za Biashara kwa Biashara (B2B) zinazotolewa na biashara ya kigeni kwa Shirika la Taifa la Kodi nchini Japani. JCT haitawekwa kiotomatiki kwenye ada za huduma za programu yako.

Kenya

Wasanidi programu wote

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT ya Kenya kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja walio nchini Kenya.

Wasanidi programu wanaoishi nchini Kenya

Ikiwa unaishi Kenya, Google itatumia tozo ya VAT ya eneo husika kwenye ada ya huduma. Kiasi cha VAT kitaonyeshwa tofauti na kiasi cha ada ya huduma.

 

Lishenteni

Google inawajibikia kubaini, kutoza na kuwasilisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika programu zote zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu wa maudhui dijitali na huduma unaofanywa na wateja walio Lishenteni kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play. Google itatuma kwa mamlaka husika kodi ya VAT ya ununuzi unaofanywa na wateja walio Lishenteni kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play. Huhitaji kukokotoa na kutuma kodi za VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi Lishenteni kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play.

Kwa ununuzi unaofanywa na wateja waliopo Lishenteni kwa kutumia mfumo mbadala wa utozaji ikiwa ni sehemu ya jaribio la chaguo mbadala la utozaji au mpango mbadala wa utozaji bila kujumuisha chaguo kwa mtumiaji, una wajibu wa kubaini, kutoza na kuwasilisha malipo yoyote ya VAT yanayostahili kulipwa ya miamala iliyofanyika kwa mamlaka husika.

Malesia

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma kodi ya huduma kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Malesia. Huhitaji kukokotoa na kutuma kodi ya huduma kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Malesia.

Wasanidi programu wanaoishi nchini Malesia

Google itatoza na kutuma asilimia 8 ya kodi ya huduma kwa mamlaka husika, inapohitajika. Kodi ya huduma ya asilimia 8 itaonyeshwa tofauti na ada ya huduma.

Meksiko

Wasanidi programu walio nchini Meksiko

Iwapo unaishi Meksiko, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa ununuzi wote wa maudhui dijitali katika Duka la Google Play unaofanywa na wateja walio Meksiko.

Kuanzia tarehe 1 Agosti 2020, Google itatoza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 16 kwenye ada ya huduma inayotozwa kutokana na kupanuliwa kwa mamlaka ya kodi nchini Meksiko. Ada ya VAT ya asilimia 16 itaonekana kando na ada ya huduma.

Wasanidi programu wasioishi Meksiko

Kuanzia tarehe 1 Aprili 2021, iwapo unaishi nje ya Meksiko, Google ina jukumu la kubaini, kutoza na kuwasilisha asilimia 16 ya VAT kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Meksiko.

Huhitaji kukokotoa na kutuma VAT kando kwa wateja wanaoishi nchini Meksiko.

Moldova

Wasanidi programu walio nchini Moldova

Iwapo unaishi nchini Moldova, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya Moldova kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Google Play na wateja wanaoishi nchini Moldova.

Wasanidi programu wasioishi nchini Moldova

Iwapo unaishi nje ya Moldova Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT ya Moldova kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Moldova. Huhitaji kukokotoa na kutuma VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Moldova.  

Google haiwezi kukupa ushauri wa kodi na unapaswa kuwasiliana na mshauri wako wa masuala ya kodi.

Nepali

Wasanidi programu wote

Google ina jukumu la kubaini, kutoza na kuwasilisha VAT ya Nepali kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja walio nchini Nepali.

Naijeria

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT ya Naijeria kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Naijeria.

Ikiwa unaishi nchini Naijeria, Google pia hutoza VAT kwenye ada ya huduma inayotozwa kwa ununuzi unaofanywa na wateja duniani kote. Tozo ya VAT itaonyeshwa kando na ada ya huduma katika ripoti zako za mapato. Google haiwezi kukupatia ushauri wa kodi na unapaswa kuwasiliana na mshauri wako wa masuala ya kodi.

Norwe

Wasanidi programu wote

Google ina wajibu wa kubainisha, kutoza na kuwasilisha VAT kwa programu zote zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu wa maudhui dijitali na huduma unaofanywa na wateja walio Norwe kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play. Google itatuma kwa mamlaka husika kodi ya VAT ya ununuzi uliofanywa na wateja walio Norwe kwenye mfumo wa utozaji wa Google Play. Huhitaji kukokotoa na kutuma kodi za VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi Norwe kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play.

Kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi Norwe kwa kutumia mfumo mbadala wa utozaji ikiwa ni sehemu ya jaribio la utozaji chaguo la mtumiaji au mpango wa utozaji mbadala bila kujumuisha chaguo la mtumiaji, una wajibu wa kubaini, kutoza na kuwasilisha malipo yoyote ya VAT yanayostahili kulipwa ya miamala iliyofanyika kwa mamlaka husika.

Wasanidi programu wanaoishi nchini Norwe

Ikiwa unaishi nchini Norwe, tozo ya VAT ya eneo husika haitakatwa kwenye ada ya huduma unayolipa Google, lakini huenda ukahitaji kutathmini tozo ya VAT.

Omani

Wasanidi programu wanaoishi Omani

Iwapo unaishi nchini Omani, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Omani.

Wasanidi programu wasioishi Omani

Kuanzia tarehe 16 Aprili 2021, Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT ya 5% kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Omani.

Huhitaji kukokotoa na kutuma VAT kando kwa wateja wanaoishi nchini Oman. 

Pwetoriko

Wasanidi programu wote

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma malipo ya kodi na mauzo (SUT) nchini Pwetoriko kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Pwetoriko kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play.

Kwa ununuzi unaofanywa na watumiaji wanaoishi Pwetoriko kwa kutumia mfumo mbadala wa utozaji, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma malipo yoyote ya kodi ya mauzo yanayostahili kulipwa ya miamala iliyofanyika, kwa mamlaka husika.

Wasanidi programu walio Pwetoriko

Ikiwa unaishi Pwetoriko, Google itatumia SUT ya Pwetoriko kwenye ada ya huduma. Kiasi cha SUT kitaonyeshwa tofauti na kiasi cha ada ya huduma.

Urusi

Wasanidi Programu wanaoishi Urusi

Ikiwa unaishi Urusi, una wajibu wa kubaini, kutoza, na kutuma VAT kwa ununuzi wa ndani ya programu na programu zote zinazolipiwa, zilizonunuliwa na wateja wanaoishi Urusi.

Wasanidi programu wasioishi Urusi

Kutokana na sheria za kodi za nchini Urusi, Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma asilimia 20 ya VAT kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Urusi.

Huhitaji kukokotoa na kutuma VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Urusi.

Saudia

Wasanidi programu wanaoishi Saudia

Ikiwa unaishi Saudia, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Saudia.

Wasanidi programu wasioishi Saudia

Kutokana na sheria za kodi za Saudia, Google ina jukumu la kubaini, kutoza na kutuma asilimia 15 ya VAT kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa ndani ya programu na wa programu zinazolipishwa unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Saudia.

Ikiwa huishi nchini Saudia, huhitaji kukokotoa na kutuma VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Saudia.

Ikiwa unaishi nchini Saudia, tozo ya VAT ya eneo husika haitakatwa kwenye ada ya huduma unayolipa Google, lakini huenda ukahitaji kutathmini tozo ya VAT.

Serbia

Wasanidi programu walio nchini Serbia

Ikiwa unaishi Serbia, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT ya ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Serbia. Google itatumia tozo la VAT ya nchini kwenye ada ya huduma. Kiasi cha VAT kitaonyeshwa tofauti na kiasi cha ada ya huduma.

Wasanidi programu wasioishi Serbia

Iwapo huishi Serbia, Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT ya Serbia kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Serbia.

Singapoo

Wasanidi programu walio nchini Singapoo

Ikiwa unaishi nchini Singapoo, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma asilimia 9 ya Kodi ya Bidhaa na Huduma (GST) ya Singapoo kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Singapoo.

Google inaweza kutoza Kodi ya Bidhaa na Huduma (GST) kwenye ada ya huduma, pale inapotumika. Tozo ya Kodi ya Bidhaa na Huduma (GST) itaonekana kando na ada ya huduma.

Wasanidi programu walio nje ya Singapoo

Ikiwa unaishi nje ya Singapoo, Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma asilimia 9 ya GST ya Singapoo kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Singapoo. Huhitaji kukokotoa na kutuma GST kando na ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Singapoo.

Afrika Kusini

Wasanidi Programu Wote

Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT ya Afrika Kusini kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Afrika Kusini kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play.

Kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Afrika Kusini kwa kutumia mfumo mbadala wa utozaji, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma malipo yoyote ya VAT yanayostahili kulipwa ya miamala iliyofanyika kwa mamlaka husika.

Wasanidi programu wanaoishi Afrika Kusini

Iwapo unaishi nchini Afrika Kusini, VAT ya eneo husika itatumika kwenye ada ya huduma unayolipa Google.

Nambari yako ya VAT ya Afrika Kusini inaonyeshwa kwenye ankara za Google. Unaweza kuipatia Google taarifa zako za kodi za Afrika Kusini kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Ingia katika Kituo cha malipo ya Google.
  2. Chagua Mipangilio kwenye menyu ya juu.
  3. Katika sehemu ya "Nambari ya VAT ya Afrika Kusini", bofya aikoni ya penseli Badilisha kisha uweke Nambari yako ya VAT ya Afrika Kusini.
  4. Bofya Hifadhi.
Korea Kusini

Wasanidi programu walio Korea Kusini

Iwapo unaishi Korea Kusini, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa maudhui yote dijitali kutoka Duka la Google Play yanayonunuliwa na wateja walio nchini Korea Kusini.

Iwapo hutaipatia Google Nambari yako ya Usajili wa Biashara, Google itatoza na kutuma asilimia 10 ya VAT kwenye ada ya huduma yenye ankara kwa mamlaka husika. Tozo ya asilimia 10 ya VAT itaonyeshwa tofauti na ada ya huduma pale inapotumika.

Hali yako ya usajili hubaini kodi unazotozwa nchini Korea Kusini. Unaweza kuipa Google Nambari yako ya Usajili wa Biashara kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo   (Mipangilio Mipangilio > Taarifa za malipo).
  2. Katika sehemu ya "Mipangilio", bofya Dhibiti mipangilio.
  3. Nenda chini hadi kwenye "Taarifa za kodi za Korea Kusini" kisha ubofye aikoni ya penseli Aikoni ya penseli / aikoni ya kubadilisha.
  4. Weka Nambari yako ya Usajili kwenye sehemu ya “Nambari ya Usajili wa Biashara”.
  5. Bofya Hifadhi.

Wasanidi programu walio nje ya Korea Kusini

Kutokana na sheria za kodi za Korea Kusini, Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma asilimia 10 ya VAT kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa kwenye Duka la Google Play na ununuzi wa ndani ya programu, unaofanywa na wateja walio Korea Kusini, kwa niaba ya wasanidi programu walio nje ya Korea Kusini.

Iwapo wateja wako hutumia mfumo wa utozaji wa Google Play, huhitaji kuhesabu na kutuma VAT kando kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi nchini Korea Kusini.

Iwapo utachagua kuweka mifumo ya ziada ya utozaji ndani ya programu kwa wateja walio Korea Kusini kwa mujibu wa Sera yetu ya malipo, Google itakusanya pesa kutoka kwako, kwa ajili ya kodi zinazotakiwa kutozwa kwenye bidhaa au huduma unazouzia wateja walio Korea Kusini, zinazochakatwa kwenye mifumo kama hiyo ya ziada ya utozaji ndani ya programu na itatuma kodi kama hizo kwa mamlaka husika

Uswizi

Una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Uswizi.

Wasanidi programu wanaoishi nchini Uswizi

Kutokana na sheria za nchini Uswizi, katika hali fulani Google inahitajika kutoza kodi ya asilimia 7.7 kwenye ada ya huduma unayolipa Google.

Taiwani

Google inawajibika kubaini, kutoza na kuwasilisha VAT kwa programu zote zinazolipishwa na huduma za ununuzi wa ndani ya programu zinazofanywa katika Duka la Google Play na wateja walio Taiwani. Wasanidi programu hawahitaji kukokotoa na kutuma VAT kivyake.

Wasanidi programu walio Taiwani

Iwapo hutaipatia Google Nambari yako ya VAT ya Taiwani, huenda ikatoza kodi ya VAT ya asilimia 5 kwenye ada ya huduma unayolipa Google. Tozo ya VAT ya asilimia 5 itaonyeshwa tofauti na ada ya huduma, pale inapotumika.

Taarifa zako za mlipa kodi ndizo zitakazobainisha kodi unazotozwa nchini Singapoo. Unaweza kuipatia Google taarifa zako za kodi ya Taiwani kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye Taarifa za malipo  (Mipangilio Mipangilio > Taarifa za malipo).
  2. Katika sehemu ya "Mipangilio", bofya Dhibiti mipangilio.
  3. Nenda chini kwenye "taarifa za kodi za Taiwani" kisha ubofye Badilisha Aikoni ya penseli / aikoni ya kubadilisha.
  4. Weka Nambari yako ya Mlipa Kodi wa VAT katika sehemu ya “Nambari ya VAT.”
  5. Bofya Hifadhi.
Tailandi

Wasanidi programu walio nchini Tailandi

Iwapo unaishi nchini Tailandi, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya Tailandi kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Tailandi.

Ikiwa hujasajiliwa kulipia VAT, Google itatoza na kutuma asilimia 7 ya VAT kwenye ada ya huduma kwenye mamlaka husika, inapotumika. Ada ya VAT ya asilimia 7 itaonekana kando kwenye ada ya huduma.

Hali yako ya usajili wa kodi hubaini kodi unazotozwa nchini Tailandi. Unaweza kuipa Google taarifa ya kodi ya Tailandi kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye Taarifa za malipo  (Mipangilio Mipangilio > Taarifa za malipo).
  2. Katika sehemu ya "Mipangilio", bofya Dhibiti mipangilio.
  3. Nenda chini kwenye "taarifa za kodi za Tailandi" kisha ubofye BadilishaAikoni ya penseli / aikoni ya kubadilisha.
  4. Weka Nambari yako ya Usajili wa VAT katika sehemu ya “Nambari ya VAT ya Tailandi.”
  5. Bofya Hifadhi.

Wasanidi programu wasioishi nchini Tailandi

Ikiwa unaishi nje ya Tailandi, Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma asilimia 7 ya VAT ya Tailandi kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Tailandi.

Uganda

Wasanidi programu wote

Google ina jukumu la kubaini, kutoza na kuwasilisha VAT ya Uganda kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja walio Uganda.

Wasanidi programu wanaoishi Uganda

Ikiwa unaishi nchini Uganda lakini hujajisajili kulipa VAT, umejiandikisha ili kutoa mfumo mbadala wa utozaji na unawauzia wateja ukitumia mfumo mbadala wa utozaji, Google itatoza VAT kwenye bili ya ada ya huduma. Kiasi cha VAT kitaonyeshwa tofauti na kiasi cha ada ya huduma.

Ikiwa umesajiliwa kulipia VAT nchini Uganda na kuipa Google taarifa zako za kodi, Google haitatoza VAT ya eneo kwenye ada ya huduma, lakini huenda ukahitaji kutathmini VAT mwenyewe.

Hali yako ya kodi hubaini kodi unazotozwa nchini Uganda. Unaweza kuipa Google taarifa za kodi za Uganda kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo.
  2. Katika sehemu ya "Mipangilio", bofya Dhibiti mipangilio.
  3. Nenda chini hadi kwenye sehemu ya "taarifa za kodi za Uganda" kisha ubofye aikoni ya penseli Aikoni ya penseli / aikoni ya kubadilisha.
  4. Sasisha taarifa zako za kodi.
  5. Bofya Hifadhi.
Ukraini

Google ina jukumu la kubaini, kutoza na kuwasilisha asilimia 20 ya VAT ya Ukraini kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja walio Ukraini.

Ikiwa wewe ni Mjasiriamali Binafsi aliyepo Ukraini, tozo ya VAT ya eneo husika zitatumika kwenye ada ya huduma unayolipa Google. 

Ikiwa wewe ni mfanyabiashara na unaishi nchini Ukraini, tozo ya eneo husika haitakatwa kwenye ada ya huduma unayolipa Google, lakini huenda ukahitaji kutathmini tozo ya VAT.

Hali yako ya usajili wa kodi hubaini kodi unazotozwa nchini Ukraini. Unaweza kuipa Google taarifa ya kodi ya Ukraini kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Ingia katika Kituo cha malipo ya Google.
  2. Bofya Mipangilio.
  3. Sasisha taarifa yako ya kodi ya Ukraini.
  4. Bofya Hifadhi.
Muungano wa Falme za Kiarabu

Wasanidi programu wanaoishi katika Muungano wa Falme za Kiarabu

Ikiwa unaishi katika Muungano wa Falme za Kiarabu, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi katika Muungano wa Falme za Kiarabu.

Ikiwa unaishi katika Muungano wa Falme za Kiarabu, tozo ya VAT ya eneo husika haitakatwa kwenye ada ya huduma unayolipa Google, lakini huenda ukahitaji kutathmini tozo ya VAT.

Wasanidi programu wasioishi katika Muungano wa Falme za Kiarabu

Kutokana na sheria za kodi za Muungano wa Falme za Kiarabu, Google ina jukumu la kubaini, kutoza na kutuma asilimia 5 ya VAT kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi katika Muungano wa Falme za Kiarabu.

Ikiwa huishi katika Muungano wa Falme za Kiarabu, huhitaji kukokotoa na kutuma VAT kando, kwa ununuzi unaofanywa na wateja wanaoishi katika Muungano wa Falme za Kiarabu.

Uingereza

Wasanidi programu wanaoishi nchini Uingereza

Ikiwa unaishi nchini Uingereza, tozo ya VAT ya eneo husika haitakatwa kwenye ada ya huduma unayolipa Google, lakini huenda ukahitaji kutathmini tozo ya VAT.

Marekani

Alabama, Maeneo ya Alaska, Arizona, Arkansas, California, Colorado, Connecticut, District of Columbia, Florida, Georgia, Hawaii, Idaho, Illinois, Indiana, Iowa, Kansas, Kentucky, Louisiana, Maine, Maryland, Massachusetts, Michigan, Minnesota, Mississippi, Missouri, Nebraska, Nevada, New Jersey, New Mexico, New York, North Carolina, North Dakota, Ohio, Oklahoma, Pennsylvania, Rhode Island, South Carolina, South Dakota, Tennessee, Texas, Utah, Vermont, Virginia, Washington, West Virginia, Wisconsin na Wyoming

Kwa mujibu wa masharti ya kodi ya mauzo, Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma malipo ya kodi ya mauzo ya ununuzi wa programu na wa ndani ya programu katika Duka la Google Play unaofanywa na wateja wanaoishi katika majimbo haya kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play. Google itakusanya na kutuma kodi ya mauzo kwa mamlaka husika ya kodi, panapohitajika.

Huhitaji kukokotoa na kutuma kodi ya mauzo kandokando kwa wateja wanaoishi katika majimbo haya. Tutazingatia masharti haya hata kama huishi Marekani.

Kwa ununuzi unaofanywa na watumiaji wanaoishi katika maeneo haya kwa kutumia mfumo mbadala wa utozaji, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma malipo yoyote ya kodi ya mauzo yanayostahili kulipwa ya miamala iliyofanyika kwa mamlaka husika.

Uzibekistani

Wasanidi programu walio nchini Uzibekistani

Iwapo unaishi nchini Uzibekistani, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya Uzibekistani kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi nchini Uzibekistani.

Ikiwa wewe ni Mtu Binafsi au Mjasiriamali Binafsi uliye nchini Uzibekistani, Google itatumia tozo la VAT ya eneo husika kwenye ada ya huduma. Kiasi cha VAT kitaonyeshwa tofauti na kiasi cha ada ya huduma katika ripoti zako za mapato.

Ikiwa wewe ni shirika la Biashara lililo nchini Uzibekistani, Google haitatumia tozo la VAT ya eneo husika kwenye ada ya huduma, lakini huenda ukahitaji kutathmini mwenyewe tozo la VAT. 

Hali yako ya kodi hubaini kodi unazotozwa nchini Uzibekistani. Unaweza kuipa Google taarifa ya kodi kwa kufuata utaratibu huu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo.
  2. Katika sehemu ya "Mipangilio", bofya Dhibiti mipangilio.
  3. Nenda chini hadi kwenye "Taarifa za kodi za Uzibekistani" na ubofye aikoni ya penseli Aikoni ya penseli / aikoni ya kubadilisha.
  4. Sasisha taarifa zako za kodi.
  5. Bofya Hifadhi.

Wasanidi programu wasioishi Uzibekistani

Iwapo unaishi nje ya Uzibekistani, Google ina jukumu la kubaini, kutoza na kuwasilisha VAT ya Uzibekistani kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Uzibekistani.

Vietnamu

Wasanidi programu wanaoishi nchini Vietnamu

Iwapo unaishi Vietinamu, una wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Vietinamu.

Google itatoza na kutuma kwa mamlaka husika asilimia 5 ya VAT ya ada ya huduma yenye ankara, pale inapohitajika. Ada ya VAT ya asilimia 5 itaonekana tofauti na ada ya huduma.

Wasanidi programu wanaoishi nje ya Vietinamu

Ikiwa unaishi nje ya Vietnamu, Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma VAT kwa mamlaka husika kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa katika Duka la Google Play na wateja wanaoishi Vietnamu.

Zimbabwe

Wasanidi Programu Wote

Una wajibu wa kubaini, kutoza na kulipa VAT kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa unaotokana na ununuzi wa ndani ya programu ambao unafanywa katika Duka la Google Play na wateja walio Zimbabwe.

Wasanidi programu walio Zimbabwe

Google itakata tozo la VAT ya nchi husika kwenye ada ya huduma. Kiasi cha VAT kitaonyeshwa kivyake tofauti na kiasi cha ada ya huduma.

Nchi na maeneo mengine

Kutokana na sheria za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Bidhaa na Huduma (GST), Google ina wajibu wa kubaini, kutoza na kutuma malipo ya VAT au GST kwa ununuzi wote wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu unaofanywa na wateja wanaoishi katika maeneo yanayotumia mfumo wa utozaji wa Google Play ambapo Google ni muuzaji rasmi (MOR) na katika maeneo yafuatayo:

  • VAT: Albania, Georgia, Kazakistani, Moroko, Uturuki

  • GST: Nyuzilandi

Google itatuma VAT au GST za programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu uliofanywa na wateja katika nchi hizi kwa mamlaka husika. Huhitaji kukokotoa na kutuma VAT au GST kando, ikiwa unaishi katika nchi hizi.

Hivi ndivyo unavyokagua viwango vya VAT au GST vinavyotumika katika ununuzi wa programu zinazolipishwa na ununuzi wa ndani ya programu katika nchi hizi:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo   (Mipangilio Mipangilio > Taarifa za malipo).
  2. Bofya Dhibiti kodi ya mauzo.

Kubadilisha bei za programu

Ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kuweka na kubadilisha bei za programu, nenda kwenye sehemu ya kuweka bei na kusambaza programu.

Iwapo unasambaza programu katika nchi zinazojumuisha kodi, kiwango cha kodi kilichowekwa katika Dashibodi ya Google Play kitatumika kwa bei zako zilizopo, zisizojumuisha kodi.

Katika nchi ambako wasanidi programu wana wajibu wa kutuma VAT kwa mamlaka husika ya kodi, Google itampa msanidi programu kiasi chote cha kodi kilichokusanywa, kisha iondoe ada ya huduma kwenye bei ya mwisho ya bidhaa.

Angalia mfano
Kwa kuchukulia kwamba bei katika nchi ni JPY100 na VAT ni 20%:

Msanidi programu hupokea kutoka Google: JPY75

Msanidi programu hutuma malipo ya VAT: JPY17

  • Mfano: JPY100 - (JPY100* 1/1.2) = JPY17
  • Bei ya programu - (Bei ya programu * 1/(1+kiwango cha kodi))

Mapato ya msanidi programu baada ya mgawanyo wa 70/30 na kutuma malipo ya VAT: JPY 58

  • Mfano: JPY 83 * 0.7 = JPY 58
  • Bei kabla ya VAT * 70%
Kuleta faili za CSV za bidhaa za ndani ya programu

Kama unaleta faili za CSV zilizo na bidhaa za ndani ya programu, tafadhali zingatia bei zinazojumuisha kodi.

  • Ukitumia bei inayogeuzwa kiotomatiki, unaweza kutoa bei chaguomsingi isiyojumuisha kodi. Bei zinazojumuisha kodi zitageuzwa kiotomatiki.
  • Kama hutumii bei zinazogeuzwa kiotomatiki, ni lazima bei zijumuishe kodi.

Bei za ndani ya nchi kwa bidhaa za ndani ya programu

Ili uzuie bei za sarafu chaguomsingi ya nchi yako zisijazwe kiotomatiki kwa bidhaa za ndani ya programu, unahitaji kubainisha bei ya bidhaa za ndani ya programu mara mbili katika faili za CSV utakazoleta:

  • Bei ya kwanza huweka bei chaguomsingi ya bidhaa ya ndani ya programu.
  • Bei ya pili huweka bei ya nchi husika ya bidhaa ya ndani ya programu.

Kumbuka: Ili upakie faili za CSV zenye bidhaa za ndani ya programu, nenda kwenye sehemu ya kuweka bidhaa ya ndani ya programu.

Nchi nyinginezo

Iwapo programu yako inalipishwa au inatoa huduma za ununuzi wa ndani ya programu kwa wateja katika hali nyingine tofauti na zile ambazo Google inawajibika, una wajibu wa kuamua kiwango cha kodi ya mauzo yako na kutuma kodi kwenye mamlaka husika ya kodi (ambayo inaweza kuwa tofauti na mamlaka ya kodi kwenye eneo lako). Viwango vya kodi utakavyobainisha vitatumika kiotomatiki mnunuzi anaponunua bidhaa. Google haiwezi kukupa ushauri wa kodi na unapaswa kuwasiliana na mshauri wako wa kodi.

Kuangalia na kurekebisha viwango vyako vya kodi

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Taarifa za malipo   (Mipangilio Mipangilio > Taarifa za malipo).
  2. Katika sehemu ya "Kodi ya mauzo", bofya Dhibiti kodi ya mauzo.
  3. Tafuta eneo ambapo ungependa kubadilisha mipangilio ya kodi.
  4. Bofya aikoni ya penseli Aikoni ya penseli / aikoni ya kubadilisha.
  5. Katika safu mlalo ya eneo ambako ungependa kurekebisha viwango vya kodi, bofya kishale cha chini katika "Chaguo la kodi."
  6. Chagua moja kati ya zifuatazo:
    • Hamna kodi
    • Kiwango cha mipangilio iliyowekwa mapema kwenye Google: Tumia kiwango cha mipangilio iliyowekwa mapema ya kodi katika eneo hili.
    • Kiwango maalum cha kodi: Weka kiwango cha kodi.
  7. Ikiwa umefanya mabadiliko, bofya Hifadhi.
Angalia mfano

Kiwango cha kodi ya mauzo kitakuwa asilimia ya bei ya programu yako. Kwa mfano:

Kiwango cha kodi ya mauzo Bei ya programu Kodi ya mauzo Jumla ya bei ya programu
20% $10 $2.00 $12.00

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3410684573354604074
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false