Kuweka bidhaa ya ndani ya programu

Kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play, unaweza kuweka bidhaa za ndani ya programu zinazotoza watumiaji mara moja. Bidhaa za ndani ya programu zinaweza kujumuisha vipengee kama vile bidhaa pepe (kwa mfano, viwango au vipengee maalum vya mchezo) na huduma zinazolipishwa ndani ya programu yako kwenye Google Play.

Pia, unaweza kuanzisha usajili, ambao unatoza watumiaji kwa vipindi vinavyojirudia.

Muhimu: Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play na ada za huduma hutumika kwenye bidhaa za ndani ya programu na usajili.

Upatikanaji

Ikiwa upo katika eneo linaloruhusu huduma ya usajili wa wauzaji, unaweza kutumia mfumo wa utozaji kupitia Google Play.

Ikiwa upo katika eneo ambako huduma inapatikana na ungependa kuanza kutumia vipengele vya mfumo wa utozaji wa Google Play katika programu zako, weka taarifa za malipo na upate maelezo kuhusu kuweka mipangilio ya mfumo wa utozaji wa Google Play kwenye tovuti ya Wasanidi Programu wa Android.

Ili bidhaa ya ndani ya programu ipatikane kwa ajili ya ununuzi, sharti iwe inatumika, na programu husika inahitaji kupatikana katika nchi au eneo ambako watumiaji wanaishi. Bidhaa ya ndani ya programu inaweza kununuliwa ilimradi inatumika, hata ikiwa programu husika haijachapishwa. Sharti uondoe bidhaa ya ndani ya programu ikiwa hungependa ipatikane.

Ikiwa unatumia akaunti ya majaribio, nenda kwenye tovuti ya Wasanidi Programu wa Android ili upate maelezo zaidi kuhusu kujaribu ujumuishaji wa Maktaba ya Malipo kupitia Google Play.

Baada ya kuweka bidhaa ya ndani ya programu, itapatikana kwa watumiaji wanaotumia toleo jipya zaidi la Duka la Google Play.

Ruhusa zinazohitajika

Ili ujumuishe bidhaa ya ndani ya programu, unahitaji kubainisha ruhusa ya com.android.vending.BILLING kwenye faili ya maelezo ya APK ya programu yako. Ukisambaza programu yako kote, bado unaweza kuchapisha programu zinazotumia ruhusa ya com.android.vending.BILLING katika nchi zote.

Kuweka bidhaa za ndani ya programu

Weka bidhaa moja ya ndani ya programu

Kabla hujaweka bidhaa, hakikisha umepanga Vitambulisho vya Bidhaa zako kwa makini. Vitambulisho vya bidhaa vinapaswa kuwa vya kipekee kwa kila programu na haviwezi kubadilishwa au kutumiwa upya baada ya kuwekwa.
  • Sharti Vitambulisho vya Bidhaa vianze kwa herufi ndogo au nambari, na viwe na herufi ndogo (a-z), nambari (0-9), vistari chini (_) na vituo (.).
  • Huwezi kubadilisha au kutumia upya kitambulisho cha bidhaa baada ya kuweka bidhaa.
  • Kumbuka: Huwezi kutumia kitambulisho cha bidhaa cha android.test pamoja na vitambulisho vyote vya bidhaa vinavyoanza kwa android.test.

Ili uweke bidhaa ya ndani ya programu, fuata hatua zifuatazo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Nenda kwenye ukurasa wa Bidhaa za ndani ya programu (Chuma mapato > Bidhaa > Bidhaa za ndani ya programu).
  3. Bofya Weka bidhaa.
  4. Weka maelezo ya bidhaa yako.
    • Kitambulisho cha Bidhaa: Kitambulisho cha kipekee cha bidhaa ya ndani ya programu.
    • Kichwa: Jina fupi la kipengee (hadi herufi 55, lakini tunapendekeza vichwa visipite herufi 25 ili vionekane inavyostahili katika miktadha yote) kama vile "Dawa za usingizi."
    • Maelezo: Maelezo ya kina kuhusu kipengee (hadi herufi 200), kwa mfano "Huwasaidia viumbe kupata usingizi papo hapo."
    • Aikoni: Picha sahihi na ya kipekee inayoonyesha bidhaa yako. Usijumuishe maandishi, matangazo au chapa. Aikoni ya bidhaa yako itaonyeshwa kwenye ukurasa wa programu katika Google Play na wakati wa ununuzi.
      • PNG ya biti 32
      • Pikseli 512 x 512
      • Hadi MB 1
    • Bei: Weka bei katika sarafu ya nchi uliko au uchague kiolezo cha bei.
    • Bidhaa nyingi: Ruhusu huduma ya kulipia bidhaa nyingi kwa wakati mmoja kwenye bidhaa hii. Watumiaji wataweza kununua bidhaa nyingi kulingana na kiwango cha nchi au eneo wanakoishi. Kumbuka yafuatayo:
      • Ili kuweka mipangilio ya huduma ya kulipia bidhaa nyingi kwa wakati mmoja kwenye Dashibodi ya Google Play, programu yako inahitaji Toleo la 4.0 la Maktaba ya Malipo kupitia Google Play. Tembelea Tovuti ya Wasanidi Programu wa Android ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kujumuisha Maktaba ya Malipo kupitia Google Play kwenye programu yako.
      • Huduma ya kulipia bidhaa nyingi kwa wakati mmoja haipatikani katika baadhi ya nchi au maeneo.
      • Katika nchi au maeneo mengi ambako huduma ya kulipia bidhaa nyingi kwa pamoja inapatikana, kikomo cha bei cha SKU ni takriban Dola 100 za Marekani. Ili uruhusu huduma ya kulipia bidhaa nyingi kwa wakati mmoja, unahitaji kurekebisha bei (kabla ya kutozwa ushuru) iwe chini ya kiwango cha juu zaidi kinachoruhusiwa katika kila nchi au eneo.
    • Google Play Points pekee: Fanya bidhaa yako ipatikane tu kupitia mpango wa Google Play Points.
  5. Hifadhi mabadiliko yako kisha ubofye Chapisha ili kufanya bidhaa yako ya ndani ya programu ipatikane kwa watumiaji.

Lugha na tafsiri

Bidhaa za ndani ya programu hutumia lugha chaguomsingi inayotumika na programu. Ili uweke tafsiri katika lugha mahususi, chagua bidhaa ya ndani ya programu, kisha ubofye Dhibiti tafsiri halafu utumie lugha unazotaka. Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kujanibisha maudhui kwa ajili ya watumiaji wa programu yako, angalia ukurasa wa Kutafsiri na kujanibisha programu yako.

Weka kundi la bidhaa kadhaa za ndani ya programu

Ili uweke bidhaa kadhaa za ndani ya programu kwa wakati mmoja, pakia faili ya CSV iliyo na maelezo kuhusu kila bidhaa yako.
Faili za CSV hutumia koma (,) na nusu koloni (;) kutenganisha vipengee kwenye data. Koma hutenganisha vipengee vya msingi kwenye data, nayo nusu koloni hutenganisha vipengee vidogo.
Unapounda faili ya CSV yenye bidhaa za ndani ya programu, bainisha sintaksia ya CSV kwenye safu mlalo ya kwanza, ikifuatiwa na maelezo ya bidhaa kwenye safu mlalo zinazofuata.
Muhimu: Sharti kila kipengee kiwe kivyake kwenye mstari mmoja katika faili ya CSV.

Pakia faili ya CSV ya bidhaa za ndani ya programu

Ili upakie faili ya CSV, fuata hatua zifuatazo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Nenda kwenye ukurasa wa Bidhaa za ndani ya programu (Kuchuma mapato > Bidhaa > Bidhaa za ndani ya programu).
  3. Bofya Pakia.
    • Kutuma data ya bidhaa nyingi kwa kupakia faili ya CSV kutafuta data iliyopo ya bidhaa ikiwa tu Kitambulisho cha Bidhaa katika faili ya CSV kinalingana na Kitambulisho cha Bidhaa iliyopo ya ndani ya programu kwenye orodha ya bidhaa. Hatua ya kufuta bidhaa haifuti bidhaa za ndani ya programu ambazo hazijajumuishwa kwenye CSV.
  4. Dondosha faili yako ya CSV ili upakie au bofya Pakia.

Kuhamisha faili ya CSV ya bidhaa zilizopo za ndani ya programu

Ili uhamishe faili ya CSV, fuata hatua zifuatazo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Nenda kwenye ukurasa wa Bidhaa za ndani ya programu (Kuchuma mapato > Bidhaa > Bidhaa za ndani ya programu).
  3. Bofya Hamisha.

Angalia mfano wa faili ya CSV

Huu ni mfano wa sintaksia ya CSV na mifano mitatu ya bidhaa za ndani ya programu:
  • Mfano wa kwanza unafafanua kichwa na maelezo katika lugha mbili tofauti (sw_TZ na es_ES). Kiolezo cha bei kinafafanua bei ya bidhaa.
  • Mfano wa pili hautumii kiolezo cha bei. Badala yake, unabainisha bei kwa nchi changuomsingi (Marekani). Dashibodi ya Google Play hutumia viwango vya ubadilishaji sarafu na viwango vya bei katika eneo husika kuweka bei kiotomatiki katika nchi zingine zote ambako programu inasambazwa.
  • Mfano wa tatu pia haujumuishi kiolezo cha bei. Bei ya bidhaa hubainishwa na msanidi programu kwa kila nchi ambako programu inasambazwa.

Mfano wa sintaksia ya CSV

Kitambulisho cha Bidhaa, Hali ya Uchapishaji, Aina ya ununuzi, Tafsiri Kiotomatiki, Lugha; Kichwa; Maelezo, Jaza Bei Kiotomatiki, Bei, Kitambulisho cha Kiolezo cha Bei

Mifano ya bidhaa za ndani ya programu

Mfano wa 1

basic_sleeping_potion,published,managed_by_android,false,sw_KE; Dawa za Kawaida za usingizi; Hufanya wanyama wadogo walale.; es_ES; Poción básica de dormir; Causa las criaturas pequeñas ir a dormir.,false,,4637138456024710495

Mfano wa 2

standard_sleeping_potion, published,managed_by_android,false, sw_KE; Dawa za Msingi za usingizi; Hufanya wanyama wote walale kwa dakika 2.,true, 1990000,

Mfano wa 3

invisibility_potion,published, managed_by_android,false,sw_TZ; Dawa ya Kukufanya Usionekane; Maadui hawataweza kukuona kwa dakika 5.,false, US; 1990000; BR; 6990000; RU; 129000000; IN; 130000000; ID; 27000000000; MX; 37000000,

Vipengee vya data kwenye faili za CSV

Kila safu mlalo katika faili ya CSV ya bidhaa za ndani ya programu inaweza kujumuisha vipengee vifuatavyo lakini angalau kipengee kimoja kati ya hizi hakijabainishwa katika safu mlalo:
Kitambulisho cha Bidhaa

Kubainisha kipengee hiki kwenye faili ya CSV ni sawa na kubuni Kitambulisho cha Bidhaa unapoweka bidhaa mpya ya ndani ya programu.

Ukibainisha Kitambulisho cha Bidhaa kwa bidhaa ya ndani ya programu ambayo tayari ipo kwenye orodha ya bidhaa, data ya bidhaa iliyopo ya ndani ya programu itabadilishwa ili ilingane na vipengee ulivyobainisha katika faili ya CSV.

Hali ya Kuchapisha Hii lazima iwekwe kuwa imechapishwa au haijachapishwa. Hii ni sawa na kuweka bidhaa ya ndani ya programu kuwa Inatumika au Haitumiki.
Aina ya Ununuzi

Thamani hii lazima iwekwe kuwa managed_by_android.

Kutafsiri Kiotomatiki

Sharti uteue chaguo kuwa sivyo kwa sababu kipengele cha kutafsiri kiotomatiki hakitumiki kwa maelezo ya bidhaa ya ndani ya programu.

Ikiwa ungependa kutoa tafsiri ya jina na maelezo ya bidhaa ya ndani ya programu, bainisha wazi tafsiri hizi kwenye sehemu ya Lugha.

Lugha, Jina, na Maelezo

Ukijumuisha lugha moja pekee kwa kipengee, sharti ubainishe lugha chaguomsingi itakayotumika kwenye programu yako, na jina na ufafanuzi chaguomsingi wa kipengee:

app_default_locale; item_default_title; item_default_description;

Unapoweka thamani ya Lugha, unaweza kutumia misimbo yoyote ya lugha inayoonekana wakati wa kuweka tafsiri za ukurasa wa programu katika Google Play.

Kumbuka: Unapobainisha Kichwa na Maelezo, tumia mikwajunyuma kutanguliza nusu koloni (\;) na mikwajunyuma (\\).

Ikiwa ungependa kujumuisha matoleo yaliyotafsiriwa ya kichwa na maelezo ya kipengee, ni lazima uorodheshe lugha chaguomsingi, kichwa na maelezo, na kufuatwa na lugha, vichwa na maelezo ya kila tafsiri. Katika mfano ufuatao, bidhaa ya ndani ya programu inatumia sw_KE (Kiswahili cha Kenya) kama lugha chaguomsingi na es_ES (Kihispania cha Uhispania) kama tafsiri:

sw_Tz; Vazi la Kukuficha; Hufanya usionekane.; es_ES; Capote Invisible; Se vuelven invisible.

Kumbuka: Programu ina lugha moja chaguomsingi, lakini kila bidhaa ya ndani ya programu ina orodha ya tafsiri zake. Hata ikiwa lugha ya kwanza kwa kila Lugha ya kipengee sharti iwe sawa kwenye faili yote ya CSV, lugha zingine zinaweza kutofautiana kwa vipengee tofauti.

Jaza Bei Kiotomatiki, Nchi, na Bei

Unaweza kuteua chaguo la Kujaza bei kiotomatiki kuwa ndivyo au sivyo. Iwapo bidhaa ya ndani ya programu inatumia kiolezo cha bei, unapaswa kuteua chaguo la Kujaza Bei Kiotomatiki kuwa sivyo, na usibainishe Bei.

Kumbuka: Unapobainisha bei ya bidhaa kwenye faili ya CSV, weka bei katika vipimo vidogo, ambapo viwango 1,000,000 vidogo ni sawa na kipimo 1 cha sarafu halisi.

Tumia bei zinazojazwa kiotomatiki

Sehemu zifuatazo zinafafanua jinsi kipengele cha Kujaza bei kiotomatiki huathiri sintaksia na kipengee cha Nchi na Bei.

Ukiteua chaguo la Kujaza bei kiotomatiki kuwa ndivyo, unapaswa tu kubainisha bei chaguomsingi ya kipengee; hupaswi kujumuisha kipengee cha Nchi.

Kwa mfano, katika hali zifuatazo:

  • Lugha chaguomsingi ya programu yako ni sw_TZ.
  • Bei chaguomsingi ya bidhaa ya ndani ya programu kabla ya kutozwa ushuru ni Dola 1.99 za Marekani.
  • Ungependa bei za nchi zingine zijazwe kiotomatiki.

Unapaswa kuweka mipangilio ya Kujaza kiotomatiki na Bei mwishoni mwa safu mlalo katika faili ya CSV kama ifuatavyo: true,1990000,

Kubainisha bei kwa kila nchi

Ukiweka hali ya Kujaza Bei Kiotomatiki kuwa sivyo badala yake, unaweza kubainisha vipengee vya nchi na bei kwa nchi zote ambako unasambaza programu yako, ikiwemo nchi inayotumia lugha chaguomsingi ya programu yako. Kila kipengee kinachoashiria nchi kinajumuisha herufi mbili kubwa za msimbo wa nchi wa ISO unaowakilisha nchi ambako programu yako inasambazwa.

Kumbuka: Sharti uweke msimbo wa nchi na bei katika kila nchi ambako programu yako inalenga. Ili uangalie na ubadilishe orodha ya nchi ambako programu yako inasambazwa, tumia kichupo cha Nchi au maeneo kwenye ukurasa wa Toleo la umma.

Kila bei inawakilisha gharama ya kila bidhaa katika viwango vidogo vya sarafu inayotumika katika nchi husika.

Kwa mfano, iwapo unauza programu yako kwa bei zifuatazo (zikijumuisha ushuru) katika nchi zingine:

  • R$6.99 nchini Brazil
  • ₽129 nchini Urusi
  • ₹130 nchini India
  • Rp 27,000 nchini Indonesia
  • $37 nchini Meksiko

Unaweza kuteua chaguo la Kujaza Bei Kiotomatiki, Nchi na Bei mwishoni mwa safu mlalo katika faili ya CSV kama ifuatavyo:

sivyo, BR; 6990000; RU; 129000000; IN; 130000000; ID; 27000000000; MX; 37000000;

Kitambulisho cha Kiolezo cha Bei

Ikiwa kipengee kinahusiana na kiolezo cha bei, sharti ubainishe hali ya Kujaza Bei Kiotomatiki kuwa sivyo na usiteue bei kwenye safu wima ya Bei. Iwapo kipengee hakihusiani na kiolezo cha bei, hupaswi kubainisha Kitambulisho cha kiolezo cha bei. Badala yake, unapaswa kubainisha chaguo la Kujaza bei kiotomatiki, Nchi na Bei kulingana na jinsi ambavyo ungependa kuweka bei za bidhaa za ndani ya programu.

Ukipakia faili ya CSV, unaweza kusasisha hali kati ya bidhaa za ndani ya programu na violezo vya bei. Ili bidhaa iambatane na kiolezo mahususi cha bei, bainisha Kitambulisho cha Kiolezo cha Bei kulingana na Kitambulisho husika cha kiolezo cha bei. Ili utenganishe bidhaa ya ndani ya programu na violezo vyote vya bei, usibainishe Kitambulisho chake cha kiolezo cha bei.

Unaweza kujumuisha bei za hadi programu 1000 au bei za bidhaa za ndani ya programu kwenye kiolezo mahususi cha bei. Kwa hivyo, usibainishe Kitambulisho cha kiolezo cha bei katika zaidi ya safu mlalo 1000 kwenye faili ya CSV.

Haki ya Kujiondoa kwa Wanaoishi EEA

Iwapo unasambaza kwa watumiaji katika nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA), unapaswa kubainisha DIGITAL_CONTENT au HUDUMA katika sehemu hii.

Viwango Vilivyopunguzwa vya VAT

Iwapo unauza habari dijitali, magazeti, majarida, vitabu, video, muziki, maudhui ya sauti au vitabu vya kusikiliza katika nchi au maeneo mbalimbali, huenda ukastahiki punguzo la viwango vya VAT.

Kwa viwango vilivyopunguzwa, vipengee katika sehemu hii vitafuata mpangilio huu:

CountryCode;VATRate;

Kila jozi ya nchi au kiwango inapaswa kufuatiwa na nusu koloni kabla ya kuongeza jozi mpya ya nchi au kiwango.

Kwa mfano:

CA;BOOKS_1 kubanisha Vitabu katika kiwango cha 1 ambavyo VAT yake imepunguzwa nchini Kanada.

FR;NEWS_1; GR;NEWS_2 kubanisha Habari katika kiwango cha 1 ambazo VAT yake imepunguzwa nchini Ufaransa na Habari katika kiwango cha 2 ambazo VAT yake imepunguzwa nchini Ugiriki.

Unaweza kubainisha viwango kwa kutumia BOOKS_1, NEWS_1, NEWS_2, MUSIC_OR_AUDIO_1, LIVE_OR_BROADCAST_1 (herufi kubwa au ndogo).

Ushuru wa mawasiliano na burudani

Iwapo ungependa kukusanya ushuru wa mawasiliano na burudani unaotozwa na serikali, sharti ubainishe kuwa programu au bidhaa yako ni ya kutiririsha kisha uteue INASTAHIKI kwenye sehemu hii, vinginevyo, usijaze sehemu hii.

Kwa sasa, ushuru huu unatumika tu nchini Marekani.

Kawaida, sehemu hii hujazwa:

CountryCode;Eligibility;Rate

Kwa mfano:

US;ELIGIBLE;VIDEO_RENTAL

Iwapo programu inastahiki, unaweza kuteua mojawapo ya kategoria zifuatazo:

VIDEO_RENTAL kwa utiririshaji wa video - usajili, ukodishaji au kulipia unachotazama tu

VIDEO_SALES, kwa utiririshaji wa video - mauzo

VIDEO_MULTI_CHANNEL kwa utiririshaji wa video - vituo vingi

AUDIO_RENTAL kwa utiririshaji wa maudhui ya sauti - usajili au ukodishaji

AUDIO_SALES kwa utiririshaji wa maudhui ya sauti - mauzo

AUDIO_MULTI_CHANNEL kwa utiririshaji wa maudhui ya sauti - vituo vingi

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13524838464488701683
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false