Kutumia Play Integrity API kugundua shughuli hatari na kukabiliana na matumizi mabaya

Unaweza kutumia Play Integrity API kulinda programu na michezo yako dhidi ya matumizi hatari. Kwa kutambua matumizi haya, programu yako inaweza kuchukua hatua inayostahili ili kupunguza hatari ya mashambulizi na matumizi mabaya.

Jinsi inavyofanya kazi

API ya Uadilifu hujumuisha vipengele vya Google Play vya kuzuia matumizi mabaya na mkusanyiko wa algoriti za uadilifu ili kuwasaidia wasanidi programu na michezo ya Android kugundua shughuli ambazo huenda ni hatari na za ulaghai. Huenda shughuli hizi zikatokana na matoleo yaliyobadilishwa ya programu au mchezo wako, vifaa visivyoaminika au mifumo mingine isiyoaminika. Kwa kugundua shughuli hizi, unaweza kuchukua hatua inayofaa ili kupunguza mashambulizi na matumizi mabaya kama vile ulaghai, udanganyifu na ufikiaji usioidhinishwa.

Mtumiaji anapofanya kitendo katika programu au mchezo, seva yako itaelekeza msimbo wa upande wa mteja kutekeleza API ya Uadilifu. Seva ya Google Play itatoa jibu lililosimbwa kwa njia fiche linaloonyesha uadilifu hivyo kubainisha kuaminika au kutoaminika kwa kifaa hiki pamoja na mfumo wake wa jozi. Kisha programu yako itasambaza jibu hilo kwa seva yako ili kuthibitisha. Seva yako inaweza kuamua hatua ambayo programu au mchezo wako unapaswa kuchukua baada ya hapo. 

API hutoa uamuzi wa uadilifu katika jibu linalojumuisha maelezo yafuatayo:

  • Mfumo halisi wa jozi wa programu: Kubaini ikiwa unatumia mfumo wako wa jozi ambao haujarekebishwa unaotambuliwa na Google Play.
  • Usakinishaji halisi wa Google Play: Kubaini ikiwa akaunti ya mtumiaji inayotumika sasa imepewa leseni, kumaanisha kuwa mtumiaji alipata programu au mchezo kwa kuusakinisha au kuulipia kwenye Google Play.
  • Kifaa halisi cha Android: Kubaini ikiwa programu yako inaendeshwa kwenye kifaa halisi cha Android kinachoendeshwa na huduma za Google Play (au tukio halisi la Michezo ya Google Play kwenye kompyuta binafsi).
  • Kutokuwepo kwa programu hasidi zilizotambuliwa: Kubaini iwapo Google Play Protect imewashwa na iwapo imepata programu hatari au za kudhuru zilizowekwa kwenye kifaa.

Vidokezo:

Weka mipangilio na udhibiti Play Integrity API

Washa API ya Uadilifu katika programu yako

Muhimu: Kwa kufikia au kutumia API ya Uadilifu, unakubali Sheria na Masharti ya API ya Uadilifu kutoka Google Play.

Ili uruhusu majibu ya API ya Uadilifu katika programu yako, unahitaji kuunganisha mradi wa Wingu la Google katika Dashibodi ya Google Play. Ili uunganishe mradi wako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu).
  2. Nenda kwenye sehemu ya "Play Integrity API".
  3. Chagua "Unganisha mradi uliopo" na mradi unaotaka kuunganisha nao
  4. Bofya Unganisha mradi wa wingu.

Ili uanze kujumuisha Integrity API katika programu yako, unahitaji kufanya yafuatayo:

  • Kwenye programu za Java/Kotlin, weka toleo jipya zaidi linalopatikana la maktaba ya Android ya Play Integrity API kutoka Hazina ya Maven ya Google.
  • Kwa michezo ya Unity,  sakinisha toleo la hivi karibuni la Programu Jalizi za Google Play kwa ajili ya Unity. Matoleo yote ya 2019.x, 2020.x na mapya zaidi yanatumika. Ikiwa unatumia Unity 2018.x, sakinisha 2018.4 au toleo jipya zaidi. Ikiwa unatumia Unity 2017.x, sakinisha 2017.4.40 au toleo jipya zaidi. Unity 5.x na matoleo ya awali hayatumiki.
  • Kwa programu na michezo Asili, sakinisha toleo la hivi karibuni la SDK Kuu Asili ya Google Play.

Sasa unaweza kufuata hatua hizi kwenye tovuti ya Wasanidi Programu wa Android ili uanze kutumia Play Integrity API katika mchezo au programu yako.

(Si lazima) Kuweka mapendeleo ya majibu ya Integrity API 

Ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kuweka mipangilio ya majibu ya API integrity, tembelea tovuti ya Wasanidi Programu wa Android

Ili ubadilishe majibu yako ya API:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu).
  2. Nenda kwenye sehemu ya "Play Integrity API".
  3. Bofya Mipangilio.
  4. Nenda kwenye sehemu ya "Majibu".
  5. Bofya Badilisha.
  6. Chagua au batilisha uteuzi wa visanduku vya kuteua vilivyo karibu na majibu ya API unayotaka kubadilisha.
  7. Bofya Hifadhi mabadiliko.

Muhimu: Mabadiliko utakayofanya kwenye majibu ya API yatatekelezwa papo hapo baada ya kuyahifadhi, ikijumuisha kipindi ambapo programu yako inapatikana kwa umma. Kabla hujabadilisha majibu ya API kwenye Dashibodi yako ya Google Play, hakikisha umeweka mipangilio ili seva iweze kutekeleza majibu hayo.

(Si lazima) Weka mipangilio ya maombi ya awali

Kwa chaguomsingi, Google hudhibiti usimbaji fiche wa maombi yako ya awali. Hata hivyo, unaweza kuchagua kudhibiti mwenyewe usimbaji fiche wa majibu yako ukipenda. 

Muhimu: Hatua ya kubadilisha usimbaji fiche wa majibu kati ya kudhibitiwa na Google na kudhibiti mwenyewe inahitaji ubadilishe msimbo kwenye seva yako inayoshughulikia sehemu ya nyuma ya mfumo wa programu.

Ili udhibiti mwenyewe usimbaji fiche wa majibu yako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu).
  2. Nenda kwenye sehemu ya "Play Integrity API".
  3. Bofya Mipangilio.
  4. Nenda kwenye sehemu ya "Maombi ya awali". Karibu na "Usimbaji fiche wa majibu," hali itakuwa "Inadhibitiwa na Google" kwa chaguomsingi. Bofya Badilisha.
  5. Chagua "Dhibiti na upakue funguo za usimbaji fiche wa majibu yangu " kisha bofya Hifadhi mabadiliko. Google itazalisha funguo za usimbaji fiche wa majibu ili uzipakue na uzidhibiti. Sharti usasishe mantiki ya seva inayoshughulikia sehemu ya nyuma ya mfumo wa programu ili utumie funguo kusimbua majibu.
  6. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili uzalishe faili ya .pem kisha upakie faili hiyo ya .pem ndipo upakue funguo zako za API.
  7. Utaona ujumbe kwenye skrini unaothibitisha kuwa udhibiti wa usimbaji fiche wa majibu umesasishwa.
  8. Pakua funguo zako mpya za usimbaji fiche wa majibu na usasishe seva yako inayoshughulikia sehemu ya nyuma ya mfumo wa programu ili uzitumie kusimbua majibu kwenye utayarishaji. Rejea kwenye kichupo cha API ya Uadilifu kwenye ukurasa wa Uadilifu wa Programu ili uruhusu Google Play ianze kutumia funguo mpya za usimbaji fiche wa majibu badala ya funguo za awali. Mabadiliko haya yatatekelezwa papo hapo.

Ikiwa ungependa kurejesha udhibiti wa Google kutoka udhibiti unaojifanyia:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu).
  2. Nenda kwenye sehemu ya "Play Integrity API".
  3. Bofya Mipangilio.
  4. Nenda kwenye sehemu ya "Maombi ya awali". Karibu na "Usimbaji fiche wa majibu," hali itakuwa "Udhibiti unaojifanyia" kwa sababu ulibadilisha awali. Bofya Badilisha.
  5. Chagua "Ruhusu Google idhibiti usimbaji fiche wa majibu yangu (inapendekezwa)" kisha ubofye Hifadhi mabadiliko. Google itazalisha na kudhibiti funguo za usimbaji fiche wa majibu yako. Seva yako inayoshughulikia sehemu ya nyuma ya mfumo wa programu itatuma amri kwenye seva ya Google Play ili kusimbua majibu.

Kujaribu ujumuishaji wako wa Play Integrity API

Ili ujaribu ujumuishaji wako wa Integrity API, unaweza kuweka orodha ya akaunti za Gmail na. Kwanza, hakikisha kwamba wachunguzaji wako wana uwezo wa kufikia toleo lako. Chapisha programu yako kwenye toleo la jaribio la ndani au toleo ambalo ungependa kufanyia majaribio. Kisha, fuata maagizo ya kutumia anwani ya barua pepe kudhibiti wanaojaribu programu au kutumia Vikundi kwenye Google kuwawezesha wanaojaribu programu kufikia toleo lako.

Ili uweke mipangilio ya kujaribu programu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu).
  2. Nenda kwenye sehemu ya “Play Integrity API”.
  3. Bofya Mipangilio.
  4. Nenda kwenye sehemu ya "Kujaribu".
  5. Bofya Unda jaribio la programu mpya.
  6. Chagua orodha ya anwani za barua pepe au uunde mpya.
  7. Bofya Unda jaribio.

Kuweka mapendeleo kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play watumiaji wanapotembelea kutoka vidirisha vya Integrity API

Unaweza kutumia kidirisha cha suluhu cha Integrity API kuwaomba watumiaji waliopata programu yako kwa njia isiyo rasmi waipate kupitia Google Play. Watumiaji wanapogusa kwenye kidirisha, wataelekezwa kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play ambapo wanaweza kugusa kitufe cha kuweka kwenye kifaa (au kununua au kusasisha) ili programu yako iwekwe katika maktaba ya Google Play ya mtumiaji.

Unaweza kuweka mapendeleo kwenye vipengee vya ukurasa wa programu yako katika Google Play kwa watu wowote wanaoutembelea wanaogusa vidirisha vya suluhu vya Integrity API, ikiwa ni pamoja na jina la programu, aikoni, maelezo na vipengee vyako vya picha. Ili uweke mapendeleo kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play watumiaji wanapotembelea kupitia kidirisha cha Integrity API:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu).
  2. Nenda kwenye sehemu ya "Play Integrity API" .
  3. Bofya Mipangilio.
  4. Nenda kwenye sehemu ya "Weka mapendeleo kwenye ukurasa wa programu katika Google Play" .
  5. Bofya Unda ukurasa wa programu katika Google Play.
  6. Fuata maagizo kwenye ukurasa wa Unda ukurasa maalum wa programu katika Google Play kisha ubofye Hifadhi.

Pia, unaweza kuunda kurasa maalum za programu katika Google Play kwa vidirisha vya Integrity API moja kwa moja kwenye ukurasa wa ‘Kurasa maalum za programu katika Google Play’:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Kurasa maalum za programu katika Google Play (Kukua > Kurasa maalum za programu katika Google Play).
  2. Bofya Unda ukurasa wa programu katika Google Play, chagua iwapo ungependa kuunda ukurasa mpya wa programu katika Google Play au kurudufisha uliopo, kisha ubofye Inayofuata.
  3. Chini ya "Maelezo ya ukurasa wa programu katika Google Play," tafuta sehemu ya "Hadhira" .
  4. Chagua Kulingana na URL na uandike ‘playintegrity’ kwenye kisanduku cha maandishi.
  5. Weka maelezo mengine yote kisha ubofye Hifadhi.

Kidokezo: Kigezo cha URL cha ‘playintegrity’ ni neno muhimu maalum ambalo limehifadhiwa litumike kwenye viungo mahususi vya uadilifu kwa hivyo ni sharti liwekwe jinsi lilivyo unapoweka mipangilio ya ukurasa maalum wa programu katika Google Play.

Kuongeza kiwango chako cha idadi ya juu ya maombi ya kila siku ya Play Integrity API

Programu zinaweza kutuma hadi maombi 10,000 kwenye Integrity API kwa siku kwa chaguomsingi.

Ili uone idadi ya maombi ambayo programu yako hutuma kila siku:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu).
  2. Nenda kwenye sehemu ya “Play Integrity API”.
  3. Angalia idadi yako ya kila siku ya maombi. Ili uangalie data zaidi, badilisha kipindi na utumie vichujio, bofya Angalia ripoti ya Integrity API.

Ili uone kiwango cha juu cha maombi ya kila siku cha programu yako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu).
  2. Nenda kwenye sehemu ya “Play Integrity API”.
  3. Bofya Mipangilio.
  4. Angalia kiwango cha matumizi ya programu yako.

Unaweza kuomba kufanya zaidi ya maombi 10,000 kila siku. Ili utimize masharti ni lazima:

  • Uthibitishe utekelezaji sahihi wa mantiki ya API ikijumuisha upakiaji upya.
  • Chapisha programu yako kwenye Google Play pamoja na huduma nyingine zozote za usambazaji.

Ili kuongeza kiwango cha juu cha maombi yako ya kila siku, jaza fomu hii.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14733913882982037775
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false