Ada ya huduma

Programu na bidhaa za ndani ya programu zinazouzwa kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play au Mfumo Mbadala wa Utozaji (jinsi ilivyobainishwa hapa chini) kwa mujibu wa Sera ya Malipo zitatozwa ada ya huduma.

Hakuna ada ya jumla ya huduma kwani Google Play inazingatia kwamba wasanidi programu hufanya kazi katika hali tofauti zinazohitaji usaidizi wa viwango tofauti ili kuunda biashara endelevu. Asilimia 97 za wasanidi programu wanasambaza programu zao na kunufaika na huduma zote za Google Play bila malipo. Kati ya wasanidi programu hao wanaotozwa ada ya huduma, asilimia 99 wanastahiki kutozwa ada isiyozidi asilimia 15 kwa kushiriki katika mipango tofauti inayotolewa na Google Play.    

Jedwali hili linatoa muhtasari wa ada za huduma za Google Play:

Aina ya ada ya huduma Ada ya huduma

Wasanidi programu waliojiandikisha katika kiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15

Asilimia 15 ya mapato ya milioni $1 (USD) anayopata msanidi programu kila mwaka

Asilimia 30 ya mapato yanayozidi milioni $1 (USD) anayopata msanidi programu kila mwaka

Usajili

Asilimia 15 ya bidhaa zinazolipiwa zinazosasishwa kiotomatiki zilizonunuliwa na waliojisajili, bila kujali mapato anayopata msanidi programu kila mwaka

Miamala mingine

Asilimia 15 au chini yake kwa wasanidi programu wanaostahiki ambao wanakidhi vigezo chini ya mipango kama vile Play Media Experience Program

 

Kwa wasanidi programu wanaotoa mfumo mbadala wa utozaji kupitia Google Play mbali na mfumo wa utozaji wa Google Play kwa miamala inayofanywa na watumiaji walio Korea Kusini au India, kwa mujibu wa Sera ya malipo na sheria na masharti ("Mfumo Mbadala wa Utozaji") yanayotumika ya huduma ya miamala kama hiyo inayotumia Mfumo Mbadala wa Utozaji inalingana na ada ya huduma inayotozwa kwa miamala inayofanywa kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play, ikiwa imepunguzwa kwa asilimia 4. Pata maelezo zaidi kuhusu kutoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji walio Korea Kusini katika makala haya ya Kituo hiki cha Usaidizi au India katika makala haya ya Kituo cha Usaidizi

Pata maelezo zaidi kuhusu ada ya huduma zetu kwa kutembelea Kuelewa Ada ya Huduma ya Google Play.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9792597459048702400
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false