Mabadiliko kwenye ada ya huduma ya Google Play katika mwaka wa 2021

Mnamo Machi 2021, tulitangaza mabadiliko kwenye ada yetu ya huduma ili kusaidia kuimarisha ufanisi wa wasanidi programu katika Google Play. Kuanzia tarehe 1 Julai 2021, ada ya huduma ya kila msanidi programu itakuwa asilimia 15 kwa mapato ya milioni $1 (USD) za kwanza unazopata kila mwaka unapouza huduma au bidhaa dijitali.

Makala haya yanafafanua jinsi kiwango cha 15% cha ada ya huduma kitatozwa na jinsi ya kujisajili.

Kujiandikisha

Ili ujiandikishe rasmi kwenye kiwango cha ada ya huduma cha 15%, ni sharti: 

Ili ujiandikishe katika mpango wa ada ya huduma ya asilimia 15:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Akaunti za wasanidi programu zinazohusishwa.
  2. Fuata maagizo haya ili ufungue Kikundi cha Akaunti na utufahamishe ikiwa una Akaunti zozote za Wasanidi Programu Zilizounganishwa (ADA) au la.
  3. Ukimaliza kuweka mipangilio ya Kikundi chako cha Akaunti, unaweza kujiandikisha kwenye mpango wa kiwango cha ada ya huduma ya asilimia 15 kwenye ukurasa wa Akaunti za wasanidi programu zinazohusishwa. Kwenye ukurasa huo, utaona bango lenye kichwa: "Ukimaliza kuweka mipangilio ya kikundi chako cha akaunti, jiandikishe katika mpango wa ada ya huduma ya asilimia 15." Chini yake, bofya Kagua na ujiandikishe.
    • Muhimu: Ni lazima kikundi chako cha akaunti kijumuishe Akaunti zako zote za Wasanidi Programu Zilizounganishwa (ADA) kabla ujiandikishe. Hutaweza kujiandikisha ikiwa una maombi ambayo hujajibu au ikiwa baadhi ya Akaunti za Wasanidi Programu hazijajibu ombi lako la kuziweka kwenye kikundi chako cha akaunti. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti maombi hapa
  4. Soma na ukubali Sheria na Masharti ya ada ya huduma ya 15%.
  5. Bofya Kubali na ujiandikishe

Baada ya kujiandikisha, unaweza kuangalia hali yako ya kujiandikisha wakati wowote kwenye sehemu ya chini ya ukurasa wa Akaunti za wasanidi programu zinazohusishwa. Ukijiandikisha kabla ya tarehe 1 Julai 2021, kumbuka kuwa ada ya huduma ya 15% itatekelezwa kuanzia tarehe 1 Julai 2021. Ukijiandikisha baada ya tarehe 1 Julai, ada ya huduma ya 15% itatekelezwa kuanzia tarehe utakayomaliza kujiandikisha.

ada ya huduma ya asilimia 15 kwa milioni $1 (USD) za kwanza za mapato

Kuanzia tarehe 1 Julai 2021, ada ya huduma itakuwa asilimia 15 kwa mapato ya milioni $1 (USD) za kwanza unazopata kila mwaka unapouza huduma au bidhaa dijitali.

Ikiwa una akaunti Akaunti nyingi za Wasanidi Programu Zinazounganishwa (ADA) kwenye Kikundi cha Akaunti yako, kiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15 kitatumika mradi jumla ya mapato yote ya ADA zote kwenye kikundi kiwe chini ya milioni $1 (USD) na kila ADA itapokea manufaa ya kiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15. Jumla ya mapato inapozidi milioni $1 (USD), Akaunti zote za Wasanidi Programu Zilizounganishwa (ADA) zitatozwa ada ya huduma ya asilimia 30 kwa kipindi cha mwaka kilichosalia.

Mapato yatakokotolewa kila mwaka (Tarehe 1 Januari hadi 31 Desemba). Kwa kuwa mpango unaanza mwaka ukiwa umefika katikati (Tarehe 1 Julai 2021), kiwango cha kipindi cha pili cha mwaka wa 2021 kitagawanywa kuwa $500,000 (USD).

Kumbuka: Kitengo cha ada ya huduma cha asilimia 15 kitaanza kutumika tarehe 1 Julai 2021 kwa wasanidi wote wa programu watakaomaliza kujiandikisha kabla ya tarehe hii. Kwa wasanidi programu watakaojiandikisha baada ya tarehe 1 Julai 2021, ada ya asilimia 15 itatumika kuanzia tarehe ambayo wamemaliza kujiandikisha.

Kuelewa Akaunti za Wasanidi Programu Zinazohusishwa (ADA)

Vigezo vya kubaini Akaunti zako za Wasanidi Programu Zinazohusishwa (ADA) vimefafanuliwa kwa kina kwenye faharasa ya Kikundi cha Akaunti. Ielewe faharasa hii ili uwe na uelewa kamili wa maneno kama vile "Akaunti ya Msanidi Programu Inayohusishwa" na "Akaunti ya Msingi ya Msanidi Programu."

Vikundi vya Akaunti ni kipengele kipya katika Dashibodi ya Google Play kinachotusaidia kufahamu Akaunti za Wasanidi Programu ambazo unahusishwa nazo. Kutoa maelezo haya hutusaidia kuhakikisha unatimiza masharti ya kiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15 kwa milioni $1 (USD) na ya mipango mingine ya wasanidi programu wa Google Play na vipengele vya Dashibodi ya Google Play na kutoa manufaa ya baadaye.

ADA zote ni sehemu ya Kikundi cha Akaunti, ambacho kinawakilisha kujiandikisha mara moja kwenye kiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15. Akaunti ya Msingi ya Msanidi Programu itatumika kwa niaba ya akaunti zote za Wasanidi Programu zilizounganishwa (ADA) kwenye kikundi.

Kuanzisha kikundi hakutaweka au kuruhusu ufikiaji wa ziada kwenye Akaunti za binafsi ya Msanidi Programu kwenye kikundi. Mmiliki wa Akaunti ya Msingi ya Msanidi Programu hatakuwa na uwezo wa kuangalia au kudhibiti maudhui yoyote (ikiwa ni pamoja na programu ) ya ADA yoyote iliyowekwa kwenye Kikundi cha Akaunti, wasimamizi wa kila Akaunti za Msanidi Programu wasipoweka au kurekebisha kwa njia dhahiri ruhusa za watumiaji au za akaunti.

Kufungua Kikundi chako cha Akaunti

Nenda kwenye Kufungua na kudhibiti Kikundi chako cha Akaunti ili upate maelezo zaidi kuhusu Vikundi vya Akaunti .

Maswali yanayoulizwa sana

Kunja Zote Panua Zote

Nini maana ya Kikundi cha Akaunti na ni kwa nini Google Play inaniomba nianzishe kikundi cha akaunti?

Kwa kuwa kiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15 hutumika kwa kila msanidi programu, si kwa kila akaunti, tunahitaji kufahamu akaunti unazohusishwa nazo ili tuweze kutekeleza ada ya huduma kwa usahihi. 

Kwa wasanidi programu walio na akaunti moja pekee, utaanzisha Kikundi cha Akaunti katika Dashibodi ya Google Play kwa kutumia akaunti moja unayomiliki. Kwa wasanidi programu walio na akaunti nyingi, tutakuomba ufungue Kikundi cha Akaunti kinachoorodhesha Akaunti za Wasanidi Programu Zinazounganishwa (ADA). Hizi ni pamoja na akaunti zozote unazomiliki na akaunti zinazomilikiwa na kampuni tanzu ambazo huchapisha programu au michezo inayotumia vipengee vya chapa yako. Kiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15 kitatumika katika jumla ya mapato yako katika ADA zote. 

“Vipengele vya chapa” ni nini?

Vipengele vya chapa vimefafanuliwa kwenye Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu (DDA). Baadhi ya mifano ni pamoja na mali ya uvumbuzi ambazo watumiaji wanaweza kutambua na kuhusisha na msanidi programu, programu/mchezo au mfululizo mmoja, kama vile: 

  • Jina la msanidi programu
  • Jina la programu au mchezo
  • Kufanana kwa wahusika, majina ya wahusika, majina ya sehemu na mipangilio ya msuko
  • Majina na kufanana kwa kipengee mahususi/kinachotambuliwa
  • Nembo, fonti na sentensi mahususi na dhahiri
Kwa nini Google inatumia vipengele vya chapa kubaini uhusiano wa akaunti?

Ikiwa unadhibiti kampuni nyingine zinazochapisha programu na michezo kwenye Google Play kwa kutumia vipengele vyako vya chapa utahitaji kuziweka kwenye Kikundi cha Akaunti. Lengo la Google Play ni kuhakikisha kuwa tumetumia kiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15 kwa kila msanidi programu kwa njia inayofaa. Tunachukulia kuwa vipengele vya chapa ni kiashiria dhahiri cha akaunti za msanidi programu kwa sababu vipengele hivi vya chapa vinahusisha orodha ya mali ya programu na michezo ya msanidi programu kwa watumiaji na kuchangia sababu zao za kusakinisha na kulipia programu hizo kwenye Google Play.

Kikundi cha Akaunti yangu kitajiandikisha vipi kwenye kiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15?

Akaunti ya Msingi ya Msanidi Programu ya kikundi itatumika kwa niaba ya Akaunti zote za Msanidi Programu kwenye kikundi kwa kujiandikisha mara moja. Ada ya huduma itatumika kwenye mapato ya jumla katika akaunti zote kwenye kikundi. Mradi mapato jumla ya mapato yawe chini ya milioni $1 (USD), kila akaunti kwenye kikundi kitapokea ada ya huduma ya asilimia 15. Jumla ya mapato inapozidi milioni $1 (USD), ada ya huduma itabadilika kuwa asilimia 30 katika akaunti zote kwenye kikundi katika kipindi cha mwaka kilichosalia.

Itakuwaje ikiwa ninamiliki Akaunti za Msanidi Programu zisizotumia mfumo wa utozaji wa Google Play?

Kwa sasa, Vikundi vya Akaunti vinapatikana tu kwa Akaunti za Wasanidi Programu zilizo na maelezo ya akaunti ya malipo katika Dashibodi ya Google Play. Ikiwa unamiliki akaunti zisizo na maelezo ya akaunti ya malipo, huhitaji kuziorodhesha kama Akaunti za Wasanidi Programu Zinazounganishwa kwa sasa. Tutatoa Vikundi vya Akaunti kwa akaunti hizo kwenye Dashibodi ya Google Play baadaye.

Je, uhamishaji wa programu unaruhusiwa?

Ndiyo. Kumbuka kwamba programu inapohamishwa kati ya akaunti za wasanidi programu kwenye Vikundi tofauti vya Akaunti, mapato yote ya programu yatajumuishwa kwenye jumla ya kila Vikundi vya Akaunti katika mwaka huo.

Kwa mfano, ikiwa akaunti ya msanidi programu kwenye Kikundi cha Akaunti cha A kina programu iliyopata mapato ya $100,000 (USD) katika mwaka huu ambayo inahamishwa kwenye akaunti nyingine ya msanidi programu katika Kikundi cha Akaunti cha B, mapato haya ya $100,000 (USD) yatajumuishwa kwenye jumla ya mapato ya Vikundi vyote viwili vya Akaunti ya A na B kwa madhumuni ya kukokotoa kiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15 katika mwaka huu.

Je, ninaweza kufanya mabadiliko kwenye Kikundi changu cha Akaunti baadaye?

Ndiyo. Unaweza kuweka au kuondoa Akaunti za Msanidi Programu kwenye kikundi chako ili kuonyesha mabadiliko katika umiliki wa akaunti. 

Kumbuka kwamba Akaunti ya Msanidi Programu inapohamishwa kati ya Vikundi tofauti vya Akaunti, mapato ya akaunti hiyo yatajumuishwa kwenye jumla ya Vikundi vyote viwili vya Akaunti katika mwaka huo.

Je, mapato ya kila mwaka ya msanidi programu ya milioni 1M (USD) yatahesabiwa vipi?

Mapato yatahesabiwa katika kila mwaka (Tarehe 1 Januari hadi 31 Desemba). Kwa sababu mpango unaanza mwaka ukiwa umefika katikati (Tarehe 1 Julai 2021), kiwango cha kipindi cha pili cha mwaka wa 2021 kitagawanywa kuwa $500,000 (USD).

Kumbuka: Kitengo cha ada ya huduma cha asilimia 15 kitaanza kutumika tarehe 1 Julai 2021 kwa wasanidi wote wa programu watakaomaliza kujiandikisha kabla ya tarehe hii. Ikiwa msanidi programu atajiandikisha baada ya tarehe 1 Julai, asilimia hii 15 itatumika kuanzia tarehe ambayo amemaliza kujiandikisha.

Je, sarafu zisizo za USD zitazingatiwa vipi?

Mapato ya wasanidi programu ya milioni $1 yamebainishwa katika USD. Miamala katika sarafu nyingine zitageuzwa kwa kutumia viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni vinavyofaa ambavyo vitasasishwa siku yote.

Wasanidi programu watapokea ada ya huduma ya asilimia 15 lini?

Kiwango cha ada ya huduma cha asilimia 15 kitatumika baada tu ya msanidi programu kukamilisha hatua zinazohitajika za kujiandikisha kwenye Dashibodi ya Google Play na kitaonekana kwenye kipindi kinachofuata cha malipo ya kila mwezi.

Kampuni yangu inamiliki akaunti mbili tofauti za wasanidi programu ambazo hazishiriki vipengele vya chapa. Je, ninaweza kuunda Vikundi viwili vya Akaunti?

Kwa sababu unamiliki akaunti zote mbili za wasanidi programu, unapaswa kuunda Kikundi kimoja cha Akaunti. Vikundi vya Akaunti vinatakiwa kuwa na kila akaunti ya msanidi programu unayomiliki, pamoja na akaunti nyingine zozote za wasanidi programu zinazomilikiwa na kampuni tanzu au washirika wanaotumia vipengele vyako vya chapa.

Kampuni yangu ilinunuliwa, lakini tunaendelea kufanya kazi kwa kujitegemea. Je, ninapaswa kuwa sehemu ya Kikundi cha Akaunti cha kampuni ambayo sasa inamiliki kampuni yangu?

Hapana, ili mradi hamshiriki vipengele vya chapa na kampuni yako kuu au huchapishi programu au michezo yao. Ili ujiandikishe, unda Kikundi cha Akaunti ambacho ni tofauti na Kikundi cha Akaunti cha kampuni yako kuu. Kumbuka kujumuisha akaunti nyingine zozote za wasanidi programu unazomiliki, pamoja na akaunti zozote za kampuni unazomiliki au za washirika wanaoshiriki vipengele vyako vya chapa.

  • Mfano A: Kampuni yako imemnunua msanidi programu kama kampuni tanzu, na msanidi programu huyo anatenganisha orodha yake ya chapa na programu/mchezo kuwa tofauti na ile ya kampuni yako. Katika mfano huu, msanidi programu anaweza kutengeneza Kikundi cha Akaunti tofauti.
  • Mfano B: Kampuni yako imemnunua msanidi programu aliyebadilisha jina lake la mchapishaji ili kurejelea lile la kampuni yako, amechapisha baadhi ya IP zako au ametumia vipengele vingine vya chapa kutoka katika kampuni yako au orodha yako ya programu/mchezo. Katika mfano huu, msanidi programu anatakiwa kutumia Kikundi cha Akaunti pamoja na kampuni yako.
Kampuni yangu inamiliki kampuni zaidi ya moja zilizo na akaunti za wasanidi programu kwenye Google Play. Je, ninahitaji kuunda Kikundi cha Akaunti kwa kampuni zote ninazomiliki?

Ikiwa kampuni unazomiliki hazichapishi programu au michezo inayoshiriki vipengele vya chapa, wanaweza kujiandikisha kwenye programu hii kivyao na kuunda Vikundi vya Akaunti zao wenyewe. Hata hivyo, kampuni zozote unazomiliki ambazo zinashiriki vipengele vya chapa zinatakiwa kuwa kwenye Kikundi kimoja cha Akaunti. Kumbuka kwamba, kama unamiliki kampuni zinazochapisha matoleo ya programu au michezo yako iliyojanibishwa au kubadilishwa chapa kwa ajili ya maeneo mahususi, programu hizi zitachukuliwa kama programu zako na akaunti za wasanidi programu ambazo zitachapisha zitachukuliwa kuwa akaunti zako za wasanidi programu waliohusishwa, na watatakiwa kuwepo katika kikundi chako.

Mfano: Kampuni yako inamiliki kampuni tanzu ambayo inachapisha programu au michezo yako katika maeneo mahususi au inashiriki na wewe vipengele vingine vya chapa. Kampuni tanzu yako inajanibisha baadhi ya programu au michezo hii. Katika mfano huu, unatakiwa kutumia Kikundi cha Akaunti pamoja na kampuni yako.

Kampuni yangu inachapisha programu na michezo yenye leseni na vipengele vya chapa vinavyomilikiwa na kampuni nyingine. Je, ninapaswa kuwa kwenye kikundi kimoja pamoja nao?

Ilimradi hakuna uhusiano wa umiliki au udhibiti wa maslahi kati ya kampuni mbili hizo, kila kampuni inaweza kuunda Kikundi chake cha Akaunti. Vikundi hivi vya Akaunti lazima vijumuishe akaunti za wasanidi programu zinazomilikiwa na kila kampuni, pamoja na kampuni tanzu na washirika ambao wanashiriki vipengele vya chapa pamoja nao.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11811101085808693830
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false