Maswali Yanayoulizwa Sana Kuhusu Toleo Jipya la Dashibodi ya Google Play

Mnamo 2020, tulizindua toleo jipya la Dashibodi ya Google Play. Tumebadilisha zana na vipengele vingi, tukaongeza vipya na tukaboresha hali ya usogezaji ili kupanga vizuri vipengele vinavyohusiana.

Tuna uhakika kuwa hali mpya ya bidhaa itakusaidia udhibiti na usambaze programu zako kwa njia bora. Na, tunatambua kuwa baadhi ya mabadiliko yatachukua muda ili yaeleweke. Makala haya yanakupa majibu ya baadhi ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara ambayo tumepokea kutoka kwa wasanidi programu wanaoanza kutumia toleo jipya la Dashibodi ya Google Play.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Kunja Zote Panua Zote

Nitapakia wapi faili za kuambatisha za ufumbuzi au za ReTrace au za alama za utatuzi?

Faili za kuambatisha za ufumbuzi na ReTrace zilizojumuishwa kwenye App Bundle yako kupitia majukumu ya kawaida ya Gradle zitahusishwa na mradi wako na kutumiwa kufumbua ufuatiliaji wako wa rafu bila kuhitaji uchukue hatua ya ziada. Iwapo ungependa au unahitaji kupakia faili hizi mwenyewe, una chaguo zifuatazo:

  • Pakia faili unapoandaa toleo lako: Kwenye menyu ya vipengee vya ziada vya vizalia vya programu katika jedwali la vizalia vya programu, chagua Weka faili ya kuambatisha ya ReTrace.
  • Pakia faili za toleo lililopo: 
    • Katika jedwali la vizalia vya programu unapokagua maelezo ya toleo, au
    • Kwenye ukurasa wa kichunguzi cha App Bundle, chagua kichupo cha Faili Zilizopakuliwa. Katika sehemu ya "Vipengee", bofya ishara ya kupakia kwenye sehemu ya kulia ya faili ambayo ungependa kuweka. 

Hakikisha umesoma makala ya Fanya ufuatiliaji wa rafu za matukio ya programu kuacha kufanya kazi ufumbuliwe au utambuliwe kupitia ishara ili upate maelezo zaidi.

Nitaweka wapi kiungo changu cha sera ya faragha?

Unaweza kuweka sera yako ya faragha kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu, chini ya "Sera ya Faragha." Ukurasa wa Maudhui ya programu ni mahali ambapo unatufahamisha kuhusu maudhui ya programu yako ili kuhakikisha yanatii sera za Google Play.

Yafuatayo ni makala muhimu kuhusu kutayarisha programu yako ili ikaguliwe.

Uchapishaji unaoratibiwa unapatikana wapi kwenye toleo jipya la Dashibodi ya Google Play?

Utendaji huu umeboreshwa. Sasa unaitwa Uchapishaji Unaodhibitiwa na ni sehemu ya "Muhtasari wa Uchapishaji" kwenye sehemu ya juu kushoto ya usogezaji wako.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu Uchapishaji Unaodhibitiwa katika chapisho kwenye blogu, Kuboresha mchakato wa kuchapisha programu yako ukitumia vipengele vipya vya Dashibodi ya Google Play na Chagua wakati ambapo masasisho ya programu yako yanachapishwa kwenye Uchapishaji unaodhibitiwa cha Chuo cha Google Play.

Ili kufahamu tofauti zote kati ya uchapishaji unaoratibiwa na unaodhibitiwa, unaweza pia kusoma Dhibiti wakati mabadiliko ya programu yanachapishwa kwenye uchapishaji unaodhibitiwa.

Toleo jipya la Dashibodi ya Google Play litaniarifu vipi kuhusu matukio na ilani? Katika toleo la zamani la Dashibodi ya Google Play, kulikuwa na kengele ya arifa iliyo na nukta nyekundu katika sehemu ya juu kulia kwenye skrini.

Nafasi ya kipengele cha awali cha arifa imechukuliwa na Kikasha chako, kinachopatikana katika sehemu ya juu ya kidirisha cha kusogeza cha kushoto. Nukta ya samawati inaonyesha kuwa una ujumbe ambao hujasoma. Unaweza kuweka mapendeleo ya arifa kwenye ukurasa wa Arifa (Mipangilio > Arifa).

Ninaweza kubadilisha vipi lugha ya kuonyesha kwenye Dashibodi ya Google Play?

Unaweza kubadilisha lugha ya kiolesura cha Dashibodi ya Google Play kupitia URL iliyo na kigezo cha GET ( inajulikana pia kama mifuatano ya hoja au vigezo vya URL) ambayo itaendelea kutumika hadi uibadilishe.

Kwa mfano, ili ubadilishe lugha ya kiolesura cha Dashibodi ya Google Play iwe Kihispania, unaweza kuweka hl=es kwenye URL yako: https://play.google.com/console?hl=es.

Ninaweza kunakili wapi maelezo kuhusu toleo la awali katika toleo jipya?

Unapoandaa toleo, bofya Nakili kutoka toleo la awali juu ya sehemu ya "Maelezo kuhusu toleo" katika sehemu ya "Maelezo kuhusu toleo".

Nitapakua wapi APK (Kifurushi cha Programu za Android) za usambazaji zilizoambatishwa cheti na Google au APK niliyopakia?

Unaweza kupata zote mbili, pamoja na App Bundle au APK kwa kila mipangilio ya kifaa mahususi, kwenye kichupo cha Faili zilizopakuliwa cha kichunguzi cha App Bundle.

Hakikisha umesoma makala ya Kagua matoleo ya programu ukitumia kichunguzi cha App Bundle ili upate maelezo zaidi.

Ninaweza kubatilisha uchapishaji wa programu wapi kwenye Google Play?

Unaweza kubadilisha upatikanaji wa programu yako kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina (Toleo > Mipangilio > Mipangilio ya kina), kwenye kichupo cha Upatikanaji wa programu.

Ninaweza kubadilisha maelezo ya programu yangu wapi?

Unaweza kubadilisha maelezo ya programu yako (kama vile ufafanuzi, picha za skrini na video ya matangazo) kwenye Ukurasa mkuu wa programu katika Google Play (Kuza > Upatikanaji katika Google Play > Ukurasa mkuu wa programu katika Google Play). Maelezo ya mawasiliano sasa yanapatikana kwenye ukurasa wa Mipangilio ya duka.

Ninaweza kubadilishia wapi nchi ninazolenga?

Unaweza kubadilisha upatikanaji katika nchi kwenye kichupo cha Nchi au maeneo kwa kila kikundi lengwa.

Chaguo za mtoa huduma ziko wapi?

Sasa unaweza kuwasha au kuzima ulengaji wa mtoa huduma kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina (ToleoMipangilio > Mipangilio ya kina), kwenye kichupo cha Ulengaji wa mtoa huduma. Ukiwasha, unaweza kupata kitufe cha Mipangilio ya mtoa huduma kwenye kichupo cha Nchi au maeneo kwa toleo lako la umma.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14017452241569713547
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false