Pata manufaa kamili ya kukusanya michango kwenye YouTube

YouTube inaweza kuwa na mchango mkubwa sana ulimwenguni, iwe ni kwa kukuza uelewa au kuchangisha fedha kwa ajili ya harakati na mashirika unayoyajali.

Tunafahamu kuwa wengi wenu mnatafuta njia za kusaidia jamii zenu na kuleta mabadiliko. Ili kusaidia kutimiza malengo yako, hii ni baadhi ya mifano ya jinsi ya kupata manufaa kamili kupitia michango kwenye YouTube.

Baadhi ya mifano ya hatua unazoweza kuchukua:

  • Kuchangisha pesa ukitumia Uhisani wa YouTube: Vituo vinavyostahiki katika maeneo fulani vinaweza kuchangisha fedha kwa ajili ya mashirika yasiyo ya faida yanayopatikana kwa kuweka Kitufe cha kuchanga kwenye video zake na mitiririko mubashara. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka mipangilio ya michango hapa.
  • Ikiwa hustahiki kwa ajili ya Uhisani wa YouTube: Tumia Skrini za Mwisho ili kuunganisha kwenye mchango wa nje. Skrini za mwisho zinaweza kuwekwa kwenye sekunde 5 hadi 20 za mwisho wa video. Kuna tovuti kadhaa zilizoidhinishwa za wahusika wengine (kama vile GoFundMe, JustGiving) zinazoweza kuunganishwa kwenye skrini za mwisho.
  • Kuchanga mapato yako mwenyewe kutoka video mahususi: Tayarisha maudhui halisi ambayo hadhira yako inapenda kutazama. Unaweza kuwaambia watazamaji wako kwamba utachanga pesa unazochuma kwa shirika mahususi. Lakini, hupaswi kuwahimiza kubofya au kutazama matangazo ili kuongeza mchango.

Baadhi ya mifano ya mambo usiyoruhusiwa kufanya:

  • Usihimize shughuli taka kama vile kurudiarudia kutazama na kubofya matangazo kwenye video zako. Kumbuka kuwa shughuli taka ni ukiukaji wa Sera yetu dhidi ya Shughuli Bandia na sera zetu na video yako inaweza kuondolewa. Tunapogundua tabia hii, watayarishi hawatalipwa kwa utazamaji na mibofyo ya aina hii na watangazaji hawatatozwa.
  • Usipakie kazi ya watayarishi au wasanii wengine bila kufanya mabadiliko ya kutosha. Ikiwa utatumia kazi ambayo hukutayarisha mahali unapotaka kupeleka michango, video yako inaweza kudaiwa kwa mujibu wa ulinzi wa hakimiliki.
  • Usitoe madai ya uongo kuhusu kuchangia shirika au shirika lisilo la faida. YouTube haiwajibiki kuthibitisha kuwa ahadi za watayarishi za kuchanga zinapokelewa na mashirika yasiyo ya faida.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2630083875747358618
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false