Kudhibiti gumzo la moja kwa moja

Kudhibiti gumzo lako la moja kwa moja hukuwezesha kuwasiliana na hadhira yako na kuratibu hali yako ya utumiaji wa Mtiririko mubashara kwa njia inayokufaa. YouTube hukupa zana unazohitaji kuimarisha usalama wako na wa watazamaji wako.

Kumbuka: Kila mtu anayeshiriki kwenye gumzo la moja kwa moja anaweza kumripoti au kumzuia mtumiaji mwingine.

How to Moderate Live Chat on YouTube

Kabla ya kuanzisha gumzo lako la moja kwa moja

Jiandae kwa kipindi chako cha gumzo la moja kwa moja kwa kuweka mipangilio ya zana hizi za udhibiti. Baadhi ya zana hizi zinaweza kutumiwa wakati wa mtiririko wako mubashara na baada ya mtiririko huo.

Gumzo la moja kwa moja la wanaofuatilia chaneli pekee

Unaweza kufanya gumzo la moja kwa moja lipatikane tu kwa wanaofuatilia chaneli yako na unaweza kubainisha muda ambao watazamaji hao wanapaswa kuwa wamefuatilia chaneli. Unaweza kubadilisha mipangilio hii kabla au wakati wa mtiririko mubashara au wakati wa Onyesho lako la kwanza.

Ili kuwasha gumzo la moja kwa moja la wanaofuatilia chaneli pekee kwa Maonyesho ya kwanza:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye Maudhui, chagua Onyesho la kwanza unalotaka kusasisha.
  3. Kwenye Maelezo, nenda kwenye Onyesha Zaidi kisha Gumzo la Moja kwa Moja.
  4. Katika hali ya Washiriki, chagua Wanaofuatilia.

Unapowasha gumzo la wanaofuatilia chaneli pekee, hadhira yako itaarifiwa kuwa umefanya hivyo na muda ambao wanapaswa kuwa wamefuatilia chaneli yako ili waweze kutuma ujumbe.

Unaweza kuwasha hali ya polepole na gumzo la wanaofuatilia chaneli pekee kwa wakati mmoja. Huwezi kuwasha gumzo la wanachama pekee na gumzo la wanaofuatilia chaneli pekee kwa wakati mmoja.

Ili uwashe gumzo la wanaofuatilia chaneli pekee:

  1. Nenda kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja.
  2. Kwenye mtiririko wako mubashara, bofya Hariri.
  3. Bofya Gumzo la moja kwa moja.
  4. Kwenye sehemu ya “Wanaoweza kutuma ujumbe,” chagua Wanaofuatilia.
  5. Si lazima: Chagua muda ambao watazamaji wanapaswa kuwa wamefuatilia chaneli yako ili waweze kutuma ujumbe wa gumzo la moja kwa moja.
  6. Bofya Hifadhi.
Kumbuka: Mtazamaji akishiriki kwenye gumzo la moja kwa moja la wanaofuatilia chaneli pekee, watazamaji wengine wataona hadharani kuwa mtazamaji huyo anafuatilia chaneli husika.

Gumzo la moja kwa moja la wanachama pekee

Unaweza kuandaa gumzo za moja kwa moja ambazo zinahusisha wanachama wako pekee. Ili uwashe gumzo la moja kwa moja la wanachama pekee kwenye kompyuta yako:
  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Upande wa juu kulia, bofya ANZISHA kisha Tiririsha mubashara.
  3. Upande wa kushoto, bofya Tiririsha.
  4. Anzisha mtiririko:
    1. Ili unakili mtiririko wa awali: Chagua mtiririko wa awali kisha ubofye Tumia mipangilio tena.
    2. Ili uanzishe mtiririko mpya: Weka maelezo ya mtiririko wako kisha ubofye Anzisha mtiririko.
  5. Kwenye upande wa juu kulia, bofya Hariri.
  6. Kwenye sehemu ya "Gumzo la moja kwa moja," chagua Washa gumzo la wanachama pekee.
  7. Bofya Hifadhi.

Ili uwashe gumzo la wanachama pekee kwa Maonyesha ya kwanza:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye Maudhui, chagua Onyesho la kwanza unalotaka kusasisha.
  3. Kwenye Maelezo, nenda kwenye Onyesha Zaidi kisha Gumzo la Moja kwa Moja.
  4. Katika hali ya Washiriki, chagua Wanaofuatilia.

Hali ya maoni mubashara

Unaweza kuweka mipangilio kwenye gumzo lako la moja kwa moja ili uruhusu tu watumiaji uliowaidhinisha kama washiriki wa gumzo la moja kwa moja wakati wa kipindi cha mtiririko mubashara. Watumiaji uliowachagua tu ndio wanaweza kutuma ujumbe wa gumzo la moja kwa moja, watazamaji wengine wanaweza kuangalia ujumbe huu pamoja na onyesho la kwanza au mtiririko wako mubashara.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Upande wa juu kulia, bofya ANZISHA kisha Tiririsha mubashara.
  3. Kwenye sehemu ya Kuweka mapendeleo, chagua kisanduku cha Gumzo la moja kwa moja ili uwashe Gumzo la Moja kwa Moja.
  4. Chagua ‘Maoni mubashara’ ili uwashe. (Unaweza kusasisha orodha ya ‘Watumiaji Uliowaidhinisha’ kwenye mipangilio ya jumuiya).
  5. Si lazima: Weka URL za chaneli kwenye orodha ya watumiaji uliowaidhinisha. Kumbuka: ikiwa hakuna chaneli zozote kwenye orodha yako ya ‘Watumiaji Uliowaidhinisha’, chaneli yako ndio tu itakuwa imeidhinishwa kutumia gumzo la moja kwa moja.
  6. Bofya Endelea ili uhifadhi.

Ili kuwasha hali ya Maoni mubashara kwenye Maonyesho ya kwanza:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye Maudhui, chagua Onyesho la kwanza unalotaka kusasisha.
  3. Kwenye Maelezo, nenda kwenye Onyesha Zaidi kisha Gumzo la Moja kwa Moja.
  4. Katika hali ya Washiriki, chagua Wanaofuatilia.

Kuweka wadhibiti

Mdhibiti ni mtu unayemwamini ili akusaidie kujenga hali bora na salama ya utumiaji wa chaneli kwa ajili ya jumuiya yako. Mdhibiti husaidia kukagua na kudhibiti maoni yanayotolewa na watumiaji kwenye video au ujumbe unaotumwa na washiriki wakati wa gumzo la moja kwa moja kwenye mtiririko. Kuna aina mbili za wadhibiti: mdhibiti wa kawaida na mdhibiti mkuu. Mdhibiti mkuu ana ruhusa zaidi kuliko mdhibiti wa kawaida. Pata maelezo zaidi hapa.

Programu ya YouTube

  1. Fungua programu ya YouTube .
  2. Anzisha mtiririko wako mubashara kwa kubonyeza alama ya Kuongeza, kisha Moja kwa Moja, ili uanzishe gumzo la moja kwa moja.
  3. Karibu na ujumbe wa gumzo, bofya menyu '' kisha uchague ”Mweke awe mdhibiti mkuu” au “Mweke awe mdhibiti wa kawaida”.

Programu ya Studio ya YouTube

  1. Fungua Studio ya YouTube.
  2. Upande wa kushoto, bofya Mipangilio kisha Jumuiya.
  3. Kwenye kichupo cha Vichujio vya Kiotomatiki, weka URL ya chaneli kwenye kisanduku cha “Mdhibiti mkuu” au “Mdhibiti wa kawaida”.
  4. Bofya Hifadhi.

Kuzuia ujumbe ulio na maneno fulani

Ili uzuie ujumbe wa gumzo la moja kwa moja ulio na maneno fulani au unaolingana kwa karibu na maneno hayo, unda orodha ya maneno yaliyozuiwa katika Studio ya YouTube.
  1. Fungua Studio ya YouTube.
  2. Upande wa kushoto, bofya Mipangilio kisha Jumuiya.
  3. Kwenye kichupo cha Vichujio vya Kiotomatiki kisha “Maneno yaliyozuiwa,” weka orodha ya maneno yaliyozuiwa. Ujumbe ulio na neno lolote kati ya maneno haya utazuiwa kwenye gumzo lako la moja kwa moja.
  4. Bofya Hifadhi.

Kuzuia ujumbe wa gumzo la moja kwa moja ambao huenda haufai ili ukaguliwe

Unaweza kuruhusu YouTube izuie ujumbe wa gumzo la moja kwa moja ambao huenda haufai. Ukijijumuisha, ujumbe wa gumzo la moja kwa moja ambao mfumo wetu utatambua utazuiwa ili ukaguliwe kwenye mipasho ya gumzo. Una uhuru wa kufanya uamuzi wa mwisho wa kuonyesha au kuficha ujumbe huu wa gumzo. Hakuna mfumo ulio bora kikamilifu, lakini kipengele hiki kitakurahisishia mchakato wa kudhibiti ujumbe wa gumzo la moja kwa moja kwenye mtiririko wako mubashara.
Washa au uzime kipengele cha "zuia ujumbe ili ukaguliwe"
  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
  2. Upande wa kushoto, gusa Mipangilio kisha Jumuiya kisha Mipangilio chaguomsingi.
  3. Kwenye sehemu ya “Ujumbe kwenye gumzo lako la moja kwa moja,” chagua au ubatilishe uteuzi wa Zuia ujumbe ambao huenda haufai ili ukaguliwe.
Baada ya kuwasha "zuia ujumbe ili ukaguliwe," unaweza kuficha au kuonyesha ujumbe ambao YouTube imezuia.
  • Ukichagua ONYESHA: ujumbe wa gumzo utaonyeshwa kwenye mtiririko wa gumzo katika wakati halisi ambao ujumbe huo ulitumwa.
  • Ukichagua FICHA: ujumbe wa gumzo huendelea kufichwa usionekane kwa watazamaji.
  • Usipochukua hatua yoyote: ujumbe wa gumzo huendelea kufichwa usionekane na watazamaji.

Hali ya polepole

Hali ya polepole hukuwezesha kudhibiti mara ambazo kila mtumiaji anaweza kutoa maoni kwa kuweka kikomo cha muda baina ya maoni. Mmiliki wa chaneli, wadhibiti na wanachama wa chaneli ya YouTube hawaathiriwi na kikomo hicho.
Kuwasha katika Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja kisha Kutiririsha
  1. Anzisha mtiririko mubashara.
  2. Bofya Hariri.
  3. Bofya Kuweka mapendeleo.
  4. Kwenye sehemu ya "Ucheleweshaji wa ujumbe," chagua Hali ya polepole. Weka muda ambao ungependa washiriki wasubiri kabla ya kutuma ujumbe mwingine.

Kuwasha au kuzima Gumzo la moja kwa moja

Unaweza kuwasha au kuzima Gumzo la moja kwa moja wakati wowote, hata baada ya tukio kuanza. Huwezi kuzima Gumzo la moja kwa moja kwenye Maonyesho ya kwanza.

Upande wa juu kulia, bofya Badilisha kisha Gumzo la Moja kwa Moja kisha Washa gumzo la moja kwa moja.

Wakati wa gumzo lako la moja kwa moja

Dhibiti shughuli za udhibiti kwenye mipasho ya gumzo la moja kwa moja

Unaweza kuwasha au kuzima shughuli za udhibiti kwenye mipasho ya gumzo la moja kwa moja. Mipangilio ya udhibiti wa gumzo la moja kwa moja kwa chaguomsingi huwa imezimwa.

Kwenye mipasho ya gumzo la moja kwa moja

  1. Kwenye mpasho wa gumzo la moja kwa moja, bofya Zaidi ''.
  2. Kisha ubofye Zaidi kisha Geuza shughuli za udhibiti.

Kidokezo: ukifuta akiba yako ya kivinjari au ukiwa una chaneli zingine, angalia mipangilio yako ya shughuli za udhibiti ili kuhakikisha kuwa shughuli za udhibiti zimewashwa au zimezimwa.

Kudhibiti ujumbe na watazamaji kwenye mipasho ya gumzo la moja kwa moja

Kwenye kompyuta yako, shikilia 'ALT' / 'Option' kwenye kibodi yako ili usitishe mipasho ya gumzo na uelekeze kwenye ujumbe. Utaona chaguo za:
  • Futa ujumbe.
  • Mzuie mtumiaji asichangie.
  • Mfiche mtumiaji kwenye sehemu ya mipasho ya ujumbe wa gumzo au maoni kwenye chaneli yako.

Kidokezo: Wadhibiti wanaweza kupata maelezo zaidi kuhusu mshiriki wa gumzo la moja kwa moja kwa kwenda moja kwa moja kwenye chaneli yake.

  • Kwenye kompyuta: Wekelea kiashiria juu ya ujumbe, bofya Zaidi '', kisha Nenda kwenye chaneli.
  • Kwenye kifaa cha mkononi: Gusa ujumbe, kisha Nenda kwenye chaneli.

Kufikia Shughuli kwenye Chaneli katika mipasho ya gumzo la moja kwa moja

Kumbuka: Kwa sasa, inapatikana tu kwenye kompyuta ya mezani.
Wewe na wadhibiti mnaweza kufikia historia ya watumiaji ya umma kwenye mipasho ya gumzo la moja kwa moja kwa kubofya Shughuli kwenye Chaneli katika Menyu. Itaonyesha:
  • Picha ya wasifu ya umma ya mtumiaji 
  • Utambulisho wa mtumiaji wa umma
  • Tarehe ya kujjiunga kwenye YouTube
  • Idadi ya wafuatiliaji wa mtumiaji
  • Ujumbe wa gumzo la moja kwa moja wa umma (ujumbe usiozidi 50 kwa kila mtiririko)

Pia itakuwa na jumla ya idadi za vitendo vya udhibiti vilivyochukuliwa dhidi ya mtumiaji mwaka uliopita:

  • Ujumbe uliofutwa
  • Matukio ya muda kuisha
  • Matukio ya kufichwa

Kuficha au kuonyesha mtazamaji kwenye gumzo la moja kwa moja

Hatua ya kuficha mara nyingi hutumiwa kwa washiriki wanaopuuza mwongozo na maonyo na ambao hutuma ujumbe usiofaa mara kwa mara. Unapoficha mtu kwenye chaneli, ujumbe wake wa gumzo na maoni hayataonekana tena kwa watazamaji wengine. YouTube haimjulishi mtumiaji kuwa umemficha.
Kwenye mipasho ya gumzo la moja kwa moja
  1. Kwenye mpasho wa gumzo la moja kwa moja, tafuta ujumbe wa mtazamaji unayetaka kumficha.
  2. Karibu na ujumbe huo, bofya Zaidi '' kisha Ficha mtumiaji.
Kwenye Studio ya YouTube
  1. Fungua Studio ya YouTube.
  2. Upande wa kushoto, bofya Mipangilio kisha Jumuiya.
  3. Kwenye kichupo cha Vichujio vya Kiotomatiki kisha “Watumiaji waliofichwa,” andika jina la mtazamaji unayetaka kumficha.
  4. Ili uonyeshe mtazamaji, bofya X karibu na jina lake. Sasa anaweza kuweka maoni na ujumbe wa gumzo la moja kwa moja kwenye chaneli yako.
  5. Bofya Hifadhi.
Kumbuka: Hatua hii pia itamficha mtumiaji kwenye maoni. Utaona watumiaji uliowaficha kwenye sehemu ya Watumiaji Waliofichwa katika Mipangilio ya Jumuiya.

Baada ya gumzo lako la moja kwa moja

Kipengele cha Kuonyesha tena gumzo la moja kwa moja

Baada ya mtiririko mubashara kuisha, kipengele cha Kuonyesha tena gumzo la moja kwa moja kitapatikana kwenye kumbukumbu zote za mtiririko. Kipengele hiki kitaonyesha tena gumzo pamoja na mtiririko kama ulivyokuwa wakati wa kutiririshwa mubashara. Kipengele cha kuonyesha tena gumzo la moja kwa moja kimewashwa kwa chaguomsingi kwenye mitiririko yako yote mubashara.
Ili kuzima kipengele cha Kuonyesha tena gumzo la moja kwa moja
  1. Nenda kwenye youtube.com/my_videos.
  2. Bofya kichupo cha Mubashara.
  3. Chagua video.
  4. Bofya kichupo cha Weka mapendeleo.
  5. Acha kuchagua kisanduku kilicho karibu na "Kipengele cha kuonyesha tena gumzo la moja kwa moja."

Kuangalia au kufuta Historia yako ya gumzo la moja kwa moja

Unaweza kuangalia Gumzo za moja kwa moja ambako umeshiriki wakati wa mitiririko mubashara ya YouTube.
  1. Nenda kwenye Historia.
  2. Upande wa kulia wa ukurasa, bofya Gumzo la moja kwa moja.
  3. Nenda chini ili upate ujumbe wa gumzo la moja kwa moja Ili uufute, wekelea kiashiria kwenye ujumbe huo kisha ubofye X.
Ikiwa una gumzo zinazofadhiliwa au Super Chat, unaweza kuziona pia. Pesa hazitarejeshwa ukifuta ujumbe wa Super Chat baada ya mtiririko mubashara kuisha.
Kumbuka: Kulingana na ripoti za watumiaji, YouTube inaweza kuzima kipengele cha Gumzo la moja kwa moja kwenye video yako ikiwa maudhui ya mtiririko au Gumzo la moja kwa moja linakiuka mwongozo wetu wa jumuiya.

Kuangalia maoni baada ya mtiririko wako kuisha

Gumzo la moja kwa moja halipatikani baada ya mtiririko wako mubashara kuisha, lakini maoni yataonyeshwa chini ya kicheza video.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17520877590840490455
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false