Pata taarifa kuhusu maudhui yanayohusiana na afya

Kumbuka: Ikiwa unataka kituo chako kistahiki kwa ajili ya vipengele vya afya vya YouTube, pata maelezo zaidi hapa.

Hapa YouTube, tunajitahidi kukuunganisha na maudhui ya afya kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika ili uendelee kupata habari na uishi maisha yenye afya bora. Tumebuni vipengele kadhaa vya kukupa muktadha zaidi kuhusu maudhui ya afya unayopata kwenye YouTube.

Huenda vipengele vilivyo hapa chini visipatikane katika nchi au maeneo yote na kwa lugha zote. Tunajitahidi kuanzisha vipengele hivi katika nchi au maeneo zaidi na kwa lugha zaidi.

Vidirisha vya taarifa vinavyotoa muktadha wa chanzo cha maelezo ya afya

Unapotazama video ya YouTube kuhusu mada inayohusiana na afya, unaweza kuona kidirisha cha taarifa kinachotoa muktadha wa chanzo chini ya video. Kidirisha hiki kinanuiwa kukupa maelezo zaidi ili kukusaidia kuelewa vyema vyanzo vya maudhui ya afya unayoyapata na kuyatazama kwenye YouTube.

Ili kutambua vyanzo vya maelezo ya afya vinavyotimiza masharti ya kutumia kipengele hiki, tulianza nchini Marekani kwa kutumia mkusanyiko wa kanuni na ufafanuzi ulioandaliwa na jopo la wataalamu walioletwa pamoja na Chuo cha Kitaifa cha Tiba (NAM) na kukaguliwa na Shirika la Afya ya Umma la Marekani (APHA). Kanuni hizi za msingi zilichapishwa kwenye utafiti ulioitwa Kutambua Vyanzo vya Kuaminika vya Maelezo ya Afya katika Mitandao Jamii: Kanuni na Sifa.

Tunapojumuisha maeneo mengine nje ya Marekani, tunarejelea kazi iliyofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Mwaka 2022, WHO na NAM ziliandaa mkutano wa wataalamu kutoka nyanja mbalimbali kote duniani ili kuhakiki na kuthibitisha kanuni zilizoandaliwa kwa ajili ya Marekani kwa matumizi ya duniani kote. Ili kujumuisha juhudi hizi duniani kote, tunaweza pia kurejelea kazi zilizofanywa na mashirika mengine, kama vile ya nchini Uingereza.

Awamu ya hivi punde ya kazi yetu, inaturuhusu kutambua vyanzo vya kuaminika vya maelezo ya afya miongoni mwa watu binafsi na mashirika yasiyoidhinishwa. Kanuni za kutambua vyanzo vya kuaminika ziliandaliwa na jopo la wataalamu walioletwa pamoja kwa ushirikiano kati ya Baraza la Vyama Maalum vya Madaktari (CMSS), NAM na WHO.

Kanuni za vyanzo vya kuaminika vya maelezo ya afya katika tafiti husika zinabainisha kuwa vyanzo vinapaswa kuwa vya kisayansi, viwe huru, wazi na viwajibike. YouTube ilitumia kanuni hizi kutambua aina ya vyanzo vya maelezo ya afya vinavyoweza kuchukuliwa kuwa vya kuaminika:

  • Mashirika yaliyo na mbinu maalum za kuhakiki (ikijumuisha mashirika ya afya, taasisi za kielimu, idara za afya ya umma na mashirika ya kiserikali). Mbinu za kuhakiki zinajumuisha kutambuliwa rasmi, kunakiliwa katika faharasa ya jarida la elimu na kuhusishwa kwenye kanuni za uwajibikaji za serikali. Kwa maelezo zaidi, kagua mchoro wa 1 katika Utafiti wa NAM.
  • Watu binafsi na mashirika ambayo hayajaidhinishwa yaliyo na vituo vya YouTube vinavyoangazia maudhui ya afya. Watu binafsi na mashirika sharti yatume maombi na yapite katika mfululizo wa vipengele vya ukaguzi wa kutimiza masharti ili wapate kidirisha cha maelezo. Kama sehemu ya mchakato huo wa kutuma ombi, tunakagua iwapo mhusika au mtu kutoka shirika lisiloidhinishwa anayesimamia na kukagua maudhui ya kituo hicho, ni mtaalamu wa matibabu mwenye leseni. Kwa sasa, aina hii ya chanzo cha maelezo ya afya inaweza kuonekana tu katika idadi ndogo ya nchi.

Mashirika yaliyo na mbinu maalum zilizopo za kuhakiki

Mashirika yaliyo na mbinu maalum za kuhakiki. Unaweza kukagua sehemu iliyo hapo chini ili upate maelezo zaidi kuhusu maudhui nchini Uingereza.
Aina ya chanzo cha maelezo ya afya inayotimiza masharti kwa sasa Mbinu maalum iliyopo ya uchunguzi Marejeleo ya Jopo la Wataalamu

Taasisi za Elimu, kwa mfano*

  • Shule za Matibabu
  • Shule za Uuguzi
  • Shule za Afya ya Umma

* mifano yote haijajumuishwa katika nchi au maeneo yote

Mchakato wa Uidhinishaji

Mfano: Shirika la kuidhinisha rasmi vyuo vya matibabu.

Kiambatisho B kwenye Nakala ya NAM

Mashirika ya Afya, kwa mfano*

  • Hospitali
  • Kliniki

* mifano yote haijajumuishwa katika nchi au maeneo yote

Mchakato wa Uidhinishaji

Mfano: Shirika linaloidhinisha rasmi hospitali.

Kiambatisho B kwenye Nakala ya NAM
Majarida ya Kimatibabu

Kunakili katika Faharasa Jarida la Elimu

Mfano: majarida ya afya na matibabu “sharti yatimize viwango vya ‘upeo na habari, sera na taratibu za uandishi’, miongozo na sayansi, uchapishaji na usimamizi, na ufaafu”.

Ukurasa wa 12 kwenye Nakala ya NAM
Mashirika ya Serikali Kanuni za Uwajibikaji za Serikali Kisanduku cha 7 kwenye Nakala ya NAM

Watu binafsi na mashirika ambayo hayajaidhinishwa yaliyo na vituo vya YouTube vinavyoangazia maudhui ya afya

Watu binafsi na mashirika ambayo hayajaidhinishwa yaliyo na vituo vya YouTube vinavyoangazia maudhui ya afya.
Aina ya chanzo cha maelezo ya afya inayotimiza masharti kwa sasa Utaratibu wa nje unaotumika katika kutimiza masharti Marejeleo ya Jopo la Wataalamu

Wataalamu binafsi wa afya waliodhinishwa, kwa mfano*

  • Madaktari walioidhinishwa
  • Wauguzi walioidhinishwa
  • Wataalamu wa afya ya akili walioidhinishwa

* mifano yote haijajumuishwa katika nchi au maeneo yote

Mtu binafsi lazima awe na leseni inayotumika ili aweze kutekeleza taaluma yake katika eneo husika

Mfano: Shirika la utoaji leseni kwa madaktari

Jedwali la 1 katika Ripoti ya CMSS/NAM/WHO

Mashirika ambayo hayajaidhinishwa yanayowakilishwa na wataalamu wa matibabu walioidhinishwa, kwa mfano*

  • Mashirika ya kutoa misaada ya afya
  • Wachapishaji wa maudhui ya afya
  • Kampuni za afya 

* mifano yote haijajumuishwa katika nchi au maeneo yote

Shirika lazima liwakilishwe na mtaalamu wa matibabu aliyeidhinishwa kusimamia na kuhakiki maudhui ya YT ya shirika husika

 

Mfano: Shirika la utoaji leseni kwa madaktari

 

Kumbuka: Hii ndio hatua yetu ya kwanza ya kutambua na kubainisha vyanzo vya kuaminika vya maelezo ya afya kwenye YouTube. Aina za sasa za vyanzo vya maelezo ya afya, hazijumuishi vipengele vyote katika aina hizi na masharti ya vipengele yanaweza kubadilika. Tunaendelea kujitahidi kujumuisha vyanzo kulingana na kanuni na sifa hizi. Tunajitahidi kupata njia za kupanua ujumuishaji wa aina zaidi za vyanzo vya taarifa za afya katika vidirisha hivi.

Kumbuka: Iwapo kidirisha cha maelezo kinachotoa muktadha wa chanzo cha taarifa za afya kina lebo isiyo sahihi au iwapo huluki ya afya ina kituo kisicho sahihi au haina kituo kinachohusishwa nayo, tuma maoni ukitumia #healthinfo.

Kumbuka: "Mkutano wa WHO wa mashauriano mtandaoni wa kujadili kanuni za kimataifa za kutambua vyanzo vya kuaminika vya maelezo ya afya kwenye mitandao jamii" kwa hisani ya Shirika la Afya Duniani umepewa leseni ya CC BY-NC-SA 3.0 IGO.

Kwa Uingereza

Nchini Uingereza, tulishirikiana na Huduma za Afya za Kitaifa kubuni mwelekeo wa kubaini vituo vinavyotimiza masharti ya kuonyeshwa kwenye kidirisha cha taarifa. Huduma za Afya za Kitaifa ni neno la jumla linalorejelea mifumo ya huduma za afya inayofadhiliwa kwa mapato ya umma nchini Uingereza. Mwelekeo huu ulijumuisha hatua mbili zilizotekelezwa na Huduma za Afya za Kitaifa (NHS) 1) kukagua kanuni zilizobuniwa na jopo la wataalamu walioletwa pamoja na NAM katika muktadha wa Uingereza na 2) kuandaa chapisho la Kanuni za Kubuni Maudhui ya Afya, linalobainisha mwongozo wa masharti muhimu na mbinu bora zinazopaswa kufuatwa na mashirika, ili kubuni maudhui ya afya yenye ubora wa juu.

Katika hatua hizi za kwanza nchini Uingereza, mashirika ya NHS ndiyo tu yanayoalikwa kujithibitisha yenyewe kwa mujibu wa Kanuni za NHS za Kubuni Maudhui ya Afya. Kwa kukamilisha mchakato wa uthibitishaji wa kujifanyia, kituo cha shirika la NHS kitatimiza masharti ya kuonyeshwa kwenye vidirisha vya maelezo kama chanzo kinachoaminika na NHS.

Mwelekeo huu wa Uingereza ulikaguliwa na Muungano wa Vyuo vya Matibabu Vyenye Idhini ya Kifalme (AoMRC). AoMRC ilibaini kwamba mwelekeo huu unasaidia kutoa msingi maalum wa kutambua kiwango cha kuaminika cha vyanzo vya taarifa za afya kwenye mitandao jamii.

Rafu ya maudhui ya afya

Ukitafuta kwenye YouTube mada inayohusiana na hali mahususi ya afya ya mwili au akili, unaweza kuona rafu iliyo na maudhui ya afya kwenye matokeo yako ya utafutaji. Rafu ya maudhui ya afya itajumuisha video zinazohusiana na mada ya afya uliyotafuta na huenda ikajumuisha maudhui kutoka nchi au maeneo mengine ambayo yanalingana na lugha yako ya utafutaji.

Tunatumia kanuni zilizoandaliwa na wataalamu walioletwa pamoja na NAM, WHO na CMSS ili kushauri kuhusu vituo vinavyostahiki kuonyeshwa kwenye rafu. Kanuni hizi zilisaidia kubainisha orodha ya awali ya vyanzo vinavyostahiki vya mashirika ya afya yaliyoidhinishwa, majarida ya elimu ya tiba na huluki za serikali na zinazingatiwa kwenye mchakato wa maombi wa wataalamu binafsi wa afya na mashirika ambayo hayajaidhinishwa.

Nchini Uingereza, huluki kuu ya serikali ya masuala ya afya ni NHS. Kwa sababu hiyo, mashirika yote ya NHS yametimiza masharti kwa sasa. Vituo vya mashirika ya NHS ni sharti pia vijithibitishe kwa mujibu wa Viwango vya NHS vya Kutayarisha Maudhui ya Afya ili vitimize masharti ya kuonyeshwa kwenye rafu.

Nchini Ufaransa, ni lazima madaktari na wauguzi wasajiliwe na shirika la Répertoire Partagé des Professions de Santé (RPPS). Unaweza kusoma zaidi kuhusu mchakato na vigezo vya kujisajili kwenye tovuti yao.

Huenda rafu za maudhui ya afya zisipatikane kwa magonjwa yote katika matokeo ya utafutaji. Tunajitahidi kujumuisha magonjwa zaidi katika rafu na kupanua ustahiki kwa vituo zaidi.

Vidirisha vya taarifa za afya katika utafutaji

Unapotafuta mada zinazohusiana na afya kwenye YouTube, kama vile COVID-19, unaweza kuona kidirisha cha taarifa za afya katika matokeo yako ya utafutaji. Vidirisha hivi huonyesha taarifa kama vile dalili, uzuiaji na chaguo za matibabu. Taarifa hizi hutoka kwenye vyanzo ya kuaminika kama vile Shirika la Afya Duniani na taasisi nyingine za matibabu.

Vidirisha vya taarifa za afya pia hukuunganisha kwenye tovuti za taasisi ili upate maelezo zaidi. Tunakupa muktadha huu ili upate taarifa zinazoaminika zaidi kuhusu mada zinazohusiana na afya zinazofaa mahali uliko.

Katika baadhi ya nchi au maeneo, unaweza pia kuona viungo vinavyoelekeza kwenye njia za kimatibabu zilizothibitishwa za kujichunguza kutoka Google au kwa mamlaka za afya katika eneo. Kulingana na majibu ya kujichunguza, utapata maelezo zaidi kuhusu aina za usaidizi au huduma za matibabu ambazo zinaweza kukufaa.

Vyanzo vya taarifa

Tunahakikisha kuwa taarifa zilizo kwenye vidirisha vya taarifa za afya katika YouTube zinatoka kwenye taasisi za serikali, wizara za afya na taasisi nyingine za afya zinazoheshimika. Tutaendelea kuboresha vidirisha hivi na kujumuisha mashirika na mada zaidi zinazohusiana na afya baadaye.

Maelezo ya huduma ya kwanza kwenye utafutaji

Kwa hali mahususi za afya, rafu ya Huduma ya Kwanza kutoka kwa Vyanzo vya Afya inaweza kubandikwa juu ya matokeo ya utafutaji. Rafu itaangazia video ambazo ni rahisi kufuatilia kwa lengo la kuwasaidia watu wapate nyenzo za huduma ya kwanza kutoka vyanzo vinavyoaminika wanapohitaji bila kusoma au kusikiliza maagizo yanayochanganya.

Rafu itaonyeshwa kwa mada mbalimbali za huduma ya kwanza, kama vile CPR, kukabwa na kutekeleza mbinu ya Heimlich, kutokwa na damu, mashambulizi ya moyo, kiharusi na kifafa na zaidi.

Rafu kwa sasa inapatikana tu Marekani kwa Kiingereza na Kihispania.

Wakati unaopaswa kupata ushauri wa mtaalamu wa matibabu

Taarifa zinazohusiana na afya kwenye YouTube haziwezi kutumika kwa kila mtu wala si ushauri wa kimatibabu. Iwapo una tatizo la kimatibabu, hakikisha unawasiliana na mtoa huduma za matibabu. Iwapo una dharura ya kimatibabu, wasiliana na daktari wako au upige nambari ya dharura mahali uliko.

Taarifa ambazo YouTube huhifadhi kuhusu utafutaji wako

Vipengele vya afya huonekana tu iwapo utafutaji wako wa sasa au video unayotazama inahusiana na mada ya afya. Historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta haisababishi vipengele hivi, lakini iwapo ungependa kupata na kuondoa utafutaji wako, nenda kwenye data yako kwenye YouTube. Unaweza pia kupata maelezo kuhusu jinsi ya kuona na kufuta historia na mambo uliyotafuta.

Ripoti taarifa isiyo sahihi

Tuma maoni iwapo kuna matatizo kuhusu vipengele vya afya kwenye YouTube; au iwapo una pendekezo:-

  • Tuma maoni kupitia sehemu ya Zaidi '' katika vidirisha, au
  • Tutumie maoni ukitumia Menyu iliyoko kwenye picha yako ya wasifu.
  • Tafadhali jumuisha “#healthinfo” kwenye maoni yako ukiwa na maoni yoyote kati ya yafuatayo kuhusu kidirisha chenye muktadha wa vyanzo vya maelezo ya afya:
    • Kituo kina kidirisha cha maelezo kisicho sahihi.
    • Kidirisha cha maelezo kiko kwenye kituo kisicho sahihi cha huluki fulani ya afya.
    • Unaamini kituo kinafaa kuwa na kidirisha cha taarifa kuhusu muktadha wa chanzo cha taarifa ya afya na hakina, tafadhali kumbuka kuwa watu binafsi na mashirika yasiyoidhinishwa yaliyo na vituo vya YouTube vinavyoangazia maudhui ya afya yatahitaji kutuma ombi la idhini ya kufikia.
Kumbuka: Unaweza tu kutuma maoni kwenye rafu za maudhui ya afya kwa kutumia Menyu iliyo kwenye picha yako ya wasifu.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8562827024412317266
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false