Sera ya muziki uliohifadhiwa

Ikiwa una akaunti ya YouTube Music, huenda ukapewa nafasi ya seva ambapo utaweza kupakia na kuhifadhi baadhi ya maudhui kutoka kwenye kompyuta yako (kwa mfano faili za muziki zinazoweza kuwa na metadata na sanaa ya albamu) (“Faili za Muziki Ulizohifadhiwa”). Ukichagua kupakia Faili za Muziki Ulizohifadhiwa, utahifadhi haki zako zote zilizopo za Faili za Muziki Ulizohifadhiwa na nakala itahifadhiwa kwa niaba yako. YouTube itahakikisha kuwa unaweza kufikia Faili za Muziki Ulizohifadhiwa kupitia akaunti yako ya YouTube Music. Utaweza tu kufikia Faili za Muziki Ulizohifadhiwa kupitia akaunti yako ya YouTube Music na huwezi kuzituma kwa yeyote mwingine, ikiwa ni pamoja na watumiaji wa YouTube ambao wanaweza kuwa sehemu ya akaunti yako ya Google au Mpango wako wa Familia wa YouTube. Unawajibikia kisheria Faili za Muziki Ulizohifadhiwa unazopakia kwenye YouTube Music na huruhusiwi kujumuisha mali ya uvumbuzi ya wengine (kama vile nyenzo zenye hakimiliki) isipokuwa uwe na ruhusa kutoka kwa mhusika huyo au ukiwa na idhini ya kisheria ya kufanya hivyo.

Huenda tukahitaji kufanya mabadiliko machache yanayofaa kwenye Faili za Muziki Ulizohifadhiwa kama yanavyohitajika ili kuwezesha kipengele cha kucheza muziki kwenye YouTube Music au kupitia programu ya YouTube Music. YouTube haitatuma kwa wengine Faili za Muziki Ulizohifadhiwa.

Kumbuka: Baadhi ya vipengele kwenye programu ya YouTube Music havipatikani kwenye akaunti zinazodhibitiwa. Pata maelezo zaidi kuhusu matumizi yetu yanayosimamiwa kwenye YouTube hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1426890576511875870
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false