Masasisho yajayo na ya hivi karibuni ya mwongozo wa matangazo

Ukurasa huu unatoa muhtasari wa masasisho yajayo na ya hivi majuzi ya mwongozo wa matangazo kwa mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Pata maelezo zaidi kuhusu masasisho mengineyo ya sera za YouTube hapa.

Masasisho ya hivi karibuni

Masasisho kutoka miezi 3 iliyopita

 

Aprili 2024

Tunatoa mifano ya lugha chafu iliyokithiri na lugha za chuki au matusi katika sehemu ya “hakuna mapato ya matangazo” katika Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji ili kufanya sera yetu iliyopo kuwa dhahiri zaidi. Hakuna badiliko katika sera, maneno tunayoyachukulia kuwa “lugha chafu iliyokithiri" au jinsi video zako zinavyokaguliwa ili kubaini ufaafu kwa watangazaji.
 

Januari 2024

Tumesasisha mwongozo wetu wa Matukio Nyeti, ikiwa ni pamoja na lugha ili kufafanua kuwa maudhui yanayofaidika kutokana na au yanayotumia vibaya Tukio Nyeti huenda yasichume mapato. Hakuna mabadiliko ya sera, hali inayomaanisha kwamba hakutakuwa na tofauti kwenye mchakato wa kukagua video zako ili kubaini ufaafu kwa watangazaji.
 

Novemba 2023

Tumesasisha sehemu ya mwongozo wetu inayohusu Maudhui ya watu wazima katika maeneo mawili:

  • Kunyonyesha: Maudhui yanayohusu kunyonyesha ambapo mtoto anaonekana, hata chuchu zikiwa zinaonekana, sasa yanaweza kuchuma mapato ya matangazo. Hapo awali, maudhui kama haya yaliweza tu kuchuma mapato ikiwa hakuna chuchu zinazoonekana. Pia, vijipicha vya kunyonyesha vinavyolenga matiti bila kuonyesha chuchu sasa vinaweza kuchuma mapato ya matangazo.
  • Kucheza dansi za kimahaba:  Maudhui ya dansi yasiyodhihirisha ngono yanayohusisha miondoko ya mwili yenye mdundo, kama vile kutingisha makalio au kugusisha sehemu za siri, pamoja na dansi zinazoangazia mavazi mafupi sasa yanaweza kuchuma mapato ya matangazo. Hapo awali maudhui kama haya hayangeweza kuchuma mapato.

Tunafanya mabadiliko haya kwenye mwongozo wetu wa Maudhui ya watu wazima ili kuruhusu watayarishi kuchuma mapato ya matangazo kutokana na maudhui ambayo yanaonyesha dansi zisizodhihirisha ngono, kama vile kutingisha makalio, pamoja na maudhui yanayohusiana na unyonyeshaji.

Pia, makala ya Michezo ya video na uchumaji wa mapato yamesasishwa ili kuonyesha mabadiliko haya ya sera.

Masasisho ya awali

Masasisho yaliyofanyika zaidi ya miezi 3 iliyopita

2023

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji (Oktoba 2023)

Tumesasisha jina la sera yetu dhidi ya “Vitendo hatari au vyenye madhara” kuwa “Vitendo hatari na maudhui yasiyotegemeka.”  Pia tumeongeza lugha inayofafanua kuwa maudhui yanayotoa madai yanayoonekana wazi kuwa si ya kweli na yanaweza kudhoofisha kwa kiasi kikubwa hali ya kushiriki au imani katika mchakato wa uchaguzi au wa kidemokrasia hayachumi mapato ya matangazo. Kwa mfano, maelezo kuhusu taratibu za upigaji kura wa umma, ustahiki wa wagombea wa kisiasa kulingana na umri au mahali walipozaliwa, matokeo ya uchaguzi au maelezo ya hali ya kushiriki kwenye sensa yanayokinzana na rekodi rasmi za serikali. Maudhui yanayotaja madai ya uongo kuhusu mada hii huku yakionyesha wazi kuwa si ya kweli, kama vile maudhui ya kielimu, kihalisia au maoni yanaweza kuchuma mapato ya matangazo.

Hatujabadilisha jinsi tunavyotekeleza sera hii, kumaanisha kwamba hakutakuwa na tofauti katika jinsi video zako zitakavyokaguliwa ili kubaini ufaafu kwa watangazaji.

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji (Septemba 2023)

 Tumesasisha mwongozo wetu kuhusu Masuala tata. 

  • Kuwaruhusu Watayarishi wapate mapato zaidi ya matangazo kwenye maudhui yanayojadili mada kama vile utoaji mimba na unyanyasaji wa kingono kwa watu wazima. Hii inamaanisha kwamba maudhui yanayojadili mada hizi bila kufafanua maelezo ya kuogofya yanaweza kuchuma mapato kikamilifu. Tunajua kwamba video zinazoangazia mada kama hizi zinaweza kuwa nyenzo muhimu kwa watumiaji, kwa hivyo tunataka kuhakikisha kuwa inapowezekana, Masuala tata yanayojadiliwa kwa njia isiyo ya maelezo na isiyo ya kuogofya hayazuiwi kwa njia ya kukomesha uchumaji wa mapato. Pia tunafahamu vyema kuwa baadhi ya jumuiya za watayarishi huhisi kama zinapata aikoni nyingi za manjano kwa sababu zinapakia maudhui kuhusu mada zinazowaathiri kwa njia isiyo na uwiano. Tunatumai kuwa mabadiliko haya yanaweza kuwapa Watayarishi wote nafasi zaidi ya kujadili mada hizi na kustahiki kuchuma mapato ya matangazo. 
  • Pia, tunapangilia mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji kuhusu matatizo ya ulaji pamoja na Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube. Maudhui yanayoangazia matatizo ya ulaji na vichochezi vya ushiriki kama vile mwongozo kuhusu ulaji wa chakula kingi kwa haraka, kuficha au kuweka akiba ya chakula au kutumia vibaya dawa zinazosaidia kitendo cha kwenda choo hayatapokea mapato ya matangazo. 
    • Mabadiliko haya yatahakikisha kuwa maudhui kama haya hayatuzwi mapato ya matangazo na kwamba mwongozo wetu wa uchumaji mapato na jumuiya utaendelea kusawazishwa. 
    • Kumbuka kuwa maudhui ya kielimu au hali halisi na maudhui ya mtu aliyenusurika yanayorejelea vipengele hivi vya kuwa na matatizo ya ulaji bila kutangaza shughuli kama hizo hayataathiriwa na mabadiliko haya.

Pia, makala ya Michezo ya video na uchumaji wa mapato yamesasishwa ili kuonyesha mabadiliko haya ya sera.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu taarifa hii, tazama video yetu ya Creator Insider.

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji (Machi 2023)

Tumesasisha mwongozo wetu kuhusu lugha isiyofaa. Lugha chafu (kwa mfano, matusi ya kingono) inayotumiwa katika sekunde 7 za kwanza au katika sehemu kubwa ya video inaweza kupata mapato machache ya matangazo badala ya kutopata mapato ya matangazo, kama ilivyotangazwa awali hapo chini. Matumizi ya maneno kama vile “malaya”, “bwege”, “fala” na “takataka” kwenye maudhui ya video yanafaa kwa aikoni za kijani. Lugha chafu inayotumiwa katika sekunde 8 hadi 15 za kwanza sasa inaweza kupata mapato ya matangazo. Pia, tumefafanua mwongozo wetu kuhusu jinsi ambavyo lugha chafu katika muziki inavyoshughulikiwa; lugha chafu zaidi inayotumika kwenye muziki wa chinichini, nyimbo zinazosindikiza, muziki wa utangulizi au utamatishaji inaweza kuchuma mapato ya matangazo.

2022

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji (Novemba 2022)

Tumesasisha mwongozo wetu ili kujumuisha lugha iliyo wazi zaidi, mabadiliko ya mwongozo mahususi na mabadiliko ya ufaafu wa kuwekwa matangazo. Tazama hapa chini uone mwongozo ulioathiriwa pamoja na mifano ya orodha ambayo haijataja vipengele vyote vya kile kinachobadilika:

  • Maudhui ya watu wazima
    • Vijipicha, mada na video zenye maandishi yenye maudhui ya ngono (kama vile viungo, umri zaidi ya miaka 18), lugha chafu, picha (kama vile makalio halisi au yaliyohuishwa yaliyofunikwa kidogo), sauti (kama vile kushiriki vidokezo vya ngono au uzoefu wa kufanya kazi) na vitendo vinavyochochea ngono (kama vile kujamiiana kwa wanyama au vitendo vya ngono vinavyoangaziwa) huenda zisipate mapato ya matangazo.
    • Utekelezaji wa sera kuhusu sanaa za kitamaduni zinazoonyesha vitendo vya ngono, dansi zinazochochea ngono, elimu ya ngono bila nia ya kuamsha hamu kwa hadhira bado haijabadilika na inaweza kupokea mapato ya matangazo.
  • Vurugu 
    • Maudhui yenye maiti zisizoogofya zinazowasilishwa bila muktadha wowote, vurugu za mchezo zinazoelekezwa kwa mtu halisi aliyetajwa au vitendo vinavyotengenezwa ili kuleta matukio ya kushtua (kama vile mauaji ya kikatili), wakati unaodokezwa wa kifo (kama vile kulipua jengo likiwa na watu ndani) huenda yasipokee mapato ya matangazo.
    • Mchezo wa kawaida ambapo majeraha mabaya yanatokea baada ya sekunde 8 za kwanza, maudhui yasiyo ya picha na matokeo yake (kama vile video za mji uliosombwa na maji) au kutekwa na polisi kama sehemu ya utekelezaji wa sheria kunaweza kupokea mapato ya matangazo.
  • Matendo hatari au ya kuumiza 
    • Vitendo hatari ambapo watoto ni washiriki au waathiriwa (kama vile watoto wanaoshiriki katika majaribio au mashindano yanayohusisha vitendo visivyofaa watoto) havitapokea mapato ya matangazo.
  • Matukio nyeti
    • Mada zote zinazohusiana na Makundi ya Ulanguzi wa Dawa za Kulevya (DTO) na Mashirika ya Kigeni ya Kigaidi (FTO) yatapatikana chini ya Vitendo Hatari au hatarishi badala ya Matukio nyeti.
    • Lugha inayohusiana na Matukio nyeti imesasishwa ili kuhakikisha kuwa ni ya wazi na inaeleweka, lakini utekelezaji wa sera haujabadilika. 
  • Lugha isiyofaa
    • Namna yetu ya kushughulikia lugha chafu inabadilika. Aina zote za lugha chafu sasa zinashughulikiwa kwa usawa, kumaanisha kuwa hazitofautishwi kulingana na viwango vya athari (kwa mfano, athari kiasi, ya wastani, kubwa au kubwa zaidi) na hatuchukulii ‘bure’ na ‘shenzi’ kama lugha chafu tena. Kwa hivyo, lugha chafu inayotumiwa katika jina, vijipicha au katika sekunde 7 za kwanza za video au inayotumika mara kwa mara kwenye video huenda isipokee mapato ya matangazo.
    • Lugha chafu zinazotumiwa baada ya sekunde 8 za kwanza za video zinaweza kupokea mapato ya matangazo. Msimamo wetu wa kutochuma mapato kwa maudhui yenye lugha chafu kote au unaojumuisha video nyingi kwenye video haubadiliki.
  • Dawa za kujistarehesha na maudhui yanayohusiana na dawa
    • Matumizi na utumiaji wa dawa za kulevya, kama vile kujidunga sindano au uvutaji wa pamoja wa sigara katika maudhui ya michezo ya video, hayatapokea mapato ya matangazo. 
    • Uuzaji wa dawa za kulevya au kutajwa kwa dawa katika maudhui ya michezo ya video kunaweza kupokea mapato ya matangazo.

Pia tunaleta mwongozo mpya chini ya mwongozo wa Kuendeleza tabia danganyifu. Maudhui yafuatayo sasa yatakuwa katika upeo wa “Maudhui haya hayatapata mapato ya matangazo”: 

  • Kujifanya kuwa mfanyakazi wa duka la rejareja bila ruhusa ya mwenye mali au kukiuka kanuni zake za maadili (kama vile kuendelea kufungua baada ya saa zao za kazi). 
  • Kutumia au kuhimiza matumizi ya programu ya udukuzi katika michezo yenye ushindani kwenye intaneti.

Makala ya Michezo ya video na uchumaji wa mapato pia yamesasishwa ili kuonyesha mabadiliko haya ya sera.
 

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji (Oktoba 2022)

Ukurasa wa Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji umesasishwa ili kuweka wazi kwa jumuiya ya Watayarishi kwamba mwongozo wa leo wa uchumaji wa mapato ulioainishwa unatumika katika muundo wa VOD (Mfumo wa Kufikia Video Unapohitaji) na Video Fupi. Hakuna mabadiliko ya sera, ikimaanisha kwamba hutaona badiliko lolote kwenye mchakato wa kukagua video zako ili kubaini ufaafu kwa watangazaji. Tutatoa taarifa zaidi masasisho yanapofanyika. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu wakati ambapo ugavi wa mapato ya matangazo ya Video Fupi unaanza hapa.

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji (Agosti 2022)

Tumesasisha mwongozo wa uchumaji wa mapato unaohusu maudhui ambayo huenda ni hatari au yenye madhara. Video zilizopakiwa zinazoonyesha shughuli za sungusungu hazitaonyesha matangazo. 

Ukurasa wa Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji umesasishwa ili kuonyesha mabadiliko haya. Hakuna mabadiliko ya sera, ikimaanisha kwamba hutaona badiliko lolote kwenye mchakato wa kukagua video zako ili kubaini ufaafu kwa watangazaji.

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji kwenye mwongozo wa maudhui yasiyofaa kwa watoto na familia (Aprili 2022)

Hivi karibuni tumesasisha mwongozo wa matangazo kwa maudhui “yanayolenga watoto” ili kusaidia kuwaongoza watayarishi kuhusu maudhui yanayofaa na yasiyofaa kuonyesha matangazo. Tumeweka mwongozo mpya unaoitwa “Maudhui yasiyofaa kwa watoto na familia” wenye aina tatu: Maudhui yanayohimiza tabia mbaya, Maudhui ya watu wazima yanayowalenga watoto na Maudhui ya kuogofya yanayowalenga watoto. 

Masasisho yanayohusiana na vita vya Ukraini (Machi 2022)

Tumechapisha mwongozo kwenye ukurasa wa Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji kuhusiana na vita inavyoendelea Ukraini: 

Kutokana na vita inavyoendelea Ukraini, maudhui yanayopuuza, kuhalalisha au yenye nia ya kujinufaisha na vita hiyo hayatakidhi vigezo vya uchumaji wa mapato hadi ibainishwe vinginevyo. Lengo la sasisho hili ni kufafanua na katika hali fulani kupanua mwongozo wetu unaohusiana na vita hivi.

2021

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji kwenye maudhui ya watu wazima (Desemba 2021)

Tumesasisha mwongozo wa uchumaji wa mapato unaohusu maudhui yanayoonyesha vifaa vya utambulisho wa kijinsia. Video zilizopakiwa zinazoonyesha vitu vinavyofanana na viungo vya uzazi pasipo kuonyesha uchi, kama vile matiti au uume, vinavyowasaidia watayarishi kuelezea hali zao wakiwa wanataabika na utambulisho wao wa kijinsia, zinaweza kuonyesha matangazo.

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji kwenye matendo hatari au yenye madhara (Octoba 2021)

Tumesasisha mwongozo wetu ili kujumuisha mifano dhahiri zaidi katika maeneo yafuatayo ya sera: Maudhui ya watu wazima, Maudhui yanayohusiana na bunduki, Vurugu, Maudhui ya kuogofya, Maudhui ya matusi na chuki, Matukio nyeti na Maudhui ya dawa za burudani na yanayohusiana na dawa za kulevya. Pia, tumeweka sehemu mpya ya Ufafanuzi ili kuelezea maneno ya msingi yaliyotumika kwenye mwongozo mzima.

Isitoshe, tunaleta mwongozo mpya: Kuwezesha nyendo danganyifu. Hatua hii inatoa mwongozo kuhusu masharti ya kuonyesha matangazo kwenye maudhui yanayohusiana na kuingia mahali bila ruhusa, kudanganya au udukuzi kwa kutumia kompyuta ambao ni binafsi au unaolipishwa.

Vilevile, tunahamisha mwongozo wetu unaohusu uchumaji wa mapato kupitia maudhui yanayohusiana na COVID-19 kutoka kwenye ukurasa wake wa awali na kuuweka moja kwa moja katika Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji ili kurahisisha usomaji. Watakaotembelea ukurasa wa awali wataelekezwa kwenye Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji.

Makala ya Michezo ya video na uchumaji wa mapato pia yamesasishwa ili kuonyesha mabadiliko haya ya sera.

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji kwenye matendo hatari au yenye madhara (Octoba 2021)

Mnamo mwezi Novemba, tunasasisha mwongozo wa uchumaji wa mapato kuhusu maelezo ya kupotosha ya mabadiliko ya tabianchi, ili kubainisha kwamba maudhui yanayochochea madai kuhusu mabadiliko ya tabianchi yaliyo kinyume cha maelezo yanayoaminika ya kisayansi, hayataonyesha matangazo. Maudhui ya elimu, habari au video za maisha halisi zinazohusu mada hii zinaweza kuendelea kuonyesha matangazo.

Tembelea Kituo cha Usaidizi cha Google Ads hapa ili upate maelezo zaidi kuhusu sasisho hili.

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji kwenye Maudhui yanayohusiana na bunduki (Septemba 2021)

Tunafafanua mwongozo wetu wa uchumaji wa mapato kuhusu Maudhui yanayohusiana na bunduki. Video za kutenganisha na kuunganisha silaha kwa madhumuni ya matengenezo zinaweza kuonyesha matangazo. Pia, tunaboresha mwongozo wetu wa aina nyinginezo za maudhui ya bunduki.

Ukurasa wa Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji utasasishwa mwezi Octoba ili kuonyesha mabadiliko haya, chini ya sehemu ya Maudhui yanayohusiana na bunduki.

Masasisho ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji kuhusu Vurugu (Julai 2021)

Tunasasisha mwongozo wa uchumaji wa mapato kuhusu vurugu, ili kufafanua kwamba video zinazoonyesha wanyama katika hali ya hatari iliyosababishwa na binadamu hazitaonyesha matangazo.

Masasisho ya sera mbalimbali katika Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji na makala ya Michezo ya video na uchumaji wa mapato (Aprili 2021)

Kutokana na maoni ya watayarishi na watangazaji, tumesasisha mwongozo wetu ili kuruhusu aina zaidi ya maudhui kutimiza vigezo vya uchumaji kamili wa mapato (aikoni ya kijani) huku tukiendelea kudumisha viwango vya sekta ya utangazaji. 
 
Kwanza, tunapanua uchumaji wa mapato kwa maudhui ya elimu, habari au video za maisha halisi yanayoweza kujumuisha matendo ya kikatili yanayofanywa na polisi, dawa za burudani na maudhui yanayohusiana na dawa za kulevya au matukio nyeti. Pia, tunapanua uchumaji wa mapato kwa maudhui yenye masuala tata, ambapo video inajumuisha majadiliano yasiyo na upendeleo na yasiyoogofya ya masuala tata. 
 
Pili, tunapanua uchumaji wa mapato ili kurushu mada za watu wazima zinazowasilishwa kupitia muktadha wa vichekesho (k.m. mapenzi au matani yanayohusu kuchumbiana) na matumizi ya lugha chafu kiasi (k.m. mbwa na shonde) kwenye sekunde 30 za mwanzo.

Pia, ili kufafanua mwongozo tumeweka mifano zaidi kwenye sehemu zifuatazo: Maudhui ya watu wazima, Matendo hatari au yenye madhara na sehemu zinazohusiana na Bunduki kwenye Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji.
 
Sehemu ya Vidokezo vya kuchuma mapato kwenye video za michezo iliyopo katika makala ya Michezo ya video na uchumaji wa mapato imesasishwa pia ili kuonyesha mabadiliko haya ya sera.

Mwongozo umeongezwa kwenye maudhui yenye Lugha isiyofaa, Vurugu, Dawa za burudani na dawa za kulevya, pamoja na masasisho kwenye sera yetu ya uchumaji wa mapato inayohusiana na COVID-19 (Februari 2021)

Sasa makala ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji yanajumuisha mifano zaidi katika sehemu za “Unaweza kuwasha matangazo kwa maudhui haya” kwa ajili ya mwongozo wa maudhui ya Lugha isiyofaa, Vurugu, Dawa za burudani na maudhui yanayohusiana na dawa za kulevya.

Vilevile, masasisho yamefanyika katika makala ya Sasisho la uchumaji wa mapato kwenye maudhui ya COVID-19 pamoja na sehemu ya Matendo hatari au yenye madhara ya mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji, ili kutoa mwongozo zaidi juu ya maudhui yanayohusiana na kuchanja.

Tumeweka ukurasa mpya unaochambua mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji kulingana na muktadha kwa maudhui ya michezo ya video (Januari 2021)

Ili kuwasaidia Watayarishi wa YouTube wa maudhui ya michezo ya video kuelewa zaidi mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji, tumechapisha ukurasa mpya kusaidia kuleta mada ya michezo ya video na uchumaji wa mapato katika muktadha. 

Ukurasa huu mpya ulibuniwa kwa lengo la kufanya mwongozo wetu ueleweke kwa urahisi zaidi, hususani kwenye suala la maudhui ya michezo ya video na kusaidia kuboresha kuelewa uthibitishaji unaojifanyia kwa Watayarishi wa YouTube wa maudhui ya michezo ya video. 

Hakuna mabadiliko ya sera, ikimaanisha kwamba hutaona badiliko lolote kwenye mchakato wa kukagua video zako ili kubaini ufaafu kwa watangazaji. 

Masasisho ya sehemu mbalimbali za Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji ili kutoa taarifa zaidi na mifano, makala ya Kadiria maudhui yako kupitia Uthibitishaji Unaojifanyia imeacha kutumika (Januari 2021)

Sasa makala ya Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji yamesasishwa kwa kuongeza mwongozo na mifano zaidi ya uthibitishaji unaojifanyia. Kutokana na hatua hii, makala ya Kadiria maudhui yako kupitia Uthibitishaji Unaojifanyia imeacha kutumika. 

Mifano mipya na ya kina imewekwa chini ya sehemu ya “Unaweza kuwasha matangazo lakini ni biashara zilizojijumuisha tu ndizo zitaonyesha matangazo” (Matangazo Yaliyodhibitiwa) na “Unapaswa kuzima matangazo kwa maudhui haya” (Usionyeshe Matangazo) kwa ajili ya sera za Maudhui ya watu wazima na Maudhui ya matusi na chuki ili kufafanua zaidi maudhui yaliyopo kwenye upeo. Pia, tumetenganisha sera za Matukio nyeti na Mada tata ili kuhakikisha tunatoa mwongozo wa sera ulio wazi na mahususi zaidi. 

Mabadiliko madogo yamefanywa kwenye sera za Matendo hatari au yenye madhara ili kuonyesha mifano ya ziada ya maudhui yanayoweza kusababisha hali ya Matangazo Yaliyodhibitiwa au "Usionyeshe Matangazo". 

Dokezo jipya limewekwa kwenye Maudhui yanayochochea na kushusha hadhi, Maudhui yanayohusiana na tumbaku na Mada za watu wazima katika sera za maudhui ya familia ili kufahamisha wasomaji kwamba hizi zimewekwa pamoja na sera nyinginezo katika dodoso la uthibitishaji unaojifanyia kwenye Studio ya YouTube.

Hakuna mabadiliko ya sera, ikimaanisha kwamba hutaona badiliko lolote kwenye mchakato wa kukagua video zako ili kubaini ufaafu kwa watangazaji.

2020

Masasisho ya sehemu mbalimbali za makala ya Kadiria maudhui yako kupitia Uthibitishaji Unaojifanyia yanayotoa taarifa zaidi na mifano (Octoba 2020)

Sasa makala ya Kadiria maudhui yako kupitia Uthibitishaji Unaojifanyia inajumuisha mifano zaidi ya kina kwenye sehemu ya “Unaweza kuwasha matangazo kwa maudhui haya” kwa ajili ya sera za Vurugu na Maudhui ya watu wazima ili kufafanua zaidi maudhui yaliyopo kwenye upeo. Pia, tumefafanua maana ya “matukio nyeti” na “angazia” kwenye sehemu ya Mada zenye utata na Matukio nyeti.

Mabadiliko madogo yamefanyika kwenye sehemu za Lugha Zisizofaa na Matendo Hatari au yenye Madhara ili kuonyesha mifano zaidi ya mizaha inayosababisha mfadhaiko wa kihisia na kufafanua kwamba matumizi ya mara kwa mara ya lugha chafu zaidi yanaweza kupelekea hali ya Matangazo Yaliyodhibitiwa au Usionyeshe Matangazo. 

Hakuna mabadiliko ya sera, ikimaanisha kwamba hutaona badiliko lolote kwenye mchakato wa kukagua video zako ili kubaini ufaafu kwa watangazaji.

Mwongozo mahususi wa Habari umeongezwa kwenye Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji (Agosti 2020)

Mwongozo wa Vurugu na Mada zenye utata na matukio nyeti utafafanuliwa ili kujumuisha jinsi sera zetu zitakavyoathiri kuripoti habari za hivi punde. 

Sasisho hili litachapishwa mwezi Agosti.

Mwongozo wa Maudhui ya Kuogofya umeongezwa kwenye Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji (Agosti 2020)

Mwongozo wa Maudhui ya Kuogofya huwakilisha ufafanuzi wa sera zilizopo na huangazia maudhui ambayo huenda yakakasirisha, kuchukiza au kuogofya watazamaji. Tunafanya mabadiliko haya kwenye nyenzo hizi ili kusaidia kuboresha uelewa wa Watayarishi kuhusu maudhui yasiyoweza kuonyesha matangazo.

Sehemu mpya itaongezwa kwenye dodoso la uthibitishaji unaojifanyia. Masasisho pia yafanyika mwezi Agosti kwenye Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji na kwenye makala ya Kadiria maudhui yako kupitia Uthibitishaji Unaojifanyia ili kutoa maelezo mengi iwezekanavyo kwa Jumuiya ya Watayarishi. 

Hakuna mabadiliko ya sera, ikimaanisha kwamba hutaona badiliko lolote kwenye mchakato wa kukagua video zako ili kubaini ufaafu kwa watangazaji.

Masasisho kwenye Lugha isiyofaa (Juni 2020)

Maneno kwenye sehemu hii yamerekebishwa ili kufafanua kwamba maneno yenye lugha chafu yaliyoandikwa yakiwa na makosa ya tahajia kwenye jina au kijipicha kwa madhumuni ya kuzuia matokeo yenye lugha isiyofaa kwenye hali ya Matangazo Yaliyodhibitiwa au Usionyeshe Matangazo. Watayarishi wanaweza kusoma masasisho hapa.  

Hakuna mabadiliko ya sera, ikimaanisha kwamba hutaona badiliko lolote kwenye mchakato wa kukagua video zako ili kubaini ufaafu kwa watangazaji.

Masasisho ya makala ya Kadiria maudhui yako kupitia Uthibitishaji Unaojifanyia (Mei 2020)

Sasa makala haya yanajumuisha mifano ya aina za maudhui yanayoweza kuingia kwenye mojawapo kati ya machaguo yaliyobainishwa kwenye dodoso linalopatikana kwenye akaunti yako. Pia, tumejumuisha fafanuzi za dhana muhimu, kama vile uchi zilizorejelewa kwenye dodoso zima.

Hakuna mabadiliko ya sera, ikimaanisha kwamba hutaona badiliko lolote kwenye mchakato wa kukagua video zako ili kubaini ufaafu kwa watangazaji.

Masasisho yanayohusiana na COVID-19 (Aprili 2020)

Maudhui yanayorejelea na/au kuangazia COVID-19 pamoja na kufuata Mwongozo wetu wa Jumuiya na Maudhui Yanayofaa Watangazaji sasa yanaweza kuchuma mapato (na Watayarishi wataona aikoni ya kijani). Pata mwongozo wa kina zaidi kuhusu kuchuma mapato kupitia maudhui ya COVID-19 hapa.

Masasisho ya Mada zenye utata na matukio nyeti pamoja na Lugha isiyofaa (Februari 2020)

Sasa makala haya yanajumuisha orodha ya kina ya mada zinazochukuliwa kuwa zenye utata na maelezo ya jinsi tunavyofafanua matukio nyeti. Tumefafanua mwongozo wetu kuhusu Lugha Isiyofaa.

Hakuna mabadiliko ya sera, ikimaanisha kwamba usitegemee badiliko lolote kwenye mchakato wa kukagua video zako ili kubaini ufaafu kwa watangazaji.

2019

Sasisho la Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji (Juni 2019)

Makala haya sasa yanajumuisha mifano zaidi ya maudhui yatakayopokea matangazo machache au yasiyopokea matangazo kabisa. 

Hakuna mabadiliko ya sera, ikimaanisha kwamba usitegemee badiliko lolote kwenye mchakato wa kukagua video zako ili kubaini ufaafu kwa watangazaji.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
598799736163588501
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false